Kafulila: Watanzania Wanachagua Mtu, Siyo Sera!

Yaani majimbo 23 tu ambayo ukweli zaidiya nusu yake yamepatikana kutokana na magomvi ya ndani ya CCM na sio kukubalika kwenu kwa dhati tayari arrogance ya power imewazidi kiasi hiki?
Hicho ndicho kitu ambacho hata kukisikia hawataki ndio maana hata JM alipowaambia kwamba jimbo la tarime walilipoteza kutokana na kutokuwa na umoja wa vyama, wao waliendelea kubisha na kudai sababu ni kuibiwa ndipo tofauti ya kura 1000 ikapatikana. wamesahau kuwa kura zaidi ya elfu kumi kama zingepigwa kwa chama chao kingevuka kwa kishindo kiasi gani katika jimbo lile. wengi wao wanaamini katika UMIMI na si katika UMOJA!
Labda katika huo UBINAFSI kuna mafanikio!?
 
kama alivyosema kafulila Ubepari hauziki kwa watanzania walio wengi na ujamaa bado una mvuto wa kuwezesha kupata kura hata kama huaamini katika sera hizo....
Give me a break please...... Hivi ni watanzania wangapi wanajali hizi so called definitions za ujamaa na ubepari......

In this day and age watanzania masikini wengi wanajali yafuatayo

Kuona kwamba viongozi wao hawafilisi nchi yao (viongozi waadilifu, sio wanaojilimbikizia mali) i.e Mafisadi

Kupata huduma za lazima kama elimu; afya (affordably)

Kuondokana na ugumu wa maisha (How... Kuwa na ajira za kutosha... hence kupata kipato, Therefore kuweza kuishi na kupata mkate wa kila siku)

Now Chama Chochote ambacho kitawaconvice the above people will be happy with it no matter kinasema kinafata mlengo gani
 
Hii ya kodi ni sehemu tu ya INCOME yao mkuu wangu.

Wana vyanzo vyao vingine vingi vya hela na Malikia hajalala na kusafiri kama Vasco Dagama wetu.

Mwisho ni kuwa hii ya wanapata wapi hela ni topic nyingine. Ila ukweli ni kuwa wao pamoja na kujisema kuwa Ni Mabepari wakubwa, mwisho wa siku wanatoa hizo huduma bure. Sasa usitake kupindisha hapa habari na kusema sisi tunadanganya. Wewe ndiyo ulitaka kutudanganya hapa na ukafikiri tutanunua. Kama kweli wewe huwa unakaa na viongozi wa Chadema na wengine wanakukimbia basi hao ni Vilaza au umetudanganya. Sidhani kama ukikaa na Slaa na atakukimbia.

Hayo ya bima ya afya ni kweli yapo na kwa nchi tajiri kama EU, ipo sana. Ila hao hao EU wanasaidia sana watu wao. Wakulima wanapewa hela mara mambo yakienda vibaya. Wanapewa hela ili wapunguze uzalishaji, wanapewa hela wakiwa na mashamba ya miti/misitu, wanagawa chakula bure kwa watoto wa masikini, wana nyumba kwa watu wasio na nyumba na wala kazi, nk nk. Sasa sijui Wazee, vilema, watoto, Walevi watakuwa na BIMA gani au Kodi gani wanalipa. na hawa hawafi njaa au kulala nje kwenye hiyo mi Baridi mikali kama la mwaka huu linavyowatesa.

Danganya wengine kabisa mkuu na siyo hapa. Tutakutoa baru ukija na nondo zako hafifu.
Nchi zilizotajwa, kuna kodi chungu nzima zinalipwa na watu wake kwa sababu ya kulipia huduma mbalimbali za kijamii. hakuna cha bure kwenye nchi za kibepari na ndio Tanzania imeanza kuiga taratibu kitu kinaitwa bima ya afya - tuseme ni wanaohudumiwa ni bure kwa bima hiyo ama walishalipia? danganyeni ambao wako nje ya dunia. Nilishasema mtu akiona pumba - apete ili apate mchele, vinginevyo ni kujilisha upepo
 
Hawa wanasiasa kila siku nazidi kujiuliza kama hawajui wanalolisema hence they are stupid au wanajua walitendalo bali wanataka kupotosha jamii.

Kwahiyo kama wananchi wangechagua sera je CCM ingeshinda? Je yeye walimchagua sababu yeye ni yeye au sababu ya sera ya NCCR MAGEUZI?
Mhh!!! Mr Kafulila is better placed to respond ...
 
Mimi nadhani kuwalaumu wanasiasa haswa hawa wa kizazi cha baada ya mfumo wa chama kimoja kuhusiana na suala la itikadi mtakuwa mnawaonea. Tatizo la mkanganyiko wa kitikadi katika vyama vyetu ni kubwa sana na lenye athari kubwa katika utamaduni wa kisiasa hapa nchini. Na hli linatokana na kuwa watanzania wengi hawana ama hawaamini katika umuhimu wa siasa za kiitikadi.

Nijuavyo CHADEMA kama chama na kwa mujibu wa katiba yao kinafuata itikadi za kibepari kama ilivyo kwa upande wa CCM kinapaswa kufuata itikadi za kijamaa. Lakini ama kwa kukosa umakini ama uthubutu wa kisiasa wanasiasa wengi wamekuwa wakikimbilia kupigia debe sera zinazokingana na itikadi rasmi za vyama vyao na kwa kuwa watanzania walio wengi tumekosa nidhamu ya kufuatilia na kupima mambo kwa mapana yake basi huwa tunaishia kuwashabikia wanasiasa wa aina hiyo. Tumefikia hata kutokuwa na uthubutu wa kutohoji mwenendo wa kisera na kiutekelezaji wa nchi yetu ambayo kikatiba inatamkwa kuwa ni nchi inayofuata siasa za ujamaa na kujitegemea wakati mengi yanayoamuliwa na kutekelezwa yanakinzana na itikadi hiyo.

Naamini moja ya suala linaloibua umuhimu wa kuwa na katiba mpya ambayo itapatikana kupitia mchakato wa kuhusisha watanzania wote ni umuhimu wa watanzania kukubaliana kama tunapaswa kufuata itikadi gani na kama kuna ulazima wa suala la itikadi likawa suala la kikatiba ama likabaki kuwa suala la kisera.

Tukija kwa ndugu zangu kina Kafulila, Zitto na Mnyika. Nijuavyo hawa wote wanavutiwa na itikadi ya Ujamaa kuliko Ubepari. Na kwa muda mrefu wamekuwa wakijaribu kukivuta CHADEMA kuelekea upande huo kiitikadi lakini bado hawajaweza kufanikiwa kwani chama bado kiko mikononi mwa waumini wa sera za KIBEPARI.

Kiasili Chadema ni chama cha maslahi ya mabwanyenye ambao wakati wa Mwalimu waliminywa na kushindwa kujitanua kisiasa. Lakini hadi sasa kikatiba Chadema ni chama kinachofuata itikadi ya Ubepari ingawa mara nyingi wamekuwa wakipigia chepuo sera zenye mrengo wa kijamaa. Suala ni kama wanaamini katika sera hizo ama ni kwa kuwa sera hizo zinalipa kisiasa?

Suluhu: Sina jibu hadi sasa ni jinsia gani tutajinasua katika tatizo hili.....

come again man???????? are you seriously,unaelewa kweli Chadema ni nini?You have quote it wrong man naomba mtafute mtu anayejua Chadema akueleze mfumo wa chadema ni nini,stop being bias it is better to be realistic.msitafute dhambi.

hivi JF siku hizi imevamiwa na virusi wa namna gani ambao they can't think and research before presenting issues?
 
Yaani majimbo 23 tu ambayo ukweli zaidiya nusu yake yamepatikana kutokana na magomvi ya ndani ya CCM na sio kukubalika kwenu kwa dhati tayari arrogance ya power imewazidi kiasi hiki?

What do you mean brother.... Magomvi ndani ya CCM ndio yaliyofanya CCM ishindwe.... Who cares what made the outcomes.... What matters is the outcomes.....

What do you think brother kwamba watu wanashares na CCM people are tired and just looking for a better life.... so when someone with a track record promises them change... they will go for it... No matter of the name au itikadi ya that someone
 
Mtu yeyote ambaye anatumiwa na mafisadi au yeye mwenyewe ni fisadi basi mimi simwoni kama ana akili. Huyu dogo anaposema Chadema ni chama cha kibepari ana maana gani kama si kufilisika kimawazo.

Mimi namhurumia huyu dogo maana CCM na mafisadi wanamtumia sana kwa manufaa yao na si yeye anafanya mambo kwa manufaa ya watanzania.

Hana Akili hata kidogo. Ni sawa na watu wengine wa kawaida, hata ubunge wake ameupata kwa usanii wa kupewa hela na mafisadi.
Huo ndio mfumo rasmi wa Chadema, kinyume na hivyo ni kutia viraka kama ilivyo katiba ya Tanzania.
Wanasema funika kombe mwanakharamu apite!
 
