Kafulila na Zitto wanaivuruga NCCR - Moses Machali

Status
Not open for further replies.
Umeongelea hisia zako, lakini ukweli Zitto ni mtata. Kama CHADEMA ingekuwa kama CCM ya leo ingesambarataratika kwani Zitto amewahi kukituhumu chama kwa udini na ukabila. Kama hiyo haitoshi mara baada ya uchaguzi mkuu 2010 Zitto alitangaza kugombea urais 2015 kinyume na taratibu za chama, kama si hekima za uongozi wa CDM na mama mzazi wa zito tusingefika hapa tulipo. Hii yote ni kwa sababu anaamini ana wapenzi wengi.

Watanzania tubadilike tuache mapenzi ya mtu kwenye siasa tuangalie sera za chama. Tujifunze KWA JK WENGI WALIMPENDA KWA STAILI KAMA HII YA ZITTO LAKINI NAAMINI LEO JK HATA UKIMPA UKUU WA SHULE YA SEKONDARI HATA FANYA VIZURI
Naona upo off hoja ni NCCR vs ZITTO, KAFULILA
 
mimi nina hakika asilimia mia moja.anachosema machali ni ukweli na huyu jamaa na mpaka vizuri na kafulila pia nimeishia naye.hivyo huo ndy ukweli h6nhesa macia
 
Na sisi watanzania tusipende kusema bila kufanya uchunguzi,tujiulize ni kwa nini asemee mwanahalisi.Na yeye anatumiwa na nani.ni mbatia au ni nani hasa.

Tangu lini Mbatia akawa mpinzani hadi ionekane anayetaka kumpindua ni mhaini asiye na nia nzuri. Ni nani ndani ya hicho chama chao alishawahi kuhoji dhamira ya mbatia hasa pale anaposimamia mstari tata wenye mwelekeo wa mahaba na CCM.

Tatizo wenyeviti wa vyama vya siasa Tanzanzania hawataki challenge wanandhani uenyekiti ni haki ya kuzaliwa.hizi hulka za do or die political mentality zinadumaza demokrasia. Baadhi ya Wenyeviti wa vyama vya siasa na hasa upinzani wana mawazo ya kijima katika kufanya siasa na imefikia hatua wanaogopa watu wanaowapa changamoto za kweli na hasa vijana.Hili ni pigo kwa demokrasia.

Sitaki kuingilia mambo ya ndani ya NCCR lakini tujiulize ina maana huko NCCR hakuna mwenye haki ya kupinga mwenyekiti au kugombea nafasi ya juu ya uongozi ndani ya chama hicho...na je ina maana Mbatia ndiye mwenye kauli ya mwisho katika kupitisha nani awe mgombea urais kupitia NCCR....

WanaJF, ukiona Mbunge anajadili watu bila kuwa na uhakika wa anachosema ujue ni dalili za watu kuwa na ombwe la fikra. Sisi tunaingia mkenge kisa kasema mtu ambaye unamkubali SANA ! ! ! Tunaacha kufikiri kwa sababu mtu unayemkubali sana kasema, tuwe makini yasije yakatukuta yale ya Kibwetere kule Uganda
Hata TZDAIMA imo hii habari. HOJA Hapa ni USALITI WA ZITO BASI.. Ya kafulila wala sina haja nayo
 
Kama kweli ndivyo ilivyo: basi NYEPESI hawatakii mema wananchi wa Nchi hii.
Kwa karne hii hakuna anayeweza kuhama sehemu kwa kufuata mkumbo. huyo NYEPESI asifikili kupata urahisi ni kazi ndogo, kwa ushawishi gani atautoa ili jamii imuelewe na hatimaye wana CDM waweze kuhamia NCCR!!. Hii inadhihirisha kuwa CDM ina watu ambao ni vichwa pengine akijiringanisha anaona hawezi kufua dafu.
Sasa hivi tunafikilia ni namna gani nchi ikombolewe kutokana mikononi mwa Wafisadi, anaye leta mchezo wa kuvuruga vyama kisa apate nafasi ya kugombea u-rais kwa matakwa yake binafsi naye ni Fisadi na wala hapaswi kupewa nafasi.
 
