Kafulila: Nimerejea CHADEMA rasmi leo

Kafulila: Nimerejea CHADEMA rasmi leo

Kama angepata ubunge angehamia CHADEMA? Jibu hapana.

Kwa nini anadhani CHADEMA ni bora kuliko NCCR-Mageuzi wakati ukisimamishwa kugombea na NCCR-Mageuzi unapigiwa kampeni na vyama vilivyoko Ukawa.

Kwa hiyo anatupa ujumbe kuwa NCCR-Mageuzi limebaki jina tu.

Nini hatima ya Ukawa nchini? Au ndio kama yale madai yanayosema Tanganyika imevaa koti la Muungano!

Kwa sasa CHADEMA imevaa koti la Ukawa!
Waa waa makofi kwa hoja kioja
 
Hivi hawa wanasiasa wanasumbuliwa na nini? Ngoja tusubiri kina seif, mtatiro na wengine pia wakikimbilia uko
 
ulitaka ccm?

swissme
 
Hivi hawa wanasiasa wanasumbuliwa na nini? Ngoja tusubiri kina seif, mtatiro na wengine pia wakikimbilia uko
lazima wote viongozi makini waje chadema tuungane tulitoe hilo gonjwa ccm linaloturudisha nyuma badala ya kwenda mbele 54 yrs hata dawa MSD hakuna.unashabikia mtu anakusanya pesa za kodi kisha anapeleka kwenye mambo ya hajabu.

swissme
 
Yeye ni bora hata watanzania wajua ndio maana kaja chadema kwa watu makini wenye hoja zilizo simama.wewe unatuletea shobo tu go back to school Dude.

swissme
Ha haaa haaa.... sioni ulilo andnika ambalo ni tofauti na mimi.... namkubali sana tu... ila si alikuwa cdm? Kwa nini alitoka? Thats my point..... atulie ajenge chama... kashfa za shule peleka kwa familia yako ....
 
Namshukuru Mungu kwa siku ya leo kurejea CHADEMA rasmi. Kwa heshima kubwa Namshukuru Mungu kwa tukio la leo. Namshukuru sana Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa heshima kwa kunikabidhi kadi mbele ya kikao muhimu cha Kamati Kuu leo jijini Mwanza. Ninaawaahidi wanachadema na wazalendo wote mnaopigania mabadiliko ya taifa hili kuwa nitatumia nguvu na akili yangu kuchangia mabadiliko tunayoamini! Ni wito wangu kwa wazalendo wote tuunganishe nguvu CHADEMA kuliokoa taifa letu linalopita nyakati ngumu kiuchumi na majaribu makubwa kiuongozi.
ila kafulila ujue hii sio chadema uliyoiacha. ile iliyokua imebeba matumaini ya wengi. hii chadema uliyorudi ni mali ya tajiri mmoja unamjua vizuri. hii chadema ya sasa iliuzwa na mwenyekiti wake kwa usaliti mkuu ili kutumika na huyo tajiri kuingia ikulu. kama umerudi kupambana kukomboa chama..kila la kheri. kama ni kuendeleza maslahi binafsi kwa kufanya siasa kama kazi tafadhali usiingie kwenye mtego wa uongo na uzushi kuliombea taifa kila baya ili champion jpm ashindwe kutekeleza malengo yake mema kwa taifa.
 
ila kafulila ujue hii sio chadema uliyoiacha. ile iliyokua imebeba matumaini ya wengi. hii chadema uliyorudi ni mali ya tajiri mmoja unamjua vizuri. hii chadema ya sasa iliuzwa na mwenyekiti wake kwa usaliti mkuu ili kutumika na huyo tajiri kuingia ikulu. kama umerudi kupambana kukomboa chama..kila la kheri

hahahaha sasa chadema linaimalika

TIMU

SWISSME
 
Bado Zitto Kabwe! Muda si mrefu kile chama cha Lake Tanganyika kitagundua kinapambana na wakati ambao ni ukuta. Hapo ndipo mwana mpotevu atarudi kwa baba yake na kuandaliwa karamu kubwa maana mtoto akinyea mkono hatuukati. Baada ya kuungama na kutubu 'dhambi zake za kisiasa' na kutuahidi kujivika joho la Zitto wa 2005-2007 atakuwa na haki ya kukisogelea kiti kikuu.

Lakini hii ni ndoto tu maana ZZK mwenye vipawa vya akili na maarifa ambavyo hapendi kuvitumia yeye mwenyewe bali kupenda vitumiwe na watu wengine hawezi kubadilika. Kutumiwa ni hulka ya mtu, yaweza kufunikwa lakini sio kufichwa.
 
ila kafulila ujue hii sio chadema uliyoiacha. ile iliyokua imebeba matumaini ya wengi. hii chadema uliyorudi ni mali ya tajiri mmoja unamjua vizuri. hii chadema ya sasa iliuzwa na mwenyekiti wake kwa usaliti mkuu ili kutumika na huyo tajiri kuingia ikulu. kama umerudi kupambana kukomboa chama..kila la kheri
Mkuu umeumia? Mbona ngonjela nyingi? Kwani tajiri mmoja tu kuwa upande huu kwako ni shida? Kwemye chama cha kijani wamebaki wangapi? Tuliza ball mkuu.....
 
Nadhani huyu analenga kwenda kugombea kule kwa yule mbunge aliyefungwa miezi sita....ama kweli kufa kufaana!
 
Namshukuru Mungu kwa siku ya leo kurejea CHADEMA rasmi. Kwa heshima kubwa Namshukuru Mungu kwa tukio la leo. Namshukuru sana Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa heshima kwa kunikabidhi kadi mbele ya kikao muhimu cha Kamati Kuu leo jijini Mwanza. Ninaawaahidi wanachadema na wazalendo wote mnaopigania mabadiliko ya taifa hili kuwa nitatumia nguvu na akili yangu kuchangia mabadiliko tunayoamini! Ni wito wangu kwa wazalendo wote tuunganishe nguvu CHADEMA kuliokoa taifa letu linalopita nyakati ngumu kiuchumi na majaribu makubwa kiuongozi.
Kaka yako Zitto hajambo?
 
Back
Top Bottom