Just in: UDSM wafukuzwa

Just in: UDSM wafukuzwa

Ningekuwa bado nafundisha UDSM ningetoa pendekezo kwa UDASA kwamba tugome kuishinikiza serikali ifafanue hizo 111.3 bn/= zimetumikaje, na iwarudishe wanafunzi na kutoa fedha za kufidia kufundisha vipindi vilivyopotea.

Augustine Moshi

UDASA ya siku hizi siyo kama ile ya zamani; UDASA ilikwisha pale Professor Chachage alipofariki. Waliopo sasa hivi ni wababishaji tu. Tangu watoto wale wafukuzwe sijasikia tamko lolote la UDASA, jambo ambalo zamani ilikuwa ni kawaida kabisa.
 
Mzee Moshi,

Heshima mbele mkuu, mbona Mtikila hakugoma kuhusu wagombea binafsi, alienda kwenye sheria ndugu yangu, siku hizi mambo huamuliwa kwenye sheria sasa kama wanafuzni wa Mlimani hawafahamu hilo, je sisi wananchi wa kawaida itakuwaje?

Kilichowashidna kul;ipeleka sula hilo kwenye sheria ni nini? Ninarudia tena kuwa serikali haiwezi ku-reward mgomo, hizo enzi zilishapita kama ziliwahi kuwepo!
 
wanabodi nataka muelewe kuwa ELIMU sio bure,hawa vijana wanakopeshwa.je mkopo ni pesa ya bure au ndio imani yetu watanzania ndio maana hata mabenki yanaweka interest kubwa,but all in all hii ni mikopo!! sio bure...na tayari waliokopa miaka ya nyuma na kupata ajira,waajiri wao wamepewa taarifa ya kuanza kuwakata mishahara kugharamia mikopo.

mzee E..embu kwa pamoja tufanye pressure group kudai mchanganua wa matumizi ya hii mikopo,nahisi kuna ghost students wengi hapa!! kati ya udhaifu wetu wadanganyika ni KUKOSA KUMBUKUMBU ,UTAONA TUNASHIKIA BANGO JAMBO..BAADA YA MUDA MFUPI TUNASAHAU,...mf..hii kesi ya ditto hata kutajwa haitajwi as you said,wale ndugu zake tibaigana aliahidi kuwakamata na kuwashtaki hadi leo bado, huo ni mlolongo wa mambo kuna wakati tegeta wakishika kiwanda cha unga.,,,kesi ilitajwa mara moja tu hadi ikasahaulika...tena wakulaumiwa zaidi ni waandishi wahabari hao wanauwezo wakuiandika habari sana..lakini ghafla wanaacha kuifuatilia hadi inasahaulika[kuna harufu ya rushwa ..]
 
Tunachoshindwa kuelewa ni kwamba madai ya wanafunzi yanahusu haki ya msingi ya wanacnhi kupata Elimu na hilo ni jukumu la serikali kuwaelimisha raia wake.Njia ipi itumike ?ndiyo kila taifa lina njia yake ya kutekeleza hilo,Sisi tumeamua mikopo basi tuitoe hiyo mikopo na isiwe Blaah balaah! Na wale waliokopeshwa awali warudishe ili wenzao nao wapate hiyo mikopo tuwe na huruma na uzalendo,wajameni!
 
21/4/2007
Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete
Rais
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ikulu
Dar es Salaam

Mheshimiwa:

RAI YA VIJANA KWA RAIS KUHUSU SUALA LA MIKOPO YA ELIMU YA JUU

Aprili 17, 2007 Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam(UDSM) uliwasimamisha masomo wanafunzi wote wa shahada ya kwanza kutoka kampasi ya Mlimani, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Chang’ombe, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Mkwawa, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi na Taaluma ya Usanifu wa Majengo, na Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma. Aidha Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) nacho kimechukua uamuzi kama kwa wanafunzi wake. Sababu ikiwa ni migomo ya wanafunzi kupinga uchangiaji wa asilimia 40 ya gharama ya elimu pamoja na ada ya matibabu (laki moja kwa upande wa UDSM). Baada ya vyuo kuchukua uamuzi huo kauli mbalimbali zimetolewa kupitia vyombo vya habari na uongozi wa wanafunzi (kupitia DARUSO, TAHLISO, SUASO), Serikali ( Wizara inayohusika, Waziri Mkuu nk), wanafunzi, wazazi, Asasi za Kiraia (LHRC, TANLET nk), vyama vya siasa (CUF, NCCR,TLP, UPDP), wabunge (wakiwemo wa CHADEMA), wazazi, viongozi wa dini na baadhi ya wananchi kwa ujumla. Kwa kipindi cha zaidi ya wiki moja CHADEMA tumelifuatilia kwa karibu suala zima na kutafakari matukio yaliyotokea na hoja mbalimbali zilizotolewa. Tunatoa rai kwa kuzingatia zaidi matukio na misimamo kuhusu suala hili katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam tukiamini kwamba maamuzi ya utatuzi wa suala hili katika chuo hiki yatahusisha pia vyuo vingine vya umma. Kwa barua hii vijana wa CHADEMA tunawasilisha kwako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania rai kwa ofisi yako ili kuchukua hatua na kutoa mwelekeo kuhusu suala hili kwa kuzingatia yafuatayo:

1. Ofisi yako iweze kuwasiliana na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ili kusimamisha(suspend) utaratibu na masharti yaliyotolewa kwa wanafunzi ambayo wanapaswa kuyatimiza kabla ya Mei 4, 2007 ili kuweza kuendelea na masomo. Masharti ambayo yameelezwa kwamba kama mwanafunzi hayatimiza hapaswi kuandika barua chuoni wala kurejea masomoni. Serikali isitishe utaratibu wa malipo ya wanafunzi kuchangia 40% (wa mwaka wa kwanza), na kulipa ada ya matibabu (laki moja) na wanafunzi kwa ujumla wao warudishwe bila masharti. (Masharti haya na mengine yalitolewa na UDSM kwa taarifa yake kwa vyombo vya habari la Aprili 18, 2007).

2. Kama Uongozi wa Chuo hauwezi kusitisha masharti hayo (hususani Sharti la Wanafunzi kulipa 40% na ada ya Matibabu kupitia benki na kuwasilisha hati ya malipo(pay-in-slip) pamoja na barua kabla ya Mei 4, 2007 kama kigezo cha Msingi cha kurudishwa masomoni), basi ofisi ya Rais itoe maelekezo kwa wanafunzi wa vyuo wasio na uwezo ni wapi wawasilishe maombi yao ya kusaidiwa kukopeshwa 40% na ada ya matibabu na kupewa hati za malipo(pay-in-slip) mapema iwezekanavyo ili wawahi kuwasilisha barua zao waweze kuendelea na masomo yao. Hii ni kwa sababu Mheshimiwa Rais uliahidi Februari 3, 2007 kwamba hakuna mwanafunzi atakayeshindwa kuendelea na masomo kutokana na michango hiyo na Waziri Mkuu amerudia kusisitiza kwamba Serikali itatekeleza ahadi hiyo (Rejea hotuba ya Waziri Mkuu alipoahirisha Kikao cha Bunge cha Aprili,2007).