Mbatia aondolewe mapema iwezekanavyo, sioni umuhimu wake kwenye siasa za upinzani zaidi ya kupika majungu dhidi ya wenzake.
 
Na sisi watanzania tusipende kusema bila kufanya uchunguzi,tujiulize ni kwa nini asemee mwanahalisi.Na yeye anatumiwa na nani.ni mbatia au ni nani hasa.

Tangu lini Mbatia akawa mpinzani hadi ionekane anayetaka kumpindua ni mhaini asiye na nia nzuri. Ni nani ndani ya hicho chama chao alishawahi kuhoji dhamira ya mbatia hasa pale anaposimamia mstari tata wenye mwelekeo wa mahaba na CCM.

Tatizo wenyeviti wa vyama vya siasa Tanzanzania hawataki challenge wanandhani uenyekiti ni haki ya kuzaliwa.hizi hulka za do or die political mentality zinadumaza demokrasia. Baadhi ya Wenyeviti wa vyama vya siasa na hasa upinzani wana mawazo ya kijima katika kufanya siasa na imefikia hatua wanaogopa watu wanaowapa changamoto za kweli na hasa vijana.Hili ni pigo kwa demokrasia.

Sitaki kuingilia mambo ya ndani ya NCCR lakini tujiulize ina maana huko NCCR hakuna mwenye haki ya kupinga mwenyekiti au kugombea nafasi ya juu ya uongozi ndani ya chama hicho...na je ina maana Mbatia ndiye mwenye kauli ya mwisho katika kupitisha nani awe mgombea urais kupitia NCCR....

WanaJF, ukiona Mbunge anajadili watu bila kuwa na uhakika wa anachosema ujue ni dalili za watu kuwa na ombwe la fikra. Sisi tunaingia mkenge kisa kasema mtu ambaye unamkubali SANA ! ! ! Tunaacha kufikiri kwa sababu mtu unayemkubali sana kasema, tuwe makini yasije yakatukuta yale ya Kibwetere kule Uganda
Ben!
Hapo re:si kwa upinzani tu sema hata CCM
tunataka mbatia aondolewa kwa kushindwa kuendesha chama na si kwa mizengwe ya kutoa mwanya kwa flani flani kugombea 2015.
Challenges wanazokutana nazo wenyeviti ziwe na nia ya kujenga na sii watu (vijana) wenye ajenda za siri ya kutwaa madaraka ndani ya
ya chama ili watekeleze maagizo ya WALE WALIO NJEE YA CHAMA.
 
Gazeti la mwanahalisi lina habari nzito tena za kushtusha.

Mbunge wa Kasulu mjini Moses Machali amemshutumu vikali David Kafulila kwamba anatumiwa na Naibu Katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe kukivuruga chama hicho.

Mbunge huyo wa Kasulu anadai lengo kubwa la Kafulila ni kumwondoa mwenyekiti wa chama hicho James Mbatia ili yeye awe mwenyekiti.

Pili Machali amedai kwamba baada ya Kafulila kuwa mwenyekiti atamkaribisha Naibu Katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe ili awe mgombea Urais kupitia NCCR.

Moses machali ameendelea kudai kuwa baada ya mpango huo kukamilika watatumia mbinu mbalimbali kuivuruga Chadema kwa kuhama na kundi kubwa la wanachama wake.

Mbunge huyo ameendelea kudai kuwa kamwe hatakubali mbinu hiyo kwani Zitto na Kafulila wanatumika kuua upinzani.

Alipoulizwa kwanini watake kumuondoa Mbatia kwanza amesema hiyo ni kutokana na sababu kwamba kamwe Mbatia hatamkubalia Zitto kugombea urais kupitia NCCR.

Source: MwanaHalisi

Inawezekana ni kweli Kafulila anakiaribu chama,lakini sidhani kama ana mpango wa kumleta Zitto kugombea uraisi....NCCR watatue matatizo yao kwa wao wenyewe bila kubebesha mzigo watu wengine...
 
