Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Ishu hii ni ngumu haijadiliki!!!
Nakumbuka bunge liligawanyika wakati likijadili hoja ya kadhi. Rais kikwete kwenye ilani ya uchaguzi ya ccm ya kipindi chake cha kwanza kadhi ilikuwa ni moja ya ahadi zake kwa wananchi lakini imeshindikana na hakuna tamko rasmi la swala hili, shida inaonekana kuwa kadhi ikiruhusiwa kwenye nchi yetu italeta udini na sharia. Ndugu wa tz mimi mtazamo wangu jambo hili ni rahisi tu kwani kadhi hashighulikii kesi za jinai yeye hushughulikia mambo ya waisilamu tena ya ndoa tu, haijishughulishi na wezi wala wabakaji au majambazi.

Ushauri wangu, mbona uchaguzi wa mashekhe, maimamu,maaskofu na wachungaji haupo kwenye katiba? Na viongozi hao wanatuongoza. Tukumbuke kuwa tanzania kila mtu anaruhusiwa kuabudu chochote anachoona ni sawa kwake bila kuvunja sheria za nchi. Shida kwa kadhi ni kutaka pesa kutoka serikalini tu na sio kuitambua, kwani shekhe kaandikwa wapi kwenye katiba na mbona anawaongoza?? Mbona kesi zetu za ndoa wanamabaraza ya kuziamua? Mbona mwapeana talaka kidini na serikali haingilii, nduguzangu kinacho tafutwa hapani sidhani kuwa ni kuwa na kadhi tanzania ila ni kuipa kadhi nguvu dhidi ya mahakama, na jambo hilo halitawezekana. Muislamu akihukumiwa na kadhi vibaya lazima aende mahakama za kisheria za serikali kutafuta haki sasa hili ndio watu wanajaribu kuzuia ili mtu akihukumiwa na kadhi asiwe na pa kwenda.

Mbona wenzenu wakrito wao kesi zao nyingi za ndoa na za kanisa zipo mahakamani??

Uwezo wa kumlipa kadhi mnao msitegemee fedha za ushuru wa bia, sigara na riba kuongoza dini ni mwiko.

Uislamu unauwezo wa kujiendesha na sio kutegemea pesa za kodi za riba na pombe.

Hayo ni mawazo yangu tuu na sio kwa niaba ya mtu.
 
Wewe vp mwenzetu umesoma au bado una matatizo ya udini?

Hata nikikuletea aya hutaielewa na sana sana utakabehi kwani huna nia ya kujifunza hata chembe nishakufatilia muda mrefu hivyo sijihangaishi huko. Nakuletea mistari ya sheria na moja ya principle za sheria ni mihimili ya dola (Doctrine of Separation of Power) na kila moja in a democratic state has its own independence. Amongst them ni Judiciary (au Mahakama) na ndani ya mahakama kuna sheria zimewekwa kuhakikisha amani na upendo katika jamii.

Kwakuwa mnadai this is a secular state and a democratic one hivyo mahakama ni haki ya msingi ya mtanzania yeyote. Sasa iweje haki hiyo mpewe nyie ndugu zetu wakristo na waislamu tunyimwe? Mahakama za sasa zimeshindwa kutatua matatizo ya ndoa, mirathi kiasi kwamba mali za waislamu zimekuwa zikiibiwa na mafisadi kila mahali. Mfano hai ni viwanja vya mayatima na wakfu ambavyo vingi vimeenda kwa watu wasio waaminifu wakitumia taasisi za kidini wakati wazazi wa hao waliofariki wameshatangulia. Sasa nikuulize iko wapi haki ya watanzania hawa???? Au waislamu sio Watanzania.

Vatican mkubwa huna reference ati unadai ni sawa na any Islamic State pambaf kabisa sijui mwenzetu wewe kihiyo. Labda nikuulize kwanini sasa hivi basi US na European allies wanapinga Papa asishitakiwe ICC for crimes against humanity against wale wanaharakati wanaotaka kumshitaki papa kwa kutofanya lolote kuzuia maaskofu wake wasilawiti vitoto vidogo???


