Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Mahakama ya kadhi ipate ruzuku kutoka serikalini kwa kuwa waislam wanalipa kodi hivyo ni haki yao wala sio hisani
 
Nafikiri kama WaTz mtatumia akili zenu na kuangalia Hoja hii kiuchumi na kuweka nyume nyuma UDINI basi mtaona namna ilivyowapuruchuka. Lakin mngetazama kwa wenzenu Uganda na hata msumbiji.

Kwani kama nyie mlishindwa kusoma lakin hata kuangalia jirani zako wakoje mnashindwa.

Poleni sana

naomba uorodheshe faida wanazopata msumbiji na uganda mkuu? unionyeshe pia tofauti ya kiuchumi kati ya tanzania na nchi hizo mbili kutokana na OIC na kadhi.
 
Mahakama ya kadhi ipate ruzuku kutoka serikalini kwa kuwa waislam wanalipa kodi hivyo ni haki yao wala sio hisani

sadaka mnazotoa kazi yake ni nini? au unafikiri sadaka ikitolewa huwa baadae sheikh anafanya fund transfer kwa njia ya TISS au EFT kwenda kwa Mungu? nafikiri ni busara mkitumia sadaka kuendesha hiyo biashara yenu, kodi ya Tanzania inatokana na pombe sijui kama ni halali kuendesha ofisi ya dini kwa kutumia ruzuku ya pombe labda kama kuna wasanii wanataka wawe wanapiga hela kupitia uchochoro huu, vinginevyo ni ngumu, hapa sadaka ndo kila kitu msiwe mnatoa sadaka kama maiti mnatakiwa kuhoji matumizi ya sadaka na hesabu zikaguliwe, toa ndugu kila ulicho na nacho sio kwa kizazi hiki cha watoto wa nyoka.
 
Mahakama ya kadhi ipate ruzuku kutoka serikalini kwa kuwa waislam wanalipa kodi hivyo ni haki yao wala sio hisani

Na ikumbukwe wenzao wakristo wanazoa 91 Bilion kila mwaka kufuatia MoU kati ya kanisa na Serikali ya JMTz.
 
naomba uorodheshe faida wanazopata msumbiji na uganda mkuu? unionyeshe pia tofauti ya kiuchumi kati ya tanzania na nchi hizo mbili kutokana na OIC na kadhi.

Mbona nimeyayabainisha sana sana humu barzani lakin kwa kukusaidia angalia mADA UA Mou ya kanisa na Serikali ya JMTz utaona nimebainisha kila kitu na nimejikita zaidi sababu za kiuchumi .
 
Mbona nimeyayabainisha sana sana humu barzani lakin kwa kukusaidia angalia mADA UA Mou ya kanisa na Serikali ya JMTz utaona nimebainisha kila kitu na nimejikita zaidi sababu za kiuchumi .

rudia kusoma swali langu naona hatuelewani? swali la nyongeza kuna sheria inakatza msikiti kuingia mou na serikali?
 
Na ikumbukwe wenzao wakristo wanazoa 91 Bilion kila mwaka kufuatia MoU kati ya kanisa na Serikali ya JMTz.

andaa mou upeleke serkalini ili msikiti nao uwe unapewa mara mbili ya hiyo, sijui kama unajua mou inaandaliwa vp na una justify na nini? sio nipewe kwa sababu fulani anapewa, unaweza ukapewa hiyo pesa yote ukaenda kununua mikeka na korani vitu ambavyo pay back period yake ni infinity.
 
Hujui unalonena.

Hata richmond ilikuwa hivi hivi. Kila mtu aandike kwa nia ya kudhulumu na kuiibia serikali yenu masikini.

Nakupa Pole.

Lakin ukweli lazima usemwe hata kama hamtasikia lakin siku moja mambo yatakuwa sawia tu. Soma bandiko la Mou uone nilichobainisha kwa kina ili kikusaidie na kukuwezesha kujenga hoja na ilikuleta uhondo kwenye mnakasha huu.

hakuna serikali inatoa hela bila justification ya kile kinachokwenda kufanyika na hiyo pesa na uhakika hata hiyo OIC haiwezi kutoa hela kwa sababu shehe ponda kaomba lazima wafanye appraisal na kuridhika na ombi lako, serikali imeingia mou na kanisa kwa sababu kanisa lina hospital, lina vyuo, lina mashule yaliyojengwa kwa sadaka yametapakaa everywhere na ni kwa watanzania wote, nani kawakatazeni kujenga mashule, hospitali na vyuo kwa kutumia sadaka ?
 