Huyo Zitto vipi?? Mara wanasema anatumiwa na CCM sasa hapa tena anatumika kutaka kumwondoa Mbatia madarakani??, vitu vikirudiwa rudiwa sana basi vinaonesha kuwa Zitto anaweza asiwe mtu mzuri nki maanisha ni kigeugeu na si dhani kama mtu kigeugeu anaeweza kuwa na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi zaida ya personal gain
 
Inawezekana magamba yametengeneza habari hii kupunguza nguvu ya zitto na kafulila

Zitto mwenyewe ni gamba, hoivi hamkuona mawasiliano ya zitto na Mkurugenzi wa usalama wa taifa na Rostam??? au wengi wenu huwa hamsomi magazeti? Toka kipindi kile nilimtoa kwenye wapigania ukombozi na kuona ni msaliti nambari moja. dogo anapenda sana madaraka na ujiko yule na ndo mzimu unaomfuatilia.
 
Jaman jamani kwani ZITO atakuwa katimiza miaka 40? Acheni unaa
 
Hiki chama hakieleweki mara tatizo ni M/kiti leo ZITTO mara Kafulila
asingekuwa Kafulila wangepata hata huo ushindi wanao uona leo wa 4mps. Tatizo ni nini ? kama hawalioni wafanye uchaguzi mpya chama kisukwe upya kuanzia juu hadi chini

Mkuu,
Hapo kwenye ushindi wa wabunge Kafulila hakuwa na mchango wowote. Yeye mwenyewe alibebwa na Zito na serikali. Umewahi kujiuliza kwa nini wabunge wao wote wametoka Kigoma? Siikubali NCCR, lakini mwenendo wa Zitto na Kafulila ni hatari kwa mustakabali wa maisha ya watanzania. Mark my words.
 
Huyo Zitto vipi?? Mara wanasema anatumiwa na CCM sasa hapa tena anatumika kutaka kumwondoa Mbatia madarakani??, vitu vikirudiwa rudiwa sana basi vinaonesha kuwa Zitto anaweza asiwe mtu mzuri nki maanisha ni kigeugeu na si dhani kama mtu kigeugeu anaeweza kuwa na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi zaida ya personal gain
Mabosi zake ndani ya ccm wapo taabani (Rostam) kwa hiyo Zitto hana wafadhili wa CCM
 
Ben!
Hapo re:si kwa upinzani tu sema hata CCM
tunataka mbatia aondolewa kwa kushindwa kuendesha chama na si kwa mizengwe ya kutoa mwanya kwa flani flani kugombea 2015.
Challenges wanazokutana nazo wenyeviti ziwe na nia ya kujenga na sii watu (vijana) wenye ajenda za siri ya kutwaa madaraka ndani ya
ya chama ili watekeleze maagizo ya WALE WALIO NJEE YA CHAMA.

Dada Marytina,

Kuna wanasiasa wanaopenda kuficha udhaifu wao kwa kufanya accusations.Naelewa sana aina ya siasa zetu za upinzani,naelewa tunakoelekea na tusiporekebisha mentality zetu hatma yetu inajua itakuwa wapi

Ninachojaribu kusizitiza ni kwamba tuache demokrasia ichukue mkondo wake.Tupambanishe ajenda,kwa kawaida utekelezaji wa democracy ni uchaguzi wa hoja dhidi ya hoja.Kama ndani ya upinzani kuna vijana wenye hoja na ajenda za kusogeza vyama vyao mbele zaidi basi waache wanachama waamue at large.Mbinu zozote na ghiliba za kuzuia mawazo mbadala zitatupeleka pabaya na kila siku ndani ya upinzani tutakuwa tunapanda mbegu za uasi kwenye vyama vyetu.To be a worthy politician, you must learn to love people no matter the challenges.Kama Kafuliala anataka kugombea tatizo ni nini hasa? Tuache kujiita wana-demokrasia huku tukiogopa hoja na sanduku la kura.Vinginevyo tutaishia kuwa kama CCM inayojiita chama vcha mapinduzi lakini inaogopa mawazo ya ki-uanamapinduzi.Bunch of jokers! ! !

