Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,340
- 51,900
Habari za Mwaka Mpya Wakuu!
Kuna Watu ni wepesi sana kutoa vibanzi katika macho ya wenzao ilhali wao wako na boriti.
Serikali imeshindwa!
Rais gani huyo!
Viongozi wa nchi hii ni wajinga sana!
Maneno ni mengi.
Sawa. Ni haki yao. Lakini Haki inapotea pale ambapo mtu hastahili kukosoa kile ambacho yeye mwenyewe kimemshinda.
Mwizi hana haki ya kumhukumu mwizi mwenzake. iko hivyo.
Kipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzake.
Kabla hujaanza kusema Wenzako waliobahatika kuwapata viongozi wa nchi. Wenyewe mnaita kuisema Serikali. Jitathmini, wewe umeweza kuongoza nini kwenye maisha yako? Kama hiyo haitoshi kama unafamilia, jiulize umefanikiwa kuweza kuongoza familia yako?
Familia ni serikali ndogo. Je sheria za familia yako ni za haki? Au ndio zile sheria za Baba hakosei, au mzazi hakosei?
Je unatimiza majukumu yako kama kiongozi ndani ya familia?
Je umeweza kuitiisha familia yako?
Je malengo uliyoyapanga katika familia yako yametimia?
Elewa kuwa, kama wewe katika level ya uongozi wa familia unachangamoto zinazokusibu mpaka kufikia kushindwa kuongoza familia yako ndio hivyohivyo katika level ya kitaifa nako kuna changamoto kubwa za kiwango cha kitaifa zinazoifanya serikali ishindwe kufanya mambo yake.
Kama wewe kwenye uongozi wako wa familia hakuna uaminifu baina yako na mkeo au watoto ndio hivyohivyo katika level ya serikali nako kuna Watu wasio waaminifu.
Kama kwenye familia yako hamna umoja na kila mtu ni mbinafsi. Yaani mkeo anajali maslahi yake na wewe unajali maslahi yako. Ndio hivyohivyo ndani ya serikali mambo yanavyoendelea. Kila kiongozi anajali maslahi yake na familia yake.
Elewa kuwa kama unaona serikali ndio kikwazo cha wewe kuongoza familia yako vizuri basi ndio hivyohivyo hiyo serikali yako nayo inawakubwa wake huko duniani wanayoifanya ishindwe kuongoza vizuri.
Kulaumu wengine kwa jambo lilelile unalolifanya hata kama ni kwa level ya chini ni dalili ya kutojitambua, ubinafsi na kiburi.
Elewa kuwa, viongozi wengi kabla ya kuingia madarakani hufikiria kuwa wakipata madaraka wataleta maendeleo na kufanya makubwa kwa nchi lakini wakiyapata hayo madaraka huona mambo tofauti kwa sababu kumbe kuna changamoto zinazolingana na ukubwa wa madaraka yao. Na wapo wakubwa huko duniani ambao nao wanamaslahi na nchi.
Kama wakati unaanzisha familia yako ulivyokuwa unandoto ya kuongoza familia nao kuipa furaha lakini mambo yanavyoendelea kwa sasa huamini kama kweli ni wewe ya mwingine. Ndio hivyo.
Hakuna cha kusema serikali sijui ina vyombo vya dola, sijui usalama wa taifa sijui nini.
Utawala unahusu zaidi Mtazamo, falsafa, ideology, maadili, Akili na maarifa, utayari, kujitoa, maono.
Hivyo kama ni maendeleo. Huanza katika ngazi ya familia.
Taikon acha apumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam