Kabwe Vs. Wangwe - kisa cha mafahali wawili?

Habari, habari, habari na habari zaidi kuhusu mifarakano yenu Mh. Zitto! Nimeamua kuibandika hapa ilihali bado upo hapa unaweka msimamo wako sawa kwa WanaJF...
Today, 11:19 AM: Currently Active Users Viewing This Thread: 15 (9 members and 6 guests)
SteveD, jamco_za, mfwatiliaji, kilitime, Zitto, MADELA WA- MADILU, Mama Lao, ibambasi, Adolf

Source link: Mwananchi.


SteveD.
 


Ni kampuni gani ya madini iimeuza madini yake nje ika declare kwamba imeuza kwa hasara?

Au usemapo hasara una maana gani?

Serikali huchukua % ya kilichozarishwa kutokana na mkataba sasa kama mkataba unampa mwekezaji ulaji mkubwa, hatuwezi sema tumepata hasara kama taifa kwa vile sehemu kubwa ya mauzo kachukua mwekezaji.
Swali la kujiuliza ni nani katika kundi la Viongozi wenye vichwa vilivyojaa mvi kaingia mkataba wa kujitafuna?

Au tuseme Mashavu makubwa,Mvi na Mashati ya Kijani siku hizi ni kipimo cha Ujinga na Upumbavu usiobebeka?


Uangaliapo pato la taifa unaangalia kilichouzwa toka ndani ya nchi.

Mgawanyo wa nani kapata mgao mkubwa nani kidogo na nani kapata nunge hilo ndo tatizo ambalo kijana wetu Zitto amelivalia njuga na mshipi kiunoni mpka kieleweke.

Fact kwamba mauzo ya bidhaa zetu nje yameongezeka ipo pale pale.
Fact kwamba sisi Watanzania hatufaidiki na ongezeko la mauzo ya bidha za Tanzania nje ya nchi nayo iko pale pale.
Mpka sasa sielewi Kinacho bishwa na kupingwa kwa nguvu zote.

Mimi siyo mchumi, lakini najiuliza ni vipi kama serikali haikuhusika moja kwa moja kuchimba dhahabu neno hasara linatumika pale serikali ipatapo mapato kidogo wakati mauzo yanaonyesha wazi wachimbaji wameuza dhahabu ya thamani kubwa?
 

Najua ungependa majibu yatoke kwa Zitto moja kwa moja, lakini naomba pia nitumie uhuru wangu kukijibu mengine mepesi tu!

Kwanza tutakuwa watu wa ajabu sana, kama hatutakubali kwamba ukame na tatizo la umeme 2005/2006 limechangia kwa kiasi kikubwa kurudisha uchumi kutoka kwenye 7.3% kurudi kwenye 6.2%, lakini kwa wale ambao wamesahau watakumbushwa na takwimu ambazo zinaonyesha kwamba uchumi kwa mwaka 2007/8 utakuwa kwa 7.2 to 7.3%

Je, Kasi yetu ya kukua kwa uchumi unailinganishaje na nchi nyingine za Afrika? Je, inaridhisha?
Ndiyo na Hapana, ndio in number,,, hapana kwa source ya ukuaji, Zitto amesema ingekuwa kilimo ndio kinachangia tungekuwa poa.


Je, kwa rasilimali na fursa tulizonazo- je, unaridhishwa na kiasi chetu cha kukua kwa uchumi kiasi cha kutembea kifua mbele kujigamba kwa uchumi unakuwa?
Zitto, wabunge, Rais, Report mbalimbali zinasema ili kuwa kifuambele tunahitaji uchumi ukue kwa 10% kwa miaka mingi kidogo!!! say 10.

je, hakuna haja ya kuweka tahadhari kwamba uchumi wetu unakuwa katika kiwango kisichoridhisha na katika mfumo ambao Air Uchumi inapaa huku abiria wakiwa wanashangaa?
Hili liko wazi!!!

Je, ni kwa kiasi gani uchumi wetu unanufaisha sisi wanawake?

