Hashim Issa: Rais Samia na chama chake wameshindwa kuongoza nchi, waondoke Madarakani

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
127
420
Katiba ya Warioba ishakulinda wewe, ishakutoa kwenye lawama, kwamba wewe hulaumiwi na CCM sababu hii ni katiba waliyoitaka watanzania. Lakini, kwanini huwatakii mema wafaidika wa mwanzo wa Katiba hii, ndugu zako Wanzibari? Sisi ndio tutafaidika mwanzo sababu sisi tumefungwa jela, tumefungwa minyororo, tangu wakati wa Nyerere mpaka saivi Kikwete.

Hiki kiti cha umoja wa Mataifa kinachotumika cha Umoja wa Mataifa sio cha Tanzania wala cha Tangangika, hiki kiti cha Zanzibar. Lakini wazanzibari tumenyimwa, tumenyang’anywa kiti chetu.

Wewe Mama Samia umekaa kimya, hiyo sijui kujenga Mabarabara na nini, hata ujenge barabara za dhabahu haina maana. Wazanzibari hatuna uhuru wa kujitawala, mpaka leo sisi tunachaguliwa Rais kutoka Dodoma, na wewe unajua mama Samia.

Ndio maana nimeanza speech yangu kwa kusema wewe mama Samia ni mbinafsi, unaangalia maslahi yako wewe na familia yako. Huna faida yoyote kwa Wazanzibari.

Wewe ni mwislamu, na sisi waislam tunaamini kila kinachotokezea huo ni mtihani wako, wewe umepewa mtihani. Hata mie ni mwenyekiti wa Baraza la Wazee, mimi siwezi kujisifu, hawa wote wanaweza kushika nafasi yangu mimi na kufanya vizuri, lakini mwenyezi Mungu kanipa mimi huu ni mtihani wangu, siyo uhodari, ni mtihani, haunipi usingizi.

Hii nchi ufisadi umewashinda. Unaletewa ripoti na CAG hii hapa, wizi huu umefanyika, ufisadi huu umefanyika, hakikisha unaondoa ufisadi. Umeshindwa kuondoa ufisadi, maana yake nini? Umeshindwa ondoa, hufai na chama chako. Mshachoka, hamfai tena kuongoza hii nchi

Mzee Hashim Issa Juma
Mwenyekiti Baraza la Wazee, CHADEMA
 
Back
Top Bottom