Waberoya
Platinum Member
- Aug 3, 2008
- 15,169
- 10,785
Ujamaa umeshakufa, na hakuna mwenye muda wa kufufua mfumo ambao hauna dira wala muelekeo. Kusema CDM ni chama kinachofuata sera za Kibepari nadhani pia ni kukosea. CDM nao hawana sera za kipepari wala za kijamaa. Lakini swala muhimu ni moja, katika karne hii ya 21 hakuna nchi inayoshikilia sera za upande mmoja bila kuchanganya. Ubepari wa Adam Smith umeshakwisha na ujamaa wa Max umeshakwisha. Hivyo chama chenye dira na muelekeo kinapaswa kusoma nyakati na kuchanganya au kuiba kutoka kwenye kila upande wa ideology. Mfano free education kwa watoto wetu mpaka form six hii ni idea ya kijamaa ambayo Tanzania tunaihitaji. Kuondoa serikali kuongoza makapuni ya uzalishaji hii ni sera ya kibepari ambayo tunaihitaji.
Tukija kwenye swala la Kafulila, kwanza angalia political model wake ni nani? Ni dhahiri kwamba Zitto amechangia kwa kiasi kikubwa Mh. Kafulila kufika hapo alipo, sasa ni wazi kabisa Mh. Kafulila anataka kutumia same political style ambazo Mh. Zitto alianza nazo, kitaalamu tunaita Political Gotcha. Mfumo ambao unatafuta popular issues ili uweze kushinda au kupata mass support. Hizi ni siasa ambazo ni dead end.
Ushauri kwa Mh. Kafulila, kwanza soma viongozi wenzio mbali mbali Duniani walifanya nini kufikia malengo yao. Kuwa msikivu kutoka kwenye pande zote mbili. Achana na personal attack politics kwani ni dead end. Mwisho jifunze ni jinsi gani sera zinafanya kazi na sio kuropoka ropoka bila research.
Na kwa wabunge vijana, Watanzania wamewapa dhamana kubwa sana. Vijana hawa ndio watatoa hatima ya Tanzania. Nashauri vijana hawa wasome baadhi ya vijana wenzao wa chache mwaka 1961. Wajifunze njia za uongozi, waelewe kwamba Ubunge sio kazi mchezo, ni dhamana kubwa sana ambayo ni ngumu kuilinda. Watanzania ni masikini wakutupwa, mfumo unaowaongoza hawa masikini unatengenezwa na watu wenye imani kwamba umasikini hautokomezeki.
Kampeni zimekwisha sasa, tunataka execution ya sera zote ambazo tumezisikia. Badala ya kupigizana kelele nani wajamaa nani mapebari nendeni mkabadilishe maisha ya Watanzania.
well said wa kwetu!