Kagame tells Kikwete "I will hit you......"

Kagame tells Kikwete "I will hit you......"

Status
Not open for further replies.
Ni majigambo tu ya kitutsi hana lolote. Kiongozi gani ana majigambo roho mbaya na majibu ya kifedhuli kwa kupewa ushauri kupata amani nchini kwake. Eti atatu-hit kwa kua tumemwambia aongee na wahutu ili kukomesha udikteta wake. Nyau kweli haka kajamaa. eti kanajidai ni kaliberation fighter kama samora kwa kuweka serikali ya kikaburu rwanda.
 
huyu kagame hana adabu amuulize baba yake mlezi museven bila sisi angekua rais leo? shenzi huyu atapata anachokitaka
 
Wengi mnaochangia humu mnadhani vita ni kama taarabu!mwenye maneno mengi ndiye mshindi!Hamfikirii tulipo hapa hatuna vita lakini watu wengi ufukara unawatesa,je ni vipi nchi ikiingia vitani?Hamjajiuliza jinsi matabaka ya walio nacho na wasionacho yanavyokuza chuki miongoni mwetu na kuwajengea baadhi ya watu roho za kikatili hadi kufikia kuua binadamu wenzao mf albino kwa kisingizio cha kutafuta utajiri?hawa watawezaje kuwa na uzalendo na wapigane kwa ajili ya nani anayefaidi keki ya nchi hii?Je mnadhani watanzania waliobaki na matumaini mioyoni mwao ni wangapi kama sio hao mnaoishi Dar tu na wachache sana walioko mikoani?Hivi mkisikia watu wanajiua kwa sababu ya ugumu wa maisha mnadhani ni vichaa wachache tu wanaopungua idadi,na hivyo waliobaki wanamaisha mazuri yenye matumaini?Adui namba moja ni shetani lakini anayefuatia ni umaskini!Hayo mambo ya kudharauliwa sijui kutukanwa ni sehemu ya maisha yetu maskini tumeyazoea!ila kitu kimoja tu ambacho hakizoeleki ni umaskini!Mnataka hata kidogo tulichonacho mtunyang'anye mkapiganie vita?Watanzania tupigane na umaskini,ujinga,maradhi na ufisadi!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Tusifikirie kabisa vita, hivi unafikiri hawa wanaopigwa kwenye mikutano kila siku na Policcm na wale waliopigwa risasi watasupport majeshi yetu kweli, let's not even think about getting into war for now.

Na it could be that they know they will get support from within. Serikali ya Kikwete haijatengeneza mshikamano wa kitaifa.
You are right! Mazingira ya sasa si kama yale ya Nyerere kabisa. Wakati ule mtu alikuwa anajivunia kuitwa mtanzania na alikuwa yupo tayari kufa kwa ajili ya nchi yake. Hivi leo hii yule aliyefiwa na ndugu zake kutokana kupigwa risasi na polisi unafikiri ataweza wapi kuitetea Tanzania? Atatamani majeshi ya kigeni yashinde ili utawala dhalimu uondolewe. Yaani tukiingia vitani sasa hivi tutapigwa kama alivyopigwa Iddi Amin. nawashangaa sana wanaosupport vita kwenye nchi iliyosambaratika kama hii.
 
huyu kagame hana adabu amuulize baba yake mlezi museven bila sisi angekua rais leo? shenzi huyu atapata anachokitaka
Those were Nyerere's days. Sidhani kama bado tuna influence sana kwenye international politics, japo naamini kwamba tanzania inazichanga karata zake vizuri sana. Naamini kitengo cha usalama wa taifa kinachoshughulika na mambo ya nje kipo makini sana katika masuala ya diplomasia. Ila kwamba tutamfanya nini, hicho sidhani kama hizo nguvu bado tunazo. Sisi wenyewe Rais wetu ni weak, tutaweza wapi kuwachagulia wengine Rais?
 
Siku zote ukiona mtu mzima anaongea upumbavu mbele ya media au watu dhidi ya kiongozi mwenzake ujue ana matatizo.

Rwanda ni kama sisimizi kwetu, kama anazungumzia vita Tanzania inaweza kuichukua rwanda na kuifanya wilaya kama biharamulo tu.

This idiot must be stopped now.

Kagame ni muuaji na --------, huwezi kukataa kumaliza matatizo na adui yako hata uwe nani labda tu uamini kuwa unaweza kuwaua wote ubaki peke yako. Leo tunaona marekani yenye uwezo wa kuwamaliza kabisa Taleban imekubali kukaa chini na kuongea nao sembuse Rwanda na interahamwe ambao ni wahutu na Rwanda ni nchi yao?