3. Ofisi yako ielekeze Wizara inayohusika kuendesha mjadala kuhusu Uchagiaji wa Elimu ya Juu nchini kabla ya Bunge kujadili bajeti ya Mwaka wa Fedha 2007/2008 ili kuepusha migogoro katika vyuo vya elimu ya juu nchini ambayo kwa kiasi kikubwa inasababishwa na suala hili. (Rejea taarifa ya Tume iliyoundwa na serikali miaka ya hivi karibuni kuchunguza vyanzo vya migomo na migogoro katika elimu ya juu). Baadhi ya mambo muhususi yanayopaswa kushughuliwa ni: Mifumo ya Uchangiaji wa gharama za elimu ya juu; Kusitisha mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria na. 9 ya mwaka 2004 yenye kulenga kuimarisha uwekaji wa madaraja na viwango vya asilimia katika uchangiaji wa elimu juu; Haja ya kupandisha madaraja ya utoaji mikopo na kuweka stahili ya mikopo kwa wote wenye kupata udahili (admission); mifumo ya kutambua uwezo wa wanafunzi (means testing); Kiwango cha ruzuku na menejimenti/uendeshaji wa bodi ya mikopo na mifumo ya urejeshaji wa fedha za mikopo kwa wanafunzi. Tuko tayari kutoa maoni yetu ya ziada pindi utaratibu utakapotangazwa.

MISINGI YA RAI YETU:

Msingi wa Rai yetu ni masuala yafuatayo:


1. Mfumo wa uchangiaji uliopo hivi sasa unakinzana na Sera, Sheria na ilani ya Uchaguzi ya Chama kilichopo madarakani :

Mfumo wa uchangiaji uliopo hivi sasa unakinzana na Sera, Sheria na ilani ya Uchaguzi ya Chama kilichopo madarakani. Sera ya Elimu ya Juu ya Mwaka 1999 inazungumza kuhusu uchangiaji wa elimu kwa maana ya serikali kuwa na mchango wake na wananchi kuwa na mchango wake. Kwa mfumo ulioko hivi sasa mwananchi anabeba mwenyewe mzigo wa gharama ya elimu ya juu kwa asilimia 100%. Kupitia mfumo huu hivi sasa mwanafunzi anakopeshwa 60% (ambazo anawajibika kuzirejesha) na anapaswa kutoa 40%. Hivyo mfumo huu ni ubebaji wa gharama (cost bearing) na si uchangiaji wa gharama (cost sharing). Kwa upande mwingine, sheria na. 9 ya mwaka 2004 (sheria ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu) haitamki uwepo wa mfumo wa kutoa mikopo kwa asilimia na madaraja badala yake inatamka kwamba wanafunzi wahitaji waliopata udahili wanastahili kupatiwa mikopo. Serikali imekiri kwamba sheria hii inatoa haki zaidi ya sera ya elimu lakini cha kushangaza katika kikao kilichomalizika cha Bunge imeahidi kuirekebisha sheria hii (kwa misingi ya mapendekezo ya awali yaliyotolewa na wizara husika mabadiliko hayo yanalenga kuhalalisha maamuzi yaliyokwisha kuchukuliwa hali ambayo itarudisha nyuma kasi ya kuongeza elimu ya juu nchini). Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (Uk 44. Imeahidi kuwezesha 12.5% ya wahitimu wa kidato cha Sita kufika Elimu ya Juu) pamoja na ahadi yako Mheshimiwa Rais wakati wa Kampeni (Mchinga ,Lindi Tarehe 23/8/2005 na maoeneo mengine), kwamba mtawezesha vijana wa kitanzania wapya 30,000 kuingia Chuo Kikuu kwa Mwaka. Katika mwaka 2005-2006 ahadi hii haijatekelezwa kwa ukamilifu wake (mfumo uliopo wa uchangiaji utakwamisha zaidi utekelezaji wa ahadi hii). Huu ni mkataba na wapiga kura na ni muhimu ahadi hii ikatekelezwa kwa kuwa tafiti zimeonyesha uwekezaji wa kina na makini katika elimu ya juu kwa mwaka mmoja huongeza pato la Taifa kwa asilimia 0.63 (Rejea Hotuba ya Bajeti ya Wizara husika 2006/2007) na kwamba ni msingi muhimu katika kutekeleza MKUKUTA na kutimiza Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs). Tunaamini busara zako katika suala hili zitalirudisha taifa letu katika mstari wa sheria na kutimiza matarijio ya wananchi.


