Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Mnachoongea ni jiografia ya ukatoliki! Vatican si Nchi! Hiyo ni propaganda ya kiteolojia ndani ya ukristo. Italia ndiyo nchi. Msilete Dogma! Ubalozi wa Vaticani ni crusade. Mjisomeshe msisomeshwe! Neno Ibada limetoholewa kutoka lugha ya Kiarabu .Tafuteni maana na istilahi yake.Sio kukalia benchi.

Hakuna nchi duniani ina mahusiano na nchi inayoitwa Vatican. Tulilieleza hili watu wakagoma kuelewa hadi tukakasirikiana na hatimaye wengi tukapigwa ban ya siku tatu na moderator.

Mode nadhani wanaosumbua hii forum ni pamoja na hawa waioelewa hata uwaelimishe miaka nenda rudi.

Leo tena tunawaambia hakuna ubalozi wa Vatican duniani kokote.

Elimu nzuri ililetwa hapa JF, tukajadli tukadhani ilieleweka. Kwa kweli wasioelewqa sina njia nyingine ya kuwaita. Maana sina neno la kiswahili zuri badala yake ni kuwaita vilaza.

Hebu someni hii link kwenye mabano ili mjue uwezo wenu wa kukumbuka kwamba nchi inayoitwa Vatican haijaanza mahusiano na nchi yoyote: (Miaka 80 ya Uhuru wa Vatican,, Je ?Ubalozi? unaeleweka?)
 
Hivi ndivyo itakavyokuwa kwenye mahakama ya kadhi

"Strike off the heads of the disbelievers; and after making a wide slaughter among them, carefully tie up the remaining captives" (Koran 47:4).😕
Is this part of it?
 
poor argument, afadhali ungeacha kuchangia maana uelewa wako mdogo sana kuhusu jambo hili

Did u watch channel 10 today, kipindi Je tutafika? hapo ndio utajua nani uelewa wake ni mdogo. Pole mkuu u have a long way to go.....
 
Wiki iliyopita muhubiri maarufu wa dini ya kiisilamu nchini She yahaya aliingilia suala la kadhi mkuu , huyu yeye akawa anateta hoja ya waisilamu kuwa na kadhi wa kwa ajili ya kuwatetea katika mambo yao

Hoja alizozitoa ni pamoja na kwamba eti , waisilamu wamegawanyika sana , kutokana na kuwa na misikiti mingi na madhehebu mengi kwahiyo mahakama ya kadhi itawaunganisha na kuwa na chombo chao sababu nyingine ni kwamba huu mgawanyiko unaifanya bakwata isiwe na nguvu katika maamuzi kwa waisilamu wengine kwa kuwa kuna baadhi ya watu hawaitambui bakwata .

Pia alisema mahakama za kawaida zinashindwa kutatua matatizo mengine ya waisilamu mahakama ya kadhi ndio inatosha kwa zote hizi , mimi tangia nimezaliwa miaka 24 sijawahi kusikia kwamba mahakama imeshindwa kutoa hukumu kwa mtu wowote yule kwa misingi ya dini ?

Kabla ya huyu pia siku chache mzee mwinyi nae alikuja na hoja za ukadhi , naye alitetea ukadhi , sasa najiuliza kwanini huyu mwinyi hakuleta ukadhi wakati yeye akiwa kiongozi wan chi enzi hizo alikuwa anamuogopa nani kwanini hakujadili enzi zake anazileta sasa hivi kama sio kuletea shida wengine ?

Napenda kuwasihi vijana wa kiisililamu na waisilamu wote popote walipo wasigubali kutumiwa kisiasa na watu ambao wameshashiba mamlaka wameshaishiba hii dunia hawajali wanachosema wanasema tu ilimradi waonekane wameongea lakini kuongea kwao hakuna chachu yoyote katika maendeleo ya nchi hii na watu wake .

Lazima mambo ya dini yaondolewe katika maisha ya kawaida ya mwadanamu haswa mtanzania kwanza hizi dini ni za kuja sio za asili yetu kwanini tunazingangania tangia zimeingia tumepata shida sana , tabu na majuto mengi na sasa hii mahakama ya kadhi inataka kutetenga watanzania .

