Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Kithuku,Fundi Mchundo,Mkandara,FMES,Mwanakijiji,
Game-Theory,AbdulK,Opaque,Mwita,..

..nadhani tumeshajadiliana kiasi cha kutosha suala la OIC.

..nadhani kila upande umetoa hoja nzito na zenye ushawishi wa hali ya juu kabisa.

..itafika wakati serikali itachukua uamuzi ambao inawezekana usiupendezeshe upande mmoja wapo.

..i would want you to step back, halafu mfikirie lugha ya kuwatuliza wale ambao wako-against au pro OIC, wakati serikali itakapotoa uamuzi.

..say, Kithuku umekuwa ukipinga Tanzania kujiunga na OIC. nipe kauli/sababu/nasaha ambazzo utaitumia kuwatuliza wale wanaokuunga mkono.

..hivyo hivyo Fundi Mchundo umekuwa ukiunga mkono Tanzania kujiunga na OIC. nipe kauli/nasaha utakazotumia kuwatuliza wale wanaokuunga mkono ikiwa serikali itachukua uamuzi tofauti na matakwa yao.

..huu mjadala umekuwepo kwa zaidi ya miaka 10 sasa. nadhani umefika wakati wa kuangalia jinsi ya kuvuka dharuba hii, huku nchi ikiendelea kuwa na amani na mashirikiano baina ya dini mbili za Waislamu na Wakristo.

Mkuu Jokakuu,

Samahani kwamba nilikuwa sijaangalia hii kitu huko PM, ujumbe ni mzito sana na ninakubaliana na wewe kwamba hekima kubwa na busara inahitajika kuvuka uamuzi wa serikali on this ishu.

Anyways, nimekusikia bro.
 
Sitashangaa kama liliibuka enzi za Mwinyi likatulia enzi za Mkapa sasa enzi za JK ndio liko juu tena!

Sitashangaa kama liliibuka enzi za Mwinyi, usisahau kumalizia hapa kuwa Mwenye heri Nyerere ndie aliyezuia kwa nguvu zote mpaka suala la OIC halikuzungumzwa tena!!!!!!

Kumbe James Watson ana akili sana!!!!!!!!!
 
Phillemon Mikael,
wanaofikiri tanzania inaweza kujiunga na OIC au MAHAKAMA YA KADHI wanaota ndoto za mchana...THAT WILL NEVER HAPPEN HERE ..........

Ndugu Mikael ukweli ni kwamba wale wanaofikiria kwamba Waislaam hawawezi kusimama kutetea haki zao basi mmepotea na nitasema hivi... NIA TUNAYO, SABABU TUNAYO na UWEZO TUNAO...
Haya ni maneno ya mwalimu wakati wa kumwondoa nduli Idd Amin sasa ikiwa kweli mnatangaza Udini bila shaka muwe tayari pia kupokea yanayokuja na udini...

Mkuu kwanza kabisa kila siku tunajinyonga wenyewe... Kama unakumbuka Zanzibar walitaka kujiunga na OIC, Zanzibar ambayo asilimia 99 ni waislaam tukaja na sababu zetu nje kabisa ya kwamba swala hili ni la kidini na serikali isiingilie. Tukasema hili ni swala la Kitaifa na kwa maslahi ya Taifa Zanzibar haiwezi kujiunga na OIC kama NCHI.
Ni katika mtazamo huo huo wa nchi tulikataa pia Zanzibar wasijiunge na taasisi mbali mbali za kitaifa kama NCHI - mfano FIFA, IOC (olimpiki) na kadhalika kwa sababu kikatiba nchi ilikuwa moja tu nayo ni Tanzania.
Cha ajabu hawa jamaa zetu walikubali kutojiunga na vyombo hivyo lakini bado bara hatukuishia hapo tu, timu zetu za mpira za taifa zilikuwa na wachezaji toka bara tu mara chache sana wamehusishwa na naweza kuhesabu Zanzibar walipohusishwa kikamilifu usijae mononi.. vile vile ktk timu za ziunazotuwakilisha ktk mashindano ya Olimpiki, Zanzibar tuliwaweka kando mara kibao...
Mkuu unajua unaweza kumsukuma mtu mara nyingi asifanye kitu lakini kuna wakati mtu huyo hufikia Ukutani, ikashindikana kumsukuma tena nyuma isipokuwa yeye kusukuma mbele ili apate nafasi ya kupumua.. Na hapoa ndipo tulipofika ktk maswala mengi ya Zanzibar..

