Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Nyerere ndiye aliyekuwa anapinga sana ZNZ wasijiunge na OIC. Sasa hivi kuna watu wachache ambao bado wanafuata sera za Nyerere kupinga kila kitu kinachohusu Waislamu. Lakini siku 40 zao zishafika, kila kitu kinawezakana sasa hivi, OIC, na Mahakama ya Kadhi. Baba yao Nyerere hayupo tena.
 
wahindu, wabudha, wabahai, nk nao wakitaka serikali iwaanzishie mahakama zao, patakuwa hapatoshi. nadhani tuheshimu imani ya kila mtu. nashindwa kuelewa siri ya kutaka shughuli za kidini zibebwe na serikali.
 
Lakini siku 40 zao zishafika, kila kitu kinawezakana sasa hivi, OIC, na Mahakama ya Kadhi .
Turning us into islamic country. You have your answer!
 
Nyerere ndiye aliyekuwa anapinga sana ZNZ wasijiunge na OIC. Sasa hivi kuna watu wachache ambao bado wanafuata sera za Nyerere kupinga kila kitu kinachohusu Waislamu. Lakini siku 40 zao zishafika, kila kitu kinawezakana sasa hivi, OIC, na Mahakama ya Kadhi. Baba yao Nyerere hayupo tena.

kama tz mliijinga ww na m2me mhamad basi itawezekana.
 
Kuhusu mahakama ya Kadhi kama litajadiliwa misikitini, likakubaliwa kwa wingi na wao waislamu, kisha likufanyiwa kazi na vyombo mbalimbali vya Waislamu na likatekelezwa huko huko kwa waislamu bila kuilazimisha serikali iitabue kikatiba, mimi sioni tatizo. Ninakwazwa sana na waislamu wanapotaka kilazimisha mahakama hiyo itabuliwe na itamkwe ndani ya katiba! Huu ni uchakachuaji wa mfumo wa kutafuta na utoaji haki nchini!

Sirikali haina dini, hivyo isijihusishe wala isijiingize kwenye masula ya kughalimia shughuli au uendeshaji wa mambo ya dini fulani-italeta sintofahamu katika jamii!

Hii ni kama story ya ngamia na mwarabu jangwani: Mwarabu alikuwa anasafiri jangwani, akachoka akateremka juu ya ngamia akaweka hema akapumzika. Akiwa ndani ya hema ngamia akamwambia bwana wake kwa lugha laini, saidi yangu jua linanichoma sana naomba niingize kichwa tu ndani ya hema, mwarabu akamkubalia, baadaye kidogo akasema niingize na shingo maana jua ni kali sana. Mwarabu akakubali, ngamia akaomba aingize na nudu lake, mwarabu akakubali. Alivyoingiza nundu lake akabomoa hema wote wakabaki bazi jua lika watandika barabara!

Sasa mchezo wa mahakama ya kadhi ni sawa na story hiyo ya ngamia, tukikubali watakuja na hoja nyingine, na nyingine mwisho hapatosha, patachimbika na taifa litakuwa kama Somalia! Hili suala lisiwe la kitaifa bali la waislamu wenyewe kwani BONGO HAINA DINI-FULL STOP!
 
Ndiyo, hata mimi sioni tatizo la waislamu kuanzisha Mahakama yao iwe ya kadhi au vinginevyo ili mradi kama wenzao wakatoliki, hawaihusishi kabisa serikali yaani kibajeti, wala utendaji wake.
Tatizo la ndugu zetu waislamu ni kutaka mahakama yao hiyo ianzishwe kwa sheria ya Bunge na igharimiwe kwa fedha za walipa kodi ambao wengi wao si waislamu. Katika hilo wasio waislamu wataendelea kupinga. Hakuna mtu atakayewazuia kama wenyewe watakaa na kuanzisha Mahakama ya kuwahukumu watakaoridhia kuhukumiwa nayo (Yaani waislamu wenzao) bila ya kuihusisha serikali kwa maana ya kutumia bajeti ya nchi. Vyovyote itakavyokuwa, Mahakama ya serikali iliyowekwa na Katiba ya nchi ndiyo itakayokuwa kimbilio la mwisho kwa wale watakaohisi kutoridhishwa na Mahakama hiyo ya Kiitikadi.

