omarilyas
JF-Expert Member
- Jan 24, 2007
- 2,130
- 151
well umeandika sana
1.Zitto kuwa na nia ya kuivuruga CHADEMA eti kwa mipango yake ya kuhamia ama kugombea Urais
Matendo ya Zitto yanaondoa nia safi aliyona nayo ya kuwa Rais-(ni vigumu kuamini Zitto ana nia ya kuisogeza mbele nchi kama akiwa rais kwa CDM/NCCR/CCM
Kama Zitto ni tatizo na sio uongozi wenu na siasa za kiujanjaujanja iweje kuondoka kwa Zitto Chadema kuweze kuwavuruga na sio kuwapa nafasi ya kujijenga. Lakini pia iweje Kiongozi wa CCM anapokataa kunyamazishwa eti kwa maslahi ya chama iwe haramu lakini anapotokea kiongozi wa Chadema asiyekubali kunyamazishwa ama kunyamazia mambo ya hovyohovyo iwe haramu (Double standard zisizoweza kumsaidia mtanzania kamwe)
2.kuvuruga chama chenu
zitto anautaka urais at any cost K
Hivi ni vipi Zitto akataka huo urais at any cost na sio Freeman Mbowe aliyetayari kupanga na kutekeleza mikakati haramu dhidi ya washindani wake kama Dr Slaa na Zitto? Hivi ni nani aliyesikika akilalama kuwa wale watu watatu waliokufa kule Arusha hawakutosha ili kujenga chuki zaidi kwa CCM na Chadema ifaidike kisiasa? Hivi ni nani anayeendeleza siasa za majungu katiika magazeti yenu (zinazokomaza makundi ndani ya Chadema) eti katika kuhakikisha kuwa anammaliza Zitto kwa kosa la kuthubutu kushindana naye katika nafasi za uongozi za Uenyekiti na baadaye Uongozi wa Upinzani bungeni ambao kwake yeye ni "platform" ya kujijenga kwa Watanzania ili kama asemavyo" come to 2015 awe Presidential Material"? Hivi ni nani aliyekuwa mstari wa mbele kuhonga viongozi wa Chadema majimboni ili wasabotage kampeni za wagombea wenu ambao anaona wao ni tishio kwa nafasi yake ya Uenyekiti na safari yake ya Ugombea Urais 2015
3.kujisafisha kwa udini ukabila ufisadi
udini (RAIS MUISLAM,MAKAMU MUISLAM,WAZIRI WA PESA,MAMBO YA NDANI,KIRANJA WA ZANZIBAR,MAKAMU KIRANJA ZENJI,ULINZI MUISLAM)+ufisadi (muulize mwanao wa chekechea)=hao ni CCM
Ukabila nenda TLP na CCM (ALL SINGIDA)
Ulichokiandika hapa kinathibitisha ukilaza wako katika kupambana na hoja na vizingiti vya kisiasa vinavyokumba ndoto yenu ya siasa za madaraka...Lakini pia weweukiwa kama kiongozi wa Chadema unathibitisha hisia halisi za kundi la wahafidhina ndani ya chama chenu katika mantiki nzima ya maslahi, siasa na chuki za kidini...Hivi ni nani aliyekimbilia kwa Maaskofu akiwaahidi kuwa anenda kujiendeleza kielimu ili baadae aweze kugombea urais na hata alipotishiwa kung'olewa kidemokrasia katika nafasi yake ya uenyekiti akatumia hoja ya kuwa Maaskofu hawatakuwa tayari kuona vyama vyote vikuu vinaongozwa na Waislamu
4.mizizi ya itikadi za KIJAMAA
Hata CCM wana sera za Kijamaa
hamna chama chenye sera nzuri kama CUF tuwe wakweli
Note:Sera za kwenye makabati na mezani hazisaidii kama hamna commitment (CDM wapo commited including Zitto)
NCCR inakosa watu wa aina ya CDM na sio inamkosa Zitto K.
Kweli ni kilaza. Unajifaragua kama mwanasiasa wakati unashindwa hata kujua tofauti ya itikadi na sera? Ndio maana mnambiwa muende shule na msome masuala ya siasa za dunia yetu. Siasa za kujifunzia katika magazeti ya udaku wa kijamii na kisiasa kama Mwanahalisi ni hatari kwa Tanzania ijayo.
5.nguvu na akili za Zitto
nakubali Zitto ana akili nyingi ila anaponzwa na tamaa. Zitto hana nguvu kisiasa kama mwanzoni (Baada ya Mafisadi papa kukalia kuti kavu CCM Zitto hana tena jeuri kwani ni wazi alitegemea saaaanaa msaada kutoka kwa Rostam ili aendeshe siasa ndani ya CDM kwa manufaa ya CCM na sio kwa manufaa ya nchi.
Nijuavyo katika tafiti zote zilizofanyika umaarufu wa Zitto umekuwa ukipanda na sio vinginevyo. Chuki na hisia zenu kuwa mnafanikiwa kupunguza umaarufu wa Zitto ndio zinaendeleza kuwadumaza huku mwenzenu anazidi kujitanua sio tu nchi lakini hata katika medani za siasa za kimataifa. Ninyi bakini na pety and parochial politics mkidhani watanzania hawa walioamka na kung'amua uvundo wa CCM wataendelea kuamini katika ugoigoi wa kifikira, nia za chuki na uozo wa Chadema....
My take:Kwa sasa Zitto hawezi kuhama CDM as Mapacha wamebanwa ndani ya CCM,
Kama Zitto ni jiwe kuliko CDM tunataka aondoke hata leo tena ahamie CCM asituletee undumilakuwili hapa.
Ndani ya CDM hamna mtu wa kulinganishwa na Dr. Slaa.Ni mamluki wa CCM ndani ya CDM wanaoleta ujinga na sasa wajue Zitto hatakuwa rais akiwa CDM kwa hiyo wawahi KWINGINE
Hili dua lenu la kuku kuwa Zitto atahamia CCM kamwe haliwezi kutimia. Kamwe Zitto hatahamia CCM.
Halafu angalia fikira za "wakombozi" wanaotuuzia chai za "DEMOKRASIA" wakati bado mnashindwa kujiondoa katika na utando wa siasa za kihafidhina za kuwapa Umungu viongozi wetu. Eti hakuna mtu wa kulinganishwa na Dr Slaa (ofcourse yapo ya Dr Slaa ambayo hayawezi kulinganishwa na mtu mwengine lakini sio uwezo wa kuongoza nchi na kuleta mabadiliko ya kweli na yaliyo makini yenye tija kwa watanzania). Udaktari wa Theolojia haumtoshi sasa mnaanza kumpa Umungu. Halafu baadae mtakuja lalamika viongozi haohao mnaowapa umungu wanavyogeuka kuwa miungu watu.....