Uenyekiti au uongozi wowote ndani ya vyama na serikali si haki ya kuzaliwa ya anayeshikilia.Opposition camp need strong agenda capable of restoring the tenets of democracy hitherto destroyed by the CCM in its quest to perpetuate itself in power by any means necessary and it is my desire that it must be devoid of any self serving agenda.

Watanzania tusipokuwa makini na wanasiasa wa aina hii ni kwamba they will polarize the polity and leave us in the doldrums

Gazeti la mwanahalisi lina habari nzito tena za kushtusha.

Mbunge wa Kasulu mjini Moses Machali amemshutumu vikali David Kafulila kwamba anatumiwa na Naibu Katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe kukivuruga chama hicho.

Mbunge huyo wa Kasulu anadai lengo kubwa la Kafulila ni kumwondoa mwenyekiti wa chama hicho James Mbatia ili yeye awe mwenyekiti.

Pili Machali amedai kwamba baada ya Kafulila kuwa mwenyekiti atamkaribisha Naibu Katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe ili awe mgombea Urais kupitia NCCR.

Moses machali ameendelea kudai kuwa baada ya mpango huo kukamilika watatumia mbinu mbalimbali kuivuruga Chadema kwa kuhama na kundi kubwa la wanachama wake.

Mbunge huyo ameendelea kudai kuwa kamwe hatakubali mbinu hiyo kwani Zitto na Kafulila wanatumika kuua upinzani.

Alipoulizwa kwanini watake kumuondoa Mbatia kwanza amesema hiyo ni kutokana na sababu kwamba kamwe Mbatia hatamkubalia Zitto kugombea urais kupitia NCCR.

Source: MwanaHalisi

Moja, sina mpango wowote wa kuhama CHADEMA. Kila siku nasema nimekuwa mwanachama wa chama kimoja tu cha siasa maisha yangu yote, nimekuwa mwanachama wa CHADEMA toka nikiwa na umri wa miaka 16 na namwomba Mungu kila siku nife nikiwa ndani ya chama hiki. Najua kuna watu wanapenda sana nitoke CHADEMA kwa maslahi yao ya kisiasa wakiniona mimi ni tishio kwao. Napenda kuwaambia nimetumia nguvu nyingi sana kujenga chama hiki na sitahama. Waache kabisa kunizushia na kunijengea chuki mbele ya umma.

Pili, sihusikikwa lolote lile na yanayoendelea ndani ya NCCR na wala sina interest ya kuyajua. Mbunge wa Kasulu mjini ambaye alikuwa mwanachadema na kushinda Ubunge kwa sababu ya kutumia jina langu huko kwao Kasulu anaropoka (kama kweli kasema maneno hayo) na nitakapotoka Hospitali nitamtaka anithbitishie anayoyasema. Vijana wanapojiingiza kwenye siasa za uwongo kama wazee wao ni hatari sana kwa nchi. Sihitaji kwenda NCCR ili kugombea Urais kwani chama changu ni kikubwa zaidi na kitanipa Urais kwa urahisi kuliko NCCR ambacho ni chama kisicho na rekodi yeyote ya kupigania maslahi ya nchi hata wakati kilipokuwa chama kikuu cha upinzani nchini. Katiba hainiruhusu kugombea Urais mwaka 2015 na hata kama ikibadilishwa na kuniruhusu kugombea kwangu kutategemea sana mwafaka ndani ya chama changu. Anayedhani kwamba nia yangu ya kuwa Rais wa Tanzania ni ya kufa na kupona hamjui Zitto. Sifanyi siasa za kufa na kupona. Ninao uwezo wa kuwa Rais bora maana nina ajenda na ninatoka chama bora. Lakini pia nipo tayari kufanya kazi yeyote ile ambayo chama changu kitanipa.

