Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 21,204
- 37,555
Mtu anayekataa kuundwa kwa mahakama ya kadhi lazima atakuwa na kasoro.Mahakama ya kadhi ni ibada kwa ndugu zangu waislamu.Tatizo linakuja pale watu wanapotaka kulazimisha mahakama ihudumiwe na serekali.Tangu lini serekali ikatumia kodi zake kuhudumia ibada za dini yoyote.
Mheshimiwa Pinda katoa ufafanuzi mzuri sana ndugu zangu waislamu tuwache kulalama tunatakiwa kuunda mahakama ya kadhi ndani ya taasisi zetu kama BAKWATA na taasisi nyingine zitakazoonekana zinafaa.
Tanzania inatakiwa kutumia muda na rasilimali zake kuondoa umaskini kwa wananchi wake mambo ya ibada yafanywe na taasisi za dini bila kuihusisha serekali.Serekali inaweza kusaidiana na madhehebu mbalimbali katika masuala kama elimu na afya.Baadhi ya wachangiaji wanashindwa kuona tofauti kati ya masuala yanayohusiana na imani na yale yanayosaidia jamii kama mahospital,shule na vyuo.