Viongozi wa dini nyingi walivyosema mahakama ya kadhi haitakiwi kujadiliwa hawakua wajinga na sio mbumbumbu wanajua ubaya wa mahakama hizo na wanajua kwa mifano kwa nchi zingine , hivi mfano waikrito nao wakiamua kuwa na kadhi wao itakuwaje ? wahindu nao je ?? kuna maana gani ya kuwa na katiba ya nchi kama watu wengine wataanzisha mahakama zao ?

Inasemekana hizi mahakama zitakuwa zinapewa ruzuku na serikali kwasababu ni ilani ya CCM tangia wakati wa uchaguzi mkuu wamwaka jana , nashangaa hawa CCM nani alitengeneza ILani yao ? hii ni ilani ya kutupagawisha watanzania na kutugawa mafungu kama kule Sudan , kwanini katika Ilani kuwe na hoja kama hizo za kadhi ??

Basi tuna haki ya kusema kwamba CCM ni chama cha kidini , kwa sababu katika Ilani zao za uchaguzi zina hiyo ishu ya kadhi , kadhi ni kuingilia masuala ya ndani ya dini ingine kuichokonoa .

Kikwete alivyosema kutenganisha dini na siasa basi yeye awe muazo wa kubadilisha hivyo , Aondoe ilani ya ukadhi ndani ya katika ya CCM kisha tumuelewe , na pia atoa tamke rasmi kuhusu kadhi , sisi kaama wananchi tumuelewe sio anakimbia hoja hii

Tumekuwa na malalamiko mengi kuhusu Udini katika Nchi hii watu wananyamaza sasa hivi limekuja suala la ukadhi watu wananyamaza pia – tena inahusiana na siasa iko katika Ilani ya CCM taifa

Tutambue kwamba nchi yetu ni nzuri na inapendeza kwa watu wake na mambo yake sasa haya mambo yasiharibu watu na kuwagawanyisha

Hii maana yake nini kama sio kututenganisha watanzania ??

Asante mkuu! Moja ya hoja alizotoa huyo Sheikh kuwa Mahakama ya Kadhi itawaunganisha Waislamu, imenikumbusha 'narrative' moja kwenye Biblia.

Inasema hivi: Kulikuwa na mtu tajiri sana na maskini aitwaye Lazaro. Huyu Lazaro alikuwa maskini wa kutupwa na kila mara alitegemea makombo ya huyo tajiri kwa mlo wake. Lakini tajiri alikuwa akiyatwaa na kuwatupia mbwa yale makombo kuliko kumpa Lazaro sehemu ya chakula chake.

Basi siku zikaenda baadaye wote wakafa. Lazaro alichukuliwa kwenda mbinguni na huyo tajiri motoni. Halafu huyo tajiri alipoinua macho juu akamwona huyo maskini (lazaro) akiwa kifuani mwa Abrahim. Akamwomba walau ateme mate ili yapoze kidogo makali ya ule moto.

Huyo maskini (Lazaro) akajibu kuwa haiwezekani kwa vile kati yao - yaani, wale walio mbinguni na huko motoni kuna bonde kubwa sana na hivyo haiwezekani kabisa mtu wa upande mmoja kuvuka kwenda upande wa pili.

Aliposhindwa kupata msaada wowote kisha akamwomba huyo maskini (Lazaro) kuwa kama ataweza kurudi duniani basi anamwomba awaonye ndugu zake yule tajiri ili nao wasije wakaenda huko motni.

Ibrahim akamjibu kuwa haiwezekani. Akaongeza kuwa kama hao ndugu hawakuwasikiliza Musa na manabii wanaokaa nao hata angeenda mtu kutoka mbinguni wasingemsikiliza.

Kwa hiyo, kama Waislamu wameshindwa kuungana wao kwa wao bila Mahakama ya Kadhi, hawataweza kuungana kwa sababu ya Mahakama ya Kadhi.