Zittophobics wanaishi kwa siasa za kumwaza Zitto na wamo kwenye vyama vyote vya siasa hapa nchini. Ninafanya kazi zangu za Ubunge kwa ufanisi na mafanikio makubwa sana, ninafanya kazi zangu za Uenyekiti wa Kamati ya Mashirika ya Umma kwa umakini mkubwa na ninafanya kazi zangu za Uwaziri Kivuli wa fedha katika hali ya kuridhisha sana. Maadui zangu wa kisiasa wanatamani nianguke. Kwa uwezo wa Mungu sitaanguka.

Tatu, Gazeti la Mwanahalisi limekuwa ni gazeti linalonisakama sana kila kukicha lina ajenda yake. Gazeti ambalo limepoteza mvuto wake kwa jamii halinishughulishi. Hata juzi Mzee Samweli Sitta amelishutumu kwa kununuliwa na mafisadi na kutumiwa. Niseme nini zaidi kuhusu gazeti hili linaloongozwa na mtu ambaye hata hajamaliza darasa la saba. Mwanahalisi wanajua kwamba wakiandika habari yenye jina langu mauzo yao yanakua makubwa. Hili ni gazeti mufilisi ambalo kazi yake ni kutumiwa tu.

Nne, WanaJF mnasema hili ni jukwaa ni Great Thinkers. Great thinkers huwa hawadaki habari na kuziamini na kuanza kutoa maoni bila kwanza kupata uhakika wa habari hizo.

Nasikitika kwamba watu wenye ugonjwa wa Zittophobiasis ni wengi sana humu. Ninawashauri kwamba jitahidini muwe objective na muone upande wa pili wa shilingi.

Habari hii ya Mwanahalisi ni habari ya kijinga sana kujaribu tu kunihusisha na vurugu za chama ambacho mimi si mwanachama wake. Kafulila na mimi ni marafiki na ni wabunge wa Kigoma. Lakini Kafulila na mimi hatuongei mambo ya vyama vyetu hata kidogo na yeye anajua kwamba sina interest na NCCR Mageuzi.

WanaJF msicheze ngoma isiyo yenu.
 
CDM ni zaidi ya K.Zitto chijani,ila nabaki na swali kwa machali anaposema yuko tayari kumkaribisha Zitto ili 2015 agombee urais alafu hapohapo anawataja Kafulila na Zitto kuvihujumu vyama vya upinzani ana maanisha nini?kwamba sasa kama ndivyo NCCR itapona kwa Zitto akiingia kwao
 
Sina hakika na Uraisi, ila Zitto angependa sana kupractise what he believes, kuhusu CCM kutumia hapo kuvuruga upinzani inawezekana ila "mfadhili" anaweza akatoweka so itabidi afikirie upya.
 
Huyo Zitto vipi?? Mara wanasema anatumiwa na CCM sasa hapa tena anatumika kutaka kumwondoa Mbatia madarakani??, vitu vikirudiwa rudiwa sana basi vinaonesha kuwa Zitto anaweza asiwe mtu mzuri nki maanisha ni kigeugeu na si dhani kama mtu kigeugeu anaeweza kuwa na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi zaida ya personal gain

Mwita hii ni propaganda maalumu inafanywa kwa malengo maalumu. Sijawahi kutumika na CCM maisha yangu yote na CCM wanajua hivyo. Lakini ukitaka kuua nyota ya mwanasiasa yeyote wa upinzani ni kusema anatumika. Hata marehemu Chacha Wangwe walisema anatumika na CCM ili kumvunjia heshima wala hapakuwa na ushahidi wowote wa hivyo. Mpaka anakufa alikufa na kinyongo hiki. CCM hawawezi hata siku moja kunitumia. Nimekuwa ninafanya kazi zangu Bungeni kwa umahiri mkubwa sana and yet maadui zangu wa kisiasa wanasema haya mambo ya kipuuzi kabisa.

Ni juu yako unaamini hizi propaganda au unazipuuza. Lengo ni kunivunjia heshima mbele ya jamii. Kwa muda mrefu Mwanahalisi wamekosa cha kuandika juu yangu na wameamua kutumia mgogoro wa NCCR kunihusisha ili tu kuendeleza propaganza zao chafu dhidi yangu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom