Kagoda Agriculture Ltd: Another BOT scandal

Kama haya ni kweli basi hata OJ Simpson hakuua mke wake (Not guilt) na pia Lowasa, Karamagi na wezi wote wa EPA ni watu safi sana.
Ni wanasiasa 'uchwara' waliowachafulia majina 'waheshimiwa' hao. Wivu tu, na uvivu wa kufikiri. Mbona tunaendelea nao katika serikali? Hii 'Danganyika' inaongozwa na watu makini kama hawa, 'makanjanja' acheni wivu!
 
JK anasubiri Yesu aje amuhakikishie kuwa RA ni fisadi.

Makaburi yao ndio ushindi wetu.Mapinduzi ya kimawazo na mapigano ya haki ndio suluhisho. Ni lazima yatokee makaburi ya mafisadi na makaburi ya mashujaa. La sivyo tutachonga sana usanii ni hautakwisha
 
Adhabu ya kunyongwa isifutwe, iachwe kwa ajili ya kuwanyonga hawa wanaoliibia taifa kama huyu Rostam, Manji na Chenge....!

Haiwezikani mtu aue mtu mmoja halafu ahukumiwe kifo, halafu hawa wanaoua maelfu ya wananchi kwa kuwaibia kodi zao waachiwe huru...!

Hivi hawa watu tutaendelea kuwakumbatia hadi lini?
 
Nikitazama yote yanayofahamika hadi sasa kuhusu huyu RA na genge lake, napata mshangao mkubwa kuwa bado anadunda mtaani, hayuko rumande. JK alipohutubia bunge last time alituambia maneno ya kisanii kuwa ati tusione watu waliojulikana kuwa ni matajiri, ati sasa wanayo maisha magumu sana kwa kuwa wamenyang'anywa mali zao na blah blah blah! Sasa hizo ndizo hatua za kuwachukulia wanaotenda makosa ya jinai (wizi, kuhujumu uchumi)? Nikijumlisha yote napata maana ya ile katuni iliyomwonesha JK akiwa kabebwa kiganjani na mdudu rushwa, kwamba hana uwezo na wala hathubutu kuliangusha dude linalombeba hadi sasa! Kama ninamwonea JK kwa kufikia conclusion hii, let him prove me (or us) wrong kwa kuyashughulikia haya mafisadi, lakini kwa sasa among the plausible explanations for his (spoken and unspoken) actions ni kwamba he is one of them fisadis, unless he bails himself out.
 
Nadhani sasa ni wakati mwafaka kwa mawakili wa Profesa Costa Mahalu, kuwasilisha mahakamani ombi la kutaka mteja wao afutiwe kesi ili apewe muda wa kulipa hizo dola milioni mbili kwa awamu kama wenzake wa EPA.

Hakuna sababu ya kuendelea na hiyo kesi, eti kwa sababu tu Mahalu alikuwa akimdharau JK alipokuwa Waziri wake wa Mambo ya Nje, enzi hizo za Mr. Clean
 
Jamani nadhani kuna mambo ambayo sina hakika ni kwanini Watanzania hatushituki. Tuko kama tumechomwa sindano ya ganzi.

Rostam alitangaza na kuapa kwamba hahusiki kwa vyovyote na suala la EPA na Kagoda haina uhusiano wowote na kampuni zake. Leo hii inakuja kampuni ya Afritainer Limited ambayo inaendeshwa na watu wake huku ikiwa inatumia mawasiliano yale yale yaliyotumiwa na Kagoda. Wafanyakazi hao hata leo ukiwaona wanamtumikia RA kwa kila kitu. Kampuni hiyo ilianzishwa na familia ya RA tokea mwaka 1986.
 
JK anasubiri Yesu aje amuhakikishie kuwa RA ni fisadi.

