Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi


quote_icon.png
By Dr.W.Slaa


Wana JF,

Nashukuru mwana JF aliyeweka hadharani MOU husika
. Ningependa tu kuongezea machache na hasa historia ya jinsi na kwanini MOU hiyo ilizaliwa:-

1)
Wote mtakumbuka kuwa huko nyuma Serikali ilitaifisha Shule na nyingi za madhehebu ya Dini. Utaifishaji huo uliendana pia na Ardhi, hasa ikizingatiwa kuwa wakati shule zinajengwa zilijengwa kwenye maeneo ya madhehebu ya dini na papo hapo kukukiwa na kanisa, nyumba za mapadre na kadhalika. Hii ilikuwa hivyo kwa shule nyingi za Middle School (Model Schools, Upper Primary kama mnavyojua majina yalibadilika sana kati ya 1962 hadi 1965 hivi na ndipo pia mtihani au darasa la nane lilipofutwa rasmi).

2)
Kwenye miaka ya 1980 madhehebu yakataka warudishiwe ardhi yao, hasa ardhi ambayo ina majengo mengine yasiyohusiana na shule hizo. Mchakato wa mjadala ulishika kasi, mwaka 1986 Baraza la Maaskofu Katoliki TEC, lilipopitisha azimio rasmi,na kumtaka Katibu Mkuu, awasiliane na Serikali, kuanzisha mchakato wa kufanya survey na kutenga ardhi ya shule rasmi kutoka kwenye ardhi inayotumika kwa huduma nyinginezo za madhehebu ya dini. Wakati huo mimi Dr. Slaa, ndiye nilikuwa Katibu Mkuu wa TEC baada ya kupokea rasmi kazi hiyo December, 1985. Wakati huo madhehebu yaliisha kudai yarudishiwe Shule zao kwa kuwa zimegeuka kuwa aibu kwa kukosa ukarabati, na ziko kwenye hali mbaya sana. Serikali ilikuwa imekataa ombi hilo kwa lengo la kuwa Shule hizo zinawahudumia watanzania wote bila ubaguzi, jambo ambalo ndilo lilikuwa lengo kuu la utaifishaji, na sababu ya utaifishaji ilikuwa bado inaendelelea.

3) Wakati mawasiliano yalipoanza na Serikali wakati huo kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Elimu, Serikali iliomba TEC na madhehebu ya Dini kwa ujumla, kama yanaweza kusaidia ukarabati wa shule hizo kwa kuwa ziko kwenye hali mbaya na hali ya uchumi wa nchi haikuwa nzuri na hivyo mapato ya Serikali.

4) Wakati mchakato huo kwa upande wa Elimu umeanza kulikuwa pia na mgogoro kati ya Serikali na TEC baada ya Serikali kuichukua Hospitali ya Bugando almost kwa utaratibu huo huo wa kuitaifisha. Hospitali hiyo ilikuwa kwenye awamu ya Pili ya ujenzi kwa msaada mkubwa wa Shirika la Misereor( Shirika la Maendeleo la Baraza la Maaskofu Katoliki la Ujerumani) toka Ujerumani.

5) Katibu Mkuu wa TEC alipowasiliana na Wahisani walikataa kata kata kujihusisha tena na ujenzi au ukarabati wa Shule au Hospitali ( Hospitali, vituo vya Afya na zahanati) kwa kuhofia kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikitaifisha huduma hizo bila majadiliano ya aina yeyte, na hawawezi kuwekeza fedha za walipa kodi wao ( ujerumani Madhehebu ya dini yanapata fedha rasmi kutoka kodi ya wananchi) kwa ratio waliyokubaliana kuendana na idadi ya madhehebu ya dini. Lakini walikuwa tayari kuendelea na huduma mbalimbali za kusaidia madawa na elimu kwa shule zilizoko bado chini ya madhehebu kwa kuwa hawawezi kuwaadhibu wananchi na watoto.

6) Kwa kuwa shughuli zote za Bugando zilikuwa zinaelekea kusimama na kulikuwa na mgomo kila siku, kwa madaktari na manesi na watumishi, Serikali ikaomba tujadiliane upya juu ya mambo makubwa mawili :
a) Utoaji huduma katika sekta za huduma za Jamii,
b) Kuwa na chombo cha mawasiliano na majadiliano kati ya Ikulu na madhehebu ya dini, na kwa kuwa madhehebu ni mengi wakaomba chombo hicho kiundwe na viongozi wakuu wa madhehebu yaliyokuwa yanajulikana kwa mujibu wa Sheria.

Hivyo Bakwata ( Waislamu- sitaki kuingia kwenye mjadala wa kama Bakwata ni chombo kinachowasilisha waislamu au la), Tanzania Episcopal Conference TEC na CCT ( kwa madhehebu zaidi ya 60 yaliyoko chini ya Christian Council of Tanzania) . Baada ya Mashauriano tuliunda chombo hicho kikiwakilishwa na Mwenyekiti na Katibu wa vyomb o nilivyovitaja hapo juu. Uratibu ulikuwa unabadilika kila mwaka katika ya madhehebu hayo, vivyo hivyo kwa Sekretariat. Kutokana na utaratibu huo tuliweza kupatia ufumbuzi matatizo yaliyokuwa yakijitokeza mara kwa mara na ikawa rahisi kwa Serikali kuwasiliana na chombo hicho badala ya kila dhehebu peke yake, na kwa upande wetu pia chombo hicho kikatupa nguvu ya kujadiliana na serikali (power of negotiation).

7) Kutokana na hali mbaya ya Shule Serikali, ikaomba madhehebu ya dini kusaidia ukarabati wa shule zilizoonekana zitafungwa kutokana na hali mbaya , nasi kwa upande wetu kwa nia njema ya kuisaidia Serikali lakini pia kuwahudumia watanzania tuliwasiliana na Wahisani ambao walikazia msimamo wao kuwa hawako tayari kuingia kwenye shughuli za ujenzi wala ukarabati kwa kukosa msimamo wa wazi na au wa kisheria wa Serikali ya Tanzania kuhusiana na utaifishaji wa huduma hizo. Serikali ilipojulishwa, ilichukua hatua ya kuanzisha mchakato mzima wa kupata suluhu ya jambo hilo. Ndipo akapewa jukumu hilo, Mhe. Anne Makinda wakati huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, na mkutano wa kwanza ulifanyika Kurasini Conference Centre (TEC) Mikutano ya baadaye ilikuwa ina alternate kati ya TEC na CCT. Hii ni kwa sababu huduma zilizokuwa zinajadiliwa ni za TEC na CCT ( ambao walikuwa wameathirika na utaifishaji huo). Hatimaye, Serikali ilikubali kuwa haitataifisha tena, na kwa kuthibitisha hivyo, ikawa tayari kuwekeana MOU na madhehebu ya Dini.
Ndipo tukaanzisha mchakato wa majadiliano na Wahisani, na wahisani, nao katika umoja wao kati ya dhehebu la kikatoliki Ujerumani na Kilutheri pia la Ujerumani tukaanzisha mchakato wa namna bora ya kutoa huduama za jamii. Daima Serikali ilishirikishwa kama Observer katika michakato hiyo, na kwa upande wa Ujerumani Serikali yao nayo ilishirikishwa katika timu za majadiliano. Hatimaye, makubaliano yalifikiwa, na ndipo ikazaliwa chombo kipya Christian Social Services Commission (CSSC), chenye Secretariat yake ( Katibu Mtendaji wa kwanza akawa Dr. F.Kigadye aliyekuwa Mkurugenzi wa Bugando).

Huduma za kilichokuwa Christian Medical Board (ya TEC na CCT ikavunjwa na kuwekwa chini ya CSSC) na idara za Elimu zilizokuwa chini ya TEC na CCT huduma zake zikaunganishwa na kuwekwa chini ya CSSC. Ndiyo MOU iliyosainiwa na Askofu Stanford Shauri wa Diocese ya Ruvuma, Mwenyekiti/Katibu Mkuu wa CCT wakati huo, na Askofu Josephat Lebulu, wakati huo Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, na Mwenyekiti wa TEC. Kwa upande wa Serikali kama sikosei aliweka saini Mhe. Edward Lowassa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (au Waziri sikumbuki).