Asha

Sijui
 
Hizi ndio taarifa za ukuaji wa kila sekta mwaka 2006 kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Uchumi June, 2006.
Ukuaji wa Pato la Taifa (%) mpangilio kutokana na kasi ya ukuaji

Sekta ya uchumi 2005 2006
Uchimbaji madini 15.7 16.4
Ujenzi 10.3 10.0
Bidhaa za Viwandani 9.0 8.6
Biashara na Mahoteli 8.2 8.4
Mawasiliano na Uchukuzi 6.4 7.5
Fedha na Huduma za Biashara5.3 5.5
Uendeshaji Serikali 5.1 5.1
Kilimo 5.1 4.1
Umeme na Maji 5.1 -1.8
Pato la Taifa 6.7 6.2
 

Umesaidia sana, hapa JF wengi wanabwabwanya kwenye hili!!! mimi sio mchumi lakini nilielewa hivi na ndio maana niliamini ulisema ukweli!!!

Sasa baada ya maelezo ya Jumla ya Zitto... swali nawauliza kwa wanaJF, Zitto au Wangwe nani kadanganya Watanzania?

Je ni haki kudanganya Umma wa Watanzania kwa kile kinachoitwa uko Upinzani, au ili usionekane unadandia train ya CCM, je si CHADEMA ndio yenye msimamo wa kati wa kusema mambo kwa ukweli kwa kuzingatia maslahi ya taifa mbele ?
 
Mheshimiwa Zitto,

Heshima mbele mkuu, darasa linatosha mkuu wewe kaendelee na kazi za taifa hasa za kamati ya madini, darasa ulilotoa ni kali sana na linatosha, sasa ngoja tutafakari kwanza,

However, mkuu Mnyika, tungekuomba umlete Wangwe hapa ili atoe rebuttal tujue mchelle na pumba zilipo, hatuhitaji anymore political spins hapa, tumechoka nazo, huuu mfano wako Zitto, ni wa kuigwa na ndio kumkoma kwenyewe nyani mpaka Giladi!

Heshima mbele mkuu Zitto, na kazi njema na ahsante kwa mambo hadharani.
 
Nakuunga mkono Mzee ES na maombi yako kwa Chacha Wangwe kuja hapa . Au niwape namba apigiwe moja kwa moja ?
 
Unajua mkuu Zitto maelezo yako ni sawa kabisa from an academic point of view. Unfortunately, people view whatever you say (and rightly so) from a political perspective rather than academic. Sasa kwa maelezo yaliyopo kwenye uhuru ni wazi kwamba maelezo yako yalikuwa yanaijengea uhalali serikali ya JK. Na kwa kufanya hivyo unauacha upinzani na hasa chadema in a very vulnerable and delicate position and people like Chacha have a right to be upset. Mimi binafsi siamini kwamba ni kazi ya kiongozi wa upinzani kuelezea mafanikio ya kukua kwa uchumi, kuna watu chungu nzima wameajiriwa kufanya hiyo kazi ambao wanalipwa kwa hela za walipa kodi.

Nafikiri sasa inabidi mhe Zitto uwe makini unapoalikwa kutoa mada. Inabidi ujiulize umealikwa as an academic or a politician. Ninaamini watu wengi nchini kwa sasa wanakujua as a politician rather than an academic. Na kwa hivyo wanapokualika wanakualika ili kutaka kujua na kusikia the other side of the coin. Wakitaka kusikia statistics za kukua kwa uchumi watawaalika wanauchumi wa serikali ambao wamejaa tele. Your role as an opposition, I think, is to give alternative remedial policies pale ambapo hapaendi sawa ambapo kupo tele. I maybe wrong, lakini naamini hata ingekuwa US, UK au nchi ingine ambayo wamepiga hatua sana kidemokrasia, kiongozi wa upinzani akitoa maelezo yanayoelekea kuisifia serikali iliyopo madarakani lazima azue utata ndani na nje ya chama chake. Mimi natarajia kiongozi wa upinzani mahiri kama wewe atatumia kila nafasi anayoipata kujaribu kuujenga upinzani kwa kauli na matendo yake na in a way to discredit the competitor, in this case CCM. Kutoa kauli za kuijenga serikali na chama tawala ni kuwachanganya wananchi ambao wameanza kupata matumaini na upinzani na kuona chama kinachotawala kimewaangusha. Sauti yako sasa hivi ni kubwa mno inayosikika kila kona ya nchi tena hata nje ya nchi. Sasa jaribu kuwa makini na kauli ambazo zitawahalalisha CCM kuendelea kutawala, hiyo waachie akina Akwilombe na Tambwe.
 

