Kagoda Agriculture Ltd: Another BOT scandal

Kagoda Agriculture Ltd: Another BOT scandal

Wakaguzi kuimaliza Kagoda mahakamani

Mwandishi Wetu Aprili 22, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

  • Ni wale waliosema ni wizi mtupu
  • DPP asema yote yana mwisho
MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP), Elieza Feleshi, amesema muda si mrefu watajua hatima ya wahusika wa kampuni ya Kagoda Agricultural Limited kuhusiana na wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu (BoT), na kwamba ushahidi wa wakaguzi utakua muhimu kuhusiana na kesi hiyo.

Akizungumza na Raia Mwema katika mahojiano maalumu, jana Jumanne, Feleshi alisema, “hakuna marefu yasiyo na mwisho,” na kwamba suala hilo litapatiwa ufumbuzi utakaozingatia matakwa ya kisheria ikiwa ni pamoja na sheria ya ushahidi.

Feleshi alikwepa kuzungumzia ni lini wahusika watafikishwa mahakamani, akiegemea zaidi kwenye maadili ya taaluma yake, lakini alisisitiza kwamba wapelelezi wanakamilisha kujibu maswali yote muhimu kuhusiana na kesi hiyo.

“Kila kesi inaamuliwa kwa vigezo vyake na viwango vyake vya maelezo na ushahidi unaojitegemea. Tunasubiri wakamilishe upelelezi na sisi tufanye kazi yetu. Mimi ni mwendesha mashitaka. Lazima tujiridhishe kabla ya kufanya maamuzi,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu maelezo ya wazi kutoka kwa wakaguzi na mashahidi yanayoonyesha kuwapo kwa jinai kutokana na nyaraka nyingi kughushiwa, Feleshi alisema ni lazima sheria ya ushahidi itumike ili nyaraka na maelezo ya wakaguzi na ripoti zao ziweze kutumika kama ushahidi mahakamani.

“Ni lazima tufuate taratibu za sheria ya ushahidi. Ripoti za wakaguzi haziwezi kutumika hadi taratibu zifuatwe na hapo ndipo zitaweza kuwasilishwa mahakamani kama ushahidi,” alisema Feleshi, huku akikwepa kuingia undani wa hatua waliyofikia.

Akizungumzia kuhusiana na ushahidi wa kimataifa, Feleshi alisema mambo yote hufanyika kwa kuzingatia sheria na mikataba ya kimataifa inayohusiana na masuala ya ushirikiano katika upelelezi na uendeshaji mashitaka.

“Kila nchi ina mamlaka inayosimamia usajili wa kampuni na hivyo kampuni zilizotajwa kuhusiana na EPA ni lazima zitolewe maelezo kutoka mamlaka husika. Wao ndio waseme kwa maandishi kwamba kampuni X haipo, kampuni Y imefilisika, kampuni Z ni ya fulani,” alisema DPP.

Kumekuwa na hoja kutoka kwa wanasiasa, vyombo vya habari na hata wananchi wa kawaida pamoja na watu waliokwisha kushitakiwa kuhusiana na kutofikishwa mahakamani kwa wahusika wa kampuni ya Kagoda, ambayo pekee inatajwa kuchukua sehemu kubwa ya fedha zilizoibwa katika akaunti ya EPA.

Kampuni ya Kagoda ambayo hadi sasa wamiliki na uhalali wake ni mambo yenye utata mkubwa, inatajwa kutumia nyaraka za kughushi katika kupata kiasi cha Dola za Marekani 30,732,658.82 (takriban Sh bilioni 40) kutoka BoT kwa kutumia mbinu chafu.

Mbinu hizo ni pamoja na kughushi nyaraka mbalimbali na kutumia kivuli cha siasa katika kupitisha nyaraka husika bila kufanyika kwa uhakiki wa kina wa uhalali wa nyaraka hizo, kazi iliyofanyika kwa kasi iliyowashangaza hata wakaguzi wazalendo na wale wa kimataifa waliopitia hesabu za BoT.