2. Elimu ya Juu ni hitaji la Wananchi na Serikali yetu inao uwezo wa kuweka mazingira ya wanavyuo kuweza kusoma elimu juu :

Sababu inayotolewa ya kutokuwapatia udhamini (kwa kuwakopesha) kamili wanafunzi ni kwamba nchi yetu haina uwezo na kwamba kama uchumi wetu ukikua basi serikali itabadili maamuzi yake. Hayati baba wa Taifa-Mwalimu Nyerere aliwahi kutuasa wakati wa mjadala wa uchangiaji wa elimu kwamba kama taifa hatuwezi kujua gharama ya elimu mpaka tutakapojaribu ujinga ! Tunapaswa kujiuliza-kipi kinaaza elimu ama uchumi au vyote kwa pamoja ? Kama nchi ambazo zina uchumi wa chini kuliko ya kwetu zinawekeza katika elimu ikiwemo ya juu zaidi yetu ni kwa vipi tutaendelea kwenda mbele zaidi yao ?(Mathalani rejea viwango vya idadi ya wanafunzi katika nchi za SADC-Afrika Kusini 9.11%, Kenya 1.47, Uganda 1.23, Lesotho 0.98, Malawi 0.42, Msumbiji 0.33, Tanzania 0.27). Nchi za Asia Mashariki (The Tigers) walikuwa na nguvu ya kiuchumi kama sisi katika miaka ya 1960 lakini kwa pamoja na mambo mengine kuwekeza katika elimu ya juu wameweza kufikia hatua waliyoko sasa, kwa nini sisi tuendelee kutumia umaskini wetu kama sababu ya kutowekeza kwenye elimu ? Kama Mheshimiwa Rais ulitamka ukiwa kwenye ziara ya nchi za Scandnavia kwamba nchi yetu haina wataalamu wa kutosha wenye uwezo ndio maana tunaingia katika mikataba mibovu kwa nini tusielekeze nguvu katika kuwa na wataalamu wetu wenye uwezo wengi zaidi ?. Lakini sisi tunaamini kwamba nchi yetu inao uwezo hata katika bajeti hii inayoendelea kutumika hivi sasa. Kama ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) inaonyesha kwamba kwa mwaka 2005/06 shilingi bilioni 700 hazieleweki matumizi yake na tayari tumeshazidisha bajeti kwa bilioni 900. Kama serikali kwa kipindi hiki imeweza kusamehe kodi na kwa kiasi kikubwa kwa wafanyabiashara wakubwa kwa takribani bilioni 400. Kama tumeweza kuilipa kampuni ya Dowans (kampuni iliyotokana na Richmond) shilingi zaidi ya Bilioni 100(pamoja na kwamba mpaka sasa hawajaweza kutupatia umeme wa megawatts 100 kama ilivyokuwa katika mkataba). Kama tumeweza kuongeza idadi ya magari ya thamani (mashangingi) na semina elekezi. Ni dhahiri kwamba uwezo tunao ! Katika mwaka wa fedha 2005/06 (wakati ambapo hakukuwa na uchangiaji wa 40% wala madaraja katika utoaji wa mikopo) serikali ilikopesha jumla ya wanafunzi 42,729 ambayo ni sawa ya jumla ya shilingi bilioni 62.9 (Rejea Hotuba ya Waziri wa Elimu ya Juu akiwasilisha makadirio ya Bajeti ya Serikali 2006/07). Hivyo elimu ya juu ni gharama ambayo kama taifa tunaweza kuimudu. Kwa mantiki hiyo basi baada ya serikali kulipa 60% tunaamini kwamba kiwango cha 40% kilichobaki serikali inaweza kukimudu ndani ya bajeti inayoendelea hivi sasa kwa kubadilisha mafungu ya bajeti ama kuahirisha ulipaji (isipokuwa suala la kuwalipa wanafunzi kikamilifu kwa ajili ya kwenda mafunzo kwa vitendo ambalo lipaswa kufanyika sasa) mpaka mwaka wa fedha 2007/08. Izingatiwe kuwa fedha hizi ni mkopo kwa hiyo sio gharama zinazozama (sunk cost) ni uamuzi wa kutunisha mfuko wa bodi ya mikopo ambao kwa msingi wake wa kisheria fedha zake ni za mzunguko(revolving). Ikumbukwe kwamba elimu (ikiwemo elimu ya juu) ni hitaji kipaumbele kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Ni dhahiri kwa muktadha wa Ripoti ya Hali ya Umaskini na Maendeleo ya Watu Tanzania (Poverty and Human Development Report) watanzania walio wengi hususani wa vijijini hawana uwezo wa kuchangia 40% ya elimu ya juu ambayo ni kati ya 500,000 na 1,500,000 ( ukijumlisha ada ya masomo, matibabu, gharama za mafunzo kwa vitendo na michango mingine).