Kilitime

Umekiri mwenyewe kwa takwimu zako baba kwamba ari, nguvu na kasi ya kukua kwa uchumi imeshushwa na Kikwete katika kipindi kifupi cha utawala wake. Umeleta kisingizio cha ukame, kwani sisi wenyewe ndio tulipata ukame eneo lote hili la Afrika Mashariki? Umeleta kisingizio cha umeme- hili nalo lisingekuwa tatizo kama wasanii wa Boys2Men wasingetuletea richmond wakati tukihitaji umeme wa dharura. Kwa hiyo, ni wazi kuwa katika kipindi cha miaka miwili ya mchumi Mr. Handsome Jk nguvu ya kukua kwa uchumi umepungua huko mfumuko wa bei ukiongezeka kwa kasi mpya. Zitto kama mwanasiasa makini alipaswa kusema uchumi wetu unakua katika kiwango kisichoridhisha. Alipaswa pia kuendelea kusema ukilinganisha utawala wa awamu ya Mkapa kiwango cha kasi ya ukuaji wa uchumi kimepungua. Halafu ndio angeingia kiundani kumwaga hayo matakwimu ya kisekta kuonyesha kwamba hata hizo sekta zinazokuwa kwa kasi ama zinachongia zaidi ukukuaji wa huo uchumi mkuu hazina matokeo makubwa sana katika kuboresha maisha ya wananchi waliowengi. Chacha naye aache ku-burst into sound hadharani bila kuomba ashakumu kwa Zitto na kwa wenzake.

Asha
 
Kitila,

Kwa hiyo wapinzani, kwa kutumia lugha simplest kabisa, wanaweza kuona Zitto kahongwa na kufungwa mdomo na position aliyopewa na Kikwete kwenye kamati ya madini?

Kwamaba anachukua academic figures na kuipongeza serikali wakati figures hazina impact kwa maisha ya mwananchi wa kawaida?

Is that, in very simple terms, the observation?
 

Hapa Kitila

Natofauti na na wewe 800%, Ukiwa mwanasiasa mzalendo huwezi ku-spin kwenye vitu wazi kama hivyo,,, in fact chama tawala ndio kinakumalizia kirahisi zaidi ukifanya hivyo... yapo mengi ya kuelezea kwenye issue ya Uchumi na Zitto pia ameweka wazi,,, tatizo ni kwamba hatusomi hata hizi post vizuri,

Zito alisema pamoja na uchumi kukua aliweka wazi kwamba kuna walakini akimaanisha serikali iliyoko madarakani bado ina kazi ya kufanya kuhakikisha ukuaji huo wa Uchumi unachangiwe na KILIMO,

Kuna jambo rahisi sana kama uchumi unategemea MADINI na UTALII siku majambazi yakizidi,,, UTALII utadorora, hivyo uchumi kudorora pia. Siku madini yakikataa kutoka huko yaliko,,, Uchumi utayumba..... sasa hii ndio hoja kwamba kukua kwa uchumi wetu sio sustainable na hausaidii watu wengi,,, he said forward and backward linkages... sio kusema UONGO ukidhani watu hawana AKILI,,, otherwise zitakuwa siasa zakina Mzee wa Kiraracha hapa!!!, who said siasa lazima useme UONGO....

For a wise politian s/he can remain SILENT but should not deny the TRUTH.

Kama hizi ndio mbinu za Upinzani then Mnairudisha nchi Kwenye UJIMA!!!
 