Hata kama watakuwa nayo bado wataona kitu kingine kinakosekana. Kuungana kunahitaji moyo wa unyenyekevu na mnyofu.
 
nadhani wanaotaka kadhi wala hawajui kwanza italeta tofauti gani na hali ilivyo sasa! igharamikiwe na na nani? secondly nitalipaje kodo yangu kama mkristo kuendesha mradi usio kuwa na tija kwa taifa? waislam wakae chini waianzishe kama vile NGO waombe misaada na michango ya waumini, sio kushirikisha nchi kwa masuala ya dini, je kila mtu akita nae aanzishe mahakama za kutumia Uyahudi? Kihindi?Kisukuma? tutafika? use common sense


hivi aliyekwambia kuwa waislam wametaka serikali igharamie mahakama ya kadhi ni nani? kinachotakiwa ni serikali kuwapa goa head wasilam kuanzisha mahakama ya kadhi wanasheria, uendeshaji ni suala la waislam halitamhusu mtu wa dini nyingine kwa maana hiyo mahakama haitodeal na asiye muislam na hakuna makosa ya jinai yatakayotatuliwa hapo,

kuishirikisha serikali si kosa, mahakama ni suala linaloenda na sheria, hivyo lazima serikali ikubali na kutambua kuwepo kwake, na ndio sababu waislam wakalipeleka hili jambo katika mikono ya serikali, wala msijali kuhusu kodi zenu maana waislam hawapo katika ulipaji huo wa kodi!

tatizo hivi haswa ni nini ndugu zetu, wakristo amabao mnalipotosha na kulivalia njuga suala hili, inamaana waislam hawana haki ya kutoa maoni yako au kutaka ushauri toka serikalini?

mahakama ya kadhi ni kwa waislam, haitahusiana na yeyote asiyekuwa muislam, na waislam hao ni watanzania na ndio maana wamepeleka ombi lao katika serikali ya tanzania,kwa kuzingatia kuwa kuanzisha mahakama si sawa na kufungua kituo cha kulele watoto yatima ni suala ambalo linainvolve sheria! WANGEANZISHA mngewatafutia FFU kwa kuwa wamevunja sheria sasa wanaomba idhini nayo issue lipi jema kwenu!

 
Joka Kuu Tafadhali usipotoshe "facts" kuhusu Zanzibar. Hili suala la Kadhi mnazongeka nyie , lakini siyo sisi kule Zenj. Tunaye Kadhi na anaheshimika. Please don't involve us katika mazonge yenu, na usipoteshe facts kuhusu Zenj.
 
hivi aliyekwambia kuwa waislam wametaka serikali igharamie mahakama ya kadhi ni nani? kinachotakiwa ni serikali kuwapa goa head wasilam kuanzisha mahakama ya kadhi wanasheria, uendeshaji ni suala la waislam halitamhusu mtu wa dini nyingine kwa maana hiyo mahakama haitodeal na asiye muislam na hakuna makosa ya jinai yatakayotatuliwa hapo,

kuishirikisha serikali si kosa, mahakama ni suala linaloenda na sheria, hivyo lazima serikali ikubali na kutambua kuwepo kwake, na ndio sababu waislam wakalipeleka hili jambo katika mikono ya serikali, wala msijali kuhusu kodi zenu maana waislam hawapo katika ulipaji huo wa kodi!

tatizo hivi haswa ni nini ndugu zetu, wakristo amabao mnalipotosha na kulivalia njuga suala hili, inamaana waislam hawana haki ya kutoa maoni yako au kutaka ushauri toka serikalini?

mahakama ya kadhi ni kwa waislam, haitahusiana na yeyote asiyekuwa muislam, na waislam hao ni watanzania na ndio maana wamepeleka ombi lao katika serikali ya tanzania,kwa kuzingatia kuwa kuanzisha mahakama si sawa na kufungua kituo cha kulele watoto yatima ni suala ambalo linainvolve sheria! WANGEANZISHA mngewatafutia FFU kwa kuwa wamevunja sheria sasa wanaomba idhini nayo issue lipi jema kwenu!

Hivi mahakama zenu mpaka serikali iseme 'go ahead'? Na ikiwa mwaka fulani rais au mwanasheria mkuu akawa Mkristo kweli hamtaleta matatizo tena?

Halafu je, kwani ni hilo tu la Mahakama ya Kadhi litakalo hitaji 'go ahead' ya serikali au sharia nayo itabidi muishinikize serikali ili iingizwe kwenye Katiba baada ya kufaniksha Mahakama ya Kadhi kwani kitu gani kitawazuia kudai hivyo kama mtafanikiwa hilo la Kadhi?