Mfano wa dhahiri uliotolewa tokea mwanzo ni ule wa wahusika wa Kagoda kughushi nyaraka za kampuni 12 za kigeni kuweza kujichotea kiasi cha Sh Bilioni 40,ikiwa ni pamoja na nyaraka zilizopitishwa na maofisa wa BoT bila kufanyiwa uhakiki.

Walioanza kuwasha moto wa wizi huo walikuwa ni wakaguzi wa kimataifa wa kampuni ya Deloitte & Touche, ambao walitimuliwa na serikali baada ya kutoelewana katika ukaguzi wa akaunti hiyo ambayo sasa inazidi kuchanganya wengi.

Deloitte & Touche, ambayo ilipewa kazi ya kukagua akaunti za BoT, ilikumbana na utata mkubwa katika akaunti ya EPA namba 99915091 01, na hivyo kuwa kiashirio cha kwanza cha utata mkubwa katika akaunti hiyo.

Maelezo yaliyoibua utata huo yanaonyesha kwamba aliyekuwa Gavana wa BoT, Marehemu Dk Daudi Ballali, alianza kujulishwa mapema kuhusiana na wizi huo akipewa mfano wa dhahiri jinsi Kagoda Agriculture Limited ilivyoghushi nyaraka.

Mfano uliotolewa kudhihirisha uhalifu huo ni jinsi ambavyo mikataba ya ununuzi wa madeni kwa kampuni 12 ilivyosainiwa katika kipindi kifupi cha kati ya Septemba 10, 2005 na Novemba 5, 2005, kipindi ambacho kilielezwa kuwa ni vigumu kwa wahusika kutembelea nchi mbalimbali duniani kutiliana saini.

Aidha, imefahamika kwamba nyaraka zote zilisainiwa na wakili mmoja tu Bhyidinka Michael Sanze, wa Malegesi Law Chambers ya Dar es Salaam, na kati ya hizo mikataba minne ilisainiwa Oktoba 18, 2005 na mitano ilisainiwa siku moja baadaye Oktoba 19, 2005, jambo ambalo lilitia shaka jinsi wawakilishi wa kampuni hizo za kigeni walivyoweza kusafiri kwa wakati mmoja wakitofautiana kwa saa chache, jambo ambalo lilishindwa kuthibitishwa kwa kutumia kumbukumbu za uhamiaji.

Sanze anatajwa kama shahidi muhimu ambaye maelezo yake kwa wachunguzi wa Tanzania yanawataja wanasiasa na watendaji muhimu wa serikali ambao hata hivyo hawatajwi katika kesi zilizokwisha kufikishwa mahakamani.

Katika nyaraka hizo, mikataba miwili iliyosainiwa Oktoba 18, 2005 kuhusiana na kampuni mbili za Ujerumani, Lindeteves J Export BV na Hoechst ikionyesha kwamba kulikuwa na deni la Euro 1,164,402.76 badala ya fedha za Ujerumani (Deutsche Marks.)

Wachunguzi na wakaguzi wameshitushwa na kasi ya ajabu ya jinsi marekebisho makosa hayo yalivyofanyika kwa kipindi kifupi baada ya BoT kuifahamisha Kagoda Agriculture Limited huku barua ya kutaka marekebisho yafanyike ikiwa na maelekezo ya kuidhinisha malipo ya Sh 8,196,673,600.53 kwenda kwenye akaunti ya Kagoda. Kampuni hiyo iliwasilisha mkataba uliorekebishwa siku mbili tu baada ya kujulishwa.

Pamoja na kubainika kuwa mikataba na nyaraka zote hazikuwa na nembo ya kampuni husika, nyaraka zote zilisainiwa katika ukurasa mmoja pekee wa mwisho tofauti na nyaraka za kisheria zinavyopasa kusainiwa katika kurasa zote.