3. Madai ya wanafunzi yameanza kutolewa mapema, na ahadi za kuyatatua nazo zikatolewa, ni vyema sasa yakapatiwa ufumbuzi :

Sera ya Uchangiaji wa Elimu ya Juu ilianza kutekelezwa kwa awamu kwa kuanzia awamu ya kwanza mwaka 1992 na awamu ya pili mwaka 2004/5 hivyo katika hali ya kawaida maandalizi ya utekelezaji wa awamu ya tatu yalipaswa kuanza mapema. Utekelezaji awamu hii ulianza kuleta migogoro tangu hatua za awali. Serikali iliahidi kulipatia ufumbuzi suala hili kwa pamoja na mambo mengine kuanza kutumia mifumo ya kutambua wanafunzi wahitaji wa mikopo na kuweka viwango (Means Testing) katika mwaka wa fedha 2006/07(Rejea hotuba ya Bajeti ya Wizara husika). Kushindwa kwa wizara husika kuweka utaratibu bora wa kuwatambua wahitaji na viwango mpaka sasa hakupaswi kuwa sababu ya kuweka mazingira ya wanafunzi wasio na uwezo kushindwa kuendelea na masomo na wala kuwataka wanafunzi wawasilishe hati ya malipo (pay-in slip) ndani ya siku 10 haiwezi kamwe kuwa njia bora ya kupima uwezo wa wazazi kuchangia elimu juu. Mara baada ya bajeti, utekelezaji wa uchangiaji wa awamu hii ulizua migogoro. Na hatimaye wanavyuo wakalazimishwa na utawala kusaini fomu za kukubaliana na utaratibu wa kulipa 40% kwa ahadi kwamba utaratibu utawekwa kwa ajili ya wasio na uwezo. Oktoba 22, 2006 Vijana wa CHADEMA tulitoa rai kwa wizara inayohusika kushughulikia suala zima mapema ili kuepusha migogoro na kuweka utaratibu ambao utawasaidia watanzania wasio na uwezo. Baada ya hapo zilifuata safari za wanafunzi wa vyuo mbalimbali kwenda Bodi ya Mikopo kuwasilisha hoja zao kuhusu kushindwa kulipa 40% (mathalani 16/1/2007 Wanafunzi wa SUA). Tarehe 28 Januari, 2007 Wanafunzi wa UDSM waliandamana mpaka Uwanja wa Jangwani kuwasilisha madai yako lakini siku hiyo hiyo, Waziri wa wizara husika-Prof Peter Msolla akasisitiza kwamba kuchangia asilimia 40 ni suala la lazima. Hatimaye ukafuata mkutano wako na wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dar es salaam kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya CCM tarehe 3 Februari 2007 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo (baada ya kusikiliza risala ya wanafunzi) uliahidi (kama mwenyekiti wa chama tawala) kwamba utawasiliana na chama chako kutafuta ufumbuzi wa suala hili na kwamba taarifa zingetolewa baada ya mwezi mmoja kuhusu hatua ambayo ingefikiwa. Hatahivyo ukasisitiza pia kwa namna ya pekee kwamba hakuna mwanafunzi atayeshindwa kuendelea na masomo kwa kushindwa kulipa 40%. Machi 3, 2007 mwezi mmoja ulipotimia Chuo Kikuu kiliitisha mkutano na kueleza kwamba suala hilo bado linaendelea kushughulikiwa. Lakini cha kushangaza mwezi mmoja baadaye (3-6 Aprili 2007) Waziri Msolla akiwa katika Ziara ya Vyuo Vikuu Zanzibar alisisitiza kwamba serikali haina fedha za kutosha kulipia asilimia 40 ya gharama za elimu ya juu nchini na kwamba utaratibu wa kuchangia utaendelea ( Rejea Nipashe 7/4/2007). Kwa mzazi na mwanafunzi yoyote kauli hii ilitoa picha ya namna gani ahadi yako ya Machi 3 ilikuwa ikielekea kutelekezwa badala ya kutekelezwa !. Matukio yote haya yalitokea kipindi ambacho wanafunzi walikuwa wanakaribia mitihani yao ya kufunga semista huku katika baadhi ya vyuo matamko yakitolewa na utawala wa vyuo kwamba wanafunzi ambao hawatalipa 40% hawatapewa matokeo yao. Wakati malalamiko ya 40% yakiwa bado yanafukuta yakaibuka masuala mengine ambayo kwa maoni yetu yalichangia kuongeza kasi ya mgogoro : Mosi, wanafunzi kutakiwa na uongozi wa chuo kulipa ada ya matibabu shilingi laki moja (ambayo hata haikuwepo katika mkataba). Pili, wanafunzi walitakiwa kujiandaa kwenda katika mafunzo ya vitendo (field) lakini wakaelezwa kwamba watalipwa 3,600 kwa siku badala ya 6,000 kwa siku ambayo imekuwa ikitolewa (tofauti ya 2,400 ikiwa ni 40% ambayo wanafunzi walipaswa waongeze wenyewe). Ikumbukwe kwamba kwa lengo la kuboresha ubora wa wahitimu na utalaamu (professionalism), mafunzo haya kwa vitendo hufanyika nje na makazi ya kawaida ya mwanafunzi hivyo mwanafunzi hulazimika kugharamia usafiri, malazi, chakula nk ! Viongozi wa wanafunzi wakakutana na Katibu Mkuu wa wizara husika na kuelezwa kwamba hata waende popote, uamuzi wa wanafunzi kulipwa shilingi 3,600 utabaki palepale. Kwa maneno mengine suala la kuahirisha malipo ya 40% mpaka mwaka ujao wa fedha likawa halipo tena kama inavyoelezwa kwa sababu wanafunzi wanapaswa kwenda kwenye mafunzo kwa vitendo kabla ya bajeti ya Mwaka ujao wa Fedha. Makamu Mkuu wa Chuo-Profesa Rekwaza Mukandala akaweka wazi katika kikao cha Bunge la Wanafunzi kwamba hakuna namna yoyote ya kuwasaidia (zaidi ya kupunguza idadi ya siku au kuwapangia wanafunzi mafunzo kwa vitendo maeneo ya karibu makazi yao-hoja ambazo zilikataliwa kwa kigezo cha kupunguza ubora wa taaluma) na kama watagoma basi watafukuzwa. Hatimaye wanafunzi wakagoma (kiasi kikubwa kwa amani ukilinganisha na miaka mingine) na hata kabla ya kutimia siku 3 mfululizo za kutafuta ufumbuzi kama kanuni za UDSM zinavyoelekeza, wanafunzi wakasimamishwa masomo na Chuo kikafungwa. Kipindi hiki chote hakiwezi kuitwa ‘kutoa siku mbili kwa serikali’ kama ambavyo baadhi ya viongozi wamekuwa wakilaumu. Mheshimiwa Rais, kwa kuwa umewahi kuwa Kiongozi wa Wanafunzi UDSM, ukipitia mtiririko wote wa matukio na kauli, utabaini jambo lililodhahiri ni kwamba wanafunzi wameingizwa katika mazingira ya misongo (pressure) hivyo taifa linapaswa kuwasaidia zaidi wa kuwalaani na katika kushughulikia suala hili viongozi wa wanafunzi wanapaswa kushirikishwa badala ya kutolewa kafara.