Mkuu, tulikataa Zanzibar kujiunga na OIC kwa sababu Zanzibar haikuwa nchi, sawa sasa iweje leo nchi inapotaka kujiunga na chombo hicho hicho swala linageuka na kuwa hili ni swala la dini serikali haitakiwi kutoa maamuzi yanayolenga Upande mmoja!..Na wapo wanaosema serikali haitrakiwi kabisa kuingilia maswala ya dini wakati huo huo haohao wanaosema hivyo wanapinga Waislaam kuanzisha mahakama ya kadhi..iweje swala la mahakama ya kadhi ambalo ni swala la dini ya Waislaam lirudi ktk maamuzi ya serikali wakati mwanzo imekataliwa kuwa maswala ya dini yasiingiliwe na serikali!..
Nitarudia kusema tena ni kwa kutumia katiba hiyo hiyo Nyerere alivunja chombo cha kiislaam na kuunda BAKWATA, chombo cha serikali kwa Waislaam wakati KKK na vyombo vyote vya kikristu viliendelea na kazi zake bila kuingiliwa na serikali, yet Waislaam hawakuweka manunguniko yao hadharani.. chama cha Bakwata kikaendeshwa na serikali kwa miaka mingi hadi baadhi viongozi wa Kiislaam walipoamua enough is enough wanataka chombo cha Waislaam kwa waislaam, wakaunda BALUKTA..wakitumia hoja ambayo imependekezwa na watu wengi tu.. Kuwa maswala ya dini serikali haitakiwi kuweka mkono wake lakini ajabu ni kwamba BALUKTA ilipigwa vita na viongozi wa dini ya kikristu pamoja na viongozi wa serikali ikabidi Sheikh Kassim bin Jumaa mmoja wa waasisi wachukuliwe hatua kali.. Mateso aliyopewa kifungoni hakuweza hata kuchukua muda, baada ya kuachiwa week moja tu akafariki dunia...
Mkuu nikirudi nyuma kidogo, Zanzibar kukataliwa kwake kujiunga na OIC was pure roho mbaya, hatukuwa na sababu zaidi ya kuitumia katiba kwani kuna nchi kama Canada ina jimbo la Quebec ambao ni wanachama wa umoja wa nchi za Kifaransa pamoja na kwamba idadi kubwa ya wananchi wake hawana asili wala nasaba na Ufaransa.
Tazama nchi kama Switzeland, hii ina makabila matatu makuu, wapo Wafaransa upande wa Zurich, Wajarumani upande wa Basil na Benn, na Wataliani upande wa kusini Turin, na sehemu zote hizi wamejiunga na jumuiya za makabila yao huko Ulaya na wanazungumza lugha zao, lakini bado wameweza kudumisha amani kati yao kama nchi moja na hata wakienda nje wote ni hujulikana kama Waswiss...ama WaCanada.
Tazama Germany na Ausria hawa wote ni wajarumani na wanazungumza Kijarumani lakini wamekubali kuwepo mipaka kati yao kama nchi mbili tofauti..hakuna misukosuko kama yetu.

Hata hivyo kama nilivyokwisha sema mwanzoni hatuwezi kuiga nchi za Ulaya kujenga Taifa na umoja wetu, sisi kama Waafrika hatuwezi kabisa kusimama Kitaifa na tofauti kama hizo na kuna mifano mingi ya vita kutokea kwa sababu tu kabila fulani makazi yao ni nje ya mipaka ya nchi hiyo. Historia yetu ni chafu na tofaurti kabisa na nchi za Ulaya kiasi kwamba mfumo pekee unaoweza kujenga nchi yetu utatokana na sisi wenyewe katika mzingira yetu..
Sisi tutaijenga nchi yetu kwa kutazama WATU na MAZINGIRA tuliyopo badala ya kuiga nje na kwa neema yakle mwenyezi tanzania imekuwa nchi yenye makabila zaidi ya 120, na dini tofauti zaidi ya 10 sote tukiishi kama ndugu na familia moja pamoja na kwamba tuna tofauti zetu..tofauti ambazo zinaanza toka ktk familia moja moja hadi kitaifa..na hakuna familia hata moja inayotoa amri ama maamuzi ya ndani ya nyumba based on tribe or religion kama kuna mchanganyiko na hakatazwi mtu kufanya ya kabila ama dini yake kwa kuwekewa vikwazo vya marafiki..
Ni kitu gani haswa kinachowatisha wakristu wengi?.. Hakika ni matendo yao wenyewe, Wakristu wana vyombo vya kidini ambavyo kazi yake ni kuhubiri dini tu wakitumia misaada kama mwavuli wa kuingia ktk nyoyo za watu.. vyombo kama World Vision vinatoa misaada kidini..huwezi kufungua NGO Tanzania ambayo haifundishi Biblia ukapewa msaada na vyombo vyote vya kikristu hata kama watu wanakufa njaa kama Somalia na Ethiopia..lakini pamoja na ukweli huo vyombo hivi havikuonekana kuwa tishio kwa dini ya kiislaam kwa sababu dini ni Imani. Mtu yeyote anayeingia dini kwa sababu ya msaada basi huyo sii muumini wa kweli...
Hivyo tofauti na vyombo vya kikristu, OIC inaingia pale Uislaam umekwisha simama..Ni haramu kwa muislaam kumvuta mtu ktk imani ya dini kwa kutumia shida, udhaifu na umaskini wa mlengwa tofauti kabisa na mbinu za kikristu ambazo zinahamasisha zaidi kuingia kule ambako jina la Yesu hakijafika..Na hakika mbinu yao inamvuto zaidi kwa sababu asilimia kubwa ya population duniani ni maskini..na wameweka focus yao kubwa katika kuwavuta maskini..
wakristu wanahaha sana inapofikia swala la vatican hawapendi lihusishwe na swala la OIC wakati kisheria ni haki kabisa kutumia vigezo ktk kuwakilisha hoja yako..Lakini hakuna hata mkristu mmoja anayeweza kutuambia Muislaam anafaidika vipi na Vatican? ama kuna faida gani nchi yetu kuwa na Uhusiano na Vatican kama Taasisi. Nasema tena Vatican ni Taasisi hadi pale watakapo weza kutenganisha kati ya Pope na mtawala wa nchi hiyo. Nina hakika kama kutakuwa na rais mwingine mteuliwa mbali na Pope hatapewa heshima kama anayoipata Pope kwa sababu Vatican na Pope wanaheshimika zaidi ya kuwa nchi kwa sababu ya dini...