Kwa mawazo yangu, naona ni kama msemo 'nimempa mkono akashika bega'. Serikali ikijiingiza kwenye uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi ni kama imewapa mkono na mkipewa huo mkono (yaani serikali ikishajiingiza kwenye mambo ya kidini), kwa vyovyote mtashika bega - you'll go further - mtaendelea kudai sheria zingine za Kiislamu zitumike?

Ndiyo maana, inabidi kuwe na 'open debate' ili tukubaliane cha kufanya maana tukisha haribu tu mwanzoni tutaendelea kuharibu hata hapo baadaye! Mna 'tactics' nyingi za kuingiza mambo yenu kwenye mfumo wa utawala na wakati huohuo mnaona eti watu wengine ndio wenye udini.

Serikali ilishatoa uhuru wa kutosha namna ya kuabudu. Katiba yetu inasema serikali haina dini ila watu wana dini. Halafu kiujanjaujanja mnataka muifanye serikali iegemee dini yenu. Hivi mnadhani Watanzania wengine hawalioni hilo?
 
My Two cents . Mahakama ya kadhi naona ni kwamba hamna education ya kutosha kuihusu . Wenzetu Kenya na Uganda wanayo hiyo mahakama . Swali ni , what does it deal in ? Please someni extract kutoka kwenye KATIBA ( yes it is in the constitution) ya Kenya.

66. Kadhis' Courts.
There shall be a Chief Kadhi and such number, not being less than three, of other Kadhis as may be pro- scribed by or under an Act of Parliament.
A person shall not be qualified to be appointed to hold or act in the office of Kadhi unless-
he professes the Muslim religion; and
he possesses such knowledge of the Muslim law applicable to any sect or sects of Muslims as qualifies him, in the opinion of the Judicial Service Commission, to hold a Kadhi's court.
Without prejudice to section 65 (1), there shall be such subordinate courts held by Kadhis as Parliament may establish and each Kadhi's court shall, subject to this Con stitution, have such jurisdiction and powers as may be conferred on it by any law.
The Chief Kadhi and the other Kadhis, or the Chief Kadhi and such of the other Kadhis (not being less than three in number) as may be prescribed by or under an Act of Parliament, shall each be empowered to hold a Kadhi's court having jurisdiction within the former Protectorate or within such part of the former Protectorate as may be so prescribed: Provided that no part of the former Protectorate shall be outside the jurisdiction of some Kadhi's court.
The jurisdiction of a Kadhi's court shall extend to the determination of questions of Muslim law relating to per- sonal status, marriage, divorce or inheritance in proceedings in which all the parties profess the Muslim religion
 
Mahakama ni sehemu ya serikali. Serikali ina mihimili 3, yaani Utendaji (Executive), Utunzi wa Sheria (Bunge) na Mahakama (Judiciary).

Iwapo Mahakama ya Kadhi itaanzishwa kwa sheria ya Bunge, basi itakuwa ni sehemu ya Judiciary, yaani itakuwa ni mojawapo ya mihili ya serikali. Katika nchi ambayo serikali haifungamani na dhehebu lolote, kama ilivyo Tanzania, ni kosa la kikatiba kwa Bunge kuanzisha Mahakama ya Kadhi.

Kwa serikali kupeleka hili jambo kwa wananchi ina maana gani? Kama wanataka kubadilisha katiba ili dini ya Kiislamu iwe sehemu ya serikali, basi wafanye hivyo bila kificho. Waache kupoteza fedha za nchi na muda wa wananchi.

Augustine Moshi
Sijakuelewa ni lipi unaloongelea. Lakini it is a fact kwamba Tanzania (Tanzania bara) kuna waislamu wengi tu . Hivyo wao ni sehemu ya jamii. Waislamu wana sheria zao na mambo yao yanayoongoza ustawi wa jamii. Mahkama ya kadhi huwa ndiyo inayosimamia mambo hayo (ikiwa ni pamoja na mambo ya ndoa na urithi) Sheria za Tanzania za hivi sasa hazi"consider" mtizamo wa Waislamu katika mambo hususan hayo ya ndoa na urithi. Sasa cha kufanya ni ama utafute namna ya kuwepo kwa institution (mahkama ya Kadhi) ili iweze kuratibu na kuendesha mambo hayo ya wanajamii. au uyaingize (incorporate) mambo yao katika sheria za nchi. Hili suala ni "is as simple as that". Unasemaje?
 
My Two cents . Mahakama ya kadhi naona ni kwamba hamna education ya kutosha kuihusu . Wenzetu Kenya na Uganda wanayo hiyo mahakama . Swali ni , what does it deal in ?

Lemunyake,

Nashukuru unakubali mwenyewe kwamba hakuna uelewa kuhusu mahakama ya kadhi. Hivyo kama jambo lolote kama halijulikani basi ni hicho ni kigezo cha kwanza kulikataa. Huwezi kukubali jambo geni ukitegemea utabiri kwamba liwe zuri wakati hujalipa nafasi ya kujadiliwa na likapimwa ubaya wake.

Maadam ilidhamiriwa mahakama iwe iingie kwenye katiba basi isingekuwa tena ya Waislam pekee. Kinachoingia kwenye katiba lazima kijadiliwe na wote.

Kosa kubwa mnalofanya waislamu ni kutoweka bayana muundo wa mahakama yenu ikabaki kila mmoja anahisi nini kilichojificha nyuma yake. Na mimi nauliza mmekazania nini hadi mahakama hii msiieleze kinagaubaga badala yake mnatuambia twende Kenya na kwingine inakofanya kazi. Mbona wenzenu wakatoliki mahakama yao inafanya kazi dinuani kote lakini hawakuata ubabaishaji wakaieleza inavyofanya kazi

Fungua mtandao ufuato kwenye mabano ambapo mkatoliki mmoja aliilezea hadi tukaelewa walau kidogo: (Makala -Mahakama za dini zijadiliwe kwa kina)

Kama ungemsoma vizuri huyo jamaa hizo ni dalili kwamba wakatoliki ikiruhusiwa ya Kadhi basi na wao kesho yake wanaomba iingizwe kwenye katiba ili ngoma iwe droo.
 
Serikali iache Mahakama ya Kadhi iundwe na waislam wenyewe,Halafu ipitie sheria zitakazotumika na kuona kama haivunji sheria za nchi na vipengele vitakavyokwenda kinyume na katiba yetu viondolewe 'and then' wachague kadhi wao kwa kufuata mwongozo wa dini yao.Bunge lisijihusishe na Muundo wake.Mahakama ya kadhi isajiliwe tu kama Advocates Company au taasisi zingine zisizo za kiserikali! HAPO VIPI?
 
naona watu wanaenda na kurudi na hoja ileile, ambayo si ukweli kuhus mahakama ya kadhi, waislam hatujasema serikali ituanzishie mahakama ya kadhi, tunachohitaji ni tamko la serikali tu kuwa jamani waislam mnaruhusiwa kuanzisha mahakama ya kadhi hilo tu,

na hakuna dai la waislam linalodai sheria za kiislam ziwekwe kwenye katiba...manaleta mlolongowa hadithi ambazo hata hazipo, kwa suala lisilowahusu

mnaotaka uwazi mnataka uwazi gani haswa, mbona sheikh mkuu aliishasema kuwa hii ni mahakama ya waislam kwa mambo ya waislam na si kesi za jinai, na halimhusu yeyote asiye muislam!

mnaodai waislam wajianzishie tu bado narejea hatujaanzisha tu mapovu yanawatoka je tungeanzisha si tungekuwa tunazungumza mengine hapa,


a lot has been said, naona thread hii inaweza kulead kwa kuwa na post nyingi, mwenye macho aone na mwenye masikio asikie wale wenye kupenda debate zisizonamwisho kazi kwenu...

ila mjue kelele za chura hazimzuii mnywa maji...
palipo na ukweli uongo hujitenga ...
 
Pakacha said:
Waislamu wana sheria zao na mambo yao yanayoongoza ustawi wa jamii. Mahkama ya kadhi huwa ndiyo inayosimamia mambo hayo (ikiwa ni pamoja na mambo ya ndoa na urithi) Sheria za Tanzania za hivi sasa hazi"consider" mtizamo wa Waislamu katika mambo hususan hayo ya ndoa na urithi. Sasa cha kufanya ni ama utafute namna ya kuwepo kwa institution (mahkama ya Kadhi) ili iweze kuratibu na kuendesha mambo hayo ya wanajamii. au uyaingize (incorporate) mambo yao katika sheria za nchi. Hili suala ni "is as simple as that". Unasemaje?