Yaani majimbo 23 tu ambayo ukweli zaidiya nusu yake yamepatikana kutokana na magomvi ya ndani ya CCM na sio kukubalika kwenu kwa dhati tayari arrogance ya power imewazidi kiasi hiki?
Hueleweki mkuu kama unaona hiyo si jitihada kwenye mfumo wa ukandamizaji kama wa CCM uliojaa ghiriba,dhuluma,uwizi wa mali ya umma kutumia kwenye kampeni zao basi tueleze tuu kwamba tulrudi kwenye mfumo wa chama kimoja kwa sababu unaturudisha nyuma na huna tija ya kukomboa taifa lako na kuheshimu utofauti wa kiitikadi katika nchi hata misukule kuna inayogoma kulima inapochapwa viboko na mabwana wao ,jaribuni vijana kuwa na maono ya kuendeleza nchi yetu kwa mapatano na maeleno kwa mfumo ambao ukisimamaiwa wa kidemokrasia unaweza ukasaidia wananchi tukapata viongozi tunaowahitaji lakini sio bora viongozi ,nina maana ni wenda wazimu kwa kuupuz hata hayo manifanikio madogo kwenye mfumo kandamizi wa demokrasia ,
 
I got the point . I can make a balance now . Huyo dogo ni mnafiki hata kwenye mdaharo mmoja wa star tv akiwa na Kilavi , joseph, upande wa mwanza aliongea pumba nyingine kama hizo. Aliwaponda CDM eti ni wajanja wa kisiasa kwakumtambua Rais wakati hawatambui mamlaka zilizomweka madarakani. Joseph alimjibu vizuri sina uhakika kama alielewa au laa, maana kichwa chake kina vijidudu vya UCCM.
 
Give me a break please...... Hivi ni watanzania wangapi wanajali hizi so called definitions za ujamaa na ubepari......

In this day and age watanzania masikini wengi wanajali yafuatayo

Kuona kwamba viongozi wao hawafilisi nchi yao (viongozi waadilifu, sio wanaojilimbikizia mali) i.e Mafisadi

Kupata huduma za lazima kama elimu; afya (affordably)

Kuondokana na ugumu wa maisha (How... Kuwa na ajira za kutosha... hence kupata kipato, Therefore kuweza kuishi na kupata mkate wa kila siku)

Now Chama Chochote ambacho kitawaconvice the above people will be happy with it no matter kinasema kinafata mlengo gani

Labda nikuulize Nini maana ya itikadi na nini mchangowake katika siasa za nchi? Mimi nilidhani kama msomi unapaswa kuangali mambo kwa mapana yake na sio kufuata mkumbo wa wengi ambao unadhani kwao wao hawana mpango na itikadi....

Hivi huoni kuwa mtazamo wako ambao unaadhani ndio usasa nao ni aina fulani ya itikadi yenye kuthamini vitu kuliko kitu kingine ambao ukweli unashabihiana na ubepari ingawa usingependa utambulike hivyo kwani unajua kuwa miongoni mwa watanzania walio wengi, ujamaa ndio kimbilio lao na sio ubepari ambao ndio msingi mkuu wa uhalali wa mfumo fisadi unao-inspire, kuzalisha na kulinda mafisadi.

Tatizo wengi wenu mkisikia Ujamaa mnaona dalili za kupunguziwa utamu wa nafasi zenu kiuchumi na kijamii na hivyo mnakimbilia kudai kuwa hamtambui umuhimu wa itikadi lakini mko tayari kubebwa na kula matunda ya Ubepari ambao nao ni itikadi kama Ujamaa....
 
I got the point . I can make a balance now . Huyo dogo ni mnafiki hata kwenye mdaharo mmoja wa star tv akiwa na Kilavi , joseph, upande wa mwanza aliongea pumba nyingine kama hizo. Aliwaponda CDM eti ni wajanja wa kisiasa kwakumtambua Rais wakati hawatambui mamlaka zilizomweka madarakani. Joseph alimjibu vizuri sina uhakika kama alielewa au laa, maana kichwa chake kina vijidudu vya UCCM.

