Kafulila: Nimerejea CHADEMA rasmi leo

Kafulila: Nimerejea CHADEMA rasmi leo

Kama angepata ubunge angehamia CHADEMA? Jibu hapana.

Kwa nini anadhani CHADEMA ni bora kuliko NCCR-Mageuzi wakati ukisimamishwa kugombea na NCCR-Mageuzi unapigiwa kampeni na vyama vilivyoko Ukawa.

Kwa hiyo anatupa ujumbe kuwa NCCR-Mageuzi limebaki jina tu ndani ya UKAWA.

Nini hatima ya Ukawa nchini? Au ndio kama yale madai yanayosema Tanganyika imevaa koti la Muungano!

Kwa sasa CHADEMA imevaa koti la Ukawa!
Naona mnaumia sana!! Tulia daea ikuingie gamba wewe
 
Kafulila siyo sisimizi tena?
Aliyemwita sisizi alihamia CCM dakika za mwisho kisha wakamsepasha kula bata!! Ni muda muafaka sasa wa yeye kurudi na kuyaendeleza yale anayoyaamini.

CDM haina mwenyewe, ni ya watanzania wote - welcome home comred.
 
Namshukuru Mungu kwa siku ya leo kurejea CHADEMA rasmi. Kwa heshima kubwa Namshukuru Mungu kwa tukio la leo.

Namshukuru sana Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa heshima kwa kunikabidhi kadi mbele ya kikao muhimu cha Kamati Kuu leo jijini Mwanza.

Ninaawaahidi wanachadema na wazalendo wote mnaopigania mabadiliko ya taifa hili kuwa nitatumia nguvu na akili yangu kuchangia mabadiliko tunayoamini!

Ni wito wangu kwa wazalendo wote tuunganishe nguvu CHADEMA kuliokoa taifa letu linalopita nyakati ngumu kiuchumi na majaribu makubwa kiuongozi.
Ukawa ndani ya ukawa
 
Namshukuru Mungu kwa siku ya leo kurejea CHADEMA rasmi. Kwa heshima kubwa Namshukuru Mungu kwa tukio la leo.

Namshukuru sana Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa heshima kwa kunikabidhi kadi mbele ya kikao muhimu cha Kamati Kuu leo jijini Mwanza.

Ninaawaahidi wanachadema na wazalendo wote mnaopigania mabadiliko ya taifa hili kuwa nitatumia nguvu na akili yangu kuchangia mabadiliko tunayoamini!

Ni wito wangu kwa wazalendo wote tuunganishe nguvu CHADEMA kuliokoa taifa letu linalopita nyakati ngumu kiuchumi na majaribu makubwa kiuongozi.
Hah hah njaa bana kwanini arudi Chadema na asiende CUF au abaki NCCR akabiliane na bosi wake au aende ACT,shida hapa ni kuwatumia wapiga debe wa BAVICHA ili wamsaidie kuzungusha mikono apate tena ubunge,baado kijana anaota tamu ya kuwa mbunge tena,kala matapishi yake.
 
Natumaini hutaondoka tena. Karibu Nyumbani mwana mpotevu!
Kala mitapishi yake ,kwa taarifa heri ya jana kuliko leo Kafulila,kufulia kwako ndio kunaanza safari ya milele,na kamwe hupati tena ubunge ,ukidhani kuwa Chadema ndio njia ya kulitwaa tena jimbo ulilolopoteza.
 
Siasa ni kitu cha ajabu sana, Kafulira alitimuliwa Chadema akaondoka na Kadi yake kujiunga NCCR kule akavurunda akataka kutimiliwa Akalia sana akasamehewa na kupewa Cheo kikubwa cha Uenezi wa Chama, sasa kahama Chama ndani ya Ukawa hii ni Kulinda Ukawa kweli?
Mbatia ni Mgonjwa yuko Kitandani ilitakiwa Busara basi ya Mbowe kusubiri mwenziye apone kama ana nia njema, vinginevyo Chadema ina nia ya kuvichinjia Baharini Vyama wenza wa Ukawa kwa kujijenga binafsi hii si Sawa.


FB_IMG_1484840219655.jpg
 
Mapambano yanaendele safar ya kwenda ikuli 2020
Nashaur lowasa fungua tv yako mana nape kapiga bun hawa jamaa wanabana sana ishu za wakawa
 
Nimefurahi Kafulila kurudi but nadhani it is not a big story,na hii inatokana na kwamba anatoka NCCR Mageuzi chama ambacho ni mshirika wa UKAWA, impact yake ni ndogo sana kwa UKAWA kiujumla though kuna manufaa kwa chama chetu cha CHADEMA kwamba tumepata mtu muhimu ambaye ni mpambanaji.Kwa upande mwingine ni kwamba tumemdhoofisha mshirika wetu mmoja, yaani NCCR ambaye ili tufikie malengo ya pamoja ni lazima aimarike na kuwa madhubuti hasa kipindi hiki muhimu.
 
Back
Top Bottom