8) TEC na CCT nazo zikawekeana na Wahisani Mkataba MOU yao ya ndani ili kupata misaada ya ujenzi, ukarabati na uendelezaji wa huduma zote za jamii . Huduma hizo zinaendelea hata sasa japo sasa kwa kiwango kidogo baada ya mkataba wa awali kwisha.

Narudia tena, namshukuru sana aliyeweka kwenye JF MOU hiyo.
Ninarudia kuwaomba wenzangu, tumetumia muda mrefu sana kujadiliana kwa hisia ya aina mbalimbali. Watanzania hatukuzoea huko nyuma kuulizana dini zetu, wala kabila wala ukanda. Haya mambo tukiyaendekeza Taifa letu litakuwa hatarini. Tukumbuke kubomoa ni kazi nyepesi sana, sekunde lakini kujenga tena inachukua muda mrefu na ni kaz ngumu, na wakati mwingine hata ukifanikiwa huwezi kujenga kama ilivyokuwa. Nashauri ili JF ibaki na heshima yake ya Home of Great Thinkers tupende kufanya Research zaidi kabla ya kulaumiana au kuhisiana, kama mtu hana taarifa za kina awaombe wenye taarifa. Kama mnavyoona mimi nilikuwa nafahamu historia yote, nafahamu MOU, lakini sikuwa nayo. Mtu huwezi kujua kila kitu na au kuwa na kila kitu, we need to complement each other. Tunaweza tukidhamiria, na JF itabaki na hadhi na heshima yake daima.
______________________________ _____________________
mijitu haielewi Hata ukiielewesha mifano bado haielewi wewe ngoja uhuru huu tulionao tu naona Kama ni mchezo ila siku ya watu kule a mabegi mgongoni kukimbia
 
Hivi Kadhi wa Zanzibar anafanyaje kazi bila mahakama?

Anayejua utendaji wake atujuze
 
Nilikuwa sipo samahani sana ila hili suala lipo hivi..
1. watu wote ambao kwa hiyari yao wenyewe watakubali kufunga ndoa za kiislamu watakuwa subjected kwenye mahakama ya Kadhi kwa misingi ya kuwa Ndoa,Talaka, Mirathi na waqfu yote hayo yatasimamiwa na mahakama ya Kadhi (Qadh). Hizo ndio kazi za mahakama hiyo. Jinai haihusiki hapo
2. Kulinyima bunge kupitisha sheria ya mahakama ya Kadhi ni kuwanyonga waislam nina hukumu za kesi kama 18 ambazo nimezipitia zote zikiwa zimeamuliwa ambavyo sivyo. Inatakiwa bunge lipitishe sheria ambayo itairuhusu mahakama ya Kadh kusimamia hivyo vitu sio mtu anafunga sheria kiislam halafu ikija akipewa talaka anakataa naenda kwenye mahakama nayo inasema talaka ni batili wakati kwa mujibu wa dini ni sawa kabisa. Sasa ikiwepo sheria inayo itambua mahakama hii itakuwa vizuri mahakama ya kawaida haita husika. Ila kwa mfano mke akimpiga mme au mume akimpiga mke hiyo ni jinai inaenda kwenye mahakama ya kawaida
3. kuhusu huduma ya hiyo mahakama waislam hawana shida maana makadh wanaweza wakakaa hata kwenye ofisi zao wnazotumia sasa hivi na wakalipwa kwa wao wenyewe wajuavyo ila muhimu sheria ya nchi itambue hilo.
 