Nimewasoma wote kwa makini sana na nimejifunza mengi na haswakujua kuwawatu wengi humu wanaitakia CHADEMA mema ndio maana kila mmojaalitoa mchango wamawazo wa nini kifanyike yaani way foward.

Najifunza kuwa kuna haja ya CHADEMA na haswa viongoziwake kukaa na kuamua kuwa na msemaji na vyombo vyahabarijaponajuayupo Mhe.Erasto Tumboambaye ndiomwenezi kuna haja ya kila viongozi wanapofuatwa basi wajue wao siowasemaji wa chama na ama jukumu hilolipelekwe kwamsemaji mwenyewe.

Jambola pili ni kuwakila siku wakishasema ukiwauliza wanasemakuwa vyombo vya habari vinawalisha maneno sasa wanapaswa waandike hayowanayoyasemaili watakapolishwa maneno basi ijulikane na waweze kutoa taarifa sahihi .

Ndugu, Zitto, nakushauri ujue kuwa unafanya kazi na watu ambao uelewa wao kwenye masuala na haswa haya ya kiuchumi ni mdogo na hivyousifikiri kuwa kwa wewe kuelewa kile unachosema basi na wengine watakuelewa, la hasha.Kuna haja ya wewe binafsi kuacha kuongea na media kila wakati kwani hilini hatarisana kwakop na sio vizuri kila siku ukawa kwenye front page kwani zitakuinua na kukuangusha siku moja ,jua kuwa kujenga ni kazi inahitaji miaka ila kubomoani masaa tuu yanahitajika.

Zitto, nakushauri usiwe na haraka sana na haswa kujibu tuhuma ama shutuma zinazotolewa mbele yako shauriana na viongozi wenzako kwani wewesasa ni miongoni mwa viongozi wakuu wa chama na hivyo una wengi wanakuangalia.

Zitto , kuna siku nilikuwa naongea na mwandishimmoja akaniambia kuwa wewe unauza sana magazetina hivyo waowanatafuta sana story kutoka kwako kwani unauza , na hili nijambo la hatari sana kwako binafsi na chama kwani kuna siku litakiumiza sana chama na wewe binafsi.

Chacha Wangwe, unapaswa kujua kuwa wewe ni msaidizi wa mwenyekit wakona hivyonakushauri uwe na utamaduni wakushauriana naye kila mara , na pia ujue mipaka yakoya kiutendaji kwani nilisoma sana katiba ya CHADEMA na nikakuta kuwa wewe siomsemaji wa chama , ila msemaji ni mwenyekiti wakokwa nini usiwaambie waandishi kama wanataka msimamo waende kwa mwenyekiti?

Wangwe, jua kuwa kila kauli unayoitoa kwa sasa ni habari na habari hizozinauza magazeti, kuwamakinina kauli zako kila mara kwani unaweza ukakigawa chama chakona hililitakuwa ni hatari kwaukuaji wa taifa na wananchi wako.

Nawatakia kheriila kilammoja achunge kauli zake .

Mkuu Zitto, Ngasongwa siomjinga hata siku mojakwani naye ni mchila hayuko tayari kukiri baadhi ya mapungufu ya uchumihadharani hii inatokana na yeye kujuakuwa akifanya hivyo atakiumiza sana chama chake kisiasas, nawe jua ni mchumi na kwakauli zakoutakiumiza sana chama chakokuwa amkini sana.
 