Wana topic hii mimi nakuwa na maswali mengi sana na wakati mwingine nabaki mdo wazi na nisipate majibu hata ya kukujibu ama kujibiwa,ukweli ni kwamba hawa wenzetu ni kweli kwamba hawana muda wa kuperuzi na kudadisi yan kifupi hawasomi vitu na kuelewa kabisa na hata viongozi wao wanaosema wanajua vitu hawawapi mwanga mzuri wanaowaongoza jamani ndugu zetu waislam tatizo lipo wapi?????binafsi ntapenda niongelee neno KAFIRI Na kwa nini waislam wanalitumia ndivyo sivyo? Na hii ina maana nzuri kwa muislam anayetaka mahakama ya kadh bila kuelewa madhara yake ni yapi kwa ushabiki asioujua fuatilia hii!
Neno kafiri lina asili ya kiarabu.Tafsiri yake sahihi ni MPINGAJI WA MANENO YA MWENYEZI MUNGU.Biblia ilitangulia na Quran ilifuata.Kitabu cha kwanza cha mungu kuwepo ni Biblia ,hivyo Quran imekuja kuipinga Biblia.kwa maneno haya basi,waislam wote ni makafiri kwan wanatupinga wakristo na kitabu chetu cha Biblia.Alipozaliwa Muhamad(s.a.w)mwaka 570A.D aliwakuta wakristo wapo na wameshapewa Neno la mungu(Biblia).Mkristo hawezi kumpinga muislam,bali muislam ndiye anayempinga mkristo.Ni sawa na kusema kuwa,Baba amefanana na mtoto wake,kumbe si kweli kwani mtoto ndiye anayefanana na baba yake.Huwezi kupinga kitu ambacho hakipo kwani mpaka tarehe 17.12.610A.D,Dunia nzima hapakuwepo na mwislam hata mmoja uislam umeanza mwaka huo wa 610A.D tarehe 17.12 usiku wa manane na mwislamu wa kwanza dunian alikuwa ni mkewe Muhamad Bib Khadija.{Rejea kitabu cha maisha ya Muhamad uk wa 18.
Wadau kwa maelezo hayo machache nisitoke nje ya maada ila nachosisitiza ni kwamba hawa watu wanahitaji elimu ya hali ya juu sana wapunguze jazba wasome vitu waelewe kabla ya kukurupuka tu bila msingi wowote.:crazy:
 
By marikiti Mahakama ya kadhi ipate ruzuku kutoka serikalini kwa kuwa waislam wanalipa kodi hivyo ni haki yao wala sio hisani

(kama una uhakika na hili fafanua tu si kuongea kama mnywa kahawa)
 
hakuna serikali inatoa hela bila justification ya kile kinachokwenda kufanyika na hiyo pesa na uhakika hata hiyo OIC haiwezi kutoa hela kwa sababu shehe ponda kaomba lazima wafanye appraisal na kuridhika na ombi lako, serikali imeingia mou na kanisa kwa sababu kanisa lina hospital, lina vyuo, lina mashule yaliyojengwa kwa sadaka yametapakaa everywhere na ni kwa watanzania wote, nani kawakatazeni kujenga mashule, hospitali na vyuo kwa kutumia sadaka ?
Safi sana Kamanda hawa watu wanahitaji mtazamo Chanya Kama huu sio wawe wanaropoka bila evidence
 
Wana topic hii mimi nakuwa na maswali mengi sana na wakati mwingine nabaki mdo wazi na nisipate majibu hata ya kukujibu ama kujibiwa,ukweli ni kwamba hawa wenzetu ni kweli kwamba hawana muda wa kuperuzi na kudadisi yan kifupi hawasomi vitu na kuelewa kabisa na hata viongozi wao wanaosema wanajua vitu hawawapi mwanga mzuri wanaowaongoza jamani ndugu zetu waislam tatizo lipo wapi?????binafsi ntapenda niongelee neno KAFIRI Na kwa nini waislam wanalitumia ndivyo sivyo? Na hii ina maana nzuri kwa muislam anayetaka mahakama ya kadh bila kuelewa madhara yake ni yapi kwa ushabiki asioujua fuatilia hii!
Neno kafiri lina asili ya kiarabu.Tafsiri yake sahihi ni MPINGAJI WA MANENO YA MWENYEZI MUNGU.Biblia ilitangulia na Quran ilifuata.Kitabu cha kwanza cha mungu kuwepo ni Biblia ,hivyo Quran imekuja kuipinga Biblia.kwa maneno haya basi,waislam wote ni makafiri kwan wanatupinga wakristo na kitabu chetu cha Biblia.Alipozaliwa Muhamad(s.a.w)mwaka 570A.D aliwakuta wakristo wapo na wameshapewa Neno la mungu(Biblia).Mkristo hawezi kumpinga muislam,bali muislam ndiye anayempinga mkristo.Ni sawa na kusema kuwa,Baba amefanana na mtoto wake,kumbe si kweli kwani mtoto ndiye anayefanana na baba yake.Huwezi kupinga kitu ambacho hakipo kwani mpaka tarehe 17.12.610A.D,Dunia nzima hapakuwepo na mwislam hata mmoja uislam umeanza mwaka huo wa 610A.D tarehe 17.12 usiku wa manane na mwislamu wa kwanza dunian alikuwa ni mkewe Muhamad Bib Khadija.{Rejea kitabu cha maisha ya Muhamad uk wa 18.
Wadau kwa maelezo hayo machache nisitoke nje ya maada ila nachosisitiza ni kwamba hawa watu wanahitaji elimu ya hali ya juu sana wapunguze jazba wasome vitu waelewe kabla ya kukurupuka tu bila msingi wowote.:crazy:

Ee bwana hivi, bibble alishushiwa mtume nani kama: qur-an - Muhamad,taurati-Mussa; injili -Issa na zaburi - Daudi? Kukusaidia M/Mungu alikuwa na utaratibu wa kuleta mjumbe(mtume) kila baada ya watu kupotoka/kupotosha na kuach mafundisho yake, aliwaletea mjumbe ku-revive, watakaomfuata hao wamejisalimisha kwake(waislamu),wataopinga hao ndio makafiri. Sasa baada ya Yesu kuondoka baadhi ya watu walipotosha na kubadilisha mafundisho yake na kutunga dini yao wakaiita kristo ndaniya kitibu chao kiitwacho bibble, Mungu kutaka kurudisha mafundisho sahihi ndipo alipomleta Muhammad, hivyo yoyote mwenye kumpinga yeye km kawida ataitwa kAFIri. Je wewe unampinga au anafuata mandisho yake!? Lakini pia uislamu ukiwa na maana ya 'submission to one God''haukuanzishwa na Muhammad ila aliuiisha(revive) km walivyofanya waliopita, ulikuepo tokea dunia kuanza ndoo maana haupingani na muongozo sahihi wa vitabu/mitume iliyopita km Ibrahim,Daudi,Suleiman,Enock,Mussa,Issa(Yesu) etc.
 
Mimi ninavyojua Serikali yetu haina dini. Ukitaka kila imani iwe na jinsi yake ya kuamua kesi basi unakaribisha dini ndani ya serikali na wewe ni hatari sana kuliko hata Shekh Osama Bin Laden na haufai katika jamii. Habari ya Imam ni mpang mkamilifu kutoka nchi za Kiarabu na mpango wa OIC. Tuliyoyasikia Nigeria yatakuja kwetu. Kwa nini tusiamini mahakama zetu? Kama zina matatizo basi turekebishe na sio kuingiza kitu cha imani fulani, hili halifai kabisa.
Chama kikizidiwa kinatumia mbinu chafu kulazimisha ushindi. Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Mei 1, 1995 akizungumza na wafanyakazi Mbeya alianza kuhofia mfumo wa vyama vingi na kusema: “Nataka kusema kauli ya mwisho kuhusu sheria ya uchaguzi ilivyo sasa hivi. Ninalo tatizo moja. Hili nataka kulisema kwa sababu nadhani ni la msingi kidogo. Tulipokubali tuwe na vyama vingi vya siasa tulisema kwamba hivi vyama vingi vina migogoro. Mnaweza mkawa na chama cha dini, kabila,….”
Mwalimu alionesha hofu tunayoiona leo. Tumeshuhudia viongozi wa vyama wakitugawa kwa misingi ya imani na dini zetu. Hata wakati mwingine wakihubiri udini, ukabila kwa lengo la kufanikiwa kisiasa, bila kuwa na huruma na hatima ya Watanzania au taifa hili.
Mwalimu aliongeza: “Tulisema sisi hapana ni taifa changa. Lazima tujihadhari na chama kinachoweza kutugawa. Tunataka chama kinachokubali umoja. Kwa hiyo, tukakataa vyama vya udini, ukabila na vya kutenganisha Tanzania…”
Mwalimu aliyaona haya miaka 20 iliyopita, alianza kuona jinsi ambavyo vyama vya siasa vinaweza kushiriki kutugawa kwa misingi hiyo. Leo utasikia wanaitana: “wewe msomali/Mnyaruanda, au mhindi hutakiwi kugombea hapa.” wameanza na wataishia kuuana wenyewe. Tunaitaka Tanzania yetu yenye umoja na mshikamano. Waislamu waendelee kugoma kukataa uongo wa wanasiasa.
 