Nilikuwa sipo samahani sana ila hili suala lipo hivi..
1. watu wote ambao kwa hiyari yao wenyewe watakubali kufunga ndoa za kiislamu watakuwa subjected kwenye mahakama ya Kadhi kwa misingi ya kuwa Ndoa,Talaka, Mirathi na waqfu yote hayo yatasimamiwa na mahakama ya Kadhi (Qadh). Hizo ndio kazi za mahakama hiyo. Jinai haihusiki hapo
2. Kulinyima bunge kupitisha sheria ya mahakama ya Kadhi ni kuwanyonga waislam nina hukumu za kesi kama 18 ambazo nimezipitia zote zikiwa zimeamuliwa ambavyo sivyo. Inatakiwa bunge lipitishe sheria ambayo itairuhusu mahakama ya Kadh kusimamia hivyo vitu sio mtu anafunga sheria kiislam halafu ikija akipewa talaka anakataa naenda kwenye mahakama nayo inasema talaka ni batili wakati kwa mujibu wa dini ni sawa kabisa. Sasa ikiwepo sheria inayo itambua mahakama hii itakuwa vizuri mahakama ya kawaida haita husika. Ila kwa mfano mke akimpiga mme au mume akimpiga mke hiyo ni jinai inaenda kwenye mahakama ya kawaida
3. kuhusu huduma ya hiyo mahakama waislam hawana shida maana makadh wanaweza wakakaa hata kwenye ofisi zao wnazotumia sasa hivi na wakalipwa kwa wao wenyewe wajuavyo ila muhimu sheria ya nchi itambue hilo.

Sasa mtu kama aliolewa kwa taratibu za dini ya kiislamu, halafu anapeleka malalamiko kwingine, huyo naye bado mnamwita mwislamu? Kwani akienda kwa viongozi wa dini kupeleka shauri lake serikali itamlazimisha aliondoe huko alilete mahakama za kiraia?
 
crome20 utaniswamehe moja kwa kuwa wewe mwenyewe ukiiangalia katika hadhi yangu ya uwanachama humu utaona bado ni ndogo kwa hiyo sio mjuzi zaidi katika kutumia hii forum. Najifunza ndio maana nachelewa kujibu.
Kuenda kwake kwa mahakama ya kawaida haibatilishi yeye kuwa muislam au ile ndoa kuto vunjika. Hebu niambie wewe umemuacha halafu yeye anaenda mahakama za kawaida halafu hakimu anasema ndoa hio ni batili.
Ki halisi ninazo hukumu za kesi 18 zilizo amuliwa vibaya nitaziweka hapa ndio naandika mukhtasari wake. Kuna moja iliyonichekesha ni ya huyu muhindi na mswahili walio oana na kuzaa mtoto wakaachana mtoto akiwa na miezi miwili mahakama ikaamua mwanaume amchukue mtoto na mtoto akanyonyweshwe na dada wa mume kwa kuwa ana mtoto mdogo ki sayansi sio vizuri na bado dini hairuhusu. Inatakiwa anyonyeshwe na mama mpaka miaka miwili baada ya hapo ndio baba anaweza akamchukua. Mambo kama haya ni ajabu kabisa
 
crome20 utaniswamehe moja kwa kuwa wewe mwenyewe ukiiangalia katika hadhi yangu ya uwanachama humu utaona bado ni ndogo kwa hiyo sio mjuzi zaidi katika kutumia hii forum. Najifunza ndio maana nachelewa kujibu.
Kuenda kwake kwa mahakama ya kawaida haibatilishi yeye kuwa muislam au ile ndoa kuto vunjika. Hebu niambie wewe umemuacha halafu yeye anaenda mahakama za kawaida halafu hakimu anasema ndoa hio ni batili.
Ki halisi ninazo hukumu za kesi 18 zilizo amuliwa vibaya nitaziweka hapa ndio naandika mukhtasari wake. Kuna moja iliyonichekesha ni ya huyu muhindi na mswahili walio oana na kuzaa mtoto wakaachana mtoto akiwa na miezi miwili mahakama ikaamua mwanaume amchukue mtoto na mtoto akanyonyweshwe na dada wa mume kwa kuwa ana mtoto mdogo ki sayansi sio vizuri na bado dini hairuhusu. Inatakiwa anyonyeshwe na mama mpaka miaka miwili baada ya hapo ndio baba anaweza akamchukua. Mambo kama haya ni ajabu kabisa

Nikusaidie kidogo ndugu yangu. Nina maana kuwa kama unaielewa vizuri na kuiamini dini yako, jambo kama hilo utalipeleka kwa viongozi wako wa dini. Nao watakufungulia msaafu na ufafanuzi wake, na kama unaimani na kitabu hicho basi utatulia, au utatafuta ufafanuzi wa kina kwa wale unaoona wana ujuzi wa mambo ya dini kuliko hao wa mwanzo. Hivyo kukimbilia mahakama za kiraia ni ushaidi kuwa huna imani na na mwongozo wa dini yako.

