JWTZ yakamata maafisa wanne wa Rwanda nchini Congo

JWTZ yakamata maafisa wanne wa Rwanda nchini Congo

ASKARI wa UMoja wa MAtaifa wanaolinda amani nchini KONGO (Monusco) , Wakiongozwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) , wamedai kuwakamata maofisa wanne wa ngazi za juu kabisha Wa Jeshi la RWANDA wakiwa wanawasaidia waasi wa M23. MAAFISA hao wanashikiliwa kwa mahojiano

Habari imeendelea kusema kuwa kukamatwa kwa MAAFISA hao na kusambaratishwa kwa waasi wa M23 kumefanikisha kushinda vita hiyo kwa 95% na kwamba tayari Monusco wanaoongozwa na JWTZ wameanza kufurahia ushindi huo na kwamba sasa hivi wanasubiri tamko kutoka kwa wakuu wao, ili kufahamu kinachofuata baafa ya kufanikisha hatua hiyo.

SOURCE:MTANZANIA.

You never credible before you cannot be credible today and Mtanzania na wewe wote ni class moja .Jitahidi sana kutuelezea hadi uaminike .
 
ASKARI wa UMoja wa MAtaifa wanaolinda amani nchini KONGO (Monusco) , Wakiongozwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) , wamedai kuwakamata maofisa wanne wa ngazi za juu kabisha Wa Jeshi la RWANDA wakiwa wanawasaidia waasi wa M23. MAAFISA hao wanashikiliwa kwa mahojiano

Habari imeendelea kusema kuwa kukamatwa kwa MAAFISA hao na kusambaratishwa kwa waasi wa M23 kumefanikisha kushinda vita hiyo kwa 95% na kwamba tayari Monusco wanaoongozwa na JWTZ wameanza kufurahia ushindi huo na kwamba sasa hivi wanasubiri tamko kutoka kwa wakuu wao, ili kufahamu kinachofuata baafa ya kufanikisha hatua hiyo.

SOURCE:MTANZANIA.

Mi nilidhani maafsa wa JWTZ ndo waliokamatwa!!!!!!!!!!!
 
hako ka Kagame hako nakaonea huruma mimi!
mimi naona hata kwenye kiganja hakajai vile!
kale kamjamaa nadhani tukagonge makofi ya Mwinyi tu yanatosha!
 
Ni Furaha ya Namna kuwa na Jeshi imara kama JWTZ!!!!
 
Duuh! Humu JF kuna mijamaa inapenda na kushabikia vita utadhani ilishawahi kushika bunduki hata siku moja.

Jamani vita siyo nzuri tuungane watanganyika (kwani sisi ndio tunapakana na Rwanda) na Wanyarwanda wapenda amani tupinge huu upuuzi unaotaka kuingizwa kati yetu. Hatukuenda Congo kupigana na Rwanda tuko kule kama sehemu ya jeshi la umoja wa mataifa la kulinda amani lenye mandate ya kupambana na vikundi vya waasi vya congo vyenye kuua raia. Kama Rwanda wanafadhili au kushirikiana na vikundi hivyo vya waasi kupigana na Jeshi la umoja wa mataifa hilo ni tatizo lao na wakipigwa wasiilaumu Tanzania kama nchi bali wailaumu UN na kama wanataka mawasiliano wawasiliane na BAN KI MOON. Wakiwasiliana na Tanzania watakuwa wamekosea address. Chochote kinachoendelea huko Congo kwa sasa hakituhusu kama nchi bali kinaihusu jumuia yote ya kimataifa ikiwemo Rwanda na Tanzania kwani jeshi tunalolitumikia huko ni la jumuia ya kimataifa siyo JWTZ.

Wajukuu zangu wahaya, wanyambo, wahangaza (akina Ta Muganyizi na wengineo) pazeni sauti zenu msikike mkipinga hii vita ya kijinga ndugu zetu wa huko Kagera ndio watakuwa watu wa kwanza kumwagika midomo na kuwolewa kama walivyofanywa na wale askari wa Iddi Amini alipovamia Kyaka. Nina uzoefu wa kuishi kwenye mazingira ya vita na nisingependa mtu yeyote aishi kwenye hali hiyo.

Tuna mambo muhimu zaidi ya kufanya kuinua hali za maisha yetu na ya ndugu zetu walio kwenye lindi la umaskini. Kupigana vita kwa sasa siyo mojawapo ya kipaumbele cha nchi hii. Isije ikawa hawa jamaa wanaoshadidia vita na Rwanda wanataka kutusahaulisha mchakato wa katiba mpya na ujenzi wa bomba la gesi toka Mtwara mpaka Dar kwa kuanzisha mijadala isiyokuwa na tija kwa nchi.

Kama tatizo ni kutokuelewana kati ya Kagame na Kikwete tuwaombe kwa heshima na taadhima wakutane wazungumze wayamalize au kama hawawezi watupishe sisi tuishi kwa amani ndani ya nchi zetu. Ila wahamiaji haramu waondoke warudi makwao kwa mujibu wa sheria.
 
Mods naombeni msinipige ban ila naomba tu badala ya kutaja jina la huyu mchokozi na mdokozi (kagame) tumpe jina la Mmbwa Koko
 
Muhakikishe mnawakamata wote asitoroke hata mmoja na huyo aliyewatuma.
 
Wale washenzi wa M23 walisema MONUSCO wakiondoka wanarudi tena.Kuna haja ya kuhang around for a while kwa sababu mbili - kwanza kuhakikisha washenzi hao hawarudi, pili kuwapa vijana wetu waliofanya kazi kubwa likizo na posho ya shukurani toka UN.
Mkuu unajua tulipoteza baadhi ya wanajezi wetu huko Uganda baada ya vita kumalizika! Wanajeshi wetu waliokuwa wamebaki kutoa mafunzo huko Uganda walikuwa wanafanyiwa hujuma wakitumia mbinu mbali mbali zikiwemo za kutumia mpaka wakina mama kuhujumu JWTZ, binafsi naona wakisha maliza kazi yao iliyo tukuka huko DRC, hakuna haja ya ku-hang around.
 
Hizi habari za vyanzo vyetu bila kupata any words from the AUTHORITY either MUNUSCO spokesmen hazina ukweli. Mwandishi aweza kudanganywa na hicho chanzo mathalani ni Coplo wa Jeshi la JWTZ anaependa kujisifia kwa ndugu zake waliopo Tanzania> Nimechungulia vyombo vingi vya habari mbaka muda huu hakuna kitu cha namna hiyo ati!! Tusubirie uhakika wa habari kuliko kufanya SIASA katika hili!! Ushabiki ni uzandiki ati!!
utatafuta saana hizo habari hutopata kutoka kwenye vyanzo hivyo, kwani watu hao ni muhimu saana kwa wakati huu , ujasusi unapoendelea na mazungumzo na watu wa Kimataifa (Mary Robison) na unaweza kukuta pale kibati zaidi ya nguo za kijeshi, walizoshika wanajeshi wa drc, kunawezekana communication equipment zilipatikana na mabomu/risasi zinazo thibitisha ushiriki wa Rwanda ndio maana sasa hivi wamekuwa kimya, wakijiuliza adui anajua nini au jumuia za kimataifa juu yao.
 
wanasubiria kinachofuata? kinachofuata ni kurudi nyumbani, ila anayejisikia kuingia Rwanda ruksa.
 
Back
Top Bottom