Kagoda Agriculture Ltd: Another BOT scandal

Kagoda Agriculture Ltd: Another BOT scandal

jamani tuelewane hapa, sisi wote ni watu wazima. ccm hawawezi kutaja waliorudisha na walioiba maana ni wao waliiba na ni wao wanarudisha, hii ni serikali ya wezi watupu. Nilitoa hoja hapa nadhani itanibidi niingie nijifunze kuanzisha thread nione kama nitaungwa mkono. tunahitaji mikakati mizito sana kuung'oa huu utawala ulioko sasa, ni kweli unafifia kwa kuwa milango mingi inaziba lakini bado wamo msiwaone kwa juujuu. hawatakubali wafe tu hivi, wanajipanga kuhakikisha ugali wao haupotei hivihivi. wazo langu kubwa hadi sasa kwa akili zangu mtindi, tufanye bidii kubwa kuziba sources zao za hela. Ufirauni hauendi bila hela, kama hakuna hela watakuwa pagumu sana.
 
Duh!! lakini mpaka sasa zimerudi 50Billion je hizo ni kutoka kwa Kagoda + Interest au??? na kama ni kutoka kwa watuhumiwa wengine Kagoda karudisha ngapi!!

It's about time hawa watu wawekwe hadharani bila kuficha majina na washitakiwe ili wapelekwe wanakostahili...let the suffering END. Tumechoka sana...[/QUOTE]

Njake Hotels & Tours Ltd karudisha Tzs. 800 Million through kale kabenki ka wahindi chenye makao makuu pale opposite na Kitega Uchumi.

Kwa kuwa wamegoma kusema si tutasema, ila ushahidi hatutoi, watoe wao kuwa hajalipa hizo Million 800. Naendelea kufuatilia wengine waliorudisha hela zetu.


Tabia hii ya kuficha majina ya watuhumiwa ni dalili kuwa bado tuwaogopa. Huo ndio ugonjwa mkubwa sana tulio nao katika jamii yetu, yaani kuwaogopa mafisadi.
 
Njake Hotels & Tours Ltd karudisha Tzs. 800 Million through kale kabenki ka wahindi chenye makao makuu pale opposite na Kitega Uchumi.

Kwa kuwa wamegoma kusema si tutasema, ila ushahidi hatutoi, watoe wao kuwa hajalipa hizo Million 800. Naendelea kufuatilia wengine waliorudisha hela zetu.
Reply With Quote

Mbangaizaji, hebu rudi uanike hapa JF waandishi waanze kuanika katika magazeti tena. MWaga kidogo kidogo. Naona kuna waliowekwa maalumu kuangalia hii thread, hilo lisikupe wasiwasi we mwaga data wachanganyikiwe
 
CCM wabaya, lakini at the moment it seems to be the only party ambacho kina nguvu zakutosha kumuwezesha mtu asaidie jimbo lake, if they really wanted to. Siwatetei, niwabaya, tena sana... lakini kweli wapinzani, it will take time.[/QUOTE]

ukishasema ni wabaya ujue ubaya wao ndio unaotuumiza miaka nenda rudi. kama kina uwezo wa kuwemzesha mtu kusaidia jimbo lake mbona hatuoni maendeleo yoyote miaka nenda rudi au wanasaidia matumbo yao?? mi naamini wapinzani wanaweza tuwape nafasi. hakuna aliyezaliwa anaweza.
 
Watanzania ndivyo tulivyo- ameeni, EL akigombea uraisi tutampa - Ameeni, Chenge sio mwizi kwa kuwa hajavunja nyumba ya mtu - Ameeni, Tumwacha mzee wetu mkapa apumzike - Ameeni, wezi wa EPA actually sio wezi ila walijikopesha kwa makosa lakini wanarudisha na sasa imefikia 70% - ameeni, CCM ikiwapa pilau, gongo na sh. 2000 wapigieni kura - Ameeni ..............
 
Dear all please check also date/day of respective withdrawals? Was it not enough to raise alarm at all? All stakeholders critical and systematic analysis urgently needed!
 
Thread very elucidating and helpful.We need more of this for the Parliament to take up its role.Information and informed Parliamentarians is what makes the Parliament powerful. All with pertinent information dont hesitate to post, and critical Parliamentarians will play their role. Thanks alot for the thread and contributions. More is needed to win the battle.
 
wanajamii Forum tunasubiri kusikia kesho raisi wa jamhuri atatudanganya nini tena, au ndio atatabasamu na kusema hakuna tatizo kama kawaida yake!
 
Thread very elucidating and helpful.We need more of this for the Parliament to take up its role.Information and informed Parliamentarians is what makes the Parliament powerful. All with pertinent information dont hesitate to post, and critical Parliamentarians will play their role. Thanks alot for the thread and contributions. More is needed to win the battle.
Great Dr.W.Slaa,

We look forward for you guys (MPs) to strive more & more for the better Tanzania.