Kwa hiyo kama kweli Wakristu wanakataa kabisa nchi yetu kujiunga na OIC, basi kuna kila haja ya kutazama NGO zote za kikristu zinazofanya kazi Tanzania.. Kwa sababu hoja kubwa hapa ni kuwa nchi yetu haina dini kwa hiyo hairuhusiwi kabisa Taasisi yoyote kuingia nchini ikiwa na malengo ya kuboresha (kundi la watu) dini ama dhehebu moja..
Laa sivyo basi kuna hatari kubwa ya kuvunjika Muungano ambao mwalimu aliujenga kwa miaka 23.. na dalili zake zimefikkia kikomo..hakuna kurudi nyuma tena!
 
Uhuru wa dini na mtu kuabudu ndio kitu muhimu pekee katiba inatakiwa kukilinda. mahusiano ya dini na dini husika sehemu yeyote ile ya dunia iheshimiwa. maendeleo ya dini husika na watu wake kwa kufuata uchumi wa kisasa kama vile elimu, afya, na mahusiano ya kimataifa yaheshimiwe ndani ya dini husika. uhusiano wa dini na vikundi vya dini husika vya kiuchumi duniani vibaki kati ya dini husika.
Serikali ikae mbali kabisa na maswala ya dini ya ndani na nje ya nchi ili kusitokee manung'uniko na mgawanyo ambao tayari ulianza na ukapungua sasa unarudi tena.

Uhusiano wa vatican na serikali si wa kijumuiya bali Vatican ni nchi inayojitegemea na inatoa balozi wake kama serikali yeyote ile duniani ni wajibu wa serikali kuukubali ubalozi wa Vatikan au kuukata kama tulivyo ukataa wa Israel. Hakuna mkataba wa kuwa na balozi tunaweza kuufukuza au kumkataa balozi saa yeyote. Ila jumuiya kujiunga nayo ni kukubali katiba na kufuata yaliyoyopo ndani ya katiba.

Mfano mwanachama wa UN anafuata katiba ya Un na akikiuka anaweza kuchapwa, kuwekewa vikwazo vya uchumi na nchi wanachama au kutengwa na nchi wanachama.

watanzania wanaonyesha hawaelewi kwa nini tunataka kujiunga na hiki chombo cha OIC. Serikali iweke wazi, ipeleke katiba na madhumuni ya OIC kwa watanzania waisome na waelewe yaliyomo ndani ya jumuiya hii na nia yake. halafu tupige kura kama tunahitaji kujiunga wengi wakiamua kujiunga demokrasia ifuatwe.

Ila busara lazima itumike kabla ya kufika mbali, je kutakuwa na faida kwa kufanya yote hayo hasa mshikamano na maelewano tuliyonayo. Viongozi wasifanye maamuzi muhimu kwa wananchi kwa vigezo vya kushinda uchaguzi halafu watuachie moto. Aina yeyote ile ya machafuko ya kidini ni mbaya na madhara yake hayana macho. Madhara ya machafuko hayamchagui Membe, Kikwete, Pengo au Simba wote watayapata.
 
Phillemon Mikael,

Ndugu Mikael ukweli ni kwamba wale wanaofikiria kwamba Waislaam hawawezi kusimama kutetea haki zao basi mmepotea na nitasema hivi... NIA TUNAYO, SABABU TUNAYO na UWEZO TUNAO...
Haya ni maneno ya mwalimu wakati wa kumwondoa nduli Idd Amin sasa ikiwa kweli mnatangaza Udini bila shaka muwe tayari pia kupokea yanayokuja na udini...

Mkuu kwanza kabisa kila siku tunajinyonga wenyewe... Kama unakumbuka Zanzibar walitaka kujiunga na OIC, Zanzibar ambayo asilimia 99 ni waislaam tukaja na sababu zetu nje kabisa ya kwamba swala hili ni la kidini na serikali isiingilie. Tukasema hili ni swala la Kitaifa na kwa maslahi ya Taifa Zanzibar haiwezi kujiunga na OIC kama NCHI.
Ni katika mtazamo huo huo wa nchi tulikataa pia Zanzibar wasijiunge na taasisi mbali mbali za kitaifa kama NCHI - mfano FIFA, IOC (olimpiki) na kadhalika kwa sababu kikatiba nchi ilikuwa moja tu nayo ni Tanzania.
Cha ajabu hawa jamaa zetu walikubali kutojiunga na vyombo hivyo lakini bado bara hatukuishia hapo tu, timu zetu za mpira za taifa zilikuwa na wachezaji toka bara tu mara chache sana wamehusishwa na naweza kuhesabu Zanzibar walipohusishwa kikamilifu usijae mononi.. vile vile ktk timu za ziunazotuwakilisha ktk mashindano ya Olimpiki, Zanzibar tuliwaweka kando mara kibao...
Mkuu unajua unaweza kumsukuma mtu mara nyingi asifanye kitu lakini kuna wakati mtu huyo hufikia Ukutani, ikashindikana kumsukuma tena nyuma isipokuwa yeye kusukuma mbele ili apate nafasi ya kupumua.. Na hapoa ndipo tulipofika ktk maswala mengi ya Zanzibar..

Mkuu, tulikataa Zanzibar kujiunga na OIC kwa sababu Zanzibar haikuwa nchi, sawa sasa iweje leo nchi inapotaka kujiunga na chombo hicho hicho swala linageuka na kuwa hili ni swala la dini serikali haitakiwi kutoa maamuzi yanayolenga Upande mmoja!..Na wapo wanaosema serikali haitrakiwi kabisa kuingilia maswala ya dini wakati huo huo haohao wanaosema hivyo wanapinga Waislaam kuanzisha mahakama ya kadhi..iweje swala la mahakama ya kadhi ambalo ni swala la dini ya Waislaam lirudi ktk maamuzi ya serikali wakati mwanzo imekataliwa kuwa maswala ya dini yasiingiliwe na serikali!..
Nitarudia kusema tena ni kwa kutumia katiba hiyo hiyo Nyerere alivunja chombo cha kiislaam na kuunda BAKWATA, chombo cha serikali kwa Waislaam wakati KKK na vyombo vyote vya kikristu viliendelea na kazi zake bila kuingiliwa na serikali, yet Waislaam hawakuweka manunguniko yao hadharani.. chama cha Bakwata kikaendeshwa na serikali kwa miaka mingi hadi baadhi viongozi wa Kiislaam walipoamua enough is enough wanataka chombo cha Waislaam kwa waislaam, wakaunda BALUKTA..wakitumia hoja ambayo imependekezwa na watu wengi tu.. Kuwa maswala ya dini serikali haitakiwi kuweka mkono wake lakini ajabu ni kwamba BALUKTA ilipigwa vita na viongozi wa dini ya kikristu pamoja na viongozi wa serikali ikabidi Sheikh Kassim bin Jumaa mmoja wa waasisi wachukuliwe hatua kali.. Mateso aliyopewa kifungoni hakuweza hata kuchukua muda, baada ya kuachiwa week moja tu akafariki dunia...
Mkuu nikirudi nyuma kidogo, Zanzibar kukataliwa kwake kujiunga na OIC was pure roho mbaya, hatukuwa na sababu zaidi ya kuitumia katiba kwani kuna nchi kama Canada ina jimbo la Quebec ambao ni wanachama wa umoja wa nchi za Kifaransa pamoja na kwamba idadi kubwa ya wananchi wake hawana asili wala nasaba na Ufaransa.
Tazama nchi kama Switzeland, hii ina makabila matatu makuu, wapo Wafaransa upande wa Zurich, Wajarumani upande wa Basil na Benn, na Wataliani upande wa kusini Turin, na sehemu zote hizi wamejiunga na jumuiya za makabila yao huko Ulaya na wanazungumza lugha zao, lakini bado wameweza kudumisha amani kati yao kama nchi moja na hata wakienda nje wote ni hujulikana kama Waswiss...ama WaCanada.
Tazama Germany na Ausria hawa wote ni wajarumani na wanazungumza Kijarumani lakini wamekubali kuwepo mipaka kati yao kama nchi mbili tofauti..hakuna misukosuko kama yetu.