HITIMISHO :

Mheshimiwa Rais tunatambua kwamba wewe ni kiongozi uliyeahidi hususani katika hotuba yako ya kuzindua Bunge Disemba 30 mwaka 2005 kwamba utaongozwa kwa kushirikisha wananchi na kufuata ushauri wa makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo vyama vya siasa kwa kutanguliza mbele maslahi ya Taifa. Aidha Mheshimiwa Rais kwa nafasi yako ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri, hivyo tunaamini muongozo wako unaweza kutoa mwelekeo mwafaka kwa wizara na taasisi zinazohusika. Kwa upande mwingine, ni mwenyekiti wa chama kilicho madarakani hivyo ahadi zako ni msingi wa mwelekeo wa serikali iliyoko hivi sasa. Tunaamini utaichulia rai yetu kwa uzito unaostahili kabla ya tarehe ya mwisho iliyotolewa na Chuo kwa wanafunzi kuweza kutimiza masharti yaliyoelezwa. Tunaamini katika hatua ambayo suala hili limefikia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye unayeweza kuwaepusha wanafunzi wa vyuo kushindwa kuendelea na masomo yao kwa sababu ya uchangiaji wa elimu ya juu nchini kama ulivyoahidi tukiamini kwamba kwa kuwa umepata wasaa wa kuzunguka nchi nzima unaielewa hali hali ya Taifa na wananchi wake na hivyo utachukua hatua za haraka kuepusha matabaka na migogoro katika elimu ya Juu nchini.

Tunatanguliza shukrani tukitarajia utaifanyia kazi Rai Yetu


John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana na Kaimu Katibu Mkuu
0754 694 553
vijana@chadema.net
www.chadema.net


Nakala : Makamu wa Wakuu wa Vyuo (UDSM, SUA) ; Rais wa Wanafunzi (DARUSO, SUASO) ; Vyombo Vya Habari
 
Mmh! Lets hope the gentleman has ears to listen and eyes to see.
Asijeweka hiyo barua kapuni kama zilivyo ripoti kadhaa za kamati alizounda mwenyewe!
 
Chuo Kikuu kulegeza masharti
2007-04-23 09:43:24
Na Dunstan Bahai


Masharti tisa magumu yaliyotolewa na uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa wanafunzi waliosimamishwa, huenda yakalegezwa ili kuwawezesha wanafunzi hao kurejea na kuendelea na masomo.

Hali hiyo imekuja huku kukiwa na taarifa kwamba, wanafunzi wote wameitwa leo chuoni hapo kwenda kuchukua barua za maelekezo ya namna ya kurejea.

Hatua hiyo imeelezwa kwamba, ilifikiwa baada ya Chama Cha Mapinduzi kuingilia kati kutaka kujua kiini hasa cha matatizo yanayowakabili wanafunzi hao.
Taarifa za kina zilizopatikana kutoka chuoni hapo na ndani ya CCM, zilieleza kwamba, uongozi wa juu wa CCM umeagiza kupelekewa taarifa kamili za matatizo yanayokikabili chuo hicho.
Mbali na CCM kuingilia kati kuhusu hali iliyowakumba wanafunzi hao, Usalama wa Taifa nao umeingilia kati ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanafunzi waliotimulia ambao bado wako jijini Dar es Salaam, wanakuwa katika mazingira ya usalama zaidi.