Ee bwana hivi, bibble alishushiwa mtume nani kama: qur-an - Muhamad,taurati-Mussa; injili -Issa na zaburi - Daudi? Kukusaidia M/Mungu alikuwa na utaratibu wa kuleta mjumbe(mtume) kila baada ya watu kupotoka/kupotosha na kuach mafundisho yake, aliwaletea mjumbe ku-revive, watakaomfuata hao wamejisalimisha kwake(waislamu),wataopinga hao ndio makafiri. Sasa baada ya Yesu kuondoka baadhi ya watu walipotosha na kubadilisha mafundisho yake na kutunga dini yao wakaiita kristo ndaniya kitibu chao kiitwacho bibble, Mungu kutaka kurudisha mafundisho sahihi ndipo alipomleta Muhammad, hivyo yoyote mwenye kumpinga yeye km kawida ataitwa kAFIri. Je wewe unampinga au anafuata mandisho yake!? Lakini pia uislamu ukiwa na maana ya 'submission to one God''haukuanzishwa na Muhammad ila aliuiisha(revive) km walivyofanya waliopita, ulikuepo tokea dunia kuanza ndoo maana haupingani na muongozo sahihi wa vitabu/mitume iliyopita km Ibrahim,Daudi,Suleiman,Enock,Mussa,Issa(Yesu) etc.
Chama kikizidiwa kinatumia mbinu chafu kulazimisha ushindi. Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Mei 1, 1995 akizungumza na wafanyakazi Mbeya alianza kuhofia mfumo wa vyama vingi na kusema: “Nataka kusema kauli ya mwisho kuhusu sheria ya uchaguzi ilivyo sasa hivi. Ninalo tatizo moja. Hili nataka kulisema kwa sababu nadhani ni la msingi kidogo. Tulipokubali tuwe na vyama vingi vya siasa tulisema kwamba hivi vyama vingi vina migogoro. Mnaweza mkawa na chama cha dini, kabila,….”
Mwalimu alionesha hofu tunayoiona leo. Tumeshuhudia viongozi wa vyama wakitugawa kwa misingi ya imani na dini zetu. Hata wakati mwingine wakihubiri udini, ukabila kwa lengo la kufanikiwa kisiasa, bila kuwa na huruma na hatima ya Watanzania au taifa hili.
Mwalimu aliongeza: “Tulisema sisi hapana ni taifa changa. Lazima tujihadhari na chama kinachoweza kutugawa. Tunataka chama kinachokubali umoja. Kwa hiyo, tukakataa vyama vya udini, ukabila na vya kutenganisha Tanzania…”
Mwalimu aliyaona haya miaka 20 iliyopita, alianza kuona jinsi ambavyo vyama vya siasa vinaweza kushiriki kutugawa kwa misingi hiyo. Leo utasikia wanaitana: “wewe msomali/Mnyaruanda, au mhindi hutakiwi kugombea hapa.” wameanza na wataishia kuuana wenyewe. Tunaitaka Tanzania yetu yenye umoja na mshikamano. Waislamu waendelee kugoma kukataa uongo wa wanasiasa.
 
Mwanakijiji,
Zanzibar waliomba warejeshewe Ofisi ya Kadhi Mkuu, SMZ iliitikia wito huo. Kitu cha ajabu ni malalamiko yaliyojitokeza kwamba kwanini Kadhi Mkuu ateuliwe na Raisi wa Zanzibar. Vilevile wengine walilalamika kwamba kwanini Kadhi Mkuu awe chini ya mamlaka ya Waziri ambaye ni Mkristo, Bw.Adam Mwakanjuki.

Kuleta nafasi ya Kadhi Mkuu kupitia Bunge na Katiba kutaleta migogoro isiyo ya lazima kati ya serikali na Waislamu. Naunga mkono mapendekezo yako kwamba Waislamu waungane wamchague Kadhi Mkuu bila kuishirikisha serikali na vyombo vyake.

Ikiwa Wamaasai wameweza kuwa na mfumo na utaratibu wao wa mila na uongozi sioni kwanini Waislamu washindwe kuwa kitu kimoja na kumchagua Kadhi Mkuu. Wamaasai wana utaratibu wa kuchagua Laigwanan ktk jumuiya ndogo ndogo, halafu kutokana na hao huchaguliwa kiongozi wa Laigwanan wote.

[h=3]Mahakama ya Kadhi na Hoja ya Msingi[/h]