Tatizo mmekumbatia sana siasa za chuki kiasi ya kwamba upeo wenu wa mambo hauzidi mstari wa uwao na usisi. Hivi ni kweli mimi niliongelea suala la Chadema kumsusia Rais Kikwete katika mdahalo wa wazi. Ila kama unataka ninaweza kuandaa mdahalo wa suala hilo na ukasikia mtizamo wangu ambao ninautoa bila ya kumung'unya maneno kwani tofauti yangu na yako wewe ni mshabiki wa kitu usichokijua na mimi kwa miaka mingi nimekisoma hicho kitu na kukijua vilivyo bila ya kuingiza ushabiki......

Na kama unadhani kuongea tofauti na kile mnachokitaka wengi wenu ni unafiki then ni wazi kwenu ninyi demokrasia ni chombo tu cha kufanikisha matakwa na maslahi yenu na sio mfumo wa kuwezesha mawazo mchanyato yenye kujenga jamii na taifa la maendeleo kwa wote.....simple put, ur just bongo right wingers mliojifunika kilemba cha uanademokrasia na ukombozi kwa mustakabali wenu pekee...
 
of course hata mimi nimechagua mtu wala si chama period! mtazamo wangu ni kwamba tunamhitaji mtu anaweza kufuatilia matatizo yetu kama jamii na kama nchi kwa ujumla..chama ni watu makini...kama hakuna watu makini ni sawa na bure
 
Hueleweki mkuu kama unaona hiyo si jitihada kwenye mfumo wa ukandamizaji kama wa CCM uliojaa ghiriba,dhuluma,uwizi wa mali ya umma kutumia kwenye kampeni zao basi tueleze tuu kwamba tulrudi kwenye mfumo wa chama kimoja kwa sababu unaturudisha nyuma na huna tija ya kukomboa taifa lako na kuheshimu utofauti wa kiitikadi katika nchi hata misukule kuna inayogoma kulima inapochapwa viboko na mabwana wao ,jaribuni vijana kuwa na maono ya kuendeleza nchi yetu kwa mapatano na maeleno kwa mfumo ambao ukisimamaiwa wa kidemokrasia unaweza ukasaidia wananchi tukapata viongozi tunaowahitaji lakini sio bora viongozi ,nina maana ni wenda wazimu kwa kuupuz hata hayo manifanikio madogo kwenye mfumo kandamizi wa demokrasia ,

Kwa demokrasia hii mnayohubiri ni wazi hakuna nafasi itakayopatikana kwa kuwa na kiongozi ama viongozi bora kwani kwenu ninyi kiongozi bora ni yule anayewakilisha chuki, maslahi na ndoto zenu pekee na kuwa tayari kufokea uvundo wa wengine na kufunika uozo wenu.....
 
I still am in continous pain when seeing any young man think like an old tortoise. And anyone below 50 is considered young by me.

Hata hao mafisadi pia hufikiria kama wewe....kuwa Ujamaa ama itkadi ni ushamba wakati wao kila dakika wanaendelea na jitihada zao za kushape Tanzania katika sura na maslahi ya kibepari....

Lakini pia utambue kila taifa lina misingi ambayo ndiyo inashape nature ama utamaduni wa kisiasa wa taifa hilo. Misingi ambayo inapaswa kuwa ndiyo Itikadi ya kitaifa. Upende usipende kwa Tanzania misingi hiyo imejengwa katika hatua kuu tatu...Imani za Tanu, Azimio la Arusha na Muongozo wa 1970. Haya yote yakahalalishwa rasmi na katiba ya Mwaka 1977.

Ni wazi kati ya wanaopigia upatu suala lakatiba mpya ni mategemeo yao kuwa huo utakuwa wakati muafaka kuondokana na misingi inayojenga UTANZANIA wetu na kujenga utanzania wanaotokaka kuona wao. Yaani utanzani unavumilia chuki na hata unaokumbatia ufisadi mradi tu unatoa nafasi kwao wao pia na sio wenzao wachache waliowawahi katika kufaidika na mfumo huo....Strategising for their TURN TO EAT...

Anyway, your alias tu inaonyesha wewe ni wa mrengo gani......
 
Tatizo mmekumbatia sana siasa za chuki kiasi ya kwamba upeo wenu wa mambo hauzidi mstari wa uwao na usisi. Hivi ni kweli mimi niliongelea suala la Chadema kumsusia Rais Kikwete katika mdahalo wa wazi. Ila kama unataka ninaweza kuandaa mdahalo wa suala hilo na ukasikia mtizamo wangu ambao ninautoa bila ya kumung'unya maneno kwani tofauti yangu na yako wewe ni mshabiki wa kitu usichokijua na mimi kwa miaka mingi nimekisoma hicho kitu na kukijua vilivyo bila ya kuingiza ushabiki......

