Majibu ya maswali yako ni haya, ilani ya uchaguzi ya ccm 2005 ambayo kikwete ndio alikuwa anainadi ndio ilikuwa imewaahidi waislamu mahakama ya kadhi na ukumbuke aliyekuwa anainadi ilani hiyo ni Jakaya Kikwete ambae nae ni muislamu, na Watanzania walimchaguwa na akashinda, sasa wewe badala ya kumuuliza Kikwete na ccm yake kuhusu hilo unamuuliza Dr Slaa! is it fare?
Tumetoka kwenye uchaguzi juzi tu kuna sehemu CHADEMA walinadi ilani yao kwa kuingiza mambo ya mahakama ya kadhi?
Kuhusu kujiunga na OIC hilo mimi kwangu halina mashiko, bado unapaswa kuwauliza ccm wao ndio wanaunda serikali wakiamuwa kujiunga mimi sioni shida kwani jumuiya ziko nyingi tu, hata wakitaka kujiunga na jumuiya ya mashoga ila kama kuna misaada tutapewa na wajiunge tu ruksa.
Una swali lingine?
Kwanza wewe sio Dr Slaa usimjibie on his behalf.
Pili nina haki kama mpiga kura kumuuliza hayo masuala kwasababu mimi ndiye nayemwajiri rais wa Tanzania umenifahamu hilo. Usimjibie Dr Slaa tafadhali tusitoke nje ya mada.