Wala hakupaswa kusema uwongo. Alipaswa aseme ukweli tu kuwa uchumi unakuwa katika kiwango kisichoridha(hii ni kwa ujumla toka utawala wa Mwinyi mpaka leo). Alipaswa kuongezea pia kuwa katika utawala wa Kikwete kiwango cha kasi ya ukuaji wa uchumi kimepungua. Kwa ujumla tofauti na wakati wa Nyerere ukuaji wa kipindi chote cha CCM ya sasa hauna matokeo mazuri katika kuboresha maisha ya wananchi wa kawaida. Yote haya baba Zitto ameyasema, ila ameyafumbata katikati ya mapambio kwa serikali ya CCM. Hata wale wasome wa Mlimani, kuna ambao wanaandika kwa kusifia sifia kama wakina Mukandala na kuna wanaofanya uchambuzi wa kweli kama wakina Baregu, Haroub Othman nk. Kwa hiyo suala sio academia vs potiticus hapa. Ni suala la aina tu ya uandishi. Kwa mtu kama Zitto nakubaliana na Kitila kwa kweli, maandiko yake lazima yafanane na itikadi yake. Leo Issa Shivji hata ukimwalika awasilishe mada kuhusu Simba na Yanga lazima ataingiza dhana ya class struggle jamani.

Nani ana ile habari ya UHURU iliyosemwa hapo juu atuwekee?

Nani atuletee hapa Chacha mchafuzi tumsikie naye? CHADEMA sasa nahisi wanamuona Wangwe kama mwanga hivi.

Jamani msinisute, lakini Chacha akiongea anafanana kama mvuta bangi vile. Mi nilimuona bungeni akitoa rambirambi za kifo cha Lucky Dube wakati wenzake wote walikuwa wanatoa za Salome Mbatia

Asha
 


Yes Kilitime,

Nadhani tukitaka kupata mabadiliko ya kweli lazima tujifunze kuwa wakweli. Hatuihitaji upinzani wa kusema uongo kwa ajili ya kutufurahisha! we need the truth and truth only! kama tunavo sema siku zote, call a spade a spade not...

Vinginevyo tutajikuta tukipoteza maana ya vyama vya upinzani kwa mtizamo wa kwamba wao ni kupinga kila kitu!

Sasa usipotoa maelezo yake kitaalamu si atakuwa kama JK aliye ingia na maelezo ya kisiasa, kwa kuahidi maisha bora kwa kila mtanzania, akiahidi kutatua matatizo yooooote yanayo wakabili wananchi, kwa maamuzi yake ya kisiasa bila utaalamu akaamuru pesa aka mabilioni ya JK zigawiwe kama njugu akidhani ndo akitoa maisha bora??

Nadhani kazi ya upinzani ni kuukubali ukweli kwamba sawa hizo takwimu tunazo sikia kwamba uchumi unakua ni kweli ila.. kinacho pungua ni hiki na hiki na ndo maana maisha ni mabaya tofauti na hizo takwimu! na hapo hapo kurusha turufu yao kwa kujinadi kwamba mkitupa sisi madaraka tutahakikisha hili na hili linaenda hivi na vile ili kukua kwa uchumi kuendane na maisha halisi ya mwananchi wa kawaida.

Lakini sikupingana na ukweli ulio wazi.
 

Zitto na Chacha wote wanasema kweli hapa. Tofauti ni kwamba ukisoma hizo talking notes za Zitto utabaini kwamba alikuwa anazungumza katika mkutano na wasomi ama mkutano usiokuwa wa kisisiasa. Kwa hiyo ukweli umeuvika chupi ndio maana hauonekani vizuri kiasi kwamba wengine wamesema amesema serikali imependeza. Chacha yeye alikuwa anazungumza ukweli huo huo katika lugha ya kisiasa hivyo ni ukweli uliouchi kabisa. Labda Zitto atuambie, alikuwa anazungumza wapi, na wakina nani, akifanya nini? Ukimpandisha jangwani Zitto hivi sasa azungumzie uchumi hivi atazungumza kwa lugha hiyo hapo? Gazeti la UHURU liliipata wapi hii mada ambayo haikuwepo kwenye magazeti mengine yote? Sio mkakati wa kutafuta namna ya kumchonganisha Zitto na wananchi ama Zitto na wenzake katika CHADEMA. Chacha Wangwe naye kwanini nini akadandia basi la gazeti la UHURU kwa mbele? Siku nyingine atakujwa kugongwa.

