KUTOKA MAHAKAMA YA WILAYA YA MULEBA, MKOANI KAGERA
Leo tarehe 3/10/2023 katika Mahakama ya Wilaya Muleba mbele ya Mh Lilian Mwambeleko, imeamriwa kesi ya Jinai namba 91/2023 Jamhuri dhidi ya Adilelius Vedasto Apolinary mwenyekiti wa kikundi cha ujasiliamali cha Umoja wa Vijana Youth Fund cha Muleba pia ni Katibu wa Mbunge, ambapo alishitakiwa kwa kosa la kutoa taarifa za uwongo kwa Mkurugenzi kuhusu matumizi ya fedha za uwezeshaji vijana Milioni sitini, zilizotolewa na Halmashauri ya Muleba mwaka 2022. Kinyume na kif cha 122 cha Kanuni za Adhabu Sura ya 16 Marejeo ya 2022, Kesi iliongozwa na Wakili Kelvin Murusuri.
Katika Kutoa ushahidi upande wa Jamhuri ulisema ya Kuwa Mnamo Mwezi Oktoba 2022 na January 2023 Mtuhumiwa aligushi Nyaraka na Saini za wanakikundi Cha Vijana wilayani hapo Na kudanganya Benki na Ofisi ya DED kuwa fedha anaitoa kwa Matumizi ya Mradi wa Kikundi hicho wa kufyatua tofali. Katika Hali isiyo ya Kawaida Mtuhumiwa Alichukua fedha husika na kuziingiza kwenye matumizi mengine huku Kiasi Cha Milioni 16 zikiingia kwenye akaunti ya Mke wake na nyingine Milioni 11 zikiingia kwenye akaunti Binafsi.
Pia mwendesha Mashtaka aliieleza mahakama kuwa Mtuhumiwa alijipatia Kiasi Cha Milioni 60 na mradi wa kifyatua tofali ambao ulilengwa kwa ajili ya fedha hizo haujafanyika Hadi sasa. Na mali zote alizodai kanunua hakuna hata Moja inayoonekana.
Aidha alipoulizwa na Mahakama juu ya Makosa hayo Mtuhumiwa alijitetea kuwa Madai hayo si kweli na anaiomba Mahakama imhurumie kwani Ana mke na ana watoto wadogo na anategemewa na Familia yake.
Mtuhumiwa ametiwa Hatiani na kuamriwa alipe faini ya Tsh. Laki tano 500,000/- au jela miezi sita
Pia kufuatia maombi ya Wakili Murusuri mtuhumiwa ameamriwa arejeshe fedha zote Milioni Sitini ndani ya miezi mitatu na tayari amelipa Milioni Tisa katika akaunti ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Muleba, na amelipa faini na kuachiwa.