Kafulila: Nimerejea CHADEMA rasmi leo

Kafulila: Nimerejea CHADEMA rasmi leo

Namshukuru Mungu kwa siku ya leo kurejea CHADEMA rasmi. Kwa heshima kubwa Namshukuru Mungu kwa tukio la leo. Namshukuru sana Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa heshima kwa kunikabidhi kadi mbele ya kikao muhimu cha Kamati Kuu leo jijini Mwanza. Ninaawaahidi wanachadema na wazalendo wote mnaopigania mabadiliko ya taifa hili kuwa nitatumia nguvu na akili yangu kuchangia mabadiliko tunayoamini! Ni wito wangu kwa wazalendo wote tuunganishe nguvu CHADEMA kuliokoa taifa letu linalopita nyakati ngumu kiuchumi na majaribu makubwa kiuongozi.
NCCR tulikukosea nini jamani? Mbona umetuacha hivi hivi tumezubaa?
 
Namshukuru Mungu kwa siku ya leo kurejea CHADEMA rasmi. Kwa heshima kubwa Namshukuru Mungu kwa tukio la leo. Namshukuru sana Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa heshima kwa kunikabidhi kadi mbele ya kikao muhimu cha Kamati Kuu leo jijini Mwanza. Ninaawaahidi wanachadema na wazalendo wote mnaopigania mabadiliko ya taifa hili kuwa nitatumia nguvu na akili yangu kuchangia mabadiliko tunayoamini! Ni wito wangu kwa wazalendo wote tuunganishe nguvu CHADEMA kuliokoa taifa letu linalopita nyakati ngumu kiuchumi na majaribu makubwa kiuongozi.
Katika nchi ya kidemocrasia watu wana uhuru wa kufanya maamuzi na kuchagua aina ya maisha wanayo fikiri kwamba ni sahihi. hujakosea Kafulila
 
Ila Afrika hakuna wanasiasa wenye sifa za kufanya hayo uliyotaja kwenye aya ya tatu ila ni wasanii tu na wengine ni waganga njaa wanaokimbia kulima huku.

Umekula maharage ya wapi na wewe.

Nyie ndio wale wale mnaotuletea mijitu kama hii inayovuruga nchi.

Siasa ni maisha na maisha ni siasa. Kila ukifanyacho ni lazima siasa iwepo. Siasa ni mipango,mbinu,hoja makini na zenye mantiki,sululisho,tafakuri yakinifu,taaluma,sera na mipango.

Bila siasa usingeleta kimbelembele cha kucomment hapa jukwaani.
 
Jembe langu... Karibu home kamanda... Hapa ni bampa to bampa....hadi mida ya wanga!!!
 
Kamfata mkewe. Maskini Muha wewe umekwisa kabisa. Ameogopa kwenda team Mawese. Hahahaaaaa
 
Kwa hiyo karudia matapishi tena au ndio njaa yenyewe hiyo!
 
Ile kesi ya matokeo ya ubunge iliisha? Ikitokea mahakama ikatengua ule ushindi wa mpinzani wake, atarudisha tena kadi ya CDM?
 
Mkuu;
Nimesema hii dhana ya kusema Katiba haituruhusu kuungana ni kichaka cha kuficha ukweli kwa sababu kama kweli wanataka kuunda chama kimoja wanaweza kuvunja vyama vingine na kujiunga na chama kimoja.

Hivi unaamini kuna viongozi kwenye kambi ya upinzani wenye uwezo wa kufanya maamuzi unayoyatamani.
Wavunje alafu ccm mfute usajili hiko chama kipya kma ccj???

Anyway nachosema ni kuwa idea ya kuunda chama kimoja ni muhim ila its obvious inahitaji muda sana hasa kuandaa katiba na kubadilisha mirengo na sera za chama kwa hyo njia rahisi ingekuwa kuunganisha nguvu kma coalition za cord na jubilee kila chama kivyake ila vinashirikiana kwenye uchaguzi na hta baada ya uchaguzi sema hil tulilitegemea kwenye katiba mpya kabla ya ccm kuivuruga mchakato.

Sasa kwa muda mchache uliobaki baada ya katiba kuvurgika na kabla ya uchaguzi wa 2015 ingekuwa ngumu sana kuunganisha vyama kuwa kimoja na ndio maana hilo halikufanyika zaidi walishirikiana tu ila kwa siasa zilivyo sasa na issue ya cuf naona vision ya mbatia ya kuunda chama kimoja pekee hapa Tanzania cha upinzani kitatimia
 
Naomba kujua, je amebadilika kutoka sisimizi au amekua siafu sasa
Hta chadema tuliwaita cuf waliberali also wao wakatuita wachungaji wa nguruwe its ok lakini hizo ni tofauti za kiitikadi na rivarly za kisiasa ILA inapofika wakati wa ukombozi mnaungana kwa kuridhiana hta mlipoumizana mnazika tofauti zenu za kisiasa kwa ajili ya maslahi mapana ya kitaifa..... sasa tukiendekeza mabifu unafkiri umoja wa kitaifa utapatikana ???

Tujifunze kusamehe na kujikita kwenye maslahi mapana ya taifa kuliko tofauti zetu binafsi ziathiri mfumo mzima wa siasa za mageuzi hapa tanzania
 
Ungekuja ACT wazalendo
Wakati utakapofika hata ACT mjiunge na wapinzani wengine hamuoni mlivyogawa kura vile 2015 hadi almanusura kigoma nzima ingerudi ccm wakati ilikuwa ina wabunge 5 wa upinzani?? Hizi tofauti zetu zaidi zimemnufaisha ccm zaidi ya act au chadema or nccr
 
Huyu huyu Kafulila alitoka Chadema akaenda Nccr na huko walipitaka kumfukuza na ilikuwa akose ubunge alilia kilio kama mtoto mdogo, sasa anarejea pale pale alipopakimbia kwanza akitadai chadema kuna ubaguzi. Jee leo huo ubaguzi umeisha?

Huyu bila ya msaada wa zitto hana kitu, hata huo ubunge aliupata kwa mgongo wa Zitto na linajulikana wazi, kwani hilo lilimletea zitto tatizo chadema na uhusiano wake na Dr Slaa ndipo ulipoanza kudondora, kwani mbunge wa chadema kwa msaada wa zitto angeweza chukua jimbo la kasulu.

Huyu hana shukrani na baada ya mwaka tutasikia huyo mbayuwayu tena kahamia mti mwengine
Embu acha dharau wwe ina maana kafulila 2015 laisaidiwa na zitto?? Kma sio NEC kuingiliwa na uhuni hadi kulazimisha warudie kuhesabu ndio kulisababish asiwepo mjengoni ila tuliokuwepo jimboni tunajua alishinda

Kma zitto ndio kila kitu kigoma mbona jimbo lake la kigoma kaskazini act haikushinda?? Mbona kwa mchali hakumsaidia kushinda??? Kwenye jimbo la kafulila act ilisimamisha mgombea kma zitto ndo kila kitu mbona act haikushinda zaidi mgombea wao aliachwa kura takribani 20,000 na kafulila???

Namkubali sana zitto ila sio kwa dharau hizi Kafulila wa 2010 sio wa 2015 sahvi ana CV nzito ma political experience kubwa hasa hoja zake nzito kipindi akiwa bungeni iweje umdharau hivi?? Leo hii ukisimamishwa naye nani watakuwa na shauku ya kukuskiliza wwe wamuache yye??
 
Back
Top Bottom