Kafulila: Watanzania Wanachagua Mtu, Siyo Sera!

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,829
4,164
David Kafulila mbele ya microphone.

Mbele ya macho ya Watanzania.

Anasema (nanukuu):

"Kama Watanzania wangezingatia sera za vyama wakati wa kuchagua viongozi, basi chadema kisingeshinda". Hajasema kivipi.

Sababu?

"Chadema ni chama cha kibepari" (akapigwa swali na mtangazaji, 'kwani ulipokuwa chadema ulikuwa hujui kama chadema ni cha kibepari?' hajajibu mpaka dakika hii). Akaendelea.....

"Sera za kubepari haziuzi Tanzania".

Maoni yangu.

Watanzania wa leo si wakupigia matarumbeta. Unapokosoa vyama vingine, ukumbuke na kutoa alternative. Chama gani ni bora zaidi ya Chadema?

Nilichokiona kwa bwana Kafulia ni uso wa mtu 'aliyetumwa'. wivu na chuki dhidi ya chadema. Chadema kitasimama.

Kama bwana kafulia amechaguliwa kama 'mtu' na si kwa 'sera', basi hilo ni tatizo la wananchi wake. ana kazi ya kutoa elimu ya uraia kwa wananchi wa jimbo lake. na nina uhakika kama wananchi wa jimbo lake wataipata vema hiyo elimu ya uraia 2015 atarajie kupungukiwa wabunge kwenye chama chake au kukosa wabunge kabisa.

kwa ujasiri nasema:

Chadema msikubali kuungana na CUF na hawa waganga njaa kina kafulia.
 
VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,201
1,330
Hawa wanasiasa kila siku nazidi kujiuliza kama hawajui wanalolisema hence they are stupid au wanajua walitendalo bali wanataka kupotosha jamii.

Kwahiyo kama wananchi wangechagua sera je CCM ingeshinda? Je yeye walimchagua sababu yeye ni yeye au sababu ya sera ya NCCR MAGEUZI?
 
DAR si LAMU

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
2,929
531
...Ukifuatilia mazungumzo na kauli za wanasiasa wengi tulionao, bila kujali ni ccm, cdm, cuf, nccr, n.k utaona kwamba wengi wao si makini na mara kadhaa hawajui wanachosema kina-maanisha nini.

...Nitatoa mifano michache. Kwanza, Ndugu Kafulila anaposema cdm ni cha ki-bepari, chama kipi ni cha kijamaa? halafu, mabepari huwa na sera za kutoa elimu na afya bure?....anayo mifano? Pili, Ndugu Chiligati aliposema watapeleka hoja ya kuwaondoa wabunge wa cdm kwenye vikao vya bunge, alikuwa anafahamu kanuni za bunge, je, alikuwa anafahamu au amebashiri matokeo yake yatakuwa nini kama wangefanikiwa? je, angekuwa ametia maji kwenye moto au petroli? Tatu, Ndugu Hamad Rashid alipogusia suala la posho ya kiongozi wa upinzani bungeni na marekebisho ya kanuni walizozitengeneza wao wenyewe, alikuwa anajua anatafsirika vipi? je, hakufahamu kuwa ataonekana analichukulia suala zima kuwa too personal, na pengine anasononeka kukosa posho ile na kuukosa uongozi wa upinzani.

...waTanganyika bado hatujapata viongozi makini wa kutosha na ndio maana kuna madudu mengi kila siku yanaibuka kwenye vyombo vya habari juu ya viongozi. Hutana nafasi ya kutosha kujadili issues za maendeleo, tumebaki kuongelea pumba za viongozi kila kukicha! Nchi inaenda pabaya hii.
 
Raimundo

JF-Expert Member
May 23, 2009
13,419
12,549
Hawa wanasiasa kila siku nazidi kujiuliza kama hawajui wanalolisema hence they are stupid au wanajua walitendalo bali wanataka kupotosha jamii.

Kwahiyo kama wananchi wangechagua sera je CCM ingeshinda? Je yeye walimchagua sababu yeye ni yeye au sababu ya sera ya NCCR MAGEUZI?

Wanasiasa wote duniani wako hivyo, you can imagine sera za wanafunzi wote shule ya msingi watakuwa na computer ili waweze kufundishwa kwa online katika nchi kama yetu hii si upumbavu?
Mi naona kuwe na Technologia mtu akikuudhi na yuko kwenye TV unamshuti apo apo kwenye screen na anakufa huko aliko.
 
DAR si LAMU

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
2,929
531
Wanasiasa wote duniani wako hivyo, you can imagine sera za wanafunzi wote shule ya msingi watakuwa na computer ili waweze kufundishwa kwa online katika nchi kama yetu hii si upumbavu?
Mi naona kuwe na Technologia mtu akikuudhi na yuko kwenye TV unamshuti apo apo kwenye screen na anakufa huko aliko.

...Ha ha ha
 
Ha ha haaaa Wangeshaisha wote......
 
Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,402
7,949
Nilivyoangalia mjadala wa leo imetosha kabisa binafsi kuconclude kuwa vyama visiungane bungeni kwani tofauti kati yao ni kubwa mno. Huwezi kusema chama ni cha kibepari na hakiuzi wakati huohuo unataka kuungana nacho, ili iweje, muendeleze ubepari au?? Nijuavyo mimi hakuna bepari anayeahidi kutoa elimu bure au kuondoa kodi katika vifaa vya ujenzi, nashangaa huyu Kafulia alisomea chuo gani sijui. Pia hata vyama vikiungana havitakuwa na wabunge wa kuweza kuizuia ccm isipitishe hoja bungeni kwakuwa hawatafishikisha theluthi moja ya wabunge, kwa maana huo muungano hautakuwa na manufaa yoyote. CUF ilikubali kuungana na vyama vingine 2005 kwakuwa walikuwa na wapemba watupu bila hata mbunge mmoja kutoka bara kwa hiyo ingekuwa kambi ya wapemba bungeni na sio kambi ya upinzani. Kuua soo wakaalika na vyama vingine ili kujenga taswila ya utaifa katika kambi ya upinzani, chadema wakacapitalize na kujiuza vizuri kwa watanzania. Now wamepata wabunge wa kutosha tuwaache waunde kambi tutawapima 2015, tuache wivu wa kike, huwezi kuungana na chama huku unakiombea njaa huo sio muungano bali ni unafiki braza Kafulia.....
 
KyelaBoy

JF-Expert Member
Nov 9, 2008
206
22
Umakini aliondoka nao Nyerere,wanasiasa wa siku hizi buuure kabsa unategemea kweli nchi itapiga hatua kwa wanasiasa kama hawa tulionao kama akina Kombani wanadai hawaoni sababu ya kuwa na katiba mpya,akina Masha wanang'oa vitasa,akina Serukamba wanamtetea mtoto wa Lowasa badala ya Waha wenzake,akina Rostamu wanakimbizia tenda/kufanya biashara,akina Makamba ,Chiligati,Lowasa,Chenge(mkuu wa kamati ya maadili wa CCM),akina Ridhiwani wanakimbizia viwanja duu orodha ni ndefu kama mto Nile,hata wazee waliopo nao wamekosa busara akina Kingunge wamekuwa waumini wa vijisenti uzeeni,ujamaa kwao ni historia,hii ni aibu kwa kizazi hiki, sioni kiongozi mwenye vision huenda wajukuu zetu watakaokuja hapo baadaye .
 
Raimundo

JF-Expert Member
May 23, 2009
13,419
12,549
Kafulila ana Elimu gani wandugu? CV yake tafadhali

Kafulila F1-4 Uvinza Secondary School-Div 3 (pt sikumbuki) this was 1998-2001
F5-6 Shinyanga Secondary School-Div 2 pt 11 2002-2004
Mara ya mwisho alikuwa anasoma BBA UDSM (this is an eveving class program), mwaka wa kwanza mwaka 2006/7 na kasomeshwa na Chadema anaowaita mabepari. Sina uhakika kama alimaliza mwaka wa tatu na kama alimaliza atakuwa hakufanya vizuri kwa sababu most of times alikuwa anafanya kazi za chama.
 
VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,201
1,330
Kafulila F1-4 Uvinza Secondary School-Div 3 (pt sikumbuki) this was 1998-2001
F5-6 Shinyanga Secondary School-Div 2 pt 11 2002-2004
Mara ya mwisho alikuwa anasoma BBA UDSM (this is an eveving class program), mwaka wa kwanza mwaka 2006/7 na kasomeshwa na Chadema anaowaita mabepari. Sina uhakika kama alimaliza mwaka wa tatu na kama alimaliza atakuwa hakufanya vizuri kwa sababu most of times alikuwa anafanya kazi za chama.

So hizi habari za kuwa alisoma na Zitto sio za kweli, au ni marafiki tu
 
Raimundo

JF-Expert Member
May 23, 2009
13,419
12,549
So hizi habari za kuwa alisoma na Zitto sio za kweli, au ni marafiki tu

Hajawahi kusoma na Zitto, wakati yuko Form 2 (au F3 hapa) alikuwa Naibu Katibu mwenezi NCCR Mageuzi wa either wilaya au kata (hapa uhakika sio mkubwa).
Baada ya kumaliza form 6 alijiunga na Chadema na alikuwa kwenye kampeni za Zitto (Zitto saw that the guy is potential and he was using him for his things)

Kafulila alipata nafasi ya kusoma chuo cha Tumaini University-Iringa, Chadema wakamwomba aache ili asome masomo ya jioni huku akiwa anafanya kazi za chama.

NOTE: Zitto na Kafulila wanatoka majimbo tofauti.
 
Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,829
4,164
Ni kweli, dogo alikuwa na akili sana kwa shule yake kupata div 3. You can imagine shule nzima ilikuwamoja na div 3, zilizobaki 4 na 0.

hapo kwenye red nimekusoma.

swala la kuwa na akili sasa kwake ni historia.

inaelekea siku hizi hana akili tena. kwa sababu mtu mwenye akili hawezi kuongea utumbo aliokuwa anazungumza leo star tv.

amejaa majivuno tu. kama rafiki yake.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom