Kafulila: Nimerejea CHADEMA rasmi leo

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
Namshukuru Mungu kwa siku ya leo kurejea CHADEMA rasmi. Kwa heshima kubwa Namshukuru Mungu kwa tukio la leo.

Namshukuru sana Mwenyekiti Freeman Mbowe kwa heshima kwa kunikabidhi kadi mbele ya kikao muhimu cha Kamati Kuu leo jijini Mwanza.

Ninaawaahidi wanachadema na wazalendo wote mnaopigania mabadiliko ya taifa hili kuwa nitatumia nguvu na akili yangu kuchangia mabadiliko tunayoamini!

Ni wito wangu kwa wazalendo wote tuunganishe nguvu CHADEMA kuliokoa taifa letu linalopita nyakati ngumu kiuchumi na majaribu makubwa kiuongozi.
 
Kama angepata ubunge angehamia CHADEMA? Jibu hapana.

Kwa nini anadhani CHADEMA ni bora kuliko NCCR-Mageuzi wakati ukisimamishwa kugombea na NCCR-Mageuzi unapigiwa kampeni na vyama vilivyoko Ukawa.

Kwa hiyo anatupa ujumbe kuwa NCCR-Mageuzi limebaki jina tu ndani ya UKAWA.

Nini hatima ya Ukawa nchini? Au ndio kama yale madai yanayosema Tanganyika imevaa koti la Muungano!

Kwa sasa CHADEMA imevaa koti la Ukawa!
 
Ila apunguze ukigoma .... (ubishi ) usio na tija
na kujiona ni bora.... atulie na kujenga chama... namkubali sana huyu jamaa tatizo tu ni Kale ka UKigoma ajakaacha.... Kafulila this time kaache Malagalasi tafadhali..... karibu nyumbani....

Yeye ni bora hata watanzania wajua ndio maana kaja chadema kwa watu makini wenye hoja zilizo simama.wewe unatuletea shobo tu go back to school Dude.


swissme
 
Back
Top Bottom