Mgogoro utakuwa mashehe kukubali waislamu waliohukumiwa na kadhi kwenda kukata rufaa mahakama za kiraia patakuwa hapatoshi kwani watahisi wananyanganywa power. Uuuwwiiiii Mungu tuepushe na shari
 
hili wala halihitaji mtu uwe mwana Sayansi kulitafutia ufumbuzi... Serikali ijiondoe na iwape baraka zote waislamu kuanzisha mahakama hiyo!!
... Ni Historia pekee itakayoamua uanzishwaji wake, kwani si serikali pekee yenye kuzuia uanzishwaji wa mamlaka hiyo. Na wala Waislamu sidhani kama wanaihitajia serikali juu ya suala la Kadhi, kwani ilipata kuwapo na haikukinzana na sheria za serikali iliyokuwepo. Hilo ni suala la wakati ninavyoona kwa upande wangu, kwani kipo kizazi kinachoiogopa mahakama ya kadhi ilhali wao si wahusika. Pia suala la OIC ni kama lilivyo la Kadhi, wapo ambao wapo tayari kuandamana ili isianzishwe, WATANZANIA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Mtu anakipinga kitu bila kukijua kisa "nimeambiwa na....!!" Kenya ipo, Uganda ipo na Rwanda pia Nchi ambazo waislamu wake ni wachache. Labda ikija OIC kuna watu watapoteza fursa zao!?:thinking:
 
Kwa mara nyingine tena hoja ya Bunge kupitisha sheria ya kurudisha ofisi ya Kadhi Mkuu linajitokeza tena huku waislamu wakitaka Bunge litunge sheria ya kutambua uwepo wake na wakristu wakipiga kelele kuwa kufanya hivyo ni kuvunja Katiba. Hoja yangu leo ni kuwa, Waislamu hawahitaji kibali cha serikali kuanzisha ofisi ya Kadhi Mkuu kushughulikia mambo yao yanayoendana na sheria za Kiislamu.

Waislamu wakae wao wenyewe wapitishe uwepo wa ofisi hiyo na kuendelea na shughuli zao. Ilimradi tu, maamuzi ya ofisi yao hiyo hayaingilii uhuru wa Mtanzania mwingine au utendaji kazi wa sheria zetu za makosa ya uhalifu na jinai. Pia waelewe ya kwamba uwepo wa ofisi ya Kadhi Mkuu ni subject ya Katiba ya Muungano na Mtanzania yeyote kimbilio lake la mwisho ni mahakama ya Kiraia. Zaidi ya yote, watakapoanzisha ofisi hiyo, wajue kuwa isiwalazimishe waislamu wote kutatua matatizo yao kupitia ofisi hiyo isipokuwa wale ambao kwa hiari yao wanataka kufanya hivyo.

Kanisa Katoliki kwa mfano linayo mahakama yake na sheria zinazoliongoza kanisa hilo (Canon Law) na mahakama yake hiyo ina ngazi za rufaa hadi Vaticano. Hata hivyo Mkatoliki ana haki ya kutumia sheria hizo kuhusu masuala mbalimbali ya kanisa lake, lakini anapofanya kosa la jinai, sheria za kiraia (civil law) zinakuwa na mamlaka. Hivyo basi, waislamu wasisubiri Bunge kupitisha ofisi ya Kadhi Mkuu bali waianzishe wao wenyewe huku wakiweka bayana kabisa kuwa ofisi hiyo haitahusika na makosa ya jinai au kupingana na Katiba ya nchi. Then, hakutakuwa na haja ya kugongana!!!

naunga mkono hoja
 
je serikali ya Tanzania inafikiri vipi kuhusu maneno ya Rais wa Iran ambaye anataka kutengeza silaha za Nyuklia za "kuifuta Israel kutoka katika Ramani ya Dunia?"
nadhani inaweza kuwa inafikiri kilekile ambacho Waziri mkuu wa Israel, yule ambae hafi wala haponi alichokisema juu ya Wapalestina!:smile-big:
 
... Ni Historia pekee itakayoamua uanzishwaji wake, kwani si serikali pekee yenye kuzuia uanzishwaji wa mamlaka hiyo. Na wala Waislamu sidhani kama wanaihitajia serikali juu ya suala la Kadhi, kwani ilipata kuwapo na haikukinzana na sheria za serikali iliyokuwepo. Hilo ni suala la wakati ninavyoona kwa upande wangu, kwani kipo kizazi kinachoiogopa mahakama ya kadhi ilhali wao si wahusika. Pia suala la OIC ni kama lilivyo la Kadhi, wapo ambao wapo tayari kuandamana ili isianzishwe, WATANZANIA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Mtu anakipinga kitu bila kukijua kisa "nimeambiwa na....!!" Kenya ipo, Uganda ipo na Rwanda pia Nchi ambazo waislamu wake ni wachache. Labda ikija OIC kuna watu watapoteza fursa zao!?:thinking:
Nina wasiwasi na hayo mageuko unayoyawaza wewe mwana mageuko!
Post zako nyingi huwa sizielewi elewi ila sasa naanza kupata picha za madrassa!
Alif...bee..tee...............wasalaam
 
Nilipokuwa jeshini nilifanya kosa kwa kuvunja sheria za jeshi, nilipelekwa Court Marshal (Mahakama ya Jeshi) nikahukumiwa mwezi mzima jela ya hapo hapo kambini! Hiyo ilikuwa jumuiya ya kijeshi na taratibu zinazokubalika za kutoa adhabu kwa wanaokwenda kinyume na taratibu za jeshi. Ndugu zetu Waislamu (ingawa wao wana bagua wanasema "ndugu wa mwislamu ni muislamu mwenzake" ) waanzishe mahakama ya kadhi wao wenyewe bila kuingiliwa na serikali, hasa iwe ina shughulikia kesi zao zisizo za jinai! Kila kitu waghalimie wao bila kushirikisha waumini wasio waislamu. Naomba kuwasilisha.
 
huu mchakato wa hii mahakama utakuwa mgumu,bora waisilamu waufanye wenyewe-kwa sheria zitakazo-wa bind wenyewe-NA SI KUTAKA SERIKALI IWAANZISHIE-
 
Kusema eti Uganda na Rwanda kuna wasilamu wachache lakini kuna mahakama za kadhi ni hoja ya kitoto, kwa kuwa tayari nchi hizo mbili mbegu za chuki na mgawanyo zimeota na kutia mizizi. Jamii ya Tanzania na ya nchi hizo mbili ni tofauti sana,

Kila mtu anafahamu kuwa ni bora Tanzania ibaki kama ilivyo (secular state) kuliko kuanza kuingiza vionjo vya udini. Mpaka sasa bado hakuna sababu yoyote ya kimsingi ya kuifanya Tanzania ijiunge na jumuiya ya Kiislamu na iwe na mahakama ya kadhi.

Otherwise ni bora tuigawe Tanzania sehemu mbili, sehemu ya kwanza yenye waislamu na inayofuata sharia na kuwa mwanachama wa OIC, na sehemu nyingine iwe secular. It is very low thinking kuanzia kufikiri na kuwekeza mawazo yetu kwenye mambo ya dini na udini, Ingekuwa bora kama tukiwekeza mawazo yetu na raslimali zetu kwenye elimu.
 
Nina wasiwasi na hayo mageuko unayoyawaza wewe mwana mageuko!
Post zako nyingi huwa sizielewi elewi ila sasa naanza kupata picha za madrassa!
Alif...bee..tee...............wasalaam
Hujakosea, Hapa siandiki kwa kumfurahisha yoyote wala kumuudhi yeyote bali nasimama katika ukweli na misimamo yangu. (ndio maana siungi mkono ninachoona sicho - na uovu naukemea) Mimi si mwenye kuongozwa na fikra za mwingine kama unavoonesha wewe. Wala siwachukii na kuwatusi ambao tunatofautiana ki-fikra) pia sifuati ambacho akili yangu haijaona ukweli wake na upungufu wake nachambua, nasoma na ninatafiti. Namshukuru Mungu sikujaaliwa kuwa bubusa bali mwenye uelewa. Wewe huwezi kunielewa kwa sababu hutaki kuelewa bali kuelewesha na hili kwako ni tatizo kubwa kwani ukieleweshwa na ukaelewa ambacho sicho ukija kuambiwa kuwa hiki sicho ni lazima utabisha na kusema HIKI NDICHO HIKIHIKI!! Napenda kukufafanulia hiyo Alif maana yake Aloah va Daath, ukishalijua hilo ni vema ukatafuta namna nyingine ya kashfa. Kwa sababu hujui YODI ni nini!?? Cha ajabu unamtafuta Mungu usiyemjua, kwa ufupi tafuta kitabu kiitwacho Tanakh kisha ujue maana ya maneno hayo unayodhani matusi. (Ipo Tafsiri yake kwenye NET) you can google...>>> Tafuta maarifa kwa kusoma na kutembea sio kuelezewa. Siku hizi si zamani kila kitu kipo wazi, usiishie kutafuta maarifa JF pekee, pita Seminary kuna Library nzuri sana na zina History pana kabisa ya maandiko na dini mbalimbali. 😎

Hapa ndani wapo wanaonielewa kwa upeo mpana sana NAKUSISITIZA TAFUTA MIWANI:whistle:

Pamoja
 
Kusema eti Uganda na Rwanda kuna wasilamu wachache lakini kuna mahakama za kadhi ni hoja ya kitoto, kwa kuwa tayari nchi hizo mbili mbegu za chuki na mgawanyo zimeota na kutia mizizi. Jamii ya Tanzania na ya nchi hizo mbili ni tofauti sana,

Kila mtu anafahamu kuwa ni bora Tanzania ibaki kama ilivyo (secular state) kuliko kuanza kuingiza vionjo vya udini. Mpaka sasa bado hakuna sababu yoyote ya kimsingi ya kuifanya Tanzania ijiunge na jumuiya ya Kiislamu na iwe na mahakama ya kadhi.

Otherwise ni bora tuigawe Tanzania sehemu mbili, sehemu ya kwanza yenye waislamu na inayofuata sharia na kuwa mwanachama wa OIC, na sehemu nyingine iwe secular. It is very low thinking kuanzia kufikiri na kuwekeza mawazo yetu kwenye mambo ya dini na udini, Ingekuwa bora kama tukiwekeza mawazo yetu na raslimali zetu kwenye elimu.
Siwaelewi WATANZANIA (baadhi!!!)

Hivi kuna tofauti gani ya OIC na CARE, CRS n.k???:smile-big:
Ile si kama ilivyo VATICAN, watu wanalijua hilo. kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia TIME WILL TELL.
 