Mahakama haiwafuati watu katika kesi kama hizi, ni sisi tunaopeleka madai yetu huko kama yameshindikana kwa viongozi wetu wa dini.
 
mbona rais alisha lizungumzia na akalitolea maamuzi hili swala na mufti mkuu analijua hilo
 
Kupeleka suala la mahakama ya kadhi kwa wananchi ni matumizi mabaya ya fedha za walipakodi. Ni kweli kila jambo kama hili si vibaya kupeleka kupata kibali cha serikali na kibali hicho tayari kimetolewa kwa waislamu kuunda mahakama yao ya kadhi zaidi wanataka nini kuhusu wao? Kama ni kibali wanataka kitolewe na madaraka fulani waseme mambo yaishe. Kupeleka kwa wananchi ni kutumia vibaya hele za umma kwanza umma uridhishwe na sababu za kulipeleka suala hili kwa wananchi bila upendeleo.
 
Hili jambo linaendelea kisiasa maana si kazi ya serikali yoyote isiyo ya kidini kuanzisha, kuimarisha au kuendesha ustawi wa dini yoyote zaidi ya kutoa uhuru kwa waumini kuanzisha na kustawisha dini yoyote ili mradi sheria za nchi kamwe hazivunjwi kwa lengo kuwa serikali yetu ya Tanzania haina dini. Waislamu wanasema wakianzisha mahakama ya kadhi basi wakiamua serikali isiingilie na namna ya kuhakikisha hilo wanataka Bunge lipitishe mahakama ya kadhi.

Ukweli katika nchi yoyote hakuna uhuru usio na kikomo. Waislamu watakuwa na uhuru zaidi katika kuamua mambo ya mahakama ya kadhi kama watainzasha wenyewe kuliko mahakama ya kadhi ikianzishwa na Bunge kwa sababu:
  1. Serikali iliishawapa Waislamu kibali cha kuanzisha mahakama ya kadhi.
  2. Waislamu waanzishe wenyewe mahakama ya kadhi au BUnge lipitishe mahakama ya kadhi, bado muumini atakuwa na haki ya kukata rufaa popote katika mamlaka ya nchi kama ilivyo sasa. Vinginevyo:
    • muumini ana njia nyingine ya kuasi dini kabla au baada ya hukumu ya mahakama ya kadhi na
    • uongozi kumfukuza katika dini pale anapokataa kutii hukumu ya mahakama ya kadhi.
  3. Waislamu wakianzisha mahakama ya kadhi, serikali haitaingilia maamuzi yao pale maamuzi hayo hayavunji sheria za nchi. Serikali haitaingilia uendeshaji wa mahakama hiyo isipokuwa ndani ya waumini wenyewe.
  4. Lakini watake wasitake, mahakama ikipitishwa na Bunge na kugharimiwa na serikali (yaani na walipa kodi wote) basi ni dhahiri kila mtu binafsi au kupitia uwakilishi wowote (i.e ni wadau) atakuwa na haki ya kuingilia
    • mwenendo na uendeshaji wake,
    • maamuzi yake na
    • hata baadaye ni rahisi kuvunja mahakama ya kadhi kwa manufaa ya nchi.
  5. Moja ya sababu nyingine ni kutaka walipa kodi woote katika nchi wagharimie mahakama ya kadhi kitu ambacho kitawapunguzia waislamu umiliki na uendeshaji wa mahakama ya kadhi maana serikali itataka kujua matumizi ya mahakama ya kadhi na kudhibiti matumizi hayo kwa ajili ya kuwajibika kwa walipa kodi. Ikibidi serikali inaweza hata ikawa na haki ya kuteua viongozi na mahakimu (kama sehemu ya kusimamia na kudhimiti matumizi) jambo ambalo linaweza kuleta mzozo kama ule wa Bakwata. Hawataendesha mahakama ya kadhi kwa uhuru wanaoufikiria ukilinganisha na wao wenyewe watakapoanzisha mahakama ya kadhi bila ya Bunge.
 