Hata hivyo kama nilivyokwisha sema mwanzoni hatuwezi kuiga nchi za Ulaya kujenga Taifa na umoja wetu, sisi kama Waafrika hatuwezi kabisa kusimama Kitaifa na tofauti kama hizo na kuna mifano mingi ya vita kutokea kwa sababu tu kabila fulani makazi yao ni nje ya mipaka ya nchi hiyo. Historia yetu ni chafu na tofaurti kabisa na nchi za Ulaya kiasi kwamba mfumo pekee unaoweza kujenga nchi yetu utatokana na sisi wenyewe katika mzingira yetu..
Sisi tutaijenga nchi yetu kwa kutazama WATU na MAZINGIRA tuliyopo badala ya kuiga nje na kwa neema yakle mwenyezi tanzania imekuwa nchi yenye makabila zaidi ya 120, na dini tofauti zaidi ya 10 sote tukiishi kama ndugu na familia moja pamoja na kwamba tuna tofauti zetu..tofauti ambazo zinaanza toka ktk familia moja moja hadi kitaifa..na hakuna familia hata moja inayotoa amri ama maamuzi ya ndani ya nyumba based on tribe or religion kama kuna mchanganyiko na hakatazwi mtu kufanya ya kabila ama dini yake kwa kuwekewa vikwazo vya marafiki..
Ni kitu gani haswa kinachowatisha wakristu wengi?.. Hakika ni matendo yao wenyewe, Wakristu wana vyombo vya kidini ambavyo kazi yake ni kuhubiri dini tu wakitumia misaada kama mwavuli wa kuingia ktk nyoyo za watu.. vyombo kama World Vision vinatoa misaada kidini..huwezi kufungua NGO Tanzania ambayo haifundishi Biblia ukapewa msaada na vyombo vyote vya kikristu hata kama watu wanakufa njaa kama Somalia na Ethiopia..lakini pamoja na ukweli huo vyombo hivi havikuonekana kuwa tishio kwa dini ya kiislaam kwa sababu dini ni Imani. Mtu yeyote anayeingia dini kwa sababu ya msaada basi huyo sii muumini wa kweli...
Hivyo tofauti na vyombo vya kikristu, OIC inaingia pale Uislaam umekwisha simama..Ni haramu kwa muislaam kumvuta mtu ktk imani ya dini kwa kutumia shida, udhaifu na umaskini wa mlengwa tofauti kabisa na mbinu za kikristu ambazo zinahamasisha zaidi kuingia kule ambako jina la Yesu hakijafika..Na hakika mbinu yao inamvuto zaidi kwa sababu asilimia kubwa ya population duniani ni maskini..na wameweka focus yao kubwa katika kuwavuta maskini..
wakristu wanahaha sana inapofikia swala la vatican hawapendi lihusishwe na swala la OIC wakati kisheria ni haki kabisa kutumia vigezo ktk kuwakilisha hoja yako..Lakini hakuna hata mkristu mmoja anayeweza kutuambia Muislaam anafaidika vipi na Vatican? ama kuna faida gani nchi yetu kuwa na Uhusiano na Vatican kama Taasisi. Nasema tena Vatican ni Taasisi hadi pale watakapo weza kutenganisha kati ya Pope na mtawala wa nchi hiyo. Nina hakika kama kutakuwa na rais mwingine mteuliwa mbali na Pope hatapewa heshima kama anayoipata Pope kwa sababu...

Kwa hiyo kama kweli Wakristu wanakataa kabisa nchi yetu kujiunga na OIC, basi kuna kila haja ya kutazama NGO zote za kikristu zinazofanya kazi Tanzania.. Kwa sababu hoja kubwa hapa ni kuwa nchi yetu haina dini kwa hiyo hairuhusiwi kabisa Taasisi yoyote kuingia nchini ikiwa na malengo ya kuboresha (kundi la watu) dini ama dhehebu moja..

..sikatai kuwa kwa kutumia hoja dhaifu ..ambayo inashikiliwa kama vile mfas maji anavyoshikilia jani akidhani boya ..ya wingi wa waislamu zanzibar asilimia 99% ya raia wetu 1,000,000 walio zanzibar...kama alivyosenma rais[URT]...leo inawezekana kabisa ..ukichanganya na influence ya some parts of pwani ya tanzania kuamua kujiunga OIC na KADHI........

LAKINI NASEMA KUWA UAMUZI UKIWA HUO BASI NA MUUNGANO UFE ...NA UTAKUFA ..KWA ANAYETAKA OIC ATAKUWA NA HIYARI YA KUVUKA BAHARI NA KWENDA KUFURAHIA MATUNDA UPANDE WA PILI.........DOMINANCE OF MUSLIMS IN ZANZIBAR WILL NEVER INFLUENCE SUCH DECISIONS FOR THE REST OF AS ..WHO HAVE BEEN ENYOYING FREEDOM OF ALL SORT...WE ARE NOT BOUND TO THAT......................

..kwa hiyo kimsingi mzee hatubishani kwa kuoneshana mabavu..ila simply haitawezekana......we are sorry ..thank you..!!

....
 
Hakuna mtu aliyetumia Zanzibar, mkuu unapoagiza chai hotelini hulipii na Kikombe, kunywa chai, acha kikombe mezani - Usichanganye vitu hapa!

Maelezo yangu yote umeshindwa hata kumeza mate huna hoja... hakuna mfa maji aliyewahi kushikilia jani akifikiria ni boya, hizi ni hadithi za kufikirika ambazo wakristu wachache akina NYIE mnazijengea hoja..Uliona wapi mfa maji akishika jani labda mwenzangu uliwahi kufa na hizi ndio hadithi unazotuletea toka kuzimuni maanake leo ni Haloween!
Niliyoandika hapo juu mkuu ni UKWELI mtupu hauna hata moja linalopingika.. Ni historia ambayo haikuandikwa ktk vitabu vya kufikirika!

Akili zimesimama hamuwezi tena kufikiria isipokuwa hadithi za vitabuni..Hamna point kabisa kuhusiana na swala hili kwa hiyo mnazunguka tuuu mkidhani nchi yenu wakati hata Uhuru wenyewe mmedandia jahazi!

Muungano ni swala jingine kabisa na ajabu hamkuyasema haya walipoomba kujiunga wao Zanzibar! Hapa tunazungumzia waislaam na OIC, haiwezekani basi subiri machungu yake, Tanzania haitakalika!..
Well, ITAWEZEKANA na Waislaam watabakia BARA labda itakuwa vizuri kama Wakristu wakiondoka wasogee huko Kongo na Burundi..
 