Mtu yeyote anayebishania kiimani ni mwenda wazimu, anayetaka haki kupitia dini ni mpumbavu hata kama ana masters, kuna dalili zinaozo onyesha kuwa waisilamu wanataka kupewa special treatment katika mfumo wa kisheria na kijamii, wanadai kuwa wanagandamizwa na mfumo uliopo, wanadai mfumo ulipo ni wakikristo. hizo ni fikara za kipumbafu. hawa watu wakiachiwa mwanya kidogo watafanya serikali ya tanzania kuwa serikali ya kiisilamu na kutawaliwa na sheria za dini, hili ndo wanalo litafuta.
 
Wewe vp mwenzetu umesoma au bado una matatizo ya udini?

Hata nikikuletea aya hutaielewa na sana sana utakabehi kwani huna nia ya kujifunza hata chembe nishakufatilia muda mrefu hivyo sijihangaishi huko. Nakuletea mistari ya sheria na moja ya principle za sheria ni mihimili ya dola (Doctrine of Separation of Power) na kila moja in a democratic state has its own independence. Amongst them ni Judiciary (au Mahakama) na ndani ya mahakama kuna sheria zimewekwa kuhakikisha amani na upendo katika jamii.

Kwakuwa mnadai this is a secular state and a democratic one hivyo mahakama ni haki ya msingi ya mtanzania yeyote. Sasa iweje haki hiyo mpewe nyie ndugu zetu wakristo na waislamu tunyimwe? Mahakama za sasa zimeshindwa kutatua matatizo ya ndoa, mirathi kiasi kwamba mali za waislamu zimekuwa zikiibiwa na mafisadi kila mahali. Mfano hai ni viwanja vya mayatima na wakfu ambavyo vingi vimeenda kwa watu wasio waaminifu wakitumia taasisi za kidini wakati wazazi wa hao waliofariki wameshatangulia. Sasa nikuulize iko wapi haki ya watanzania hawa???? Au waislamu sio Watanzania.
Shida yenu waislam hakuna msimamo,uvivu wa kufikiria ndio ugonjwa wenu,misikiti imewashinda mtaweza mahakama?SIMBA akisema mnampinga?serikali haina dini,ww unataka akupitishie sheria inayokutambua muislam safari yako ya motöni nini?ndio shida ya kudönoa elimu akhera na dunia unajisingizia msomi,MWEUPE kweli kichwani,majungu ndio mtaji!
 
je serikali ya Tanzania inafikiri vipi kuhusu maneno ya Rais wa Iran ambaye anataka kutengeza silaha za Nyuklia za "kuifuta Israel kutoka katika Ramani ya Dunia?"
mzee mwanakijiji ishu iliyopo si kuwa anataka nyuklia ili aifute iran no no ,desire ya kuifuta duniani Waisrael na waarabu ni ya miaka toka enzi za abuilnasser ,ila ni ovious focus iwe kuialifu israel iacahane na maeneo wanayolowea na itoke maeneo yote kwa mujibu wa mipaka ya 1965.
 
Hayo ni mawazo yangu tuu na sio kwa niaba ya mtu.
zhangwei3.jpg

zhangwei4.jpg

zhangwei5.jpg

zhangwei2.jpg
 
Tatizo lenu wachangiaji wote mnaochangia mada hii mnazungumza kishabik zaid. Suala la mahakama ya kadh ni suala la waislam, na ilivo kwa mujib wa sheria za kiislam ni lazima iwekwe na dola. Hii ni dini, ni sheria za mwenyezi mungu ambae ana mjua mwanadam vizuri kuliko tunavojifaham sisi, sio sheria za kujitunga wenyewe ambazo hazina muelekeo, ambazo leo zinaonekana zinafaa keshoyake zimepitwa na wakati. Qur-an haipitwi na wakat hata kidogo. Imeyazungumza mambo yote unayo yafaham na usiyo yafaham kuhusu mwanadam. Sheria za mwenyezi mungu should prevail wakat wote na sio sheria za kujitungia wenyewe (katiba) kama wengi mnavyo shauri. Uislam ni dini pekee ambayo inaeleza mfumo mzima wa maisha ya mwanadam, kuazia kabla hatujakuepo, tukiwopo na baada ya kuwepo (baada ya kuondoka) hapa duniani. Nawasihi waislam wenzangu tuungane pamoja ktk kuismaimisha hakki ktk dunia hii na tuweze kuondoa ufisadi na uonev uliojaa ktk dunia yetu ya sasa, kwani sisi pekee ndo tunaoweza kuiongoza dunia kwa usahihi na kila mmoja akapata haki yake bila dhulma kutendeka. Wabillah tawfeeq. Allah atuongoza na atujaalie qquli thaabit ya kalimatu-tawheed wakat wa saqratu-lmaut. Assalam alaykum warahmatullah wabaraqaat.
 
Waislam jueni kwamba kuna kitu kinaitwa shule sio madrasa tuuuu!

Shule tunazijua na ndo maana tumehitimu vyuo vikuu na watoto wetu wako huko...

Labda nikujuze kuwa waislamu wa sasa wako mbali kielimu, sio wale wa kipindi cha Nyerere....
 
Ndugu zangu ndugu zangu! Tuwe na uzalendo kwa nchi na vizazi vyetu vijavyo. Tuache mijadala yakidini haitusaidii kiuchumi.
 
Naomba watueleze ni madhara gani baadaye yatatokea






Tume ya Kurekebisha Sheria yakabidhiwa jukumu
*Wananchi na wadau wote watakiwa kutoa maoni
*Waziri Nagu awaomba Watanzania waache malumbano
*Aonya yanaweza kuipeleka nchi yetu mahali pabaya


Na Julius Samwel

BAADA ya malumbano ya kuanzishwa kwa mahakama ya Kadhi Mkuu Tanzania Bara kupanda moto, serikali sasa imeamua kuirejesha hoja hiyo kwa wananchi ili waijadili na kutoa maoni yao kama inafaa kuwepo au la.

Hoja ya kuanzishwa kwa mahakama hiyo imezua mvutano mkubwa baina ya viongozi na waumini wa dini za Kikristo na Kiislamu kwa miezi kadhaa sasa.

Wakati waislamu wamekuwa wakipigania kutaka serikali ianzishe mahakama hiyo kupitia sheria ya Bunge, Wakristo kwa upande wao wamekuwa wakiipinga kwa maelezo kuwa itasababisha madhara makubwa katika jamii siku zijazo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Dk Mary Nagu, alisema serikali imeamua kulipeleka suala hilo kwa wananchi kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria, kutokana na malumbano juu yake kuelekea katika kuleta mvutano na mpasuko miongini mwa Watanzania.

"Serikali imeiagiza Tume ya Kurekebisha Sheria kuifanyia kazi hoja hii ili baadaye tume hii iishauri serikali kuhusu ufumbuzi halisi wa suala hili kwa kuzingiatia maslahi ya taifa, historia ya nchi yetu na matakwa ya wananchi," alisema.

Alisema wakati suala hilo linafanyiwa kazi na tume ya kurekebisha sheria, wananchi wote watashirikishwa kwa uwazi mkubwa wakati wote wa mchakato wa huo.

Waziri Nagu alisema serikali itahakikisha inatumia busara na hekima katika kulishughulikia suala hilo na wadau wote watashirikishwa kutoa mawazo yao.

Aliwataka wananchi kuacha malumbano yanayoendelea kwa sasa kuhusu suala hilo na waliachie serikali ilifanyie kazi kwanza.

"Ndugu wananchi, kwa unyenyekevu mkubwa, ninawaomba kwamba malumbano yanayoendelea na yanayoelekea kuleta mvutano na mpasuko miongoni mwetu, tuyaache na kuyaacha kwa maslahi ya taifa letu, ninawaomba sana," alisema.

Alisema ni wajibu wa serikali kushughulikia mambo ambayo yanayonekana kuwa kero, likiwamo suala la kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi kama ilivyoanishwa katika ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2005.

Nagu alisema historia ya jambo hili inaonyesha jinsi ambavyo serikali ilivyolipokea na hatua ilizozichukua na inazoendelea kuzichukua ili kulitafuatia ufumbuzi na kwamba mchakato wa kulitafuatia ufumbuzi bado unaendelea.

Suala la kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi mkuu nchini lilianza 1999 na lilitolewa na na Waislamu kwa Rais Benjamin Mkapa katika kilele cha Sikukuu ya Idd el-fitr na Rais aliahidi kulifanyia kazi.

Baadaye suala hilo liliwasilishwa bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2002 kama hoja binafsi na aliyekuwa Mbunge wa Moshi Vijijini, Thomas Ngawaiya.

Baada ya kuwasilishwa kwa hoja hiyo, Spika wa Bunge, kwa kutumia kanuni za Bunge aliliwasilisha suala hilo kwenye Kamati ya Sheria na Katiba, ambayo iliunda kamati ndogo kwa ajili ya jambo hilo.

Nagu alisema kamati hiyo ilifanya ziara katika nchi za Kenya, Uganda, Musumbiji na Afrika Kusini ili kujifunza namna suala la kadhi linavyoshughulikiwa katika nchi hizo.

Alisema ikiwa Kenya, kamati hiyo iliambiwa kuwa mahakama ya kadhi inatambuliwa na katiba ya nchi na kwamba kuna sheria maalum iliyotungwa ambayo inampa madaraka Rais kuanzisha mahakama hiyo.

Alisema mahakama hiyo ina madaraka ya kusikiliza mashauri ya yanayohusu hadhi binafsi, ndoa, talaka na mirathi pale ambapo wahusika wote ni waislam. Hata hivyo, mahakama hiyo inafanya kazi katika maeneo ya ukanda wa Pwani.

Alisema nchi za Uganda na Msumbiji hazijaanzisha mahakama ya kadhi na kwamba Afrika Kusini inatambua ndoa za Kiislamu na wanaoshughulikia masuala hayo ni viongozi wa kidini wanaoitwa Amir.

Malumbano kuhusu kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi yalianzishwa na maaskofu wa Kanisa Katoliki katika mkutano wao na Rais Jakaya Kikwete miezi michache iliyopita.

Katika mkutano huo, maaskofu hao walimweleza Rais kuwa wamepata taarifa za kuandaliwa kwa muswada wa kuanzisha mahakama ya kadhi na wakaiomba serikali ichukue tahadhari kubwa katika suala hilo.

Siku chache baadaye, viongozi wengine wa kanisa hilo waliitisha mkutano na waandishi wa habari, nao wakieleza kwa kina athari zinazoweza kutokea iwapo mahakama hiyo itaanzishwa kwa sheria ya Bunge, wakisema inaweza kuleta madhara makubwa dhidi ya watu wasiokuwa Waislamu.

Hata hivyo, viongozi na waumini wa dini ya Kiislamu wamekuwa wakisisitiza waachiwe hoja hiyo kwa kuwa inawahusu wao na si waumini wa dini nyingine.

Mbali na Kanisa Katoliki, Kanisa la Kiinjili la Kiluthari Tanzania (KKKT), nalo limetoa tahadhari ya kaunzishwa kwa mahakama hiyo, likisema iwapo sheria itapitishwa na Bunge, inaweza kusababisha madhara makubwa katika jamii ya Kitanzania katika siku za baadaye.
 
Tanzania bwana wakati mwingine ni vigumu kuwaelewa watanzania nini hasa tatizo lao, kwasababu moja haikai mbili haikai.
 
<br />
<br />
Ndugu hapo kwenye malipo ya gharama za mahakama ya kadhi unazidi kupotoka. Waislam na wakristo wote kwa mujibu wa sheria za dini yao huwa wanatakiwa kulipa kitu kinachoitwa zaka. Mbona huwa hatuiombi serikali itulipie. Waislam wengi nadhani hatukumuelewa Rais au tulimuelewa ila tunataka kuendeleza ubishi tu. Alichokiona yeye na walichokiona watu wengi makini ni kwamba si halali kuiweka mahakama hii kwenye katiba sababu ikiwekwa,itaanza ku demand itengewe fungu la kuiendesha. Kumbuka pesa za serikali zinachangiwa na wa islamu,wa kristo,wa hindu, na hata wapagani wasioabudu dini yeyote kama mzee wetu Mheshimiwa Kingunge. Atakubali vipi babu yangu mkulima aliepo kijijini na ambaye ni mpagani na hamuamini allah,buddha wala yesu, pesa yake(kodi) itumike kuendeshea chombo ambacho hakitaki na wala hana mpango wa kukitaka,lakini bado babu yangu huyu ni raia halali wa Tanzania na analipa kodi zote anazotakiwa kulipa kama VAT,INCOME TAX n.k?. Think outside of a box. Mahakama ya kadhi ni jukumu letu kuianzisha wenyewe ndugu zangu waislam na hata serikali haitoweza kutuingilia kwenye mambo ambayo tumesema mahakama hii itajihusisha nayo. Mbona wakatoliki wanayo mahakama yao wana mahakinu na ma judge ambao inawalipa mishahara yenyewe na hata siku moja hawajawahi ku kinzana na serikali na kuitaka government iwalipie mishahara?

