Kilitime,
Tatizo hapo sio wananchi, tatizo ni hao wanaotoa hizo data ambazo hata hawawezi kutuhakikishia wamezitoa wapi.
Kujua au kuelewa analysis za uchumi sio lazima usomee uchumi. Na kwa taarifa tu siku hizi kwenye nchi nyingi za West, wanaopewa kazi kwenye mashirika ya maana yanayoshughulikia na mambo ya investments sio wale waliosomea uchumi na badala yake ni wasomi wa hesabu. Ukisikia hao watu wa city wanaopata malaki, wengi wao ni universities wamesomea maths.
Kitendawili hapa ni hao wanaojaribu kutulisha data ambazo haziendani na realities huko wilayani.
Kwa maoni yangu sioni sababu zozote za kugombana kati ya hawa watu wawili hasa ukitilia maanani mafanikio makubwa katika miezi ya karibuni ya kuitetemsha CCM kuhusiana na mikataba ya madini na kashfa ya BOT.
CCM wameshagundua kwamba wanaweza kabisa kumtumia huyu Wangwe ili kukisambaratisha CHADEMA. Viongozi wa juu wa CHADEMA wanatakiwa walishughulikie sakata hili mapema kwa kumpa onyo kali Wangwe au hata kumsimamisha uanachama kwa miezi sita vinginevyo wanakichimbia kaburi chama chao.
Kilitime,
Tatizo hapo sio wananchi, tatizo ni hao wanaotoa hizo data ambazo hata hawawezi kutuhakikishia wamezitoa wapi.
Kujua au kuelewa analysis za uchumi sio lazima usomee uchumi. Na kwa taarifa tu siku hizi kwenye nchi nyingi za West, wanaopewa kazi kwenye mashirika ya maana yanayoshughulikia na mambo ya investments sio wale waliosomea uchumi na badala yake ni wasomi wa hesabu. Ukisikia hao watu wa city wanaopata malaki, wengi wao ni universities wamesomea maths.
Kitendawili hapa ni hao wanaojaribu kutulisha data ambazo haziendani na realities huko wilayani.
Chama kinatakiwa kiwe na mshikamano. Katika chama chochote kile kuna kuwa na tofauti mbali mbali za viongozi wa juu wa chama ambazo ni vizuri kama zitamalizwa ndani ya chama badala ya kulumbana katika vyombo vya habari na kuwapa faida vyama vingine. Mafanikio mliyoyapata katika siku za karibuni yanatiwa dosari kubwa sana na malumbano haya ya kwenye vyombo vya habari na ndio sababu Mzee Ndesamburo anawatahadharisha kwamba yanaweza kabisa kusambaratisha chama.
Katika malumbano haya kuna baadhi ya viongozi na hata wanachama watakuwa upande wa Wangwe na wengine upande wa Zitto, hapo mgawanyiko huanza kujitokeza na kuharibu mshikamano uliokuwepo na badala ya kuelekeza nguvu zenu kupambana na ufisadi unaofanywa na CCM mtakuwa mnalumbana wenyewe kwa wenyewe na kuharibu credibility mliyojijengea kwa Watanzania mbali mbali hata wale wasio wanachama wa CHADEMA.
Haya ni mazoea tu kaka yaliyojengeka katika mfumo wa CCM. Haiwezekani all the time mkubaliane mambo kwa sababu hata kama sisi sote ni wanachama wa chama kimoja hatufikiri sawa. Cha msingi hapa ni kwamba malumbano hayajengi chuki kiasi cha kushindwa kufanya kazi pamoja na ndivyo sisi chadema tulivyo. Tunalumbana ndani na nje lakini kazi tunaendelea kuchapa na tunaendelea ku-socialise vilevile katika nyama choma na kwingineko. Hatutaki utumwa wa kuvimbia ndani kwa ndani kama ilivyo kwa CCM, watu wanazeeka ovyo kwa sababu ya kumeza mawazo na mahasira badala ya kuyatoa. Ndio maana unaona hata hapa katika JF wanachama na viongozi wengi wa chadema wanaingia hata na majina yao halisi, yote hii ni kwa sababu hiki ni chama cha watu huru, wapende demokrasia na maendeleo. We always extensively brainstorm and debate an issue bofore pressenting it to formal party structures. That is us. Usiwe na wasiwasi, chama chenu kipo makini, hakitawaangusha-kiungeni mkono tujenge demokrasia na nchi.
