Gwallo
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 3,712
- 5,325
Good news..Kwa mtindo huu kuiondoa serikali ya CCM madarakani itakuwa ni ndoto!
Hii ni habari njema kwa magamba, lazima ushabikie ili mambo yako yaendelee kuwa sawa.
Good news..Kwa mtindo huu kuiondoa serikali ya CCM madarakani itakuwa ni ndoto!
1.Kama Zitto ni tatizo na sio uongozi wenu na siasa za kiujanjaujanja iweje kuondoka kwa Zitto Chadema kuweze kuwavurugaKama Zitto ni tatizo na sio uongozi wenu na siasa za kiujanjaujanja iweje kuondoka kwa Zitto Chadema kuweze kuwavuruga na sio kuwapa nafasi ya kujijenga. Lakini pia iweje Kiongozi wa CCM anapokataa kunyamazishwa eti kwa maslahi ya chama iwe haramu lakini anapotokea kiongozi wa Chadema asiyekubali kunyamazishwa ama kunyamazia mambo ya hovyohovyo iwe haramu (Double standard zisizoweza kumsaidia mtanzania kamwe)
Hivi ni vipi Zitto akataka huo urais at any cost na sio Freeman Mbowe aliyetayari kupanga na kutekeleza mikakati haramu dhidi ya washindani wake kama Dr Slaa na Zitto? Hivi ni nani aliyesikika akilalama kuwa wale watu watatu waliokufa kule Arusha hawakutosha ili kujenga chuki zaidi kwa CCM na Chadema ifaidike kisiasa? Hivi ni nani anayeendeleza siasa za majungu katiika magazeti yenu (zinazokomaza makundi ndani ya Chadema) eti katika kuhakikisha kuwa anammaliza za Zitto kwa kosa la kuthubutu kushindana naye katika nafasi za uongozi Uenyekiti na baadaye Uongozi wa Upinzani bungeni ambao kwake yeye ni "platform" ya kujijenga kwa Watanzania ili kama asemavyo" come to 2015 awe Presidential Material"? Hivi ni nani aliyekuwa mstari wa mbele kuhonga viongozi wa Chadema majimboni ili wasabotage kampeni za wagombea wenu ambao anaona wao ni tishio kwa nafasi yake ya Uenyekiti na safari yake ya Ugombea Urais 2015
Ulichokiandika hapa kinathibitisha ukilaza wako katika kupambana na hoja na vizingiti vya kisiasa vinavyokumba ndoto yenu ya siasa za madaraka...Lakini pia weweukiwa kama kiongozi wa Chadema unathibitisha hisia halisi za kundi la wahafidhina ndani ya chama chenu katika mantiki nzima ya maslahi, siasa na chuki za kidini...Hivi ni nani aliyekimbilia kwa Maaskofu akiwaahidi kuwa anenda kujiendeleza kielimu ili baadae aweze kugombea urais na hata alipotishiwa kung'olewa kidemokrasia katika nafasi yake ya uenyekiti akatumia hoja ya kuwa Maaskofu hawatakuwa tayari kuona vyama vyote vikuu vinaongozwa na Waislamu
Kweli ni kilaza. Unajifaragua kama mwanasiasa wakati unashindwa hata kujua tofauti ya itikadi na sera? Ndio maana mnambiwa muende shule na msome masuala ya siasa za dunia yetu. Siasa za kujifunzia katika magazeti ya udaku wa kijamii na kisiasa kama Mwanahalisi ni hatari kwa Tanzania ijayo.
Nijuavyo katika tafiti zote zilizofanyika umaarufu wa Zitto umekuwa ukipanda na sio vinginevyo. Chuki na hisia zenu kuwa mnafanikiwa kupunguza umaarufu wa Zitto ndio zinaendeleza kuwadumaza huku mwenzenu anazidi kujitanua sio tu nchi lakini hata katika medani za siasa za kimataifa. Ninyi bakini na pety and parochial politics mkidhani watanzania hawa walioamka na kung'amua uvundo wa CCM wataendelea kuamini katika ugoigoi wa kifikira, nia za chuki na uozo wa Chadema....
Hili dua lenu la kuku kuwa Zitto atahamia CCM kamwe haliwezi kutimia. Kamwe Zitto hatahamia CCM.
Halafu angalia fikira za "wakombozi" wanaotuuzia chai za "DEMOKRASIA" wakati bado mnashindwa kujiondoa katika na utando wa siasa za kihafidhina za kuwapa Umungu viongozi wetu. Eti hakuna mtu wa kulinganishwa na Dr Slaa (ofcourse yapo ya Dr Slaa ambayo hayawezi kulinganishwa na mtu mwengine lakini sio uwezo wa kuongoza nchi na kuleta mabadiliko ya kweli na yaliyo makini yenye tija kwa watanzania). Udaktari wa Theolojia haumtoshi sasa mnaanza kumpa Umungu. Halafu baadae mtakuja lalamika viongozi haohao mnaowapa umungu wanavyogeuka kuwa miungu watu.....