Uchunguzi wa kina umebaini kufanana kwa mihuri ya kampuni zote zilizopitishwa ikiwa inalandana kabisa na muhuri wa kampuni za Kitanzania, tofauti ikiwa ni majina na anuani ya kampuni husika.

Mfano uliotolewa ni wa kampuni za Kitaliano za Fiat Veicoli Industriali na Adriano Gardella S.P.A pamoja na kampuni ya Kimarekani ya Valmet ambazo zote zimeonekana kuwa na mihuri na lugha zilizofanana katika nyaraka zote.

Utata mwingine uliodhihirika kughushi ni katika mkataba wa kampuni ya Valmet ya Marekani uliohusu Dola za Marekani 2,398,439.96 kusainiwa na Patrick Kevin, aliyetajwa kuwa Mhasibu wa kampuni hiyo, jambo ambalo limeelezwa kwamba ingekuwa vigumu kwa mhasibu kuachiwa kufanya kazi hiyo.

Utata mwingine uliobainika ni katika mkataba wa kampuni ya Daimler Benz AG ambao ulionyesha kusainiwa na Mkurugenzi aliyetajwa kwa jina la Christopher Williams, huku sahihi yake ikisomeka ‘W Christopher’.

Uchunguzi wa ziada ulithibitisha kwamba baadhi ya kampuni zilikwishakufa wakati mikataba hiyo ikisainiwa na kampuni za Kitanzania, jambo ambalo linaendelea kuthibitisha wizi mkubwa wa kutumia maandishi uliofanywa katika akaunti ya EPA.

Mifano hai ni kampuni za Hoechst AG iliyobadilika na kuwa Aventis mwaka 1999, Daimler Benz AG iliyobadilika na kuwa Daimler Chrysler AG mwaka 1998 na Fiat Veicoli Industriali iliyobadilishwa na kuwa Industrial Vehicle Corporation (IVECO) tokea Januar1 1, 1975.

Kampuni nyingine zilizobadilika ni Mirrlees Blackstone kuwa MAN B&W Diesel Limited mwaka 2002/03 na Valmet iliyobadilishwa na kuwa Metso Paper kuanzia Mei 10, 2000. Utata huo uliwafanya wachunguzi na wakaguzi kujiuliza ilikuwaje kampuni zote hizo kuingia mikataba mwaka 2005 kwa kutumia majina ya zamani.

Pamoja na kuingiwa kwa mikataba hiyo na kampuni zilizokwisha badilishwa majina na umiliki wake, kampuni za sasa zenye uhusiano na kampuni zilizoingia mkataba zimekanusha kufahamu watu waliotajwa kuziwakilisha katika mikataba hiyo.

Kagoda ambayo imekithiri katika uhalifu wa kughushi ilisajiliwa Septemba 29, 2005, na kujichotea Sh bilioni 40 katika kipindi cha mwezi mmoja tu, jambo ambalo limewashangaza wengi kuona kampuni ngeni isiyofahamika inawezaje kuaminiwa kiasi kikubwa cha fedha bila kuhakikiwa.

Inafahamika kwamba kati ya shilingi bilioni 90 zilizoibwa katika akaunti ya EPA, sehemu kubwa ilichukuliwa na kampuni ya Kagoda Agricultural Limited ambayo hadi sasa wahusika wake hawajaguswa pamoja na kujitokeza kwa vigogo wawili kurejesha fedha zilizoibwa na kampuni hiyo.

Vyanzo vya uhakika vinaeleza kwamba sehemu kubwa ya Shilingi bilioni 90 zilizothibitika kuchukuliwa kihalifu zilichukuliwa na makundi mawili tu, kundi la kwanza likiwa chini ya Jeetu Patel na lingine likiwa chini ya usimamizi wa vigogo wawili waliotumia kampuni ya Kagoda. Jeetu Patel amekwisha kufikishwa mahakamani.

