Mdondoaji!
Tukiweka hisia za kidini pembeni, nafikiri suala la OIC, kitaifa, tunatakiwa kulichukulia kiuchumi zaidi badala ya kidini.
Lakini cha kushangaza ni pale ambapo kujiunga na OIC kumechukuliwa kuwa ni swala la kidini, na ni kundi moja la dini fulani ndio linang'ang'ania. Nafikiri hapa ndipo tulipokosea. From the beginning, sababu za kiuchumi zingetiliwa mkazo zaidi badala ya za kidini, labda bunge na serikali wangekuwa wameisharidhia. Lakini sasa hivi wote tunaona, kwamba hii ni ajenda ya "waislam" badala ya kuwa ajenda ya Taifa.
Kwa upande mwingine, kwa uzoefu wangu wa kuwa karibu sana ndugu na rafiki waislam, sioni sababu ya "kutofanikiwa kujiunga na OIC" iwe kikwazo kwa maendeleo ya muislam yeyote. Uislam upo tu na utaendelea kuwepo whether or not kuna OIC. OIC inaweza kufa, uislam upo tu. Kwa hiyo, suala la OIC halitakiwi litugawe kama Watanzania. Nchi ni yetu wote wakati wa amani na hata wakati wa vurugu.
Madai ambayo nayaona ni ya msingi zaidi kwa waislam, ni suala la mahakama ya kadhi, kwa sababu kadhi courts zina husiana moja kwa moja na imani ya kiislam. Na hata hivyo, madai haya nayo si lazima sana kuyafanyia debate- kwa sababu katiba tayari inatambua kuwepo kwa wananchi wenye imani zao, na watu wanaruhusiwa kufanya mambo ambayo imani zao zinataka. Kwa maana nyingine ni kwamba, Waislam WAKIJIANZISHIA MAHAKAMA YA KADHI kimya kimya, hawatakuwa wamevunja katiba.
Sasa badala ya kupoteza muda kubishania kuwa Kadhi courts zitajwe kwenye katiba (ambacho sio rahisi kutokea) ingekuwa vizuri Waislam waanzishe na waziendeshe mahakama hizo. Mambo mengine inabidi kufanya taratibu, hatua kwa hatua na uvumilivu...
Miaka ya baadaye, si ajabu ikawa rahisi zaidi kuingiza kipengele hicho mnachotaka kutokana na kubadilika kwa nyakati pamoja na mazingira. Cha msingi tukubali kuwa , Katiba haijawakataza kuanzisha kadhi courts.