Hujakosea, Hapa siandiki kwa kumfurahisha yoyote wala kumuudhi yeyote bali nasimama katika ukweli na misimamo yangu. (ndio maana siungi mkono ninachoona sicho - na uovu naukemea) Mimi si mwenye kuongozwa na fikra za mwingine kama unavoonesha wewe. Wala siwachukii na kuwatusi ambao tunatofautiana ki-fikra) pia sifuati ambacho akili yangu haijaona ukweli wake na upungufu wake nachambua, nasoma na ninatafiti. Namshukuru Mungu sikujaaliwa kuwa bubusa bali mwenye uelewa. Wewe huwezi kunielewa kwa sababu hutaki kuelewa bali kuelewesha na hili kwako ni tatizo kubwa kwani ukieleweshwa na ukaelewa ambacho sicho ukija kuambiwa kuwa hiki sicho ni lazima utabisha na kusema HIKI NDICHO HIKIHIKI!! Napenda kukufafanulia hiyo Alif maana yake Aloah va Daath, ukishalijua hilo ni vema ukatafuta namna nyingine ya kashfa. Kwa sababu hujui YODI ni nini!?? Cha ajabu unamtafuta Mungu usiyemjua, kwa ufupi tafuta kitabu kiitwacho Tanakh kisha ujue maana ya maneno hayo unayodhani matusi. (Ipo Tafsiri yake kwenye NET) you can google...>>> Tafuta maarifa kwa kusoma na kutembea sio kuelezewa. Siku hizi si zamani kila kitu kipo wazi, usiishie kutafuta maarifa JF pekee, pita Seminary kuna Library nzuri sana na zina History pana kabisa ya maandiko na dini mbalimbali. 😎

Hapa ndani wapo wanaonielewa kwa upeo mpana sana NAKUSISITIZA TAFUTA MIWANI:whistle:

Pamoja
You have a problem!
I will be praying for you!
 
Siwaelewi WATANZANIA (baadhi!!!)

Hivi kuna tofauti gani ya OIC na CARE, CRS n.k???:smile-big:
Ile si kama ilivyo VATICAN, watu wanalijua hilo. kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia TIME WILL TELL.

Mkuu OIC ni jumuiya ambayo inaweza kuwagawa watanzania, ajenda yake ni dini. Inatumia issues nyingine kama elimu,afya na huduma nyingine za jamii kuadvance agenda ya uislamu. Lkini CARE international and alike hazi ajenda kama hiyo. Vatican si organisation of Christian Countries, ni kweli mission yake ni kuendeleza ukatoliki lakini haina ajenda ya kuimpose ukatoliki kwa wakristo wengine na wasio wakristo.
Nakubaliana na wewe time will tell, and it is telling now for sure tunaona ajenda iiliyo nyuma ya pazia.
Lakini nafurahi mkuu wewe at least unaongea kwa uelewa tofauti na baadhi ya wadau wanavyokuponda. TANZANIA DAIMA.
 
Siwaelewi WATANZANIA (baadhi!!!)

Hivi kuna tofauti gani ya OIC na CARE, CRS n.k???:smile-big:
Ile si kama ilivyo VATICAN, watu wanalijua hilo. kuna kitu kimejificha nyuma ya pazia TIME WILL TELL.
Ndugu yangu, tofauti ni kubwa sana. CARE na CRS ni NGO's (non governmental organisations) na hazina binding charter. OIC ni intergovernmental organization na inayo charter ambayo nchi wanachama wanapaswa kuizingatia na kuifuata. Hizi NGO's hazihitaji nchi yoyote iwe mwanachama wake ndipo zifanye kazi nayo, zinahitaji ruhusa tu. Lakini OIC inataka nchi iwe mwanachama, ikubali charter yao, itekeleze majukumu ya mwanachama ambayo yanaendana na imani katika itikadi moja ya kiislamu. Nimesoma OIC charter mara kadhaa, na haiendani hata kidogo na misingi ambayo nchi yetu imejengwa, ni charter ya kidini ilhali nchi yetu si ya kidini.

Vatican ndiyo tofauti zaidi. Ile ni makao makuu ya kanisa katoliki, sawa na makao makuu ya dini nyingine duniani, tofauti ni kuwa nchi ya Itali imewaheshimu na kuwapa eneo la utawala lenye hadhi ya dola, kwa hiyo wana haki za dola huru ikiwamo kufungua ubalozi nje ya nchi yao. Hata Mtukufu Aga Khan angekuwa na dola yake angefungua tu ubalozi Tanzania, hakuna mtu angemzuia.
 
Back
Top Bottom