jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,375
- 25,453
Teh teh teh!mkuu mbavu zangu!Inanikumbushia Uganda ilikuwa mtu akiacha briefcase yake mahali unattented wananchi wanatimkia mbali kabisa na mahali ilipo briefcase hiyo...Maana wameshadeal na mabomu ya briefcase.Acheni umbumbumbu watanzania wenzangu mnaosema eti tutaipiga rwanda kisa ni ndogo kijokrafia, ni nani aliwafundisha kuwa uimara wa jeshi ama wa taifa unapimwa kwa misingi ya ukubwa wa ardhi??? Pumbafu nyie hamjui historia mnaandika tuu....kama nchi kuwa kubwa ndiyo inakuwa na jeshi nzuri mbona tulitawaliwa na ujerumani ambao tunawapita mara tatu kiukubwa??? Pumbafu nyie... Israel ilifanya mashambulizi kule misri na syria kati mwaka 1964 na 67 kwa wakati mmoja na kuzima ubabe wa hizo nchi ilhali ndiyo nchi ndogo kuliko zote hizo. Hamjui historia nyie mawazo yenu yanaendeshwa na hisia ambazo chanzo chake ni kushindwa kufikiri na kuchambua mambo kwa kina. Tuhoji kwanza uzoefu wetu wakupigana tulinganishe na ule wa wanyaruanda, tukisikia mlio wa risasi si tunakimbiaga uvunguni mwa kitanda wote baba,mama na watoto?------- sana
Kwa bongo ukiacha briefcase somewhere watu wanalamba kumbe ndo wanalipuliwa.Ni kweli hatujazoea vita.Kwa wenzetu waliozoea vita, ukisikia mlipuko,unakimbilia mbali.Ila nakumbuka wakati wa ule mlipuko wa ubalozi wa marekani,nilikuwepo jijini Dar,watu walikuwa wakikimbilia eneo hilo,kwahiyo kama kungekuwa na a second explosion,basi maafa yangekuwa makubwa zaidi.Sasa mkuu umenichekesha sana uliposema baba,mama,na watoto wote uvunguni mwa kitanda!