Hilo la kuwaona viongozi wa juu wa CHADEMA wanakuja hapa JF na kujadiliana na Watanzania mbali mbali katika kila kona ya dunia mimi linanigusa sana na nawapeni hongera za hali ya juu kwa hili. Sijawahi kumuona W. Slaa hapa ukumbini kama hajawahi kufika naomba mumhamasishe ili afanye hivyo, maana inatia moyo kuona viongozi ambao wako tayari kutumia muda wao kujadiliana na Watanzania wengine bila woga.
Hilo la kuwaona viongozi wa juu wa CHADEMA wanakuja hapa JF na kujadiliana na Watanzania mbali mbali katika kila kona ya dunia mimi linanigusa sana na nawapeni hongera za hali ya juu kwa hili. Sijawahi kumuona W. Slaa hapa ukumbini kama hajawahi kufika naomba mumhamasishe ili afanye hivyo, maana inatia moyo kuona viongozi ambao wako tayari kutumia muda wao kujadiliana na Watanzania wengine bila woga kuhusiana na mambo mmbali mbali ndani ya nchi yetu.
Kama unaamini hayo malumbano katika vyombo vya habari kati ya Zitto na Wangwe hayataleta mmomonyoko ndani ya CHADEMA basi na iwe hivyo, na mimi nawatakia kila la heri katika kupambana na mafisadi wanaotumia nyadhifa zao wanazopewa na Watanzania kujitajirisha, kusaini mikataba mibovu isiyo na maslahi kwa Watanzania na kujinyakulia makampuni ya Tanzania katika mazingira ya kutatanisha.
Mungu ibariki Tanzania
Nakwambia tuna kazi. Sasa huyu kijana Killtime tunayemwania sana hii sijui katoa wapi tena, nimewauliza ni wapi mimi nimesema waseme uongo hawataki kwa sababu hakuna, ila wanapindisha mambo ili kupotosha hoja yangu. Ngoja tukubali kutokubaliana!
Mtanzania,
Bila kuchukua mamlaka ya Zitto,,, na kwa kuwa wewe umesoma Hisabati na Statistics,,, Nadhani utanielewa...
(A) Ukitaka kulinganisha kitu chochote kile unatakiwa uwe na reference point...
(B) Uchumi kukua kwa say 2%, 3%, 7% or x% maana yake ni ukilingalisha na mwaka uliopita,,, hii ina maada gani pato la mwaka jana kama ni 100 mwaka huu limekua kwa x% maana yake pato la mwaka huu ni [(100 + (100 *x%)]
(C)Catch 22; Do not compare the percentages!!! kwa sababu hizo percentage ni za pato/mapato tofauti, na hili ndilo linakukuta wewe na wengine... 10% ya 1996 inaweza kuwa ndogo sana kulinganisha 4% ya Mwaka 2008!
kama percentage ndiyo ingekuwa kigezo uchumi wa UK unakua kwa 2-3% kwa hiyo tungesema wao uchumi wao haukui... this is not the case.
(D)Ungeelewa zaidi kama ungekuwa unafuatilia watani wetu, kipindi cha Moi kule Kenya kuna wakati waliregister close to 0% maana yake pato la mwaka ulipita na la mwaka husika... ni hilo hilo... Leo hii kwa nchi kama ya yetu, kwa mfano, tunatakiwa ili tuwakimbilie watani wetu wao uchumi ukikua kwa 5% sisi tunatakiwa ukue kwa 10 au 12%. kwa sababu mapato yetu ni madogo kulinganisha na wao...
Huu ndio uelewa wangu!!! nachangia tu.
Mchumi mzuri ni yule mwenye first degree ya Maths ama Engineering na anapokwenda kufanya MA/MSc anaingia kwenye fani ya uchumi na anaunga mpaka PhD. Wasomi wa zama za akina Ngasongwa (sijui kama ni mchumi) hawa-fit tena kwenye ulimwengu wa wachumi wa zama hizi. Ndiyo maana US wanataka mtu anaekwenda kufanya graduate program ya uchumi lazima awe na very strong background in maths!
Keil,
Hivi bado unaweza kuingia BA Economics mlimani hata kama hujui maths?
Sidhani; hata hivyo msivi-exaggerate sana umuhimu wa maths, teeh teeh heee!
Kuna haja ya kuvijua vigezo vinavyotumika katika kupima ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Mimi naamini kabisa kwamba ama ukusanyaji wake una kasoro kubwa sana au computations zake zina walakini. Haiwezekani uchumi wa nchi ukue kwa 5% au zaidi kwa miaka karibu 10 mfululizo na kusiwe na ongezeko la ajira na kipato.