Ni dhahiri kuwa mjadala wa kurejeshwa Mahakama ya Qaadhi kwa Waislamu nchini unaendelea kuchukua sura mpya kutokana na hoja zinazoibuliwa na wadau tofauti kuhusiana na ajenda hiyo muhimu.
Hoja kuu za msingi ni zile zinazotolewa na Waislamu kupitia baadhi ya masheikh na viongozi wa juu wa baadhi ya Taasisi za Kiislamu nchini, na zile zinazotolewa na wakristo kupitia viongozi wao wa dini wa ngazi ya juu kabisa.
Waislam, wao wanadai kuwa Mahakama ya Qaadhi ni haki yako ya msingi waliyopewa na dini yao, kisha nchi yao na hatimae kuporwa haki hiyo katika mazingira ya kutatanisha mnamo mwaka 1963, hivyo kwa mujibu wa msingi huo, na hasa ikizingatiwa kuwa Chama Tawala cha CCM kiliona hoja hiyo na kuiweka katika ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2005-2010, Waislamu wanadai serikali ya CCM iliyopo madarakani hivi sasa itekeleze ahadi hiyo iliyoitoa kwa wananchi na hatimae Waislamu nchini kukipigia kura chama hicho na kushinda ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa mwaka 2005.
Lakini kwa upande mwingine, viongozi wa juu wa madhehebu ya kikristo hawakusita kutoa maoni yao bayana kuwa suala hili kama litapitishwa na Bunge basi litakuwa limekiuka Katiba ya nchi hii, ambayo maongozi yake si ya dini, na aidha itakuwa ni upendeleo kwa kuwapa baadhi ya raia haki hiyo na kuwanyima wengine, hasa ikizingatiwa kuwa Mahakama hiyo itaingizwa katika bajeti za serikali ambazo chanzo chake ni kodi za wananchi wa Tanzania wakiwemo wakristo.
Hizo ni hoja za msingi ambazo ni vema zikajadiliwa kwa utulivu na mantiki bila kuchukua mwelekeo wa ushabiki na kubezana ambako kunaweza kubadilisha sura nzima ya hoja iliyopo.
Sheria za Kiislamu ni moja miongoni mwa vyanzo vya sheria nchini Tanzania, mwaka 1964, Bunge la Tanganyika kwa wakati huo lilipitisha “Sharia ya Kiislamu (Sheria ndogo)” iliyompa madaraka Waziri aliyehusika na mambo ya Sheria kuandaa na kuchapisha kipengele cha Sharia ya Kiislamu baada ya kushauriana na wanachuoni wa Sharia za Madh-hebu za Kiislamu. Na hatimae Katibu Mkuu wa Bunge wakati huo, alikamilisha kuandika Mswada wa ndoa wenye sehemu 4 (kwa msaada wa masheikh wa madh-hebu za Kiislamu).
Mswada huu uliotolewa kama Sharia ndogo chini ya kifungu kidogo cha Sharia ya Kiislamu (Na: 56 ya mwaka 1964) ikiwa ni sehemu ndogo ya Gazeti la Serikali na Na: 34 la tarehe 27, Juni, 1967.
Ilifahamika kuwa sehemu zilizosalia, kuhusiana na kuwalea watoto na talaka n.k. zingechapishwa mapema. Lakini zoezi hili lilisitishwa na badala yake serikali ilitunga sheria ya ‘Ndoa’ kupitia Mswada wa Ndoa wa mwaka 1971.
Hata hivyo, kwa mujibu wa kumbukumbu zangu, kanuni ya Sheria ya Kiislamu 1964 bado haijafutwa na bado ni sehemu ya Kitabu cha Bunge.
Hoja ya msingi hapa ni kuwa sheria hizo zilikuwepo, pamoja na kutokuwepo kwa Mahakama ya Qaadhi, aidha sheria husika katika mswada jadiliwa zinahusiana tu na yale mambo ya Ndoa, Talaka, Mirathi, na malezi ya watoto kwa Waislamu na hazigusi kabisa uhuru wa raia wengine katika kuabudu dini zao.
Hoja nyingine ya kuwa kuanzishwa kwa Mahakama ya Qaadhi kutawabagua raia wengine wasio Waislamu, pamoja na kuwa raia wote wa Tanzania wataichangia Mahakama hiyo kupitia kodi zao, ni hoja ya msingi, lakini ni vema ikaeleweka kuwa, katika mfumo wa Demokrasia, kodi za wananchi baada ya kukusanywa na serikali, matumizi yake huidhinishwa na Bunge ambalo ndilo linalowakilisha wananchi kupitia wawakilishi wao, aidha ilani ya Chama cha Mapinduzi ilikuwa wazi kabla ya uchaguzi, na inaeleweka kuwa chama hujinadi kwa wapiga kura kupitia ilani yake ya uchaguzi, hivyo ilikuwa ni vema hoja hizi zikaibuka wakati huo, na labda kukishinikiza Chama Cha Mapinduzi wakati huo kuondoa kipengele hicho katika ilani ambayo ni ahadi kwa wapiga kura wake kwamba kama watawaingiza madarakani basi watatekeleza waliyowaahidi.
Kwa mtazamo wangu, kuitaka serikali ya CCM kuiangalia upya ahadi hiyo ambayo ni itikio la ombi la wananchi ni kutoitakia wema Serikali, na madhara yake yatakuwa ni makubwa kwa taifa letu kuliko haya yanayodhaniwa kuletwa na Mahakama ya Qaadhi, kwani yataibua hisia za chuki na kutotakiana mema baina ya waumini wa Dini mbili kuu nchini, na zitahatarisha kuondoa usamehevu (Tolerance) na kuzidisha ufa wa kitaifa.
Hoja yangu ya msingi katika mjadala huu itawahusu walengwa wa mswada huo ambao ni Waislamu, ambao dhahiri wanaonekana wamoja katika kutetea haki hii ya msingi ya kuwa na Mahakama ya Qaadhi, lakini ndani yao kuna hofu,woga na minun’guniko ya jinsi Qaadhi huyo atakavyopatikana na mipaka ya majukumu yake kwa Waislamu.
Hofu hizo za baadhi ya Waislamu, zinatokana na ukweli kuwa mara nyingi kama sio zote, serikali ya Chama Chama cha Mapinduzi imekuwa ikiangalia Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kama msemaji rasmi wa Waislamu Tanzania,na msimamizi mkuu wa maendeleo ya Waislamu nchini, jambo ambalo si sahihi.
Dhana hiyo ambayo ina ukweli mkubwa ndani yake, kama itatumika katika suala zima la kuanzishwa Mahakama ya Qaadhi,basi mahakama hiyo huenda ikakosa ridhaa za Waislamu wengi nchini, na ikalisababishia taifa hasara kubwa ya fedha na muda. Hii inatokana na ukweli usiopingika kwa mtafiti yeyote, na mfuatiliaji wa mambo ya Waislamu kuwa Bakwata kama chombo hakikubaliki kwa Waislamu wengi wa Tanzania, na wengi hawasiti kusema bayana kuwa Bakwata haipo pale kwa ajili ya maslahi ya Waislamu.
Hofu nyingine ya msingi ni jinsi Qaadhi Mkuu atakavyopatikana, zile hatua zitakazowezesha (mechanism) kupatikana kwa Qaadhi, kama atateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au atateuliwa na jopo la wanazuoni wa Kiislamu ikiwa atateuliwa na Rais, ni dhaahir kuwa atakapokuwa Rais si Muislamu uteuzi huo utapingana na aya za Qur-aan zinazozuia asie Muislamu kuwachaguliwa Waislamu kiongozi wao pamoja na kuwa baadhi ya masheikh wanaweza kuzitafsiri aya hizo ili zihalalishe uteuzi huo. Ukweli utabaki palepale, na kundi kubwa la Waislamu wanaweza kujitenga na mahakama hiyo kutokana na misingi ya itikadi zao.
Kwa upande mwingine ikiwa Qaadhi Mkuu atateuliwa na Jopo la Wanazuoni wa Kiislamu, ni taratibu gani zitakozotumika kulipata jopo hilo na kwa vigezo gani? Hasa ikizingatiwa kuwa Taasisi za Kiislamu Tanzania ni nyingi na zinatofautiana katika mielekeo na maono. Kwa mfano tu, Taasisi za Answaar Sunnah ambazo zina mtandao Tanzania nzima na zina wafuasi wengi na nguvu za kiuchumi na miundo mbinu, zitashirikishwaje katika jopo hilo na kwa kiwango gani?
Hofu yangu ya msingi ni kuwa, Waislamu wengi hawaelewi kinachoendelea na wale wanaoelewa wanaogopa kutoa dukuduku zao kwa kuogopa kuonekana wanapinga jambo la msingi katika Uislamu, au wanashirikiana na wapinzani wa mswada huu jambo ambalo si sahihi kwa dharura.
Kwa kuhitimisha makala hii ningependa kuwarejesha wasomaji katika hoja ya msingi; Mahakama ya Qaadhi haipo dhidi ya waumini wa dini nyingine, bali ni haki ya msingi ya Waislamu ambao ni sehemu ya taifa hili.
Lakini je, Waislamu wako tayari kuyapokea mabadiliko haya ya kihistoria yanayokuja katika zama za utandawazi na mabadiliko makubwa ya mifumo ya jamii? Wakati wakiwa hawana chombo kinachowaunganisha na kulinda maslahi yao? Je viongozi wa Kiislamu ambao wengi wao bado wanaongoza kwa kutumia mifumo ya karne iliyopita, wanaweza kukabiliana na changa moto ya utandawazi, soko huria, na uhuru wa kufikiri miongoni mwa wanajamii?
Kama hatutayaangalia vizuri hayo, nina wasiwasi kuwa Mahakama ya Qaadhi itakuwa ni mtihani mkubwa kwa Waislamu wa Tanzania, na historia na vizazi vijavyo havitatusamehe.
Imekopiwa kutoka Al-Hidaya
 
quote_icon.png
By Dr.W.Slaa

Wana JF,

Nashukuru mwana JF aliyeweka hadharani MOU husika
. Ningependa tu kuongezea machache na hasa historia ya jinsi na kwanini MOU hiyo ilizaliwa:-

1)
Wote mtakumbuka kuwa huko nyuma Serikali ilitaifisha Shule na nyingi za madhehebu ya Dini. Utaifishaji huo uliendana pia na Ardhi, hasa ikizingatiwa kuwa wakati shule zinajengwa zilijengwa kwenye maeneo ya madhehebu ya dini na papo hapo kukukiwa na kanisa, nyumba za mapadre na kadhalika. Hii ilikuwa hivyo kwa shule nyingi za Middle School (Model Schools, Upper Primary kama mnavyojua majina yalibadilika sana kati ya 1962 hadi 1965 hivi na ndipo pia mtihani au darasa la nane lilipofutwa rasmi).

2)
Kwenye miaka ya 1980 madhehebu yakataka warudishiwe ardhi yao, hasa ardhi ambayo ina majengo mengine yasiyohusiana na shule hizo. Mchakato wa mjadala ulishika kasi, mwaka 1986 Baraza la Maaskofu Katoliki TEC, lilipopitisha azimio rasmi,na kumtaka Katibu Mkuu, awasiliane na Serikali, kuanzisha mchakato wa kufanya survey na kutenga ardhi ya shule rasmi kutoka kwenye ardhi inayotumika kwa huduma nyinginezo za madhehebu ya dini. Wakati huo mimi Dr. Slaa, ndiye nilikuwa Katibu Mkuu wa TEC baada ya kupokea rasmi kazi hiyo December, 1985. Wakati huo madhehebu yaliisha kudai yarudishiwe Shule zao kwa kuwa zimegeuka kuwa aibu kwa kukosa ukarabati, na ziko kwenye hali mbaya sana. Serikali ilikuwa imekataa ombi hilo kwa lengo la kuwa Shule hizo zinawahudumia watanzania wote bila ubaguzi, jambo ambalo ndilo lilikuwa lengo kuu la utaifishaji, na sababu ya utaifishaji ilikuwa bado inaendelelea.

3) Wakati mawasiliano yalipoanza na Serikali wakati huo kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Elimu, Serikali iliomba TEC na madhehebu ya Dini kwa ujumla, kama yanaweza kusaidia ukarabati wa shule hizo kwa kuwa ziko kwenye hali mbaya na hali ya uchumi wa nchi haikuwa nzuri na hivyo mapato ya Serikali.

4) Wakati mchakato huo kwa upande wa Elimu umeanza kulikuwa pia na mgogoro kati ya Serikali na TEC baada ya Serikali kuichukua Hospitali ya Bugando almost kwa utaratibu huo huo wa kuitaifisha. Hospitali hiyo ilikuwa kwenye awamu ya Pili ya ujenzi kwa msaada mkubwa wa Shirika la Misereor( Shirika la Maendeleo la Baraza la Maaskofu Katoliki la Ujerumani) toka Ujerumani.

5) Katibu Mkuu wa TEC alipowasiliana na Wahisani walikataa kata kata kujihusisha tena na ujenzi au ukarabati wa Shule au Hospitali ( Hospitali, vituo vya Afya na zahanati) kwa kuhofia kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikitaifisha huduma hizo bila majadiliano ya aina yeyte, na hawawezi kuwekeza fedha za walipa kodi wao ( ujerumani Madhehebu ya dini yanapata fedha rasmi kutoka kodi ya wananchi) kwa ratio waliyokubaliana kuendana na idadi ya madhehebu ya dini. Lakini walikuwa tayari kuendelea na huduma mbalimbali za kusaidia madawa na elimu kwa shule zilizoko bado chini ya madhehebu kwa kuwa hawawezi kuwaadhibu wananchi na watoto.

6) Kwa kuwa shughuli zote za Bugando zilikuwa zinaelekea kusimama na kulikuwa na mgomo kila siku, kwa madaktari na manesi na watumishi, Serikali ikaomba tujadiliane upya juu ya mambo makubwa mawili :
a) Utoaji huduma katika sekta za huduma za Jamii,
b) Kuwa na chombo cha mawasiliano na majadiliano kati ya Ikulu na madhehebu ya dini, na kwa kuwa madhehebu ni mengi wakaomba chombo hicho kiundwe na viongozi wakuu wa madhehebu yaliyokuwa yanajulikana kwa mujibu wa Sheria.

Hivyo Bakwata ( Waislamu- sitaki kuingia kwenye mjadala wa kama Bakwata ni chombo kinachowasilisha waislamu au la), Tanzania Episcopal Conference TEC na CCT ( kwa madhehebu zaidi ya 60 yaliyoko chini ya Christian Council of Tanzania) . Baada ya Mashauriano tuliunda chombo hicho kikiwakilishwa na Mwenyekiti na Katibu wa vyomb o nilivyovitaja hapo juu. Uratibu ulikuwa unabadilika kila mwaka katika ya madhehebu hayo, vivyo hivyo kwa Sekretariat. Kutokana na utaratibu huo tuliweza kupatia ufumbuzi matatizo yaliyokuwa yakijitokeza mara kwa mara na ikawa rahisi kwa Serikali kuwasiliana na chombo hicho badala ya kila dhehebu peke yake, na kwa upande wetu pia chombo hicho kikatupa nguvu ya kujadiliana na serikali (power of negotiation).

