Kweli mkuu upo sahihi, Rwanda Inatisha wale JWTZ ni maneno tu lakini hamna kitu. Ndiyo maana walimsema sana Idd Amin mpaka akaondoka kwa hiyari ikulu ya Kampala. Hawakuishia hapo wakaenda kuwasema kweli Wareno wa Msumbiji mpaka wakaona haya wakaondoka wenyewe kwa hiyari na kuiacha Mozambique ipate uhuru wake. Wamewasema sana makaburu wa South Africa kabla ya uhuru wa SA mwaka 1994 . Walikuwa tayari wameshaandaa maneno yao ya mipasho dhidi ya Kanali Bakari kule ANJUAN Comoros mpaka jamaa kwa aibu kubwa akajifunga baibui akakimbia.
Hawa JWTZ hovyo sana nasikia pia waliwasema sana wakoloni huko Angola,Namibia na Zimbabwe mpaka makaburu wakawa wanaona aibu.
JWTZ ni maneno tu ndiyo wanaweza lakini vita hawawawezi watutsi, SI ETI EENH?