Uingereza kukosa msaada wa kupambana na Corona kutokana na kujitoa Umoja wa Ulaya

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
a8c6c8f8a110e225bbdd1f49fe2a13a0


MIEZI miwili tangu Uingereza ilipotangaza rasmi kujitoa katika Umoja wa Ulaya (EU), tayari imeanza kuonja machungu ya kujitoa katika umoja huo, baada ya kukosa fursa ya kupata msaada wa kupambana na majanga katika kipindi hiki ambacho nchi hiyo imekubwa na janga la homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (Covid-19).

Kama sehemu ya kukabiliana na ugonjwa huo wa mlipuko ambao umezitikisa nchi karibu zote duniani, Uingereza ikiwa miongoni mwa nchi zilizoathirika zaidi kufikia sasa, EU imetangaza rasmi mpango mkakati wa dharura wa kukabiliana na janga hilo, kwa kutoa fedha kwa ajili ya kusaidia nchi zote wanachama.

Katika utaratibu huo, Uingereza ambayo ilitangaza rasmi kujitoa katika EU Januari 31 mwaka huu, haitakuwa sehemu ya msaada huo ambao unatarajiwa kuongeza nguvu kwa nchi wanachama katika kukabiliana na maambukizi na athari za corona.

Tayari Uingereza imeripoti maambukizi ya virusi vya corona kwa zaidi ya watu 55,242 akiwemo Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Boris Johnson ambaye ndiye aliyesimamia nchi hiyo kujitoa rasmi EU. Mwanamfalme Charles na mama yake, Malkia Elizabeth II wa Uingereza pia wameripotiwa kuambukizwa virusi hivyo.

MFUKO WA MASHIKAMANO
Kupitia kikao cha dharura cha Machi 26 mwaka huu, Mfuko wa Mshimamano wa Umoja wa Ulaya uliidhinisha pendekezo la Tume ya Ulaya kuruhusu nchi wanachama kuomba usaidizi wa kifedha kutoka Mfuko wa Mshikamano wa EU katika mapambano yao dhidi ya Covid-19. Pendekezo hilo ni sehemu ya hatua za EU kuhamasisha rasilimali zote zilizopo za bajeti kusaidia nchi za EU kukabiliana na janga hili.

Tume ilipendekeza kupanua wigo wa Mfuko wa Mshikamano ili kuongeza changamoto mpya ya afya ya umma kwenye dharura za asili zilizokuwa zimeorodheshwa hapo awali.

Nchi wanachama zilizoathiriwa zaidi zinapata msaada wa kifedha wa hadi Euro milioni 800 mnamo 2020. Msaada utaamuliwa kwa msingi wa wingi wa kesi za maambukizi.

MSHIKAMANO WA EU
Mshikamano huu uliundwa kama majibu ya mafuriko makubwa katika eneo la Ulaya ya Kati mnamo 2002, lengo kuu la Mfuko wa Ushirikiano wa EU ni kutoa msaada wa kifedha kwa nchi wanachama wa EU zinazokumbwa na majanga ya asili.

Chini ya sheria za sasa, mfuko huo ungeweza kusaidia urejeshwaji tu kutoka kwa majanga kama mafuriko, moto wa misitu, matetemeko ya ardhi, dhoruba na ukame. Dharura za kiafya za umma kama Covid-19 hazikuangukia ndani ya malipo yake.

Hata hivyo, chini ya sheria mpya zilizopitishwa hivi karibuni, shughuli za dharura za umma na uokoaji, kama vile kurejesha miundombinu iliyoharibiwa, kusafisha maeneo na kutoa malazi ya muda kwa watu, yanakuwa masuala muhimu yanayostahili kufadhiliwa.

Sheria hizo zitaongezewa kugharamia usaidizi kwa idadi ya watu katika kesi za mizozo ya kiafya na kuchukua hatua kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza.

“Kuruhusu Mfuko wa Mshikamano wa EU kutumika kushughulikia Covid1-9 ina maana, kwa athari yake kubwa kwa watu, afya na uchumi katika sehemu zote za Umoja wa Ulaya.

Hizi sheria zote zilikusudiwa kubadilishwa kwa dharura na changamoto mpya. Hii itaruhusu EU kutenda kwa mshikamano,” anasema mwanachama wa Ufaransa wa GUE / NGL Younous Omarjee, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya kikanda.

JANGA LA CORONA LALETA MGONGANO EU
Hata hivyo, pamoja na hatua hiyo, bado nchi zinazotumia sarafu ya Euro zimeshindwa kuwa na mshikamano katika mpango wa kiuchumi wa kupambana na janga la virusi vya corona na kusababisha wasiwasi wa hali itakavyokuwa katika vita hii.

Kwanza kabisa ifahamike kwamba katika kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja mataifa ya Ulaya yamekuwa yakijaribu kushirikiana kwa karibu kushughulikia janga hili na viongozi wa Ulaya wamekuwa wakijitahidi kushirikiana kuondowa madhila ya kibinadamu na kiuchumi kufuatia janga hili duniani ambalo limeuvuruga kabisa mfumo wa maisha ya kila siku ya mabilioni ya watu na kuuporomosha uchumi wa mataifa mbali mbali ya dunia.

Lakini bado nchi hizi zinapambana na katika upande wa kiuchumi na kifedha mawaziri kutoka nchi 19 zinazotumia sarafu ya Euro zilishindwa kupata makubaliano kuhusu jinsi ya kutumia kipengele chake cha fedha na kwa umbali gani kinaweza kuimarisha mshikamano kati ya nchi masikini na zile tajiri wanachama wake.

Sasa hatua hii ya kutofikiwa makubaliano na migongano mengine imesababisha athari kadhaa ikiwemo kujiuzulu mara moja kwa rais wa baraza linalosimamia utafiti wa kisayansi barani Ulaya, Profesa Mauro Ferrari ambaye amevunjwa moyo na jinsi viongozi wa Ulaya wanavyolishughulikia suala la mapambano dhidi ya virusi vya corona.

Hatua yake hiyo imezidisha shinikizo kwa taasisi mbali mbali za EU ambazo zimeshutumiwa kwa kutoshirikiana kukabiliana na janga hili la dunia.

Benki Kuu ya Ulaya imewaambia mawaziri hao wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro kwamba huenda zikahitaji Euro trilioni 1.5 za mipango ya uokozi wa kiuchumi kutokana na janga hili la Covid-19.

Juu ya hayo huko nchini Uingereza, ambayo sasa inajisimamia yenyewe bila kutegemea ushirikiano wa EU bado kinachozungumzwa ni kuendelea kuwa katika chumba cha wagonjwa mahututi Waziri Mkuu Johnson aliyeambukizwa virusi vya corona huku hali yake ikitajwa kuendelea vizuri akiwa chini ya uangalizi wa madaktari bingwa wa magonjwa ya mapafu nchini humo.

Zaidi ya watu 55,000 wameambukuzwa na takriban 6,200 wameshafariki Uingereza.

Lakini pia mgogoro huu wa virusi vya corona umesababisha malumbano ya aina yake ambapo Rais wa Marekani Donald Trump amelikosoa Shirika la Afya Duniani (WHO) akilituhumu kujielekeza zaidi kwa China huku pia akitoa kauli mbaya akisema atasimamisha ufadhili wa Marekani katika shirika hilo.

Lakini huko China katika mji wa Wuhan vilikoanzia virusi hivi matumaini ya faraja yameripotiwa ambapo marufuku ya kutotoka nje imeondolewa baada ya miezi miwili na hali ya maisha ya kawaida inatajwa imeanza kurejea jana Jumatano.

Katika mji huu zaidi ya watu 50,000 walipata maambukizi na zaidi ya 2,500 walifariki. Ama kwa kuiangalia hali halisi duniani kufikia jana Jumatano zaidi ya watu milioni 1.38 wameambukizwa na 81,451 wameshafariki. Nchi zenye visa vya maambukizi kwa ujumla duniani ni 212.

WASIWASI MPYA WAIBUKA
Wakati viongozi wa EU kwa kuzingatia kuongezeka maambukizi ya virusi vya corona, wametoa tahadhari juu ya hatari ya kugawanyika umoja huo, mtandao wa habari wa Washington Post unaandika kwamba, ugonjwa wa Covid-19 unaotokana na virusi vya corona na unaoenda sambamba na migogoro mikubwa katika sekta za afya na kiuchumi, umezidi kupanua mpasuko barani Ulaya kiasi kwamba baadhi ya viongozi wa EU wamepatwa na wasi wasi wa kutumiwa suala hilo katika ulipizaji kisasi wa baadaye.

Ripoti hiyo inaeleza kwamba, pamoja na Uingereza kutonufaika na juhudi za mfumo wa pamoja, bado mshikamano wa EU umepata pigo kubwa baada ya hatua ya kujitoa kwake (Brexit), ikifananishwa na mgogoro wa kifedha wa mwaka 2008.

Aidha mtandao wa habari wa gazeti la Washington Post unafafanua kwamba, iwapo viongozi wa EU hawatoweza kuchagua njia moja ya pamoja, kama alivyonukuliwa akisema wiki hii mmoja wa waasisi wake, basi EU itakumbwa na hatari ya kusambaratika.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, mwanzoni mwa kuenea virusi vya corona, nchi wanachama wa EU zilionyesha aina fulani ya urafiki na kulinda maslahi na thamani za EU, lakini baada ya ugonjwa huo kuenea barani Ulaya mipaka ilianza kufungwa kati ya nchi wanachama kwa kadiri kwamba Ujerumani na Ufaransa zilipiga marufuku kusafirishwa nje vifaa vya tiba, kama vile maski na mitambo ya kusaidia kupumua, na hii ni katika hali ambayo Italia tayari ilikuwa imeomba msaada wa kufikishiwa vifaa hivyo.

MIKAKATI YAENDELEA
Pamoja na kuwepo wasiwasi na mivutano ya hapa na pale, Rais wa Tume ya EU, Ursula von der Leyen anaonya kuhusu kufungwa kwa mipaka, hatua iliyochukuliwa na nchi kadhaa za umoja huo kupambana na janga la corona huko Brussels, Machi 13, 2020.