cha ajabu na kusikitisha zaidi kwa wale wanaoikataa mahakama ya kadhi isitambulike kikatiba wana nia gani kwan kuna mtu atalazimisha watu wakatolewe hukumu huko au mbona kenya ipo na hakuna tatizo acheni chuki nyinyi
 
Kuna watu wanaotaka tuamini kuwa suala la Kadhi linawahusu waislamu wao peke yao. Ukweli wa mambo ni kuwa suala hili ni la Watanzania wote na tuna haki ya kulizungumzia. Ninazichambua hoja dhaifu za kina Ponda Issa Ponda, Khalifa Khamisi na Mufti. KLH News... yote yanazungumzika!!!

Back with a vengeance... www.mwanakijiji.podomatic.com

Masuala ya dini yashughulikiwe na dini husika bila kulazimisha ushiriki wa serikali. Serikali isiimamie kwamba hayo yanayoanzishwa na dini hizi hayavunji sheria za nchi.

HATUTAKI SERIKALI KUANZISHA MAHAKAMA ZA KIDINI TANZANIA.
 
Ni jambo la kusikitisha sana kuona viongozi wa dini wa Kikristo, hasa Wakatoliki, wakikataa katakata Tanzania kujiunga na OIC. Sababu wanayoitoa ni kwamba Tanzania sio nchi ya kidini hivyo haiwezi kujiunga na OIC ambacho ni chombo cha Waisalamu.

Wakati wanaendelea kushushumalia Tanzania isijiunge na OIC, wao wana vyombo mbalimbali vya Kikatoliki hapa Tanzania vinavyowaunganisha na Wakatoliki dunia nzima.

Kwa mfano, Balozi wa Vatican ambaye ni Mwakilishi wa Papa yupo hapa Tanzania. Isitoshe, wana chombo chao cha kimataifa kuhusu masuala ya elimu hapa Tanzania kiitwacho Tanzania Episcopal Conference ambacho kimetapakaa dunia nzima.

Kwa nini wao waruhusiwe kuwa na vyombo vya kidini vya kimataifa wakati Waislamu wakataliwe?
Kibaya zaidi ni kwamba wakati Tanzania inakataliwa kujiunga na OIC, nchi zingine kama Uganda, Cameroon, Nigeria na Mozambique, Ivory Coast ni wanachama wa OIC na wanafaidika na misaada wanayopata kutoka OIC.

Huu ni ubeberu uliopindukia. Hali hii haikubaliki hata kidogo na waislamu wataendelea kupigania haki yao hii mpaka waipate au Wakristo wa Tanzania na wao wasiruhusiwe kujiunga na vyombo vya kidini vya kimataifa.

Mods muwe wavumilivu na mawazo tofauti ya members ili mradi hayavunji kanuni za JF na sheria za nchi. Mjitahidi kuzuia unazi wenu.

Aluta Continua.
 
Ni kweli thread hii haihitaji unazi bali weledi na nguvu iwe ktk hoja. Nami nimekuwa na maswali ya howling jambo hebu waje wenye kujua kwa nini ndugu wa upande wa Pili kiimani hawataki ishu ya IOC
 
Kama msingekuwa wavivu wa kupekua au kusoma mngeshapata hicho mnachokitaka kwa sababu hii ni moja kati ya topic zilizozungumzwa kwa mapana na nmarefu humuhumu JF.
Sodhani kama kulikuwa na haja ya kufungua uzi mwingine kwa jambo hili unless kuna sababu nyingine iliyojificha

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wivu unawasumbua,B.membe alishawahi kusema mbele ya bunge kuwa tz kujiunga na oac haina tatizo,kwani hata hao wakiristo watanufaika nayo,na hii ni kutokana uchunguzi aliofanya.
 
Back
Top Bottom