,,,,,JK anajua FISADI ni CCM,,, na sio RA,ikumbukwe kwamba wakati hilo deal la EPA linafanyika RA ndo alikuwa MWEKA HAZINA wa CCM,na alikuwa na jukumu la kuhakikisha anakuwa na FUNDS za kutosha ili ushindi uwe wa KISHINDO,ss mchoro wenyewe kusudi ufanikiwe lazima ilikuwa kampuni hewa zianzishwe,,,,,Zikaanzishwa vizuri,,,tatizo limekuja hizo kampuni lazima ziwe na address etc,,ndo mzee RA akajitolea,matokeo yake kila mtu anamfikiria jamaa ni FISADI,lkn ukweli ni kwamba ule mchongo ni wa CCM,,ndo maana mambo ni kimyaaaaa!!!,,sema wale waliotumia loophole hio nao kujichotea ndo watasulubiwa hao,,,,ngoja tuone.
 
Naona hapo hauko sahihi. Hii hapa ni EPA ya mwaka 2000, mwaka ambao RA hakuwa mweka Hazina wa CCM. Lakini pia hakuna taasisi iwe CCM ama chombo kinachoweza kufanya uhalifu kama taasisi bali ni watu ndani ya chama ama taasisi kama RA, Jeetu Patel na wengine ndio wanaofanya uhalifu.

Lakini jambo la msingi hapa ni kwamba je, uhalifu huu umefanyika kwa miaka mingi na si 2005/2006 kipindi ambacho kilifanyiwa ukaguzi. Kwa hiyo Mwanahalisi wametuzindua na sasa tuulizane EPA nyingine wahusika ni kina nani? Ndio maana nadhani tunaweza kurudi tena katika ile doc ya Invisible

https://www.jamiiforums.com/jf-exclusive/18386-bank-m-connecting-dots.html

Ambayo naona hakuna anayeijadili kwa undani zaidi ya kujadili kichwa cha habari kisemacho "Bank M: connecting the dots".
 
Kampuni inayotajwa hapa inaitwa Afritainer Limited ambayo wakurugenzi waliosaini Deed ni watumishi wa Caspian Limited inayomilikiwa na RA. Watumishi hao, ni Tabu Omari na Barati Godda. Tabu ni Katibu Muhtasi wa RA ambaye amekuwa akifanya kazi nyingi za siri za bosi wake ikiwa ni pamoja na kugawa fedha kwa waandishi wa habari na wanasiasa. Waandishi wengi wa habari na wanasiasa wanasema wanamfahamu sana huyo mama, akifanyia kazi zake Nyerere Road na Upanga.

Kwa mujibu wa Mwanahalisi fedha hizo kiasi cha Sh Bilioni 13, zilichukuliwa Agosti 2000, kabla ya uchaguzi wa pili wa vyama vingi, ambao Benjamin Mkapa, aligombea tena. Wakati huo RA alikuwa tayari amekwisha kumuingia Ben kupitia kwa Ruhinda.

Katika gazeti hilo jambo la kushitusha ni kwamba Dk. Ringo Tenga wa kampuni ya uwakili ya Law Associates ndiye aliyebariki nyaraka za Afritainer. Tenga ndiye aliyekabidhiwa kazi ya uanasheria wa Benki Kuu badala ya Mkono. Lakini ifahamike pia kwamba Tenga yuko karibu na wanamtandao na hivyo kila eneo wanaweka watu wao bila kujali uadilifu.

Jambo lingine ni kwamba Dk. Idris RAshid alikwenda Akiba Bank baada ya kutoka BoT na fedha za Afritainer zilipitia Akiba Bank. Lakini jambo la muhimu zaidi ni kwamba namba za simu na fax zilizotumiwa na kampuni ya Afritainer 2861372 zimetumika pia na Kagoda Agrocultural ambayo Mwanahalisi waliwahi kuandika kwamba Kagoda ni ya RA na yeye akakanusha na kufungua mashitaka. RA kwa sasa yuko busy na uzinduzi wa kampuni yaka ya New Habari, na hivyo habari hizi zimemrudisha nyuma baada ya "kujisafisha" kwa staili ya aina yake pale Kilimanjari Kempisk, hoteli iliyokuwa na heshima wakati wa uhai wa Baba wa Taifa, Mwalimu J.K. Nyerere, lakini sasa ni sehemu muhimu ya kufanyia mikakati ya kifisadi.
 