I guess that applies to Lumumba LLC too...aaannha!!
 
Kagame is very right, kama jamaa ni MNYONGE, HIT HIM UP...

Mbona huku mitaani ipo sana wale jamaa wan
yonge wanamegewa wake zao kila siku. Wala sishangai mimi Kagame kutaka kum_Hit Kikwete, its human nature kumdharau mnyonge. Sisi tumejidhalaulisha mno kwa kutembeza bakuli dunia nzima kuomba misaada hadi majirani wanaona tu wanyonge na dhaifu. Hata Simba mgonjwa na dhaifu huvutwa sharubu tu na kukaa kimya.
Pokea 'like' manually.
 
Unajua kagame anajua mwisho wake upo mwisho na sasa mataifa hayata muunga mkono kugombea tena ashakua kero kwa mataifa makubwa
Obama alisema hapa peace itapatikana DRC so anaogopa
JK wa kuogopwa sana inapokuja masuala ya kimataifa watu na wakubwa wanamsikiliza
Kagame anajua hilo sasa hofu imemjaa
JK amesema mara moja tu kule Uganda but Kagame sasa inamchukua miezi kujitetea na kutisha


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hili liwe fundisho JK usiwe unaandikiwa kila kitu, wewe huwa unasema akili ya kwaambiwa changanya na yako. we kila unachoambiwa na kuandikiwa unakubali tu, Hongera sana Kagame.
Kwani kagame katoa fundisho gani zaidi ya kusema ujinga na kujionyesha udikteta wake. Jk kamweleza tu aongee na wapinzani wa kihutu wanaotoka kabila la wahutu ambao ni asilimia 85 ya raia wa rwanda imekua nongwa.
 
Hana noma na Tanzanai ana noma na baba Mwanaisha! I support Kagama akiingia kwa line, hit him
Ni mtoto -------- tu anaye weza kuvumilia Baba yake akitukanwa na kudhalilishwa!! he is now crossing the line, na hatupashwi kukavumilia hako ka Ngongoti!! Mimi nilidhani ka jamaa kana akili kubwa kumbe kanafikiria vita na kuua tu! Ni kosa gani kubwa Mkuu wa Kaya yetu alifanya mpaka astahili haya matusi na vitisho??!!? Hivi kuwashauri mahasimu wakae meza ya majadiliano ni sawa na kuwalazimisha wapatane?? si wanaweza kukaa na wakaamua kutokukubaliana chochote? au si wanaweza hata kukataa ushauri waliopewa badala ya kuanzisha ligi nyingine na wasio husika na matatizo yao?? jamani tusikubali Rais wetu ashikwe masharubu na kila mtu!
 
I love my country and I respect my president. However, it is stupid to try to tell someone how to negotiate a deal with a person who killed his family on the telephone from the comfort of your bedroom. For starters, you dont know how deep is the pain and you have no idea of the implications. In a way, my president would have reacted the same way (I strongly believe so) had Kagame told him to chase Pinda away and refute the '..wapigeni tu..' statement made in the parliament recently. Or else had Kagame commented on Mapinduzi ya Zanzibar, vurugu za mtwara etc. Under the same light I understand Kagame position and emotional state whenever this subject is brought up - much less by a president who have never sweated a day to make a tough and manly decision on anything. Just as Nyerere retorted strongly against Idd Amin back in the days (which gave hope and united the whole of Tanzania behind him) so is Kagame this time. Kagame has to be strong and spat fire just as he has done, because thats what a leader should do whenever a very core value of the nation is tampered with by anyone, be him small or big. Bravo Kagame, I see a leader in you. And that should teach everybody a lesson, dont go about shooting your mouth about other people's affairs so that you can earn some cheap international popularity, to you it may be a not-so-important-affair but to others is the foundation of their existence.
 
Watanzania mnaifanya issue ya Kagame kama vile mechi ya simba na yanga ambayo ikiisha kila mtu anachukua time yake. Aliyefungwa na aliyefunga. Hi issue ni serious, wengine wanasema wana jeshi zuri ukiwauliza hawana data, wengine wanasema nchi yetu kubwa hiyo nayo haina mashiko, kubwa so what? wengine wanasema wanatz wana uzalendo hawana data, na wengine wanasema tutamnyongelea mbali hawajui hata uwezo wa jeshi letu. Wapo wenye data za mwaka 47 ambazo matokeo yake tulishayaona mbagala na gongo la mboto. Na simple research kwenye mikutano ambapo polisi wakituliza ghasia wanaua, huo umakini wetu uko wapi??? mpaka tujisifu????? Hivyo hili swala sio mpira wa yanga na samba la sivyo itatu cost sana.