Fundisho hapa ni kwamba, kwa wanasiasa popote kauli yako inachukuliwa kisiasa-hata ukipaza sauti ukiwa maliwatoni unajisadia bado utanukuliwa na vyombo vya habari kama vile uko bungeni. Hivyo itakadi ya mtu lazima iwe kwenye maisha yake wakati wote kuepusha flip flopping. Nimetolea mfano wa Shivji, yeye hata wanawake wakimualika-nakumbuka pale TGNP pamoja na kuwa walimlipa fedha nyingi kuja bado akawachamba bila kuwaangalia usoni. Na kwa kweli aliwasilisha mitazamo yake ya class struggle hata ilikuwa ni katika masuala ya kitchen party.

Hivyo hata Chache ajue kabisa kama alizoea kushurutisha ng'ombe kule kwao ni tofauti na kauli za umakamu mwenyekiti, awe anajenga hoja badala ya kutuhumu, na awe anauliza kwanza sio ku-break into sound ovyo ovyo na kukitia najisi CHADEMA.


Asha
 

Mheshimiwa Zitto,

Mimi sio Mchumi ila bado nina wasiwasi sana na data ulizotumia kufikia conclusion yako kwamba uchumi unakua hasa kwa mwaka 2006 na 2007.

Inabidi ufafanue unaposema GDP imekuwa una maana GDP ipi? Una maana nominal GDP au real GDP?

Ukiangalia data ulizo post hapo juu na pia ukweli tunaoujua toka TZ ni kwamba inflation kwa kipindi hicho imepanda juu na hivyo kuwa na effect kwenye kupanda kudogo kulikokuwepo kwenye GDP.

Nitatolea mfano wa beer, huwezi kusema pato litokanalo na beer limepanda kwasababu umepata bilioni 100 mwaka huu tofauti na bilioni 95 mwaka jana wakati inflation ni asilimia 10. Ukisema hivyo utakuwa unatudanganya Wadanganyika. Ki ukweli kwenye huo mfano, pato limeshuka.

Kwa matatizo yaliyokuwepo mwaka 2006, nina uhakika hiyo GDP ambayo serikali inasema imekua kwasehemu kubwa imeletwa na inflation ambayo ilipanda juu sana kwa huo mwaka. Viwanda vingi
havikuzalisha at least 10% ya muda kwa mwaka 2006. Mfumuko wa bei uliongezeka kutokana na matatizo ya umeme na ukame. Sasa huo uzalishaji uliofanya uchumi ukue ulitokana na nini?

Ninaamini mheshimiwa Zitto utakuwa unatumia nominal GDP badala ya real GDP ambayo inapatikana baada ya kutoa effect ya inflation kwenye pato la taifa.

Kwasababu inflation iliongezeka, ili uchumi kwa mwaka 2006 ukue, ni lazima vitu na services viwe vimezalishwa zaidi sana ya mwaka 2005, kitu ambacho mimi siamini kilitokea mwaka 2006.

Hapa kwenye hili naamini umetumika kueneza propaganda za CCM na serikali yake labda bila ya wewe kujua. Kama mchumi lazima u questions uhalali wa hizo data kabla ya kuanza kuzitumia.
 
Killtime et al.,
Nimerudia kusoma post yangu sijaona hata sehemu moja ambapo nimesema Zitto adanganye. Nitachosema mimi sioni kama ni kazi ya kiongozi wa upinzani kusifia ukuaji wa uchumi. There are plenty of people employed just to do that including the Ministers Finance and Economic Planning. Kuna mambo mengi ya kuongea kuhusu ile nchi ambayo wapinzani wanapaswa kuyabebea bango ambayo CCM hawawezi kuyasema. Sasa kama na sisi tutaongea kama CCM what will be the difference? So, msijibu hoja zangu kwa kuniwekea maneno, I will be the last person kusema kiongozi wa upinzani adanganye. Mimi nimfuatiliaji kidogo wa mambo ya siasa, sijapata kuona kiongozi makini wa upinzani anasifia mafanikio ya serikali. Sanasana huwa wanatakiana kila la heri baada ya kuchaguliwa, baada ya hapo ni vigongo kwa vigongo. As a politician you must be careful in choosing your words. The last thing you can do as an opposition leader is to shower praise on your opponent, especially in a country where the government is failing in almost every aspect, that will be irony at best and foolhardy at worst!