Na kama unadhani kuongea tofauti na kile mnachokitaka wengi wenu ni unafiki then ni wazi kwenu ninyi demokrasia ni chombo tu cha kufanikisha matakwa na maslahi yenu na sio mfumo wa kuwezesha mawazo mchanyato yenye kujenga jamii na taifa la maendeleo kwa wote.....simple put, ur just bongo right wingers mliojifunika kilemba cha uanademokrasia na ukombozi kwa mustakabali wenu pekee...
I said it once and I will said it again....... Ujamaa as we know it is DEAD, tell me a country following Ujamaa...... ? Therefore majority of Tanzanians Dont care of this so called Labelling..... And lets not ge away from the point... Kafulila saying Chadema wasingeshinda kama wananchi wangefata sera was a Cheap Political Shot to Chadema (So according to Kafulila who would have won kama watu wangefata sera?)

So Kafullila comment was just presumptions with no backup evidence at all.
 
Give me a break please...... Hivi ni watanzania wangapi wanajali hizi so called definitions za ujamaa na ubepari......

In this day and age watanzania masikini wengi wanajali yafuatayo

Kuona kwamba viongozi wao hawafilisi nchi yao (viongozi waadilifu, sio wanaojilimbikizia mali) i.e Mafisadi

Kupata huduma za lazima kama elimu; afya (affordably)

Kuondokana na ugumu wa maisha (How... Kuwa na ajira za kutosha... hence kupata kipato, Therefore kuweza kuishi na kupata mkate wa kila siku)

Now Chama Chochote ambacho kitawaconvice the above people will be happy with it no matter kinasema kinafata mlengo gani

Yes my friend you have actually confirmed that Kafulila was right! isnt it?
 
Yes my friend you have actually confirmed that Kafulila was right! isnt it?

Its not about being wright or wrong its about him Using a Cheap Shot to Chadema kwamba wasingeshinda kama watu wangefata Sera.... So who would have won?, NCCR?

Also kutokana na Sera za Ujamaa na Kujitegema, watu wanahusisha Ubepari wakidhani ni (ufisadi na Ubeberu), lakini there is nothing wrong with Ubepari.... Thats what is working right now in so many countries even China is going there... Russia is already there
 
I said it once and I will said it again....... Ujamaa as we know it is DEAD, tell me a country following Ujamaa...... ? Therefore majority of Tanzanians Dont care of this so called Labelling..... And lets not ge away from the point... Kafulila saying Chadema wasingeshinda kama wananchi wangefata sera was a Cheap Political Shot to Chadema (So according to Kafulila who would have won kama watu wangefata sera?)

So Kafullila comment was just presumptions with no backup evidence at all.

U sound like someone I once decided not to urge with.....anyway, Kafulila amesema kweli na ni wazi wapenzi wa Chadema hawako tayari kukubali mapungufu yao wakidhani kuwa watanzania wameshafikia kiwango cha kukumbatia BORA MBADALA na sio lazima wajijenge kuwa MBADALA BORA.....

Nina imani Kafulila anakijua vizuri Chadema kuliko wewe. Lakini pia I wonder hata kama umewahi kutumia dakika chache kusoma Katiba na Sera za Chadema lakini pia inaelekea kwako wewe siasa ni just another game hivyo huoni mantiki ya kuisoma na kuifuatilia kwa umakini zaidi....
 
Its not about being wright or wrong its about him Using a Cheap Shot to Chadema kwamba wasingeshinda kama watu wangefata Sera.... So who would have won?, NCCR?

Also kutokana na Sera za Ujamaa na Kujitegema, watu wanahusisha Ubepari wakidhani ni (ufisadi na Ubeberu), lakini there is nothing wrong with Ubepari.... Thats what is working right now in so many countries even China is going there... Russia is already there

Really, there is nothing wrong with Ubepari??? DU..........

Lakini pia siasa za kiitikadi kama anazojaribu kuziibua Kafulila ni siasa muhimu ambazo zinakosekana katika nchi yetu na hivyo kutoa mwanya kwa wanasiasa wajanjawajanja kufaidika na siasa za majitaka na chuki zenye kukosa dira......
 
of course hata mimi nimechagua mtu wala si chama period! mtazamo wangu ni kwamba tunamhitaji mtu anaweza kufuatilia matatizo yetu kama jamii na kama nchi kwa ujumla..chama ni watu makini...kama hakuna watu makini ni sawa na bure

Wakati wa kampeni Slaa aliwaambia wananchi wachague mtu, wasichague chama.
 
Back
Top Bottom