mimi huwa nashangaa sana, kama mtu unauwezo wa kuingia jamii forum na ukapost kitu kwa nini uwezo huo huo usiutumie kwenda kwenye Google au Altavista au Ask uka-type swali lako, au unachotaka kujua kisha ukasoma maelezo yake? au huzijui hizo search engine kaka? ok do this, nenda kwa address bar yako/URL/hapo unapoingiza www.jamiiforums.com kisha weka hii Google au hii Yahoo! Search - Web Search au hata hii Ask.com Web Search halafu ingiza kwa search bar Vatican kisha ikishakupa majibu soma wewe mwenyewe ujue Vatican ni nini,(usije sema sisi ndo tumekupotosha Vatican ni nin, soma mwenyewe kadri uwezavo) halafu search pia hiyo TEC au (Tanzania Episcopal Conference) ujue nayo ni nini, kisha ndo uje hapa tujadiliane.
Fanya uchunguzi wako tu mkuu, kisha njoo na hoja mezani, tunakuahidi kuzijibu hoja zako bila tatizo na kwa uhakika.
Huwezi kuichunguza Vatican kwa ku search kwenye Google etal. Unaichunguza kuangalia mwenendo wake jinsi inavyo behave na hii hutoipata kwenye mitandao hiyo. Vatican ipo pale kujenga interests za Wakatoliki dhidi ya dini na madhehebu mengine yote duniani na kwa hiyo HAIFAI kupewa ubalozi kwenye nchi zisizo za Katoliki rasmi hasa kwenye nchi zetu hizi za kimasikini. NUKTA.