Pakacha,

..nadhani msimamo wa serikali, kama ulivyoelezewa na Waziri Chikawe pale bungeni, ulikuwa ku-incorporate sheria za Kiislamu ktk sheria za Jamhuri.

..nadhani pendekezo hilo halikupata response nzuri toka kwa wanaharakati wa Mahakama ya Kadhi.

..binafsi nadhani that was plausible COMPROMISE ktk suala hili, ila nina wasiwasi kwamba idea ile tayari imeshakuwa discarded.

..labda tatizo lilikuwa ni serikali kufikia uamuzi ule bila kuwashirikisha Waislamu.
 
The Kadhis’ Courts Act, 1985, No. 3 of 1985, (Zanzibar)!!
Buchanan
user_online.gif
Today, 01:50 AM
1. Kifungu cha 3 (1) cha Sheria hiyo kimeunda Mahakama za Kadhi kulingana na Ibara ya 99 (1) ya Katiba ya Zanzibar, 1984.
2. Kifungu cha 3 (1), Kutakuwa na Mahakama ya Kadhi Mkuu wa Zanzibar na Mahakama za Kadhi kwa kila Wilaya.
3. Kifungu cha 4 (1) na (2), Kutakuwa na Kadhi Mkuu (Chief Kadhi) ambaye atateuliwa na kuapishwa na Rais wa Zanzibar.
4. Sifa za kuwa Kadhi Mkuu [Kifungu cha 4 (3)]: Kuwa na kufuata dini ya Kiislamu, kuwa na taaluma ya Sheria za Kiislamu ambapo kwa maoni ya Rais anafaa kuteuliwa kushika nafasi hiyo (ya Ukadhi Mkuu).
5. Kifungu cha 5 (1): Kutakuwa na idadi ya makadhi, ambao hawatapungua kumi na hawatazidi kumi na watano ambao watateuliwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama (the Judicial Service Commission) kwa kushirikiana na Rais na Kadhi Mkuu.

Hayo ni machache kati ya mengi kuhusu Mahakama ya Kadhi, Zanzibar. Je, kukiwa na Rais Mkristo au wa dini nyingine atamteua Kadhi Mkuu kwa Zanzibar? Au haiaminiki kwamba Rais asiye mwislamu hawezi kuchukua madaraka Zanzibar? Je, Waislamu wa Bara nao wanataka Muundo huo wa Mahakama za Kadhi?


Habri ndio hiyo.
 
[/B]

Pakacha,

..nadhani msimamo wa serikali, kama ulivyoelezewa na Waziri Chikawe pale bungeni, ulikuwa ku-incorporate sheria za Kiislamu ktk sheria za Jamhuri.

..nadhani pendekezo hilo halikupata response nzuri toka kwa wanaharakati wa Mahakama ya Kadhi.

..binafsi nadhani that was plausible COMPROMISE ktk suala hili, ila nina wasiwasi kwamba idea ile tayari imeshakuwa discarded.

..labda tatizo lilikuwa ni serikali kufikia uamuzi ule bila kuwashirikisha Waislamu.
sasa hapo ni matatizo yenu watu wa siasa. Lakini la msingi ni kuihudumia jamii. Na katika hii jamii wamo waislamu tena ni wengi tu. Sasa kuwe na kitu wanachokiamini kuhusu mambo yao,kama ya ndoa au urithi. Hili sio suala kubwa kama linavyokuzwa. kama hutaki Mahkama ya Kadhi -incorporate mambo yao katika sheria zako za dola-Na hilo litakulazimisha uwe na kitengo maalum kwa ajili ya hiyo kitu -Sasa hiyo si ni sawa tu na Mahkama ya Kadhi, Unaonaje?.
 
