Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,226
OIC:Hamna kuna tatizo kwa Tanzania kujiunga na OIC.Wizara ya mambo ya nje ya Tanzania ilishafanya utafiti na Kuconclude kwamba hamna tatizo lolote.,na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa JK, Dk Bernard Membe alitangaza wazi wazi mbele ya waandishi wa habari (23 October 2008).na alisema Serikarli kupitia wataalam wake wake wamefanya utafiti na imejilidhisha kwamba kujiunga na OIC haina madhara yoyote .
Wasiotaka Tanzania Kujiunga na OIC ni maaskofu ambao walitahadharisha serikali ya CCM kuwa hawatafanya nayo kazi endapo Tanzania itajiunga na OIC,siku chache baada ya membe kuongea na wanahabari
Nukuu "Tuna uhakika kuwa yaliyomo ndani ya OIC ni hatari kabisa, kwani endapo yakikubalika katiba, nchi itakuwa imevunjika na Watanzania watakuwa wameingia katika migogoro itakayoua maridhiano, mshikamano, utengemano na umoja wa kitaifa, " walisema maaskofu hao katika tamko lao.
KADHI: juu ya mahakama ya Kadhi Tatizo watu wengi hawana elimu ya kutosha wanafikiri watahukumiwa kiislam(Ukiiba unakatwa mkono,Ukizini Bakora 100,ukizini ukiwa na mke/mume utapigwa viboko hadi kufa,ukilewa bakora 80,nk.)Zanzibar kuna mahakama ya kadhi ,Kenya kuna mahakama ya kadhi nani kakatwa mkono,Nani kachapwa.UNAPOPINGA AMA KUKUBALI KITU AMBACHO HUNA ELIMU NACHO NI UJINGA.
Tatizo nikwamba wakristo wanaichukia OIC na Mahakma ya kadhi kutokana na Mafundisho wanayopata kwenye makanisa yao na viongozi wao wa Dini.ambao wana hidden Agenda
Endapo hii hoja itapelekwa bungeni haiwezi kukubalika kwa sababu majority wa wabunge ni wafuasi wa dini ya kikristu.wapo zaidi ya asilimia 55,na Mtoto wa nyoka ni nyoka haiwezekani kiongozi wako wa dini akate kitu mfuasi akikubali,Halafu jumapili unakwenda kanisani kwake.
USHAURI WA BURE:Nendeni kwenye nchi ambazo kuna mahakama ya KADHI na OIC kama kuna ubaya wowote.Miongani mwa mataifa ya afrika yaliojiunga na OIC ni Cameroon, Uganda , Côte d'Ivoire, Gabon,Cameroon, Mozambique, Senegal, Benin, Togo, Gambia,n.K. Kadhi waulizeni wakenya.
Mwisho:TUACHE CHUKI KATIKA MAMBO YA MSINGI,WAACHENI WAISLLAM WAWE NA MAHAKAMA YA KADHI NA TANZANIA KUJIUNGA NA OIC IWE RUKSA
Mkuu uhakika hao watu wawili wana uwezo wa kufanya utafiti huo? ni wataalamu gani walifanya utafiti huo? Kwanini wataalamu wasitaumbie walitumia methodology gani au watuoneshe matokeo ya utafiti huo? walifanya utafiti huo kwenye nchi ngapi na kwa kipindi gani na watuoneshe evidence.
Ni kanisa gani hilo linalofunidha kuhusu sharia law hapa Tanzania? NI mahubiri gani kwenye vitabu vya Tanzania yanahusiana na Sharia law? Au ni kanisa gani linatoa mahubiri kuhusu sharia law?
Mkuu bungeni hakuna wafuasi wa dini ya kikristo, kuna waumini wa dini ya kikristo.
inawezekana ni kweli watu tusiounga mkono hoja hii ni wajinga, lakini ni vizuri tukielewesha sababu hasa ya kutaka kujiunga na OIC na kuwa na mahakama ya kadhi. Na kuna ubaya gani tusipojiunga.
Sensa inayosema Tanzania asilimia 55 ni waislamu ilifanyika lini?