Ni jambo la kusikitisha sana kuona viongozi wa dini wa Kikristo, hasa Wakatoliki, wakikataa katakata Tanzania kujiunga na OIC. Sababu wanayoitoa ni kwamba Tanzania sio nchi ya kidini hivyo haiwezi kujiunga na OIC ambacho ni chombo cha Waisalamu.
Wakati wanaendelea kushushumalia Tanzania isijiunge na OIC, wao wana vyombo mbalimbali vya Kikatoliki hapa Tanzania vinavyowaunganisha na Wakatoliki dunia nzima.
Kwa mfano, Balozi wa Vatican ambaye ni Mwakilishi wa Papa yupo hapa Tanzania. Isitoshe, wana chombo chao cha kimataifa kuhusu masuala ya elimu hapa Tanzania kiitwacho Tanzania Episcopal Conference ambacho kimetapakaa dunia nzima.
Kwa nini wao waruhusiwe kuwa na vyombo vya kidini vya kimataifa wakati Waislamu wakataliwe?
Kibaya zaidi ni kwamba wakati Tanzania inakataliwa kujiunga na OIC, nchi zingine kama Uganda, Cameroon, Nigeria na Mozambique, Ivory Coast ni wanachama wa OIC na wanafaidika na misaada wanayopata kutoka OIC.
Huu ni ubeberu uliopindukia. Hali hii haikubaliki hata kidogo na waislamu wataendelea kupigania haki yao hii mpaka waipate au Wakristo wa Tanzania na wao wasiruhusiwe kujiunga na vyombo vya kidini vya kimataifa.
Mods muwe wavumilivu na mawazo tofauti ya members ili mradi hayavunji kanuni za JF na sheria za nchi. Mjitahidi kuzuia unazi wenu.
Aluta Continua.
Hapo kwenye
red, are you serious? "Tanzania Episcopal Conferences" imetapakaa DUNIA NZIMA! Ha ha ha!
Ubalozi wa Vatican: Vatican ni nchi kama zilivyo Iran na Saudi Arabia. Rais wa Vatican (ikijulikana pia kama Holy See) ni Pope. Balozi wa Vatican yupo Tanzania akiwakilisha nchi yake sawa sawa na mabalozi wa nchi nyingine kama nilizozitaja hapo juu wanavyowakilisha nchi zao. Mwisho, Vatican ni mwananchama wa UN.
HOJA: Naomba unifahamishe "nchi" ya OIC iko wapi (bara gani au angalau iko kati ya latitudes na longitudes zipi), rais wake ni nani, na ina ubalozi katika nchi zipi, na kama ni mwanachama wa UN au la.
Nchi nyingine kuwa wanachama wa OIC: Kwanza Tanzania sio Uganda na wala sio Ivory Coast. Mbona huongelei upande wa pili wa shilingi; kwanini nchi nyingine sio wanachama wa OIC? Mbona hilo hulioni? Au ni Tanzania pekee ndio sio mwananchama wa OIC?
Katiba na Malengo ya OIC: Kaisome vizuri Katiba ya OIC, uielewe kisha uje hapa ufafanue malengo ya hiyo taasisi. Kwa kuwa baadhi yetu ni wavivu wa kusoma zaidi ya akili za kushikishwa, pata "highlights" kuhusu OIC hapa:
Oic Constitution na uache kupotosha watu.
Waislamu kujiunga na OIC: Hakuna anayekataa waislamu kama waislamu kujiunga na OIC bali kikwazo ni taifa kama taifa lenye watu wa dini mbalimbali kujifunga kwenye minyororo na taasisi ya dini moja. OIC ina vikao vyake mbalimbali na kati ya hivyo kuna vya wakuu wa nchi wananchama hapo inakuwaje?
Ushauri: Tuache kupotosha; badala yake tuzungumzie vitu kwa uhalisia wake. Kuna taasisi nyingi sana za kikristo, kihindu, kibudha, kiyahudi, n.k. duniani ambazo Tanzania sio mwananchama na haiwezi kuwa mwananchama kutokana na malengo na Katiba za taasisi hizo sawasawa na ilivyo kwa OIC. Hata hivyo taasisi husika za kidini hazizuiliwi kuwa wanachama.