Imefahamika kwamba kwa sasa kuna hekaheka kubwa za kutaka kuzuia kushitakiwa kwa wahusika wa Kagoda, lakini vyanzo vya ndani ya serikali vimeeleza kwamba kwa sasa serikali haitabiriki na lolote linaweza kutokea wakati wowote, na kauli ya Feleshi inaashiria kuendelea kwa kazi ya kuwashughulikia.

Kumekuwa na utata kuhusiana na ilipo na umiliki wa Kagoda Agricultural Limited na hakuna anayeweza kubainisha hasa zilipo ofisi na wahusika wa kampuni hiyo tata.

Kumbukumbu za Wakala wa Usajili Kampuni na Uandikishaji Leseni (BRELA) zinaonyesha kwamba ofisi za Kagoda zipo Kipawa Industrial Area Plot namba 87, Temeke, Dar es Salaam lakini eneo hilo lina makampuni tofauti jirani lakini namba iliyotajwa haionekani na badala yake eneo lenye ofisi na kampuni viwanja vyenye namba kuanzia 76, 77, 86 na 88 katika eneo hilo la viwanda.

Katika ukaguzi wake wa awali wa mkaguzi wa nje Samuel Sithole kutoka kampuni ya Kimataifa ya Deloitte & Touche yenye makao yake Afrika Kusini alionya kuhusu matendo ya kihalifu ndani ya Kagoda kabla ya kuandikiwa barua na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji kwamba fedha hizo zilienda katika mambo "nyeti" ya kiusalama.

Hata hivyo siku nne baada ya kuandika barua hiyo, Meghji alifuta barua hiyo akielezea kupotoshwa na aliyekua Gavana, Dk. Daudi Ballali, uamuzi ambao ulimgharimu kwa kiasi kikubwa mwanamama huyo makini ambaye alijikuta akiachwa nje ya Baraza la Mawaziri, pamoja na kuwa miongoni mwa mawaziri wachache waadilifu.

Wakati Rais Jakaya Kikwete akisema serikali yake haitomuingilia DPP, watuhumiwa wengi waliokamatwa na kufikishwa mahakamani walikuwa wamejiaminisha kuwa wamekwishapona na sasa waliobaki "hawalali" kuhofia kushitukizwa na kupandishwa kizimbani.
 
Feleshi atakuja kutubu hadharani....maana anatunga uongomtupu...anazungusha maneno hayo hayo tu....
 
hizi ni jitihada za uchaguzi ujao, ili wakiulizwa hili jambo waseme uchunguzi unaendelea, tuna pitia report etc etc
 
Wakaguzi kuimaliza Kagoda mahakamani

Mwandishi Wetu Aprili 22, 2009

Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Ni wale waliosema ni wizi mtupu

DPP asema yote yana mwisho

Hata hivyo siku nne baada ya kuandika barua hiyo, Meghji alifuta barua hiyo akielezea kupotoshwa na aliyekua Gavana, Dk. Daudi Ballali, uamuzi ambao ulimgharimu kwa kiasi kikubwa mwanamama huyo makini ambaye alijikuta akiachwa nje ya Baraza la Mawaziri, pamoja na kuwa miongoni mwa mawaziri wachache waadilifu.


Hayo mambo ya kufagiliana naona Raia Mwema wanataka kuleta yale mambo yao ya kwenye gazeti lililowashinda la RAI maana wameanza kumtengeneza mama Meighji eti alikuwa Waziri mwadilifu. Waandishi tunawaomba tafadhali 2010 tubuni dhambi zenu za kutuuzia mbuzi kwenye mfuko wa gunia ili muisaide nchi yenu. Kuweni wazelendo japo kwa hilo. Msiwajenge au kuwabomoa tu watu. Mama Meighji amekuwa bogust finance minister kwa kipindi kifupi nyie mnasema mwadilifu!!!
 
Hayo mambo ya kufagiliana naona Raia Mwema wanataka kuleta yale mambo yao ya kwenye gazeti lililowashinda la RAI maana wameanza kumtengeneza mama Meighji eti alikuwa Waziri mwadilifu. Waandishi tunawaomba tafadhali 2010 tubuni dhambi zenu za kutuuzia mbuzi kwenye mfuko wa gunia ili muisaide nchi yenu. Kuweni wazelendo japo kwa hilo. Msiwajenge au kuwabomoa tu watu. Mama Meighji amekuwa bogust finance minister kwa kipindi kifupi nyie mnasema mwadilifu!!!

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, hata kama mama kuna sehemu aliboronga ila ukweli wa kwamba alifuta barua yake baada ya kugundua Balali kamuingiza mkenge ni commendable
 
Tuangalia na huku, tutapata majibu ya maswali mengi kuhusiana na mafisadi na ufisadi
 
Na Mhariri
MwanaHALISI

WATANZANIA wakiulizwa wanachokitaka kuhusu ufisadi wa kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, tunaamini watasema kwa sauti kali, “kamata hao, shitaki hao sasa.”

Jibu hili litawaudhi wengi katika uongozi wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa sababu bado hawaoni kukamata wenye Kagoda na kuwashitaki kuwa ni jambo la maslahi kwao.

Lakini hata ukiuliza wananchi kwa kiasi gani hawapendi ahadi za serikali kuhusu kushughulikia Kagoda, jibu litakuja kwa kiwango hichohicho. Watasema, “Ahadi zimetutosha tunataka hatua.”

Hata hapo viongozi wa serikali hawatafurahi. Watakasirika na kukasirikia wananchi. Wanataka nini kumbe? Funika kombe mwanaharamu apite. Wanaficha wanachokijua.

Hili ndilo tatizo kubwa la serikali ya CCM na linaiangamiza kadri 2010 inavyokaribia. Pale penye ukweli na wao viongozi wakiufahamu ukweli wenyewe, hawana moyo wa kuachia ili wananchi nao waufahamu.

Kibano kinachoisibu Kagoda na wenyewe ni kikubwa kiasi cha mtu kushangaa ingekuwa serikali yetu ni makini – ile ambayo wakuu wake wana dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi – tungekwishajua moja la maana.


Serikali imeshindwa kubana wenye Kagoda na sababu ni moja tu: Kagoda imepumbaza uongozi hadi kuwa wapowapo tu. Au, kama mkondo unavyoelekeza, Kagoda ni ya baadhi ya walioko madarakani.

Serikali inaimba vita dhidi ya ufisadi lakini inacheza ngoma ya kuenzi ufisadi. Vinginevyo ingekuwa imekamata wahusika. Inawajua.


Lakini kama viongozi hawataki kukamata wenye Kagoda kwa kuwa wanaamini hawajatenda kosa lolote, si wanyamaze basi? Kwanini wanatoa ahadi?


Watanzania wamechoka kusikia viongozi wa serikali na taasisi zake wakizungumzia uchunguzi wa Kagoda na ahadi za kutoa taarifa. Hizo ni ndoto milele.

Wanajua serikali yao imeshawaangusha katika hili. Wanajua viongozi wanapotamba kupambana na ufisadi, hawako hasa makini na ufisadi wenyewe.

Hawagusi kamwe mapapa wanaonenepeana kwa miradi mikubwa na mipango ya kuchota mabilioni ya shilingi. Hawa na wao ni chanda na pete. Wamejenga ubia zamani na umesaidia kufanikisha mambo yao kwa pamoja.


Kipi kipya anachoahidi Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) au Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), na mwingine yeyote serikalini ambacho hakijapatikana kuhusu Kagoda?

Uchunguzi gani usioisha? Wananchi wamechoka kusubiri, hasa pale ambako hakuna sababu za kusubiri.


Tu watu makini. Tunafikiri na kupima. Tunajua anayesema ukweli na anayedanganya. Bali tumefika tamati. Lisemwe lililopo ili tuanze ukurasa mpya.
 
