BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,283
Manji kanywa sumu?
na Mwandishi wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
HALI ya afya ya mfanyabiashara maarufu nchini anayemiliki Kampuni ya Quality Group ni mbaya kiasi kwamba imewalazimu madaktari waliokuwa wakimtibu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam, kulazimika kumkimbiza Nairobi nchini Kenya kwa matibabu.
Habari za uhakika ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka vyanzo vya kuaminika, kwa watu walio karibu na mfanyabiashara huyo na katika Hospitali ya Aga Khan, zinaeleza kwamba, Manji alianza kuugua juzi usiku.
Kwa mujibu wa habari hizo, hali ya Manji ambaye ni mfadhili mkuu wa klabu ya soka ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, ilianza kwa kutapika mfululizo, jambo ambalo lilisababisha wanafamilia na jamaa zake walazimike kumkimbiza katika Hospitali ya Aga Khan wakihofia kwamba huenda alikuwa amekula chakula au kinywaji chenye sumu.
Mtoa habari mmoja aliyezungumza na gazeti hili alisema kwamba, mara baada ya kufikishwa katika hospitali hiyo, usiku wa kuamkia juzi alipelekwa moja kwa moja katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) akiwa katika hali iliyoonyesha kutojitambua.
Jamaa waliompeleka hospitalini hapo waliwaeleza madaktari walioanza kumhudumia kuwa, Manji alianza kutapika mfululizo baada ya kunywa kiasi kikubwa cha kinywaji anachokipenda.
Kwa mujibu wa habari hizo, madaktari waliompima, waligundua kuwa wakati akitapika, kiasi cha mapishi yake kilirudi tumboni na kingine kikaingia mapafuni, hali ambayo ilianza kutishia maisha yake.
Vyanzo vingine vya habari kutoka hospitalini hapo, vililieleza gazeti hili kuwa, madaktari walishangazwa na matapishi ya Manji na kwamba waliamua kuchukua kiasi kwa ajili ya uchunguzi zaidi kabla hawajafikia uamuzi wa kumpeleka Hospitali ya Aga Khan ya Nairobi, nchini Kenya.
Hali hiyo ilisababisha aondolewe hospitalini hapo majira ya saa 12:00 asubuhi jana na kusafirishwa kwa ndege ya kukodi kwenda Nairobi akisindikizwa na ndugu zake wachache.
Vyanzo hivyo vilieleza kuwa akiwa anaanza kupata fahamu, ndugu zake walimwambia wanamhamishia Nairobi kwa matibabu zaidi, Manji alikataa akitaka kuendelea kubaki hospitalini hapo au kurudishwa nyumbani kwake, ndipo madaktari walipotumia akili ya ziada ya kumchoma sindano ya usingizi ili iwe rahisi kufanikisha zoezi la kumhamishia nchini Kenya.
Kabla ya gazeti hili kupata habari hizo jana asubuhi, uvumi ulisambaa sehemu mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam ukihusisha ugonjwa huo wa Manji na matukio ya siku za hivi karibuni ya kufikishwa mahakamani kwa baadhi ya vigogo wakihusishwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Hali ya sasa ni tete bwana, sisi tunasikia jamaa ameingia hofu kiasi cha kuamua kunywa sumu, alisema mtoa habari mmoja aliyepiga simu katika chumba cha habari cha Tanzania Daima.
Hata hivyo taarifa hizi zilikanushwa vikali na mmoja wa wanasheria wanaofanya kazi na Manji ambaye aliuelezea ugonjwa wake kuwa ni wa kawaida na uliotokana na hitilafu za kitabibu mwilini.
Msaidizi huyo wa Manji ambaye alikiri kusikia maneno mengi kuhusu kuugua kwa bosi wake, alikanusha katakata kuwapo kwa jambo lolote linalomhusisha mfanyabiashara huyo na matukio ya hivi karibuni ya vita dhidi ya ufisadi.
Hii ni mara ya pili katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja kwa Manji kuugua na kulazwa katika Hospitali ya Aga Khan na baadaye kupelekwa Nairobi kwa matibabu zaidi.
Uvumi wamhusisha na hofu ya mahakamani