7) Kutokana na hali mbaya ya Shule Serikali, ikaomba madhehebu ya dini kusaidia ukarabati wa shule zilizoonekana zitafungwa kutokana na hali mbaya , nasi kwa upande wetu kwa nia njema ya kuisaidia Serikali lakini pia kuwahudumia watanzania tuliwasiliana na Wahisani ambao walikazia msimamo wao kuwa hawako tayari kuingia kwenye shughuli za ujenzi wala ukarabati kwa kukosa msimamo wa wazi na au wa kisheria wa Serikali ya Tanzania kuhusiana na utaifishaji wa huduma hizo. Serikali ilipojulishwa, ilichukua hatua ya kuanzisha mchakato mzima wa kupata suluhu ya jambo hilo. Ndipo akapewa jukumu hilo, Mhe. Anne Makinda wakati huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, na mkutano wa kwanza ulifanyika Kurasini Conference Centre (TEC) Mikutano ya baadaye ilikuwa ina alternate kati ya TEC na CCT. Hii ni kwa sababu huduma zilizokuwa zinajadiliwa ni za TEC na CCT ( ambao walikuwa wameathirika na utaifishaji huo). Hatimaye, Serikali ilikubali kuwa haitataifisha tena, na kwa kuthibitisha hivyo, ikawa tayari kuwekeana MOU na madhehebu ya Dini.
Ndipo tukaanzisha mchakato wa majadiliano na Wahisani, na wahisani, nao katika umoja wao kati ya dhehebu la kikatoliki Ujerumani na Kilutheri pia la Ujerumani tukaanzisha mchakato wa namna bora ya kutoa huduama za jamii. Daima Serikali ilishirikishwa kama Observer katika michakato hiyo, na kwa upande wa Ujerumani Serikali yao nayo ilishirikishwa katika timu za majadiliano. Hatimaye, makubaliano yalifikiwa, na ndipo ikazaliwa chombo kipya Christian Social Services Commission (CSSC), chenye Secretariat yake ( Katibu Mtendaji wa kwanza akawa Dr. F.Kigadye aliyekuwa Mkurugenzi wa Bugando).

Huduma za kilichokuwa Christian Medical Board (ya TEC na CCT ikavunjwa na kuwekwa chini ya CSSC) na idara za Elimu zilizokuwa chini ya TEC na CCT huduma zake zikaunganishwa na kuwekwa chini ya CSSC. Ndiyo MOU iliyosainiwa na Askofu Stanford Shauri wa Diocese ya Ruvuma, Mwenyekiti/Katibu Mkuu wa CCT wakati huo, na Askofu Josephat Lebulu, wakati huo Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, na Mwenyekiti wa TEC. Kwa upande wa Serikali kama sikosei aliweka saini Mhe. Edward Lowassa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (au Waziri sikumbuki).

8) TEC na CCT nazo zikawekeana na Wahisani Mkataba MOU yao ya ndani ili kupata misaada ya ujenzi, ukarabati na uendelezaji wa huduma zote za jamii . Huduma hizo zinaendelea hata sasa japo sasa kwa kiwango kidogo baada ya mkataba wa awali kwisha.

Narudia tena, namshukuru sana aliyeweka kwenye JF MOU hiyo.
Ninarudia kuwaomba wenzangu, tumetumia muda mrefu sana kujadiliana kwa hisia ya aina mbalimbali. Watanzania hatukuzoea huko nyuma kuulizana dini zetu, wala kabila wala ukanda. Haya mambo tukiyaendekeza Taifa letu litakuwa hatarini. Tukumbuke kubomoa ni kazi nyepesi sana, sekunde lakini kujenga tena inachukua muda mrefu na ni kaz ngumu, na wakati mwingine hata ukifanikiwa huwezi kujenga kama ilivyokuwa. Nashauri ili JF ibaki na heshima yake ya Home of Great Thinkers tupende kufanya Research zaidi kabla ya kulaumiana au kuhisiana, kama mtu hana taarifa za kina awaombe wenye taarifa. Kama mnavyoona mimi nilikuwa nafahamu historia yote, nafahamu MOU, lakini sikuwa nayo. Mtu huwezi kujua kila kitu na au kuwa na kila kitu, we need to complement each other. Tunaweza tukidhamiria, na JF itabaki na hadhi na heshima yake daima.
______________________________ _____________________
 
Back
Top Bottom