Ujumbe muhimu kwa wanafamilia wote waliovuruga familia zao kwa kushindwa kudhibiti misukosuko ya maisha.

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,486
21,959
Familia yenye nguvu ni nguzo thabiti ya misukosuko ya maisha. Ukivuruga familia yako, utavuruga amani yako.

Ikiwa unataka kuishi kwa amani basi weka mikakati na usimame kama kiongozi wa familia kudhibiti misukosuko yote.

Usiruhusu vijana wako wa kiume waige tabia za kike, vinginevyo wataingia kwenye ushoga na kukukosesha amani katika familia yako.

Ukiacha mabinti zako wakaiga tabia za kiume wataingia katika usagaji na kukukosesha amani katika familia yako. Hivyo wadhibiti wasiige ujinga na kukuletea misukosuko hadi ukose amani maishani mwako.

Kumbuka dunia ya sasa ni ya kidigtal, mambo ya sayansi na teknolojia yameleta mabadiliko makubwa kwa jamii zetu, hayo mabadiliko yanaweza kuleta misukosuko kwa familia yako usipokuwa makini.

Biblia inasema..... Mlee mwanao katika njia impasayo naye hataiacha hadi atakapokua mzee. - Mithali 22:6

Ubarikiwe.
 
Vijana wetu (hasa wa kike) wasiolelewa ipasavyo huwa hawatofautishi uchumba na ndoa hivyo hudanganyika hadi kuishi pamoja na mzinzi huku wakidhani kuwa huyo ndiye wa kuishi naye hadi kifo kiwatenganishe kumbe ni mpitaji tu.
Elimu ya ndoa wengi hawana paña mke/mme wa ndoa na ngono unaoa wa ngono we unawaza familia ye anawaza bata utadhani kuna kipya batani.
Lazm mpishane TU.
Ukiamua kuingia kwenye ndoa hakikisha umemaliza nyege zako zote ili usiwe sababu ya kumuharibia mwenzio chet Cha ndoa.
Ndoa ni kwa ajili ya watu maalumu wengine yafaa wawe single
 
Kuna mengine wanayafatilia na yanawapa furaha na sisi wazazi hatuna uelewa nayo.
Mambo yanayowapa furaha mara nyingi huwapeleka kwenye mmomonyoko wa maadili sasa ukikaza fuvu kwamba hauna uelewa wa hayo mambo yao ujue umeshapoteza maana utakuwa umewakabidhi wafubzwe na walimwengu
 
Back
Top Bottom