Huwezi kuwadanganya watu wote wakati wote. Tulidanganywa kupitia matamko "Serikali haina dini". Lakini kwa vitendo na mambo utajua kuna dini. Sasa ni wakati wa twende sasa.
 
Wachina wana msemo "Safari ya maili elfu moja huanza kwa hatua moja". Tukikubali kuwa mwanachama wa OIC basi tunakuwa ni "nchi ya Kiislamu". Ukiwa ni mmojwapo wa jumuiya ya nchi za Kiisalamu basi wewe ni nchi ya Kiisalamu.

Hatua ya pili itakuwa kutubana tuingize sheria za Kiislamu kwenye katiba yetu. Itakuwa shida kwa nchi ya Kiislamu kukataa kutumia sheria za Kiislamu.

Wanaotaka tujiunge na OIC wanatutakia mafarakano ya kidini. Tukatae, kwa njia za amani, sasa.
 
AMA KWELI TEMBEA UONE, NILIKUWA NAJUA ANGALAU WAISLAMU WASOMI, WENYE UWEZO WA KUJUA DUNIA INAENDAJE WANAWEZA WAKAWAELIMISHA WALE WASIOSOMA.

MNALAZIMISHA WATU WAONGEE VISIVYOONGEKEKA.

Chukua mfano wale ombaomba walioko mitaani , barabara zote kuu DSM , ebu fikiria jinsi wanavyowatumia watoto wadogo kuombaombaomba, watoto hawa walitakiwa wapewe elimu, wafikiriwe maisha yao ya baadae!

Tanzania kama nchi leo bila aibu inawatumia waislamu, kuomba sawa na wale ombaomba wazee wasiojiweza mitaani wanavyowatumia waotot! KICHEKESHO NI KUWA HUYU MUISLAMU ANAFURAHIA HII HALI!!! ANACHEKELEA! KANA KWAMABA AKIPATA MISAADA HII NDIYO ATAKWAMUKA KIUCHUMI!!!, WAKATI MZEE HUYU TZ, ANA MIAKA 40, hajafanya lolote la maana, wakati anaomba kura, tulijua atatumia uwezo wake na akili zake kutupeleka kwenye maisha bora , kwa kutumia rasilimali zetu na uwezo wetu, watu wetu n.k. HATA SIKU MOJA TUFIKIE KUWA NCHI BORA.

HAYA NI MATUSI NDUGU ZANGU WAISLAMU, MATUSI MAKUBWA KUWA UISLAMU , kuwa uislamu NI ALAMA YA UMASKINI TANZANIA!!

BY THE WAY, KWA NINI SERIKALI IINGIE HUKU WATENDAJI WENGI WA SERIKALI NI WAKRISTO? ...MAKAFIR?? NA HIZO HELA ZA OIC ZITAKAZO TOLEWA NA WAISLAMU HUKO...UGHAIBUNI ZIKIJA NCHINI MAKAFIRI HAWA WAKRISTO WATAZILA TU

KWANINI MSITUMIE BAKWATA NA NA VYOMBO VINGINE VYA KIISLAMU ILI MAKAFIRI WASIZIGUSE???

AU DHANA YA UKAFIR HAIKO TENA MBELE YA HELA?????? NA JE MAHAKAMA YA KADHI IKIJA SIO KWAMBA WALE WAISLAMU WENGI WATABADILI DINI?? KWA SABABU WENGI NI MASKINI, WANAISHI KWA KUBABAISHA, KUIBA, RUSHWA N.K( HII NDIYO MAANA YA BONGO ATI) AU NDIYO MAHAKAMA YA KADHI ITAKUWA KWA AJILI YA KUWAHUKUMU WANAWAKE TU!!!!!!!!!!!!, nchi zetu za dunia ya tatu wafuata dini ni wachache sana, majina ya John, juma, musa, paul yasiwatishe wala yasiwaonyeshe kuwa eti waislamu wa kufuata mahakama ya kadhi wako wengi, wengi watahama dini , watabadili majina,

narudia tena

SERIKALI IMEJAA MAKAFIR WENGI SANA, UISLAMU NA FEDHA ZAKE ZITAKUJA NA KUPITIA HUMU?? AU KWA SASA TUFUTE NENO KAFIR??

BAKWATA MKO WAPI?, MBONA UISLAMU UNATUKANWA NAMNA HII, BAADA YA OIC, MTAENDA WAPI??

waberoya

Sijaona bado muislamu akijibu hoja hii hapa juu, tafadhali , ili muonekane ni mashujaa wa kweli elezeni dhana nzima ya makafir, na uombaomba na mnatuelezaje? au makafir halipo tena mbele ya pesa, Membe ni mkristo, mnamruhusu kafir akawaandikishe kwenye jumuiya yenu ya OIC? fedha zikija wakristo wanazipokea! dhana ya ukafir sasa hivi haipo tena?? muislamu mmoja tafadhali lijibuni hili!!

waberoya
 
Waboreya,
tafadhali sana usitake kutumia matusi yako kujaribu kuharibu jina la dini ya watu..
Ni wapi ktk Kuran imesema wakristu ni Makafir?... Je, neno Wagalatia unafahamu maana yake?... Je ni kina nani watu hao!
 
