Ruvuma: Katibu wa kikundi cha Walemavu Liparamba kilichopo Nyasa ahukumiwa kwa Ubadhilifu wa Fedha za Walemavu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,280
Katika Mahakama ya Wilaya Nyasa imeamriwa kesi ya Rushwa namba 6013/2024 ya Jamhuri dhidi ya Bw. Rainely Mathias Ngonyani ambaye ni katibu wa kikundi cha Walemavu Liparamba kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.

Mshitakiwa alishtakiwa kwa kosa la ubadhilifu kinyume na Kifungu cha 28 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 mapitio ya 2022 ikisomwa pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi Sura ya 200 mapitio ya 2022 kwa kujipatia manufaa tsh. 2,000, 000/= (milioni mbili) fedha za kikundi cha Walemavu Liparamba walizopewa kutoka Akaunti ya Halmashauri ya Wilaya Nyasa kwa ajili ya kina mama, watoto na walemavu na hivyo kufanya upotevu wa kiasi hicho ambacho ni mali ya Halmashauri ya Nyasa.

Kesi iliongozwa na Wakili Mwandamizi Mwinyi Yahaya ambapo mshtakiwa ametiwa hatiani kwa kukiri kosa lake na kuthibitisha kuwa amesharejesha fedha 2,000,000/- kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyasa.

Aliomba kupata adhabu nafuu kwa kuwa ni kosa lake la awali na ni mlemavu.

Mahakama imemhukumu mshtakiwa adhabu ya *kulipa faini ya shilingi 100,000/- au kifungo cha miaka miwili jela.

Mshtakiwa amelipa faini.
 
Sheria ni msumeno.

Lakini wangeanza na wale waliotajwa kwenye Ripoti ya CAG
 
Hizo pesa milioni 2 naye ameenda kuhonga na kula pisi mpya.
Ninyi mnataka yeye abaki na genye tu??
Acheni hizo..))
 
KUNA WATU WANAPIGA NILIONI NYINGI HAWAKAMATWI, NCHI HAIKO FAIR

KATAA RUSHWA
 
Mnakomalia vihela vidogovidogo tu

Ova
Atakuwa na yeye mlemavu. Zamani Nilidhani walemavu siyo wapigaji. Lakini kuna mmoja hapa ni kipofu alipata upofu ukubwani sasa social inamtunza ila tumecheza mchezo na yeye mimi niwe personal assistant wake ameniajiri kwa iyo ninalipwa mshahara kama usd 2000 lakini jamaa kwenye iyo 2000 inabidi nimpe 600. Sasa mwaka huu mwanzoni ameongeza tena 200 eti nimpe 800.

Jamaa licha ya upofu tunapiga naye kitu cha Arusha balaa.
 
Back
Top Bottom