Thanks for the spirit and please stay with us!
 
hii kagoda inatuchanganya akili. gazeti la mwanahalisi la wiki hii limesema ni ya rostam aziz wakati mwanzo waliandika ni ya manji. which is which? naomba mwongoza plz
 
hii kagoda inatuchanganya akili. gazeti la mwanahalisi la wiki hii limesema ni ya rostam aziz wakati mwanzo waliandika ni ya manji. which is which? naomba mwongoza plz

Hapo ndio utajua Kubenea na genge la MwanaHalisi ni wababaishaji of he highest order!
 
Hapo ndio utajua Kubenea na genge la MwanaHalisi ni wababaishaji of he highest order!

kuna kitu kimejificha hapa. kama wanababaisha kwa nini wasishtakiwe? dont take it lightly the way you have put it mkuu Masatu
 
Gazeti letu mahili la mwanahalisi limedokeza hivi:

YUSUF MANJI ndiye mmiliki wa Kagoda agriculture ltd iliyochotewa tsh 30.8 b za EPA. Hii inanikumbusha kauli aliyowahi kutoa Mzee Mengi kwamba "Manji kiburi anakitoa wapi" leo nimepata jibu.Kiburi anakitoa kwa viongozi wa ngazi za juu ikulu/serikali ambao wanamkumbatia kwa kuwa kala nao hela ya EPA.
Nimetoa machozi kupata taarifa za kilichojadiliwa dodoma na CCM nec.
Namalizia kwa ku-quote alichosema mjumbe wa mkutano huo aliyesema:

"mkutano ulikuwa hauna ajenda, ulikuwa sawa mkutano wa hadhara, inasikitisha kwamba wabunge machachari wa ccm badala ya kupongezwa, wanadharauliwa na kutishwa,hakuna lolote la maana pale zaidi ya kikwete kumsafisha lowasa na wenzake"..
Kama unataka kutoa machozi kama mimi soma magazeti ya leo ya mwanahalisi na raia mwema.
Naweka kituo kwa kutamka
"uongozi wa juu wa ccm na serikali wamepoteza mwelekeo".Natamani niende rwanda nimlete kagame aongoze tanzania.
Wana JF,
Kwa kumbukumbu zote nilizonazo, Yusuf Manji ametumika tu kama camouflage. Mmiliki wa Kagoda,halisi ni lazima tuendelee kumsaka.
i) Aliyesajili Kagoda ni John Kyomuhendo, na ndiye aliyeweka saini yake kwenye nyaraka zote za Brela.
ii) Saini katika Barua iliyotoa fedha zote BOT ni ya Kyomuhendo, na ndiye pia aliyefungua akaunti CRDB. Ingelikuwa mwujiza kwa Yusuf Manji kumruhusu Kyomuhendo kuchukua hizo fedha zote, bila yeye mwenyewe kuonekana popote, mbona kwenye Akaunti zake nyingine zote yeye mwenyewe ndiye anayeshughulikia?
iii) Benki za Barclays na Kenya Commercial Bank walikataa kufungua akaunti za Kagoda kwa vile walitia mashaka na huyu mteja mpya ambaye ghafla anaweka mabilioni kwa mara moja. Ingelikuwa na Yusuf Manji kusingelikuwa na mshangao wa aina hii.
iv) Kumbukumbu zetu zinaonyesha aliyefuatilia fedha hizi BOT na negotiations zote zilikuwa zikifanywa na Rostam Aziz, wakati huo Mweka Hazina wa CCM. Memo zote zilizopelekwa kwa Balali zilikuwa zinapelekwa kwa Rostam Aziz. Manji hatajwi popote katika vimemo hivyo.

Nadhani, fumbo hili siku si nyingi litafumbuka. Nawapa hints
a) Serikali haina uchaguzi lazima iwaambie watanzania Kyomuhendo ni nani, na ushahidi wote unaonyesha alikuwa mfanyikazi wa Caspian ambayo ni ya Rostam Aziz. Ni kwanini huyu Bwana ametoweka tangu suala la Kagoda kulipuka?
b) Serikali kupitia Brella na BOT lazima watuambie Kyomuhendo ni nani, na kwanini ametoweka na kwanini Serikali haikuchukua hatua ya kumtafuta tangu alipotoweka, angalau kuweka Tangazo la kutoweka kwake? Mbona kwa matukio mengine hadi picha zinatawanywa katika jitihada za kumtafuta mhalifu? Inafichwa nini?
c) Rostam Aziz lazima aache sasa mchezo wa Mbuni awaambie Watanzania Kyoumuhendo ni nani, kwanini katoweka, na kwanini yeye binafsi alikuwa akienda BOT kufanya negotiation na Hazina ya kupata fedha hizo?
d) Malegesi, aliyetengeneza nyaraka za kugushi za makampuni ya nje ili Kagoda iweze kulipwa kwa niaba ya Makampuni hayo lazima awaambie watanzania Kyomuhendo ni nani. Haiwezekani Mwanasheria maarufu kama Malegesi na wenzake watengeneze nyaraka muhimu kiasi hicho bila kufahamu wanayemtengenezea nyaraka hizo.
e) Mwenye siri zote za EPA, hususan Kagoda ni aliyekuwa Gavana Balali. Serikali lazima ituambie Watanzania kwanini walikataa kata kata kumhoji Gavana Balali, hata kama alikuwa hospitalini. Mbona watuhumiwa wanahojiwa hata hospitalini kwa Balali nini kilikuwa kinakwepwa. Haya maswali yasipopata majibu Serikali daima ijue kuwa tutaiona kuwa imekuwa ikiwakingia kifua vigogo waliohusika kwa sababu zinazojulikana.
d)CRDB nayo inatakiwa sasa itoke hadharani kulinda image yake ya kwanini haikuweza kustuka mathalan 25 Billion zinachukuliwa siku moja kupitia matawi yake sita na kampuni ambayo haijulikani vizuri?
 
