Nafurahi kusikia JWTZ kutangaza nafasi za kujiandikisha kuwa Mwanajeshi,kwani JWTZ ni ya Wananchi na watoto wa Wananchi ndiyo wametarifiwa kuhusu nafasi za kujiandikisha.Ni fursa ya wanaohitaji kuzichangamkia.pia nasikitika kuona mwana jf mwenzetu kuhisi kuwa ukiwa MWANAJESHI UTAROGWA!kwanza atambue kuwa katika kada zote za maeneo ya kazi za Umma,JESHINI ndiyo sehemu pekee pasipo kuwa na majungu, unafiki,siasa za kijinga, kuoneana wala uchawi anaouogopa.JESHINI mambo yote huendeshwa kwa nidhamu ya hali ya juu kwa makamanda na wapiganaji.Hivyo mambo huendeshwa kwa amri na maelekezo(Line Organisation philosophy)