Asante sana ndugu yangu kwa kutuelimisha waislamu. Tunajishushia hadhi kubisha vitu bila uelewa wa kutosha
 
<br />
<br />
Ndugu hapo kwenye malipo ya gharama za mahakama ya kadhi unazidi kupotoka. Waislam na wakristo wote kwa mujibu wa sheria za dini yao huwa wanatakiwa kulipa kitu kinachoitwa zaka. Mbona huwa hatuiombi serikali itulipie. Waislam wengi nadhani hatukumuelewa Rais au tulimuelewa ila tunataka kuendeleza ubishi tu. Alichokiona yeye na walichokiona watu wengi makini ni kwamba si halali kuiweka mahakama hii kwenye katiba sababu ikiwekwa,itaanza ku demand itengewe fungu la kuiendesha. Kumbuka pesa za serikali zinachangiwa na wa islamu,wa kristo,wa hindu, na hata wapagani wasioabudu dini yeyote kama mzee wetu Mheshimiwa Kingunge. Atakubali vipi babu yangu mkulima aliepo kijijini na ambaye ni mpagani na hamuamini allah,buddha wala yesu, pesa yake(kodi) itumike kuendeshea chombo ambacho hakitaki na wala hana mpango wa kukitaka,lakini bado babu yangu huyu ni raia halali wa Tanzania na analipa kodi zote anazotakiwa kulipa kama VAT,INCOME TAX n.k?. Think outside of a box. Mahakama ya kadhi ni jukumu letu kuianzisha wenyewe ndugu zangu waislam na hata serikali haitoweza kutuingilia kwenye mambo ambayo tumesema mahakama hii itajihusisha nayo. Mbona wakatoliki wanayo mahakama yao wana mahakinu na ma judge ambao inawalipa mishahara yenyewe na hata siku moja hawajawahi ku kinzana na serikali na kuitaka government iwalipie mishahara?

Asante sana ndugu yangu kwa kutuelimisha waislamu. Tunajishushia hadhi kubisha vitu bila uelewa wa kutosha.
 
Mbona mnaongea tu mahakama ya kadhi mahakama ya kadhi, vp kuhusu jela ya kadhi? Nayo itajengwa pia ili yule atakayeadhibiwa kwa kudhulumu miradhi afungwe huko? Je ni serikali ndio itajenga hiyo jela ya kadhi? Na hao wafungwa wa jela ya kadhi watapewa maharagwe ya serikali? Mbona pagumu hapo? Mahakama ya kadhi, jela ya kadhi na wafungwa wa jela ya kadhi wote wahudumiwe na serikali? Kazi kweli kweli
 
haya mambo ya Udini mwisho wa siku yatatuingiza kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe
 
Nionavyo mimi nchi yetu imefika pabaya.nilikuwa nikiwasikia wanasiasa wakibisha kuhusu kuwepo udini nchi au la.lakini baada ya kujiunga na jamii forum nimegundua udini upo.kwa wanapost humu ndani asilimia kubwa si wanasiasa bali ni wadini.mkatae mkubali nchi hii imeshazama kwenye wimbi baya la kiimani.sasa hivi ajira,biashara na elimu hufanywa kwa udini ingawa ni kwa hali ya usiri sana.siamini wimbi hili litatuacha kugharikika ni wajibu.

Katakule,

Hivi ndio kwanza unajua kuwa nchi hii ina udini!!!!!. umecherewa mno!!. Nadhani hii inatokana na kuwasikiliza sana wana siasa na uvivu wa kusoma vitabu. nakushauri kwa uchache ili uelewa zaidi kitafute kitabu cha dokta SIVALON (Msomi Mkatoliki huyu) na Muembe chai killings and the political future of Tanzania.
 
serikali inabidi iwasikilize kilio cha waislamu juu ya mahakama ya kadhi kwasababu hii suala ya mahakama ya khadi inwahusu wao wenyewe waislamu na si wengine ,sio dini zingine ziinterfere,and also the government is there for the interest of her people,so kama waislamu wanaona hii itawafaa basi serikali iwaachie,kwasababu hii nchi ni democratic state..
 
Back
Top Bottom