Last edited:

Nimeongea na Kubenea ameniambia anao ushahidi mzito zaidi na alichoandika ni kama uchokonozi tu, mambo zaidi yanakuja ikiwa ni pamoja na nyaraka zaidi zinazoanika kila kitu. Anasubiri tu mtu akohoe
 
kuna mtu aliandika kuwa ccm na mafisadi, kama akina rostam ni kama mbwa na chatu. si kikwete au yeyote anaweza kupumua mbele ya hawa mafisadi
 
I am trying to remain calm.

This' what will kill your beloved country, don't just sit there... Do something!

Hebu nisome tena?
icon11.gif

.
 
kuna mtu aliandika kuwa ccm na mafisadi, kama akina rostam ni kama mbwa na chatu. si kikwete au yeyote anaweza kupumua mbele ya hawa mafisadi

Uko sahihi ndio maana hata hapa JF watu wamechoka, hawaoni hata sababu ya kuchangia kama ushahidi wa wazi upo na hakuna hatua
 
Mkuu siamini kwamba wote tumechoka, lakini kwa kweli hali si nzuri maana huyu jamaa inaonekana ana "uhusiano" na watu wengi na anao kina "Mtikila" wake wengi na tushingae hata humu JF kina "mtikila" wanaogopa kuambiwa walipewa Sh milioni 3.
 
kampuni inayotajwa hapa inaitwa afritainer limited ambayo wakurugenzi waliosaini deed ni watumishi wa caspian limited inayomilikiwa na ra. Watumishi hao, ni tabu omari na barati godda. Tabu ni katibu muhtasi wa ra ambaye amekuwa akifanya kazi nyingi za siri za bosi wake ikiwa ni pamoja na kugawa fedha kwa waandishi wa habari na wanasiasa. Waandishi wengi wa habari na wanasiasa wanasema wanamfahamu sana huyo mama, akifanyia kazi zake nyerere road na upanga.

Kwa mujibu wa mwanahalisi fedha hizo kiasi cha sh bilioni 13, zilichukuliwa agosti 2000, kabla ya uchaguzi wa pili wa vyama vingi, ambao benjamin mkapa, aligombea tena. Wakati huo ra alikuwa tayari amekwisha kumuingia ben kupitia kwa ruhinda.

Katika gazeti hilo jambo la kushitusha ni kwamba dk. Ringo tenga wa kampuni ya uwakili ya law associates ndiye aliyebariki nyaraka za afritainer. Tenga ndiye aliyekabidhiwa kazi ya uanasheria wa benki kuu badala ya mkono. Lakini ifahamike pia kwamba tenga yuko karibu na wanamtandao na hivyo kila eneo wanaweka watu wao bila kujali uadilifu.

Jambo lingine ni kwamba dk. Idris rashid alikwenda akiba bank baada ya kutoka bot na fedha za afritainer zilipitia akiba bank. Lakini jambo la muhimu zaidi ni kwamba namba za simu na fax zilizotumiwa na kampuni ya afritainer 2861372 zimetumika pia na kagoda agrocultural ambayo mwanahalisi waliwahi kuandika kwamba kagoda ni ya ra na yeye akakanusha na kufungua mashitaka. Ra kwa sasa yuko busy na uzinduzi wa kampuni yaka ya new habari, na hivyo habari hizi zimemrudisha nyuma baada ya "kujisafisha" kwa staili ya aina yake pale kilimanjari kempisk, hoteli iliyokuwa na heshima wakati wa uhai wa baba wa taifa, mwalimu j.k. Nyerere, lakini sasa ni sehemu muhimu ya kufanyia mikakati ya kifisadi.

mambo haya yana uzito mkubwa na wahusika wameanza kuhaha
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 2 (2 members and 0 guests)
Halisi, vstdar
 
Back
Top Bottom