Kwa mtu mpinzani makini ukiona umeongea jambo halafu gazeti la Uhuru linaiweka positively as a leading news in its front page lazima ushtuke; ujue ulichoongea kilikuwa na maslahi zaidi kwa CCM kuliko opposition, sasa nauliza tena hivyo ndivyo tunataka kiongozi upinzani awe? Yaani awe kipaza sauti cha CCM?

Zitto-usidanganyike ndugu yangu, viongozi wa CCM wamechafuka vya kutosha kiasi kwamba hakuna anayeongea na wananchi wakamchukulia seriously tofauti na watu kama wewe, Slaa, n.k. Sasa be careful CCM watakutumia mwenyewe kueneza propaganda zao bila wewe kujua. Sasa subiri 2010, watanyanyua hiyo copy ya Uhuru na kusema tazameni hata Zitto mwenyewe anasema uchumi unakua, mambo safi, huyu ndiye shujaa wa Taifa anasema hivi. nyie mnataka nini? Bwana tafadhali usituongezee kazi sisi kwenye kampeni za 2010, washikaji kibao hapa JF hawatakuwepo, sisi ndio tutahangaika na wewe kwenye majukwaa!

Tumia majukwaa unayopewa na hizo taasisi ku-expound CHADEMA's economic vision which is so far not known by the majority of people in our country. Itapendeza kama next time tutajadili hapa a controversial economic policy ya chadema badala ya stats za kukua kwa uchumi, ambazo kimsingi ni hewa!
 

Hivi Samuel Sitta si mjomba wake na Zitto Kabwe, kwanini hakumsifia kwa kutoa hoja nzuri ya Buzwagi?

Kwanini CCM huwa hawasifii CHADEMA zaidi ya kutoa matamko ya kuponda?

Asha
 

Kilitime,

Sina ambitions zozote za kuwa mtu wa CHADEMA lakini nina wasiwasi
mno na hizo data anazotumia mheshimiwa Zitto kuja kwenye conclusion yake.

Labda atufafanulie huo uchumi ulikua kwa vipi wakati kilimo ambacho kinachangia kwa asilimia 44 kiliporomoka sana. Labda atuambie je huko kwenye kukua kwake ametoa effect ya inflation?

Vinginevyo hii ndio ile ile garbage in garbage out. Unatumia data zisizo sawa, lazima utapata conclusion mbovu. Ndio maana wenzake wanamshangaa maana hali tunayojua wengi haiko hivyo.

Labda uchumu utakua huko mbeleni lakini sio kwa mwaka 2006 na 2007.
 
Pumba tu
na ZITTO wenu huyo ,
yani ninyi nani kawaloga ???
Hivi inawezekana ktk kongamano la kupata maelezo na takwimu sahihi za hali ya hewa ya dunia aende kuzielezea Enginear wa civil?? kulaleki walai Watu wa taifa lile!!!!!

Kazi ya serikali inaenda kuongelewa na wapinzani Uchumi wenyewe huo wa kubumba duuu hivi DR Watson hapa atapingika kweli kwa mawazo yake??
Hivi nani katuloga tukiitwa tusipate kuitika, tukitazama tusipate kuona?????
Hapo angeenda JK au Lowassa na kuhutubia kuwa uchumi ktk madini umepaa watu humu ungesikia vijembe
Lakini kwa vile JK na Lowasa wanapiga mabao ya visigino wakaamua kuwasukumia kipenzi wenu Kipofu ZITTO ili awapufushe vizuri.

watu wamekubali uchumi ktk madini unapaa sasa mwaka mpya akija Lowasa hapa akasema uchumi unapaa mtu hata bisha maana wameshakwisha pofushwa.
ZITO endelea kupotosha wapofu wanzako maana hata ktk vijimisemo vimo vinavyosema acha wafu wakazikane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…