The Kadhis’ Courts Act, 1985, No. 3 of 1985, (Zanzibar)!!
Buchanan
user_online.gif
Today, 01:50 AM
1. Kifungu cha 3 (1) cha Sheria hiyo kimeunda Mahakama za Kadhi kulingana na Ibara ya 99 (1) ya Katiba ya Zanzibar, 1984.
2. Kifungu cha 3 (1), Kutakuwa na Mahakama ya Kadhi Mkuu wa Zanzibar na Mahakama za Kadhi kwa kila Wilaya.
3. Kifungu cha 4 (1) na (2), Kutakuwa na Kadhi Mkuu (Chief Kadhi) ambaye atateuliwa na kuapishwa na Rais wa Zanzibar.
4. Sifa za kuwa Kadhi Mkuu [Kifungu cha 4 (3)]: Kuwa na kufuata dini ya Kiislamu, kuwa na taaluma ya Sheria za Kiislamu ambapo kwa maoni ya Rais anafaa kuteuliwa kushika nafasi hiyo (ya Ukadhi Mkuu).
5. Kifungu cha 5 (1): Kutakuwa na idadi ya makadhi, ambao hawatapungua kumi na hawatazidi kumi na watano ambao watateuliwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama (the Judicial Service Commission) kwa kushirikiana na Rais na Kadhi Mkuu.

Hayo ni machache kati ya mengi kuhusu Mahakama ya Kadhi, Zanzibar. Je, kukiwa na Rais Mkristo au wa dini nyingine atamteua Kadhi Mkuu kwa Zanzibar? Au haiaminiki kwamba Rais asiye mwislamu hawezi kuchukua madaraka Zanzibar? Je, Waislamu wa Bara nao wanataka Muundo huo wa Mahakama za Kadhi?

Habri ndio hiyo.


Kama itakuwa na mfumo unaofanana na huo, maana yake kila Wilaya awepo kadhi, na bara tuna wilaya karibu 200 hivyo kuwe na makadhi 200 walipwe na serikali na wachaguliwe na rais akishirikiana na kadhi mkuu !!! Ajira nzuri sana kumbe ndiyo kati ya zile ajira mil.1 za CCM !!!

Kazi ipo!!
 
Kama itakuwa na mfumo unaofanana na huo, maana yake kila Wilaya awepo kadhi, na bara tuna wilaya karibu 200 hivyo kuwe na makadhi 200 walipwe na serikali na wachaguliwe na rais akishirikiana na kadhi mkuu !!! Ajira nzuri sana kumbe ndiyo kati ya zile ajira mil.1 za CCM !!!
Kazi ipo!!

La kujiuliza ni je, Raisi asiye Muislamu (Kafir) atakuwa na uwezo wa kumteua Kadhi Mkuu ama litakalofuata ni mabadiliko ya katiba kuhakikisha Raisi lazima awe Muislamu - kaazi kwelix2 !
 
http://www.mwanahalisi.co.tz/index.php?id=555Na Saed Kubenea

HOJA ya kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Duniani (OIC) huenda ikazikwa mjini Dodoma mwishoni mwa wiki, MwanaHALISI limegundua.

Taarifa kutoka Riyadh, Saudi Arabia; London, Uingereza; na New York, Marekani; zinasema kuingia kwa mataifa makubwa katika umoja huo kumezua utata na migogoro ambayo "imetibua hadhi ya OIC ambayo wengi walitaka kujiunga nayo."

Taarifa za kibalozi na mashirika ya habari zinasema, hata hivyo, kwamba wimbi la kutaka kujiunga na OIC limepungua nguvu kutokana na ushindani wa mataifa makubwa kujipenyeza kwenye taasisi hiyo, wengine wakihofu kwamba ni kwa "shabaha ya kuudhoofisha."

Awali nchi masikini na zile zenye uchumi wa kati zilijiunga na jumuia hiyo kwa malengo ya kupata misaada mbalimbali, wakati mengine yalitaka kujitambulisha nayo kwa misingi ya madhehebu ya Kiislamu.

Tanzania imewahi kuwa na mjadala juu ya umuhimu wa kujiunga na OIC wakati wa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Alikuwa baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyezima mjadala huo na kujenga hoja kuwa Zanzibar iliyokuwa imejiunga, ilikuwa imekiuka katiba na kwamba kama ni uanachama, "basi inayojiunga ni Tanzania."

Tangu hapo mjadala wa kujiunga na OIC imekwenda kimyakimya hadi mapema 2006 wakati hoja hiyo ilipoanza kupamba moto upya ikienda sambamba na hoja ya Mahakama ya Kadhi nchini.

Suala la OIC linatarajiwa kuibuka kwa nguvu bungeni wakati Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe atakapowasilisha bajeti ya wizara yake Jumamosi.

Madai ya uanachama OIC yatakuwa makubwa kutokana na kauli ya serikali wiki mbili zilizopita, kuonekana kutotilia maanani suala la Mahakama ya Kadhi ambalo limepelekea baadhi ya viongozi wa Kiislam kuapa kutopigia kura Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa 2010.

Mjini Dodoma na hasa kwenye viwanja vya bunge, tayari kuna mvumo juu ya hatua ya baadhi ya wabunge kumkwamisha Membe iwapo hataonyesha uwezekano wa serikali kuruhusu kujiunga na OIC.

Membe, ambaye ameanza kuhusishwa na nia ya kugombea urais mwaka 2015, atakuwa na kibarua kigumu; hivyo atatakiwa kuwa mwangalifu katika kauli zake ili kupenyeza bajeti yake bila mikwaruzo.

Angalau wabunge watano (majina tunayo), ambao wanapiga chapuo kwa ajili ya watumainiwa wa ugombea urais mwaka 2015, wamekuwa wakijiapiza "kumpa Membe wakati mgumu."

Hata hivyo, wiki mbili zilizopita, Membe alionyesha ukomavu wa diplomasia pale alipokataa kujibu mashambulizi bungeni, akisema kwa vile suala lililoletwa na Mbunge wa Mchinga, Mudhihir M. Mudhihir linatokea mkoani kwao, basi atalipeleka kwenye vikao vya CCM vya mkoa.

Mudhihir alimtuhumu Membe kuathiri maamuzi ya ujenzi wa kiwanda cha saruji nje ya jimbo la Mchinga, akisema waziri huyo ni "nyoka kidimu."

"Katika hili, Membe ameonyesha ukomavu. Kulumbana hakuna maana, hasa unapokuwa na wadhifa kama alionao," ameeleza mmoja wa wabunge kutoka mkoani Lindi.

Suala la OIC litafuatia kauli ya Membe mwaka jana alipkuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake. Alisema, "hakuna madhara yoyote kwa Tanzania kujiunga na IOC" na kwamba ni suala linalojadilika.

Baadaye Oktoba mwaka jana, Membe alikaririwa akiwashangaa baadhi ya Watanzania kwa kile alichoita "kutoa kauli zinazoashiria kuiogopa OIC na baadhi ya nchi za Kiislamu."

Alikuwa akielezea hatua iliyofikiwa katika mazungumzo kati yake na Rais wa Iran, Mahmoud Ahmednejad iliyolenga kuomba nchi hiyo kufuta madeni inayoyadai Tanzania yapatayo zaidi ya Sh. 200 bilioni.

Membe aliwageuzia kibao waandishi wa habari na kuuliza, "Kwa nini tunashikwa na woga? Tukipewa msaada na Marekani tunaambiwa kuna mkono wa mtu; tukipewa na Iran tunaambiwa vivyo hivyo. Sasa niambieni mimi, kama Waziri wa Mambo ya Nje, niende wapi?"

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam amenukuliwa akisema, hakuna tena haraka ya kujiunga na OIC kwa vile tayari jumuiya hiyo imekumbwa na migogoro ya "wakubwa."

"Mimi siyo Mwislamu wala msemaji wa serikali, bali sioni umuhimu wa kujiunga na OIC kwa sasa; mataifa makubwa ya Marekani na Uingereza yamejiingiza huko ili kuiuwa. Kuna haja ya kuendelea kutafakari," ameeleza bila kutaka kutajwa jina gazetini.

MwanaHALISI haikuweza kumpata Waziri Membe wala naibu wake kwa kile msaidizi wake alisema "wana kikao kirefu."
 
Hakika Membe ana wakati mgumu kupambana na Kanisa katika hoja hii.
Hakika waZanzibari tunataka kwa hamu kubwa kujiunga na Umoja huu na tukisaidiwa na wabara wachache hususan waislam wa bara.

Sasa itabidi iamuliwe KUSUKA AU KUNYOA. KUWE NA MUUNGANO AU KUVUNJA MUUNGANO ZNZ IJIUNGE NA OIC.

Siku zote haki haiwezi kushindwa na batili.
 
Back
Top Bottom