Unajua Mkuu Bob,

Mimi ninashindwa kuamini kuwa haya matusi na magomvi ni ya nini hasa, wakati ukweli uko wazi kwamba OIC ni ushirika wa Waisilamu na ni mataifa ya waisilamu tu yanayotakiwa kujiunga nao, unless liwe ni taifa la wendawazimu tu ndio wanaoweza kujiunga nao bila ya kua taifa la Waisilamu.

Hawa viongozi sielewi kwa nini wanataka kutuchanganya akili, Membe hakuongelea habari za Zanzibar na OIC, huyu rais anasema ni ishu ya Zanzibar, something is not right hapo rais na waziri wake wanapojichanganya kwa sababu hwuezi kusema wanajichanganya kwa bahati mbaya.

Wananchi wa Tanzania tunahitaji kuwa waangalifu sana na hizi none ishus, ni muhimu sana tukaheshimu dini zetu na za wenzetu pia, lakini tusilazimishane kuamini maneno tofauti na ukweli ulioko mbele yetu of what OIC is, hapa ni mahali palipojaa wasomi tofauti na vijiweni huko mitaaani, sasa anytime mtu anapotalka kuleta matusi na ugomvi kujadili hii ishu, ni dalili za kutokuwa na hoja.

Mimi siamini kwamba hii ishu ni tatizo, ila ninaamini kuwa viongozi na sisi wananchi na Tanzania kwa ujumla tuna matatizo mengine kabisaa ila tunataka kujificha nyuma ya ishu ya udini, mimi ningekua rais kibarua cha Membe by now kingekua kimeshaota nyasi kwa sababu amekurupuka, ila inasikitisha kuendelea kurushiana maneno mazito kwa sababu ya uzembe wa viongozi kama hawa tulionao.
 
Mkuu Field Marshall ES,

Heshima mbele mkuu! Hawa watu unawafahamu vizuri. Membe hangeweza kusema tutajiunga na OIC kabla ya kukubaliwa na JK. Na lazima atakuwa ametumwa na JK "to test the water".

Nia ya kutuingiza OIC iko pale pale. Mikakati ya kufanya hivyo ndio inawapa matatizo. Kwa sasa, mkakati alioweza kuufikiria JK na kuuweka kwenye hotuba yake ni wa kusema wananchi tuachie uamuzi ufanywe na Membe na serikali.

Yote haya ni USANII. Anajua wazi alishamuagiza Membe atafute njia za kuiingiza Tanzania OIC. Kilichobaki ni sisi Watanzania kutafuta njia za kumzuia Rais wetu asitutumbukize kwenye mtafaruku mzito wa udini.
 
Field Marshall Es,

Mkuu nakuelewa sana ila ningependa unambie kitu kimoja tu..
Imekuwaje Canada, Province ya Quebec ni mwanachama wa Jumuiya ya nchi za Kifaransa hali nchi nzima sio mwanachama na imekubalika kikatiba na hakuna baya lililotokana na kujiunga kwao. Uswiss mwenyewe unajua kuna tabaka tatu za makabila na wameweza kujiunga na makabila nje ya mipaka ya nchi yao lakini Swiss bado ina katiba yake na hakuna matatizo!.. iweje swala hili liwe gumu kiasi kwamba watu watoke mapovu kuanza matusi ya dini na kunyoosheana vidole...
Trust me, mkuu hili swala hapa tu JF tumeshindwa kulitazama kwa fikra huru sasa fikiria taifa zima ambalo asilimia 80 ni Kabuntas wa elimu dunia, dini ama uungwana!..

Mimi nimelikalia swala hili kwa sababu najua kabisa kuwa hili swala litakuja kuwa sababu kubwa ya mtafaruku nchini na kama hatutaweza kujihadhari leo na tukaelewa kinachofuata baada ya hapa.. then tuna matatizo makubwa..
Kuhusiana na Membe, mkuu mimi naamini kabisa kuwa yule jamaa kichwa yaani zina charge!.. Yes, inawezekana kakurupuka kuhusiana na swala hili lakini mkuu wangu jamaa kalitazama swala hili kwa kufuata mifano, sababu na hata kuangalia hatari zake ambazo wengi wetu tumeshindwa kufikiria huko!..Na ajabu anashambuliwa kama mkristu aliyepotea kiasi kwamba ni dini tupu inayoongoza hoja za hapa.
Trust me hili swala halitakwisha kwa amani na inatisha sana!
 
Wakristu wakatoliki wana kitu kinaitwa Baraza la Usuluhishi. Mabaraza haya yanafanya kazi kama mahakama kwa kujadili na kusulihisha matatizo mbali mbali yanayotokea katika familia za wakristu wakatoliki. Mfano matatizo ya ndoa, ugomvi baina ya wakatoliki n.k. Mabaraza haya yako kuanzia ngazi ya jumuiya, kigango, parokia n.k. Kesi inaposhindakana katika mabaraza haya hupelekwa kwenye ngazi ya juu. Serikali haihusiki katika kugharamia vikao vya mabaraza haya, bali wajumbe hufanya kazi kwa kujitolea, na wakati mwingine posho hutolewa na kanisa.

Kwa nini waislam wasiige utaratibu huu wa kuwa na mabara yao ambayo watatumia sheria zao za uislam katika kusikiliza na kuamua mashauri? Kinachotakiwa tu ni legal authority kwamba kesi iliyoamuliwa kwenye mabaraza haya itakuwa halali kisheria.

Hata vijijini kwetu kuna mabaraza ya wazee, ambayo yanaamua kesi nyingi sana kuhusiana na mambo mbalimbali kama migogoro ya ardhi n.k ambayo hayagharamiwi na serikali.

Mimi naona hapa tatizo ni approach ya waislam katika kutekeleza swala lao, mahakama au mabaraza yao ni haki yao, lakini yawe katika mfumo ambo uko nje ya serikali ila yanatambuliwa na kudhibitiwa na serikali.
 
Mkandara,

Canada ina lugha mbili rasmi (Kiingereza na Kifaransa). Kwa hivyo, hata Canada nzima ingeamua kujiunga na Jumuiya ya Nchi Zinazozungumza Kifaransa ingekuwa sawa.

In any case, two wrongs do not make a right. Huwezi kusema ni sawa sehemu ya Tanzania kujiunga na OIC kwani sehemu ya Canada imejiunga na nchi zinazozungumza Kifaransa. Non sequitur. (It does not follow).
 
MpiganajiNambaMoja,
Mkuu hizo mahakama za ndoa hata waislaam wanazo tatizo kubwa ni maamuzi ya mahakama hizi kuhusiana mirathi na kadhalika..Wakristu tayari sheria zao zipo ktk katiba na ndizo tunazotumia leo hii, kumbuka sheria zetu nyingi ni urithi wa mkoloni Muingereza.
Binafsi, sikubaliani na mahakama ya Kadhi kwa sababu Waislaam wengi ndoa zao hazikufuata sheria za dini. Watu wameoa kwa kufuata mila zaidi ya sharia na hata Wakristu wenyewe wamefunga ndoa kidini lakini wana wake zaidi ya mmoja na pengine hata taraka zimetolewa kiholela..
Kwa hiyo utaweza vipi kuhukumu mirathi ikiwa wahusika wenyewe hawakufuata sheria za ndoa to begin with!..
Kuna waoto walizaliwa nje ya ndoa hawa watakosa haki zao!..
Kuna mshikaji wangu mmoja mhuni tu alinambia kwamba dini zote kamba tu.. nikamuuliza kwa nini anasema hivyo akaniuliza maswali mawili tu..
1. Ni wapi katika Biblia ama Msahafu kumezungumzia kubaka watoto wadogo ni dhambi?
2. Ni wapi kati vitabu hivyo hivyo kumezungumzia Rape kama ni dhambi?..

Mkuu kwa sababu elimu yangui ndogo nilibaki domo wazi... Kwa hiyo tusitake kutafuta sababu ama vigezo nje ya mazingira tuliyokuwa nayo bali tujaribu kukabiri matatizo jinsi yanavyokuja na tusipende sana kutumia dini kama sababu za kukataa Ukweli..
 
Field Marshall Es,

Mkuu nakuelewa sana ila ningependa unambie kitu kimoja tu..
Imekuwaje Canada, Province ya Quebec ni mwanachama wa Jumuiya ya nchi za Kifaransa hali nchi nzima sio mwanachama na imekubalika kikatiba na hakuna baya lililotokana na kujiunga kwao. QUOTE]

Well written and analysed, umeshasema wamekubaliana kikatiba! hatujakubaliana kikatiba hapa TZ, kuwa TZ ijiunge na OIC, kwani katiba inasema serikali haina dini!

waberoya
 
Augustine Moshi,
Swala hapa sio lugha mbili bali inaweza kuwa kabila kwa tafsiri yao kwani hata mila za Kifaransa zinatukuzwa Quebec!..Lugha ni moja ya kiungo cha jamii hiyo pamoja na kwamba wapo watu waliohamia. Sawa na Uislaam na Ukristu wapo watu wanaslimu kila siku, Biblia na Kuran ndio lugha zetu, matendo yetu ndio yanatupa Uumini wa kweli.
Kisha huwezi kusema two wrongs kwani kuna matatizo gani Canada au Swiss ambayo yametokana na jamii hizo kujiunga nje!.. Je, unataka kunambia hata sisi kuwa huru inawezekana kuwa ni makosa hivyo hakuna haja ya kuwa huru.
 
Waberoya,
Mkuu sijasema kwamba sisi tuko hatua, mguu kwa mguu na Canada ama Swiss. wao walianza hivyo na leo wana enjoy matunda yake, nasi tumefikia hatua ambayo wao walipitia ktk kutoa maamuzi.
Kwa hiyo mifano kama hii inaweza kutusaidia sisi kufikia maamuzi unless una mfano wowote ambao unaonyesha kwamba kujiunga na vyombo kama hivi kutaleta mfarakano kwa mfano nchi fulani ilitokea blaaablaa blaaa lakini hatuwezi kutoa maamuzi yetu kwa kutumia hadithi za kufikirika!
 
Back
Top Bottom