Zitto amekurupuka bila ya hata kujua ni nini kilichoandikwa kwenye magazeti. Eti huyu ndio rais mnae mtegemea, Kiukweli nilikua namuona ni mwanasiasa makini ila kwa hili la kumsambulia mwenyekiti wake na mwekahazina wa chama chake amejishusha kwangu mno.Kwako mhe Zitto. Pole na kuugua.
Sisi watanzania hatujambo! Nimeshitushwa na jinsi ulivyo na hasira za ajabu, kweli mtu anaweza onyesha uhalisia wake hata anapoaddress vitu.
Mimi nina gazeti la Tanzania daima na lina kichwa cha habari: Mbatia, Kafulila Vitani, mwandishi Betty kangonga. Habari inahusu mgogoro unaofukuta ndani ya NCCR mageuzi.
Hata hivyo habari inaongelea zaidi jinsi Machalia anavyomsema Kafulila kuwa anavuruga chama. Hakuna hata sentensi iliyokutaja wala kufumbbia mana hata huyo Mbatia naye hajatajwa kugombana ila huyu mbunge akishambulia. Usiwe mwepesi wa kupanic Kaka, utatengeneza sumu nyingi mwilini na kuongeza uadui bila sababu, mwisho watu watakuchoka na kukushusha.
Huyo Mbowe kama una ugomvi wenu ndani ya chama, usitake watu tujue wazi mana nashangaa umemtaja bila kujua habari inaongelea nini, kisa mchangiaji mmoja kakupotosha. Tulia kaka na uugue pole, kuwa mpole na watu watakuelewa. Umri unavyoenda hekima ikutawale, na hasira uzishinde. Sijafurahishwa na ww kumshambulia kiongozi mwenzako kwenye mtandao wa kijamii, while yy hajasema chochote juu yako katika hilo unalomshambulia.
Nakusihi utulie, omba wakuwekee nakala za hayo magazeti na ukirudi yasome kabla ya kupeleka malalamiko yako.
Nakutakia afya njema.
Kuna ukweli asilimia 95 kwenye hii habari, zitto na kafulila wanatumika!
Great thinkers wa JF mnanishangaza, wakati Zitto anatoa mawazo ya kujenga nchi yetu https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/190596-muswada-wa-katiba-una-matatizo-mengi-zitto.html , great thinkers wanatumia nguvu nyingi zaidi kujadili upuuzi wa mwanahalisi. Licha ya ugonjwa Zitto ameamua kukaa na kuweka mawazo yake kuhusu muswada nyeti wa katiba. Wengi mnaongozwa na chuki na wivu binafsi.
Kwahiyo unafikiri kumjadili yeye ndio mnaisaidia nchi kuendelea? Sijaona point ya maana iliyotolewa juu ya matatizo unayodai anayo, sanasana naona watu wanaongozwa na chuki na wivu tu.Ukiona hivyo jua yeye ni tatizo kama ilivyo katiba. Sasa ni ngumu sana kwa gt kujadili tatizo lililoletwa na tatizo, itakuwa unajadili tatizo kuongeza tatizo na si kuondoa tatizo. Kwa maneno rahisi watu wanamuelewa na wanakosa imani naye. Sasa kuwalazimisha watu wajadili hoja iliyoletwa na zitto kama hawamuamini hii nayo ni tatizo katika haya matatizo niliyo ya taja.
Ni kweli kabisa mkuu siasa za kungalia sura ndizo zimetufikisha hapa tulipo Watanganyika tubadilike jamaniUmeongelea hisia zako, lakini ukweli Zitto ni mtata. Kama CHADEMA ingekuwa kama CCM ya leo ingesambarataratika kwani Zitto amewahi kukituhumu chama kwa udini na ukabila. Kama hiyo haitoshi mara baada ya uchaguzi mkuu 2010 Zitto alitangaza kugombea urais 2015 kinyume na taratibu za chama, kama si hekima za uongozi wa CDM na mama mzazi wa zito tusingefika hapa tulipo. Hii yote ni kwa sababu anaamini ana wapenzi wengi.
Watanzania tubadilike tuache mapenzi ya mtu kwenye siasa tuangalie sera za chama. Tujifunze KWA JK WENGI WALIMPENDA KWA STAILI KAMA HII YA ZITTO LAKINI NAAMINI LEO JK HATA UKIMPA UKUU WA SHULE YA SEKONDARI HATA FANYA VIZURI
NOOO, baada kafulila kuondoka CDM ameongeza nguvu kubwa NCCR jiulize
- kwa nini awali hawakuwa na wabunge even 1
- kwa nini wote 4mps wanatokea Kigoma
Mkuu, wewe ndie unayejaribu kuilaani NCCR, bahati mbaya kwako hailaaniki, wamejitahidi wengi kabla yako kukiua kabisa hiki chama, hakifi, wanaweka mapandikizi yao yanafichulika.Mimi sioni tofauti kati ya Mbatia na Kafulila hawa wote kwa nyakati tofauti wametumiwa na CCM kuhujumu upinzani. Na pili naichukulia NCCR kama chama chenye laana kutokana na usaliti walifanya kwa watanzania wakati wa uongozi wa Mrema. Sitarajii hata aende nani huko kama watarudi ktk ramani ya siasa za kitaifa.