Tume ya EU pia wka sasa inapanga kupiga marufuku safari zisizo za lazima katika eneo la Schengen, ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya kupambana na maambukizi ya corona ambayo yameonekana kuongezeka katika bara hilo.

Rais wa Tume hiyo, der Leyen anasema kuwa atawaomba viongozi wa nchi za EU kutekeleza hatua hii ambayo anasema itasaidia sana kupunguza maambukizi ya virusi hivyo.

Masharti haya yatatekelezwa kwa muda wa siku 30 zijazo na pamoja na wananchi kutoka mataifa haya, marufuku haya yatawaathiri pia wananchi wa nchi ya Uingereza ambayo ilijiondoa kwenye umoja huo.

Mbali na EU, mataifa mbalilbali yamechukua hatua, yakiongozwa na Ufaransa ambayo kuanzia siku ya Jumanne, ilitoa wito kwa raia wake kuepuka safari zisizo za lazima kwa siku 15 huku mipaka na nchi jirani ikifungwa kwa siku 30.

WHO linasema kwa sasa bara la Ulaya ndio lililoathirika zaidi na maambukizi haya, huku mataifa ya Italia na Hispania yakifunga shughuli zote.

UTENDAJI WA MFUKO WA MSHIKAMANO
Ili kutoa msaada kamili kwa nchi za EU katika kuandaa maombi yao ya kusaidiwa kutoka Mfuko wa Mshikamano wa EU katika kukabiliana na dharura ya coronavirus, Tume imechapisha miongozo maalum.

Kusudi ni kutumia kuelekeza namba ya kluaonisha matumizi mengine kwenye eneo la kuchagua ufadhili chini ya bajeti ya EU kusaidia nchi za EU – pamoja na kubadilika kwa kiwango cha juu, kazi ya ziada ya kiutawala na haraka iwezekanavyo

Kama sehemu ya Mpango wa Uwekezaji wa Majibu ya Coronavirus, wigo wa Mfuko wa Ushirikiano wa EU umepanuliwa ili kujumuisha dharura kubwa za kiafya.

Hasa, itatoa msaada wa kifedha wa hadi Euro milioni 800 kwa nchi zilizoathirika zaidi katika hali hii ya kushangaza, kupunguza mzigo wa hatua za kukabiliana na haraka, pamoja na msaada kwa idadi ya watu, msaada wa matibabu na vifaa, msaada kwa vikundi vilivyo hatarini, na hatua za kuzuia kuenea kwa ugonjwa, kuimarisha maandalizi ya kukabiliana na ugonjwa na mawasiliano.

EU au nchi inayostahiki inastahili kuomba fedha hiyo ikiwa mzigo wake wa kifedha kwa umma kwa hatua hizo unazidi kizingiti cha Euro bilioni 1.5 bilioni (bei ya 2011), au asilimia 0.3 ya GNI yake. Ikihamasishwa, mchango wa Mfuko utakuwa kati ya asilimia 2,5 na asilimia 6 ya matumizi yote, kulingana na ukubwa.

HATUA ZIFUATAZO
Tume itachunguza maombi hayo na ikiwa vizingiti vimekamilishwa na maombi yakubaliwa, itapendekeza kiasi cha misaada kwa Bunge la Ulaya na Baraza ambalo linapaswa kuidhinisha kabla ya kulipwa.

Tume itashughulikia maombi yote kwenye kifurushi kimoja kimoja, sio kwa msingi wa kwanza kutumikia. Hii inahakikisha kuwa matumizi yaliyopangwa yanashirikiwa kwa usawa.

UUNDWAJI WAKE
Mfuko wa Mshikamano wa EU uliundwa ili kusaidia kukabiliana na maafa makubwa ya asili na kuelekeza mshikamano wa Ulaya kwa kanda zilizokumbwa na maafa ndani ya Ulaya.

Mfuko uliundwa kama sehemu ya kukubali wazo lililoibuliwa kwa ajili ya kukabiliana na athari za mafuriko makubwa katika Ulaya ya Kati katika msimu wa joto wa 2002.

Tangu wakati huo, imetoa zaidi ya Euro bilioni 55.5 kwa kuingilia katika matukio 83 ya majanga katika nchi 23 wanachama na nchi moja iliyokuwa mbioni kujiunga. Italia ndio mnufaikaji mkubwa wa Mfuko huu kwa kupata karibu Euro bilioni 2.8 zilipokelewa.
 
Uandishi wako mzuri ila unaboa sana kusoma kwani kuna maelezo ambayo sio ya muhimu kuwepo ili kuifnya habari isiwe ndefu na inayoeleweka.
 
Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
Ngoja kwanza waonje joto la kujitoa EU.
Waliona wakiwa nje ya EU ndio watakuwa na nguvu zaidi za kiuchumi na ushawishi huko Ulaya na duniani kwa ujumla,huenda wako sahihi.
 
Back
Top Bottom