kwa kweli hapa nimeamini jamaa yetu una chuki binafsi na zitto kabwe, maana hiyo hoja hapo juu wala haikubaliani na conclusion yako, halafu kwa siasa za aina hii ndio mnajaribu kutaka nchi? hapana, hatuwezi kushinda, maana kama wenyewe kwa wenyewe mwapigana vijembe vya masuala binafsi, vipi mtawashawishi wananchi kwamba ninyi ni wamoja?maana ndugu umekosa hoja waanza ishu za umalaya, mimi naogopa sana kashfa kama hizi maana ninavyofahamu wengi wetu si waaminifu kwenye ndoa zetu, sasa ndugu yan gu usije kuruhusu au kusababisha mlipuko wa maskendo ya watu bure hapa,
tujadili siasa na sio mambo majitaka kama haya, after all huna ushahidi wa ai na yoyote kama alikuwa na mwanamke wakati yeye kasema alikuwa na mkutano, nani hapa mwongo kama sio wewe?
ndugu spanner, mi naomba kukuuliza yafuatayo:
1)je chadema kinalea maovu?moja ya dhambi anazolalamikiwa kikwete ni kulea mawaziri/watendaji waovu,mafisadi na wezi na hachukui hatua, sasa zitto kabwe baada ya tuhuma zote hizi, chama cha chadema kimeshindwa nini kumchukulia hatua zozote za kinidhamu?je, huoni kitendo hicho cha kukaa kimya na wao wanakuwa kama CCm na JK kwa kulea watendaji wabovu? huoni kama ni busara kwa chadema sasa kumvua nyadhifa zake chadema?
kitendo cha chadema kutomchukulia hatua yoyote a)aidha haya yanayozungumzwa dhidi yake ni majungu b)viongozi wa chadema ni wazembe au c)viongozi chadema wanamuogopa zitto kabwe kwamba akifukuzwa ataathiri nguvu ya chama na kama hili ni kweli basi jibu b) linapata nguvu zaidi