Hivi hawa wahindi mbona katika kila ufisadi wapo,hawafikishwi mahakamani wanalindwa na viongozi wa chama na serekali kwa kutumia kodi zetu.Hii maana yake nini !.
Ukugusa EPA,Radar,Richmond ni wahindi wametamalaki.
 
Haya Mambo ndiyo yalivyo, na CCM kwa sasa ni chama cha Mafisadi pasipo shaka yoyote na kamwe hakitaweza kuwasaidia watanzania. Kwa bahati mbaya Tanzania kwa sasa ni Yatima maana inaonekana hata serikali mbadala hatuiioni, na nafikiri kuna haja ya kuanzishwa kwa chama cha Siasa makini maana hawa jamaa waliopo katika kambi ya Upinzani kwa umoja wao, nao hoi bin Taaban, sawa kwa mmoja moja wapo lakini wakija kama chama nao buree wanakaribiana na binamu zao CCM.
Mgoyangi,
Kwa muda mrefu tumenyamaza kila swala la udhaifu wa vyama unapotajwa. Nadhani ni vema at some stage analysts wakatusaidia kujua sababu za msingi kwanini vyama viko dhaifu. Ziko nyingi kwa mtazamo wangu:-
a) Vyama dodoki, vilivyoanzishwa kwa lengo la ku destabilize vyama makini. Mifano sasa tunayo mingi. Hutapata muungano au hata ushirikiano wa vyama katika mazingira ya divide and rule iwapo ni dhahiri kuna vyama vimeanzishwa kwa kazi hiyo tu.
ii) Kuna vyama vinatumika na vyombo vya dola hasa usalama wa taifa, kulinda maslahi ya ccm, officially or unfofficially. Inawezekana kabisa kinacholindwa ni maslahi ya watu binafsi ndani ya usalama, na au ni official na hivyo dola yenyewe inavitumia. Siku hizi kumezuka wana usalama wanaoitwa "Kanjanja" kama mmumewasikia. Hawa ndio wanaotumika sana na CCM, kama ilivyofanyika kwenye uchaguzi mdogo wa Kiteto.
iii) Kuna vyama viongozi wakishakatiwa mshiko ndio kazi yao imemalizika.
Katika mazingira haya, wakati umefika sasa Watanzania waelewe kuwa inawezekana kabisa swala la kudai mwungano wa vyama ni swala linalopandikizwa ili ukombozi ushindikane. Katika mazingira hayo, vyama serious au vitashindwa kuungana au hata kufanya siasa kama chama mmoja mmoja. Hata ulichokiita Chama makini kingelianzishwa leo, kama dynamics ya vyama vya siasa katika nchi iliyojaa ufisadi/umafia isipofanyiwa utafiti wa kina na kidhibiti mbinu hizo chafu yote yataishia katika ndoto na au matumaini yasiyotekelezeka.
Nina amini wote wenye mapenzi mema, na watanzania watakapoendelea kuelewa dynamics za siasa na uhusiano wa siasa na maisha yao ya kila siku, siasa vs umaskini/ujinga na maradhi wakapiga kelele za kutaka haki yao. Siku hiyo CCM haitakuwa na lake tena. Siku hizo haziko mbali Wazee wa EAC wanalala kwenye viwanja vya ikulu, wastaafu wa Idara mbalimbali Serikali nao wameanza kulala kwenye viwanja vya ikulu, waalimu ambao siku zote wamekuwa docile wamefika Dar kwa malori na wameanza kudai haki zao, wafanyi kazi kwenye viwanda na sekta mbalimbali wanadai haki zao. Kila moja akifika mahali anapiga kelele mabadiliko yatatokea. Kumbukeni Suharto "alipinduliwa" na wanafunzi kwa kuandamana tu mitaani kwa wiki moja hivi.
 
Hivi hawa wahindi mbona katika kila ufisadi wapo,hawafikishwi mahakamani wanalindwa na viongozi wa chama na serekali kwa kutumia kodi zetu.Hii maana yake nini !.
Ukugusa EPA,Radar,Richmond ni wahindi wametamalaki.

wahindi wanipeleka hii nchi pabaya:somaiya, jeetu patel, manji, rostam, ande chande, chavda.....nk
 
Manji ni swahiba wa karibu sana na RA huenda hilo ni lao moja.
 
Back
Top Bottom