Na Mwandishi wetu
30th June 2009


Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano, Mhe. Samwel Sitta amesema hoja za kampuni ya Kagoda na nyingine zinazotuhumiwa kwa ufisadi ni rukhsa kuendelea kujadiliwa na wabunge na kwamba hakuna katazo la kuzizungumzia tuhuma za kampuni hizo.

Amesema mbali na kampuni ya Meremeta ambayo inahusiana na shughuli za Jeshi, si kweli kwamba amekataza mjadala kuhusu Kagoda na makampuni mengine yenye tuhuma mbalimbali za ufisadi.

Akitoa ufafanuzi juu ya suala hilo bungeni jana, Spika Sitta akasema walikaa na Serikali kwenye kikao mahususi na kuelezwa kwa undani kama kamati ya uongozi, juu ya namna Kampuni ya Meremeta inavyohusiana na jeshi na usalama wa taifa.

Akasema hoja za Tangold, Kagoda na Deep Green ziko wazi na hivyo, hajazuia kujdiliwa kwake ndani na nje ya bunge, hali inayoashiria kuwa sasa kibano kitaendelea kuwa palepale kwa makampuni hayo hadi ukweli wa tuhuma zote uanikwe.

"Nilichozuia ni kile kinachohusu Meremeta ambayo ndiyo kampuni inayohusiana na jeshi. Tafsiri inajitokeza kwamba nimekataa mambo yote ya sekta ya madini... wanataja sijui Deep Green, sijui Tangold na mengine. Hoja hizo bado ziko wazi," akasema Mhe. Sitta.

Spika alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya baadhi ya vyombo vya habari kumnukuu vibaya wakati Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Slaa alipowasilisha tuhuma za ufisadi katika Kampuni ya Meremeta na kisha spika kumzuia asiijadili.

Aidha, baada ya Spika kunukuliwa kuwa amefunga mjadala wa makampuni hayo, baadhi ya Wabunge na Mashirika yasiyo ya Kiserikali yalikuja juu na kutaka makampuni hayo yanayotuhumiwa kwa ubadhilifu wa Shilingi Bilioni 155 yafanyiwe uchunguzi.

Miongoni mwa wabunge walioguswa na hatua ya Spika kutangaza kufunga mjadala huo ni Mbunge wa Simanjiro, Mhe. Christopher Ole Sendeka.

Akichangia hotuba ya Waziri Mkuu wiki iliyopita, Mhe. Ole Sendeka alisema watanyamaza kujadili ufisadi iwapo tu uchunguzi utafanyika na kuwachukulia hatua watuhumiwa wote wa ubadhirifu kwenye kampuni kama za Deep Green Finance na Tangold.


CHANZO: ALASIRI
 
Sept 11, 2009
ThisDay

INVESTIGATIONS into the notorious Kagoda Agriculture Limited company, which was behind the single largest looting of funds from the Bank of Tanzania’s external payment arrears (EPA) account, have now switched to the continents of Europe and Asia, THISDAY can reveal today.

According to our latest findings, the presidential probe team into the EPA scandal led by Attorney General Johnson Mwanyika has now decided to send investigators to Germany and Singapore to gather ”crucial evidence” about the company.

A team of investigators from various government agencies, including the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB), the police and the intelligence and security services, has been working on the long-running EPA embezzlement probe.

And well-placed sources now say after a thorough investigation of Kagoda within the country, it has been decided to send government representatives to Germany (Frankfurt in particular) and Singapore, to look into apparent connections between the company and some firms based in those locations.

Frankfurt is the financial and transportation heart of Germany, and also known as the largest financial centre in continental Europe. It is the seat of the European Central Bank, the German Federal Bank, the Frankfurt Stock Exchange, and the Frankfurt Trade Fair, along with a number of large commercial banks.

The Kagoda company was used to siphon over 40bn/- out of a total 133bn/- embezzled from the BoT’s EPA account during 2005/06, via fraudulent payments personally approved by former central bank governor Daudi Ballali (now deceased).

Both BoT auditors and government investigators have established that Kagoda company representatives presented forged documents to the central bank to facilitate payment of around $30,732,658.82 (approx. 40bn/-).

All the forged Kagoda documents were signed between September 10 and November 5, 2005. The company is shown to have signed deeds of assignment of debts with 12 different foreign creditors from across the globe.

While in Germany, government investigators are expected to try and locate the headquarters of two of those companies, Lindeteves J Export BV and Hoechst AG. The forged documents purported to show that the Kagoda company had been assigned debts owed to the two German firms.

Hoechst AG is understood to have been a German chemicals then life-sciences company, renamed Aventis after merging with Rh'ne-Poulenc S.A. of France in 1999, and now known as Sanofi-Aventis since 2004.

Our sources say the government investigators are currently trying to ascertain whether Kagoda was assigned the substantial debt by Hoechst AG before or after the 1999 merger with Rh'ne-Poulenc.

At the same time, there appears to be some confusion over the location of the head offices of Lindeteves J Export BV - whether it is either Germany or Singapore.

As already well-established, there were glaring errors evident in all of Kagoda’s documents, including the use of obsolete names of creditor companies, incompatible dates, and poorly-forged signatures.

The deeds of assignment seen by THISDAY revealed that the forger(s) of the documents used the same contractual terms and wording for all the different foreign creditor companies.

This is considered unrealistic since different companies are likely to insist on different contractual clauses.

None of the contracts and documents were written on the official letter heads of the foreign companies, with key contact details for representatives of the firms missing.

In one of the forged documents that supposedly formalized the assignment of a debt of $2,398,439.96 to Valmet USA, the forger used a fictitious name - Patrick Kevin - to sign the document purportedly as the company’s accountant.

It is against standard practice for an accountant to sign such a large contract on behalf of a company.

Another forged document involving a different German company, Daimler Benz AG, shows that the agreement was purportedly signed by a fictitious director named Christopher Williams, but the signature appeared as W Christopher.

All the Kagoda documents were signed in Dar es Salaam before the same B.M. Sanze, an advocate and notary public and commissioner of oaths.

Some documents were dated even before the Kagoda company was officially registered at the Business Registration and Licensing Authority (BRELA), thus rendering them null and void.

Samuel Sithole, lead audit and engagement director of Deloitte & Touche of South Africa which is the international auditing firm that first discovered the massive Kagoda fraud, raised serious questions regarding the use of old names for companies and the speed with which the Kagoda transactions were approved by BoT.

But following these queries by Sithole, the then BoT governor Ballali sacked Deloitte & Touche as the central bank’s official auditor.

So far, no charges whatsoever have been filed against individuals behind the Kagoda company, as pressure continues to mount on both the EPA scandal probe team led AG Mwanyika and the Director of Public Prosecutions, Eliezer Feleshi, for decisive action to be taken.
 
Wakuu, huku kuna mengi ya kujikumbusha. Kagoda haitakufa ng'o!!!!
 
Kwa nini serikali ndio itafute hayo makampuni ya nje badala ya hao kagoda kupelekwa mahakamani na watakiwe kuleta hayo makampuni ya nje kuthibitisha kuwa ni kweli yamewauzia kagoda madeni yao kihalali???? Simple.
 
Kwa nini serikali ndio itafute hayo makampuni ya nje badala ya hao kagoda kupelekwa mahakamani na watakiwe kuleta hayo makampuni ya nje kuthibitisha kuwa ni kweli yamewauzia kagoda madeni yao kihalali???? Simple.

Ukiacha hayo mengine kuhusu suala la serikali kutafuta makampuni ni kwamba Huwezi tu kumpeleka mtu mahakamani kwa style hiyo kuna kitu kinaitwa ONUS OF PROOF ....
 
Serikali haiwezi kumbana Kagoda na Meremeta ambao ndio waliowapa ulaji. Hamkumbuki maelezo ya utafiti wa kina wa mwanakijiji kwamba Mkapa aliitaka pesa hiyo kusaidia kampeni za CCM ili mdogo wake ashinde kwa kishindo? Ndio maana ushahidi wa mahakamani unasema kwamba Mkapa alipoulizwa na Yona alisema "endelea nimekubali, fanyeni haraka"

Ukitamka Kagoda unatamka CCM na unatamka Raisi wa nchi. Serikali gani inaweza kuubana mfumo wake wenye tija kwao? meremeta si mliambiwa ni ya jeshi na isichunguzwe? The story remains the same. Huwezi kujidhibiti kula kwa kujikata shingo na kutkizika kichwa chako.

Leka
 
KAGODA KAGODA KAGODA Embu naotoke authibitishie umma kwamba anasingiziwa na ule msemo wao wa kijinga eti wanaonewa wivu,ingekuwa jasho lao poa,lakini kutuibia afu kututukana haikubaliki hata kwa shetani!! lets wake up Bongoz
 
Sasa hawa jamaa wanakwenda Ulaya kumtafuta Kagoda kivipi? Huko ulaya wanakula Perdiemz bureeeeeeeee!. Sasa wanataka kutuambia InterPOL wameshindwa!. Watu wametengeneza deal la kwenda ulaya tu! Hakuna lolote!!!!!.

Jina lenyewe la Kagoda nila asili ya Tanzania. Kagoda ni "Kigoda" inayomaanisha aina ya kiti kidogo cha asili chenye umbo la duara na miguu mitatu. Anayeweza kupata picha yake atuwekee hapa. Sasa, hawa jamaa waliona kama watatumia jina la Kigoda, Mh mmoja nayeitwa kwa jina hilo angelihusishwa moja kwa moja na kashifa. Kwa hiyo, kwa lugha ya Kihasibu, tunasema wali-hedge jina, ili kupunguza risks pindi issue ikifumka!!. Sasa, mtu anakwenda kutafuta Kagoda EU wakati hata jina lenyewe linaashiria uasilia wa pale TZ ambapo pesa imechotwa! Kagoda ni rahisi kufichwa, kwa vile kanabeba umbo dogo ingawa ndiko bibi na mama zetu kule kijijini wanakatumia kutuandalia misosi!. Kwa hiyo, kamefichwa nchini TZ. Ulaya ni geresha tu. Wanarefusha muda wa kufanya maamuzi kwa visingizio vya kutokamilika kwa upelelezi!.

YETU MACHO NA MASIKIO!!!.

__________________________________________
" Ubongo wako unazeeka unapoacha kusoma"- Sisimizi
 
wataiba kila kitu ila usikubali wakaiba moyo wako,siku isiyo na jina iko njiani yaja.

Hii nimeipenda Malila, tafadhali tuongezee kidogo "wala kuigawa au kubadili mwelekeo wa akili yako!"
Ni lazima Taifa letu likombolewe!"
 
Swali hili kamuulize Rostam Aziz aka King Maker, si yeye ndiye alitajwa na Dr Slaa kwenye orodha ya mafisadi kuwa ndiye anayemiliki Kagoda? Ningeweza kukutana nae, ambacho ningekifanya kingekuwa zaidi ya kumsuta. Na sasa anataka hitman wake Noni ndio awe gavana. Nitamshangaa Kikwete kama akiendelea kujilegeza.

Anayejua jinsi ambavyo naweza kumsogelea Rostam kwa karibu awanishauri kidogo kwenye ashabdala@yahoo.com, halafu hayo mengine nitajua mwenyewe cha kufanya.

Dawa ya mafisadi ni kuwapata kwenye ule ufisadi mwingine t


Asha

Kagoda aulizwe Apson Mwango'nda ndiye Kagoda Rostam ni mshirili tu ndo maana watu wanaiogopa kuizungumzia.
Tafuta advocate Sanze na Benjamin Mwangonda waliokuwa mashahidi wakati wa kuandikishwa kwa Kagoda. Wtz mufunguke macho.
 
Back
Top Bottom