Ni kweli Mechi kati ya Nyerere na iddy Amini ilikuwa Rahisi kwani Marehemu Gen Tito Okelo na akina Mseveni na makamanda Wengineo kibao walikutwa porini Wakiwa waasi hivyo walisaidia Jeshi letu mbinu na njia za kupenya hadi kumkimbiza Amini japo mamia ya Asikari waliangamia sana
Ebu jiulize hv sasa tunahitaji vita na Kagame?au tunahitaji vita ya Maradhi ujinga na kero za kijamii kwa ujumla?kumbuka vita ni janga na huporomosha uchumi kwa kasi na Kama Tz tunataka kuludia kula Unga wa Yanga basi tuanzishe vita !tafakari jenga Nchi yako
 
kagame siyo kwamba hataki kuongea na hao wakimbizi walioko congo kwasababu walishiriki kwenye mauaji ya kimbari, kwanza wengi wao walioshiriki miaka ile ni wazee sasa na sio ajabu wengi wameshafariki kumbuka ni karibia miaka 20 sasa, na pia yeye binafsi amewashawishi baadhi yao kurudi nyumbani na wengine amewaingiza jeshini,anachoogopa kikubwa ni majadiano yatakayopelekea uchaguzi huru unaosimamiwa na international community hii ikiwa na pamoja na usimamizi wa jeshi kutoka nje kama walivyofanya burundi, anajua fika hiyo game atashidwa tu, si unajua 85pc vs 15pc, na kama kutatokea vita basi tz mtaji mkubwa ni hiyo 85pc!!!
 
Ni mtoto -------- tu anaye weza kuvumilia Baba yake akitukanwa na kudhalilishwa!! he is now crossing the line, na hatupashwi kukavumilia hako ka Ngongoti!! Mimi nilidhani ka jamaa kana akili kubwa kumbe kanafikiria vita na kuua tu! Ni kosa gani kubwa Mkuu wa Kaya yetu alifanya mpaka astahili haya matusi na vitisho??!!? Hivi kuwashauri mahasimu wakae meza ya majadiliano ni sawa na kuwalazimisha wapatane?? si wanaweza kukaa na wakaamua kutokukubaliana chochote? au si wanaweza hata kukataa ushauri waliopewa badala ya kuanzisha ligi nyingine na wasio husika na matatizo yao?? jamani tusikubali Rais wetu ashikwe masharubu na kila mtu!

..huu ushauri angewapa somalia, sio kagame, kwanini mtu yule yule anasakamwa na majirani? malawi,rwanda, kenya..mbn hamjiulizi hili swali? kuna tatizo, tusitetee matatizo,tutatue hili tatizo kwana kuliko kurukia kumjibu kagame..nani kaleta zogo?
 
kinachomuuma kagame ni kuona vifaa vya kijeshi vinapita nchini kwake kwenda kongo kwa wanajeshi wa tz.
asithubutu cuz tutamtandika vibaya mpaka sasa hv tushamweka kati ni kumpiga from east n west hana ujanja huyo. he cnt hold the pain baada ya kuona majeshi yetu kongo.
 
Ni mtoto -------- tu anaye weza kuvumilia Baba yake akitukanwa na kudhalilishwa!! he is now crossing the line, na hatupashwi kukavumilia hako ka Ngongoti!! Mimi nilidhani ka jamaa kana akili kubwa kumbe kanafikiria vita na kuua tu! Ni kosa gani kubwa Mkuu wa Kaya yetu alifanya mpaka astahili haya matusi na vitisho??!!? Hivi kuwashauri mahasimu wakae meza ya majadiliano ni sawa na kuwalazimisha wapatane?? si wanaweza kukaa na wakaamua kutokukubaliana chochote? au si wanaweza hata kukataa ushauri waliopewa badala ya kuanzisha ligi nyingine na wasio husika na matatizo yao?? jamani tusikubali Rais wetu ashikwe masharubu na kila mtu!
Hawa ndio watu wa media ya bongo with zero brain na hata reasononing hakuna,ukitoa ushauri sio lazima ukubali tena ukiwa wa kipuuzi unapata na zaidi ili siku nyingine uache kelele za kipuuzi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom