Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Na kwanini sheria za Jinai zisitumike hizo hizo za kiislamu kwa muislamu anayetaka kutumika sheria za kadhi? au ndio kuchagua iliyo bora kwako na kuacha unayo ona itakuumiza?

Hapana ni kwa kuwa sheri za jinai zinaambatana na mambo ya utawala/administrations kwa hiyo kwa kuwa nchi sio ya kiislamu... na utawala ni wakichotara.. mahakama ya ki-serikali ita-prevail...
 
Asante Kitilime, kwa mafundisho yako yalio Bora, lakini nikipata wasaa nitaomba unielimishe zaidi. Sehemu ambazo nitaona zina hitaji ufafanuzi au elimu zaidi. Au tumwite Professour Safari? Shivji/ Dr Sengondo Mvundi wataulemishe zaidi.
 
Katika sheria hiyo ya Kiislamu ndio inatambua kwamba wale watakaokuwa hawajaelewana kuhusu mgawanjo wa mirathi na n.k. watapeleka shauri lao kwenye mahakama ya kadhi.

suppose wewe umeoa, mkeo anafanya kazi n a wewe pia una kazi nzuri. mmeshirikiana kujenga nyumba, kuanzisha miradi na mmejaliwa kupata mtoto mmoja wa kike. Bahati mbaya sana (mungu apishe mbali) ukatangilia mbele ya haki. Utaridhika mkeo apate mgao wa kathumuni kwenye mirathi yako? Au pengine unieleweshe mgao hapa utakuwaje kwa mkeo na mwanao.



Hapa ndio watu wengi wanatoka nje ya mstari, ili mahakama ya sasa ikidhi haja ya mahakama ya kadhi, maana yake tusomeshe mahakimu Quran (maana hii ndio katiba yao). na hata hivyo haitakuwa suluhisho! waislamu wana hoja kwamba kama ndoa ilitambuliwa,,, namna ya kuivunja itambuliwe,,, na vyote viwili viko kwenye vitabu vyao... mahakama ya kadhi iko kwenye vitabu vyao.

hapa ndio kazi ingine inazuka. Nani atasomesha hao mahakimu Qoran? watkuwa wapya au ni wale ambao tayari ni mahakimu?
na Je, ajira ya waislam katika mahakama za kawaida itasitishwa ili ku-balance ajira kati ya waislam na wakristo katika idara ya mahakama?(au mahakama ya kadhi haitakuwa chini ya idara ya mahakama, maana inaweza kuongozwa na makafiri)
Katika kusomeshwa, at whose expense? kama ni serikali itagharamia, ita-justify vipi hizo kodi za wakristo?
na kama watajilipia, ni kigezo gani kitatumika kuhakikisha baada ya kusomeshwa wataajiriwa?

Makosa mengi ya kijinai (hapa ni mawazo yangu) ni ya kiutendaji/utawala na kwa kuwa Tanzania sio dola ya kiislamu... Mahakama ya Ki-serikali inachukua mkondo.

wezi, wagoni,wabakaji..wana adhabu zao ndani ya sheria za kiislam; haya sio makosa ya kiutendaji, ni jinai kamili. waislam watakubali kuona wagoni wao wakilipishwa faini ya sh 20,000 mahakama ya kawaida wakati mahakama ya kiislam ipo?

Kwanza sheria za dini ya kiislamu kwenye mambo ya ndoa/nirathi haziendi tofauti na hizo zinazoitwa haki za binadamu, hence hakuna haja ya kujitoka kwenye kuridhia mikataba. Only tunekuwa kwenye jinai pia huko ndio kungekuwa na tatizo ya mitazamo

Wrong! Given time naweza kukuainishia sheria/vipengele rundo zima zinazokinzana na haki za binadamu kama zinavyojulikana na katika ulimwengu wa haki za binadamu

Sasa huwezi lazimisha wenye imani zao wamwamini mdhaifu George Bush.

We have no choice my bro...beggars are not choosers...

Ume-missquote; wamekataa kuleta katiba mpya, marekebisho wanafanya kwa sasa yalishafikia 11

Marekebisho ya kuingiza suala la mahakama ya kadhi linahitaji 'major uverhauling' its more like Katiba mpya, at least ndivyo ninavyoona
 
JF amani ya Bwana iwe Nanyi...MKJJ thanx kuieleta hii Barazani...

Mahakama ya Kadhi muulizen MREMA, naye amekuwa akiipigia debe..may be nae alikuwa anatafuta kura za waislam au kuipata rangi CV yake mbele ya waislam.

Mahakama ya Kadhi ilikuwepo since ukoloni, ambayo wao ndio wamekuja kuwabatiza watu. alipokuja Nyerere yeye ndie aliivunja hii na Asasi zingine za waislam. Waislam wameenza kudai hili since wakati wa mwalim naye alikuwa akiwafunga masheikh na wengine kuwafukuza waende kwao Z'bar..wakati Muungano Tayari ushajengwa...
Mliochangia hii mada wengi hamkusoma sharia. Hata kama mngesoma the so called secular laws..basi siku moja mwalim wenu angewagusia Kuhusu ISlamic Laws...Niwaulize wajumbe hivi Kenya na Tanzania wapi kuna muslim wengi?...jibu 100% ni Tanzania...Kenya wanazo Mahakama za kadhi...
Dini zingine hazina sheria, if that is true, ukristo ukitekeleza tu zile amri 10 basi waislam wenyewe watafurahi...lkn yale ni makatazo tu hayana hukumu...

(kwa mnaotaka Takwimu nendeni taasis ya Takwim Tanzania, muone juu ya Tanzania hali ikoje...)


Mahakama ya Kadhi muulizen MREMA, naye amekuwa akiipigia debe..may be nae alikuwa anatafuta kura za waislam au kuipata rangi CV yake mbele ya waislam.

Chuma, Kama alivyofanya Mrema kutafuta kura za Waislam ndivyo CCM ilivyofanya.

Mahakama ya Kadhi ilikuwepo since ukoloni, ambayo wao ndio wamekuja kuwabatiza watu. alipokuja Nyerere yeye ndie aliivunja hii

Ni vema ujue kuwa Wakoloni wa Kiingereza waliruhusu hilo kwa makusudi ili waendelee kututawala bila upinzani; wao ndiyo walioleta nia divide and ruleili tujione kuwa tuko toafuti na kutupunguzia nguvu. Nyerere aliliona hilo ndo maana akafuta hiyo Mahakama! Pia ni vizuri ujue kuwa hao Wakenya na Wauganda unaodai kuwa wanazo Mahakama hizo wamegawanyika sana na hizo Mahaka za Kadhi zimechangia migawanyiko yao.

Dini zingine hazina sheria, if that is true, ukristo ukitekeleza tu zile amri 10 basi waislam wenyewe watafurahi...lkn yale ni makatazo tu hayana hukumu...

Ni vema ujue kuwa hakuna dini yoyote isiyokuwa na sheria; kila dini ina sheria zake tofauti na dini nyingine na kila dini ikitaka ku-impliment sheria zake Tanzania haitakuwepo tena; pia ujue kuwa hakuna haja ya kuwa na sheria mama.

Sheria za Ukristo haziruhusu mtu apigwe mawe hadi kufa kwa kosa la uzinzi lakini za Kiislamu zinaruhusu, sasa je, Musilamu akizini na Mkristo na Wakakamatwa unadhani Mkristo atatendewa haki kwa mujibu wa sheria ya dini yake?

(kwa mnaotaka Takwimu nendeni taasis ya Takwim Tanzania, muone juu ya Tanzania hali ikoje...)[/

Chuma, acha blah-blah tuletee hizo takwimu hapa; wengine wetu hawako Tanzania, tuletee hiyo source yako ili mjadala uwe na details.
 
Mimi nasema Ole!

Huko Nigeria ilishawahi kutokea Waislamu walivamia kituo cha Polisi na kumchukua Mtuhumiwa mmoja aliyedaiwa kuukashifu Uislamu na wakamuhukumu kuuwawa na wakamuua! Sasa hapa itakuwaje katika nchi yetu?

Hii inanikumbusha hadithi ya kisa cha Mwarabu na Ngamia!
 
Huko mnakoelekea mimi simo!!! hayo mambo ya statistics hayatusaidi chochote and i'm not interested even to know them.
 
Huko Nigeria ilishawahi kutokea Waislamu walivamia kituo cha Polisi na kumchukua Mtuhumiwa mmoja aliyedaiwa kuukashifu Uislamu na wakamuhukumu kuuwawa na wakamuua! Sasa hapa itakuwaje katika nchi yetu?
!

Ibrah,

Kule Nigeria kuna states zinaongozwa kiislam, hizo ndizo zina issue kama hizo, kama ilivyo nchi zinazoongozwa kwa sharia huko middle east, hapa Tanzania hakuna nia yakuwa na Islam states hivyo huna haja ya kutoa mifano mikali kwa watanzania unatakakupotosha mada...

Mahakama ya Kadhi kuwepo, ni ushahidi kamili kwamba kuna mahakama zingine za katiba, ardhi, biasha, watoto, wanawake, wanasiasa etc...............
 
Huko mnakoelekea mimi simo!!! hayo mambo ya statistics hayatusaidi chochote and i'm not interested even to know them.

Kitilime
Hizo jazba za watu wengine achana nao, hata mimi kuna mahali nikiona muelekeo haufai na kaa kimya, au nikijibu napuuza upuuzi huo nakushikilia mada inayojadiliwa.
Wewe tupe vitu vya kibusara kwa faida yetu na yule anayekosea ikiwezekana quote his/her statement then weka vitu vyako vya kibusara.Ili aelewe kuwa amepotoka na anakokuwenda siko.
Ingekuwa walokole wanasema wanamrudisha kundini. Maana amepotoka
 
Ibrah,

Kule Nigeria kuna states zinaongozwa kiislam, hizo ndizo zina issue kama hizo, kama ilivyo nchi zinazoongozwa kwa sharia huko middle east, hapa Tanzania hakuna nia yakuwa na Islam states hivyo huna haja ya kutoa mifano mikali kwa watanzania unatakakupotosha mada...

Kilitime,
Sijapotosha mada wala sina nia hiyo; NATOA ANGALIZO TU!
Na ndiyo maana nikakumbuka Kisa cha Mwarabu na Ngamia; wakijua vema kisa hicho Kilitime!

Kumbuka kuwa kuhesabu kwaanzia na namba 1 kisha waendele kuhesabu; Vivyohivyo alphabeti huanzia na A kisha B, kisha C, kisha... hadi Z! Kisha yaleyale ya Kisa cha Ngamia na Mwarabu.

Asante!
 
Ibrah,

Poa tumerudi kwenye msitari!!! (kundini); hoja nyingine?
 
Kwa uzoefu wangu, wakati wa mfungo wa Ramadhani, baadhi ya Waislam wenye maduka ya vyakula (achilia mbali migahawa), hapa Dar na hususan Zanzibar, hukataa kumuuzia mteja vitu (vyakula au vinywaji) vinavyoweza kuliwa papo kwa papo (mfano kashata, bajia, maandazi na soda) mpaka baada ya waumini kufuturu.

Kuna matukio ya watu kuadhibiwa Zanzibar kwa vile walionekana wakila hadharani (mchana) wakati wa mwezi mtukufu. Nakumbuka mmoja alifikishwa polisi (alikuwa mtalii) na mwingine alishambuliwa na "watu wenye hasira kali".

SWALI:
a) Ilikuwaje watu hao walituhumiwa kuvunja sheria inayokataza waislam kula mchana wakati wa mfungo ilhali wao hawakuwa waislam?

b)Je, Mahakama ya Kadhi inaweza kusimamia masuala kama haya?

c) Inawezekana mtuhumiwa fulani akifikishwa mbele ya kadhi akakana kuwa muislam (au kujitoa kwenye dini papo hapo) na hivyo atakuwa huru?
 
Technically waislamu ndio wengi zaidi Tanzania. Kwanza ni lazima mtambue the fact kuwa polygamy ambayo haki ya waislamu ni fertile ground ya population explotion, halafu uangalie kuwa kwenye maeneo mengi ambayo uswahili unaendekezwa kuwepo kwa bastards(children born out of wedlock). Na kuna sehemu za pwani hata watu wanajidai kwa kuwa na watoto nje ya wedlock, Mimi nadhani pamoja na kuwa mbunge alikuwa anasema kutoka hewani anaweza kuwa sahihi. Wanajambo msifiche!
 
Hayo maswali nafikiri ni muhimu watu wanaojua watujibu. Sidhani kwa jinsi maisha yalivyokwisha kuwa westernised namna hii watu waisilam watakubali mambo kama ya mirathi yaende huko kadhi!!
 
LAKINI MKUMBUKE PIA KUWA WAISLAMU WAKIANZISHA MAHAKAMA HIYO, ITABIDI WAKRISTO NAO WAANZISHE MAHAKAMA YAO, KWA SABABU HAITAKUWA FAIR kuwe na two leagl systems, nadhani hiyo mahakama ikianzishwa soon kutakuwa na sharia. KWELI BONGO KUNA SERIKALI.
 

Majibu yanafuata chini ya maswali pamoja na kwamba maswali yako nje scope ya mada hii:-
a) Ilikuwaje watu hao walituhumiwa kuvunja sheria inayokataza waislam kula mchana wakati wa mfungo ilhali wao hawakuwa waislam?
Kama nilivyowahi kusema huko nyuma, this will apply for an Islamic states only, Zanzibar is not an islamic state, hence consider as if watu wenye hasira wampiga na kumua kibaka pale manzese kwa mfuga mbwa!!! au pale Unga limited -Arusha. Hili ni tatizo la kijinai kwa hiyo linapelekwa kwenye mahakama za kichotara/ki-serikali.

b)Je, Mahakama ya Kadhi inaweza kusimamia masuala kama haya?
Hapana, out of scope, mahakama hii itajikita kwenye mambo ya ndoa na miradhi. (nukta)

c) Inawezekana mtuhumiwa fulani akifikishwa mbele ya kadhi akakana kuwa muislam (au kujitoa kwenye dini papo hapo) na hivyo atakuwa huru?
Kabla ya kwenda kwenye mahakama ambayo ni kama rufaa baada ya famili kushindwa kutatua shauri, mahakama hiyo haiwezi sikiliza chochote kama haitakuwa imedhibitisha na kujiridhisha kwamba ndoa yenyewe imefungwa kiislamu... sasa kama umedhibitsha hili, hilo la kujitoa kwenye dini wakati ambapo ulifunga ndoa ya kiislamu halitakuwa na mantiki hivyo sheria ya mahakama ya kadhi itafuata mkondo wake.
 
Kitime, majibu mazuri. Lakini itakuwaje kama mmoja wa wanandoa si mwislamu, na yeye awe na regime nyingine ya sheria kuhusu mirathi? na ile sheria ya mirathi ya kawaida Tanzania haitatumika kwa waislamu?
 
Ibra mifano ya Nigeria its irrevalent, unless Hoja za Majimbo za Chadema zikikubaliwa...maana ktk majimbo watu wenye Mila Fulani watakuwa sehem maalum...
1. Nilipokutajia Mrema, nilikusudia yeye mkristo ambaye anaUADUI Mkubwa na waislam, lkn kwa yeye kuikubali si tu ku-implement, inaonesha nae ameikubali...for whatever motives behind...

2.Hoja yako ya Waingereza kuruhusu Kadhi ilikuwa kuwagawanya watu si Sahihi, Mission ya Uingereza ilikuwa kuleta Ukristo, hivyo any mission ambaye ingeathiri kuenea kwa ukristo basi angeipiga marufuku, kama alivyopiga matumizi ya Kiarabu ktk Tanganyika ktk ngazi za Serikali na kuweka kupeleka Funds za kujenga mashule kanisani. So Suala la Kadhi waliliaccept kutokana na historia yao ya kutawala sehem zenye uislam wengi..Uingereza walishindwa kutawala Nigeria...ndio maana mtawala alieletwa Tanzania alishajua technique gani za kutumia kuishi na muslims...

3.....cont later
 
Kitime, majibu mazuri. Lakini itakuwaje kama mmoja wa wanandoa si mwislamu, na yeye awe na regime nyingine ya sheria kuhusu mirathi? na ile sheria ya mirathi ya kawaida Tanzania haitatumika kwa waislamu?

Kama mmoja wa wanandoa sio muislamu, ndo hufungwa kwa heri ya kamishna (DC)... sheria za nchi kwa mahakama za serikali zina-prevail.

Ni watu tu walioamua ndoa yao iwe ya kiislamu na pia wanaweza amua wenyewe kabla ya matatizo kwamba tu-divorce tutumie sheria za mahakama za kawaida za kiraia.
 
LAKINI MKUMBUKE PIA KUWA WAISLAMU WAKIANZISHA MAHAKAMA HIYO, ITABIDI WAKRISTO NAO WAANZISHE MAHAKAMA YAO, KWA SABABU HAITAKUWA FAIR kuwe na two leagl systems, nadhani hiyo mahakama ikianzishwa soon kutakuwa na sharia. KWELI BONGO KUNA SERIKALI.


HILI HALINA USHABIKI, WAISLAMU WANATAKA HILI KWA KUWA KITABU CHAO KINATAMKA HIVYO.

WAKRISTO KITABU CHAO HAKITAMKI HIVYO, NA WAKRISTO NI WATU MAKINI WAWEZE FANYA MAMBO KISHABIKI KAMA WANASIASA
 
HILI HALINA USHABIKI, WAISLAMU WANATAKA HILI KWA KUWA KITABU CHAO KINATAMKA HIVYO.

WAKRISTO KITABU CHAO HAKITAMKI HIVYO, NA WAKRISTO NI WATU MAKINI WAWEZE FANYA MAMBO KISHABIKI KAMA WANASIASA

Some reasoning indeed!

By the way, hujanisaidia kwenye zile issue zangu tatu hivi nilizokuuliza kwenye no.73 Majibu yako yatanisaidia kupata mwanga zaidi katika suala hili.
 
Back
Top Bottom