Wanafunzi hao waliotimuliwa chuoni, leo walikuwa waanze mitihani yao ya kumaliza chuo kwa wale wa mwaka wa tatu na kuingia mwaka mwingine kwa wale waliochini ya mwaka wa wa tatu.
Kuhusu maisha ya wanafunzi hao waliotimuliwa, imeelezwa kwamba, hali zao zinazidi kuwa mbaya na kwa upande wa wasichana wanaendelea kudhalilika kwani wengi wamekuwa wakizagaa kwenye nyumba za starehe nyakati za usiku na mchana kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo wakijifanya wasafiri lakini wakiwa katika mawindo ya ukahaba.
Hatua hiyo imefikiwa na wanafunzi hao baada ya kuuza vitu vyao kama vile televisheni, simu za mkononi, nguo na vitu mbalimbali ili waweze kujikimu na maisha ya Dar es Salaam wakisubiri hatma yao.
Masharti yaliyotolewa na Chuo kwa wanafunzi wa Shahada ya Kwanza wanaotaka kurejea chuoni hapo kwa wanaodhaminiwa na Serikali ni kulipa kwanza asilimia 40 ya fedha zote za mkopo pamoja na Sh.100,000 za matibabu.

Kiwango cha asilimia 40 ya mkopo huo, kinatofautiana kulingana na kitivo cha mwanafunzi.

Taarifa iliyotolewa na chuo wiki iliyopita ilieleza kuwa kila mwanachuo ambaye hajalipa Sh. 100,000 za matibabu, atapaswa kulipa sambamba na asilimia hiyo 40.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya awali, mwanafunzi atakayefikiriwa kupokelewa chuoni hapo ni yule ambaye atawasilisha risiti za malipo hayo.

Taarifa hiyo iliwaagiza wanafunzi hao kulipa fedha hizo kupitia Benki ya NBC tawi la Mlimani katika akaunti namba 040103001709.

Aidha, taarifa iliwataka wanafunzi wanaotaka kurudi Chuo Kikuu, kuandika barua kuanzia leo na kueleza nia ya kutaka kurejea chuoni na Mei 4, mwaka huu, itakuwa ni siku ya mwisho ya kupokelewa kwa barua zao za maombi.

Hatua ya kuwasimamisha wanafunzi ilichukuliwa kufuatia kikao maalum cha 172 cha Baraza la Chuo kilichojadili mgomo wa wanafunzi uliolenga kuishinikiza serikali kuwapatia mikopo ya elimu ya juu kwa asilimia 100 badala ya asilimia 60.

Asilimia 40, inalipwa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza, wakati wa mwaka wa pili wanapewa udhamini kwa asilimia 100.

Hata hivyo, wanafunzi wa mwaka wa pili na kuendelea licha ya kudhaminiwa kwa asilimia 100, lakini wanapaswa kuchangia Sh. 100,000 za matibabu.

SOURCE: Nipashe
 
; hakuna kazi ya mitaani hapo Dar ambayo mwanafunzi anaweza kuifanya na kuweza kulipia gharama za masomo ya chuo kikuu.

Are you sure??

Tatizo watu mkiwa ulaya mnasahau au mnadhani kwamba mambo Bongo yamebadilika sana kiasi cha mwanafunzi kupata kazi ya kufanya mtaani ili ajilipie ada kama ulaya.

Kwanza hata kama kazi zingekuwepo, miundo mbinu hairuhu mtu kufanya kazi huku anasoma chuo kikuu cha Dar es Salaam. Kama kutoak Mabibo Hostel tu kwenda Mlimani Campus wanafunzi wanagombea daladala mpaka wanapitia madirishani, itawezekanaje mtu kufanya kazi mjini halafu awahi kipindi chuoni? Foleni za magari Dar kwa sasa ni kero isiyo mithilika!

Tuacheni kubweteka kusahau kwamba Bongo mambo ni shaghala baghala zaidi ya mlivyo yaacha!
 
wajameni nimesoma post hapo juu kuhusu wattoto wetu wa kike hususan wanavyozalilika,pia nafurahi kuwa maoni ya forum hasa wale wenye huruma na watoto yanatekelezwa kwa usalama wa taifa wanafuatilia kuona hawa watoto wanakuwa katika mazingira salama[ref nipashe link above]
ila nashangazwa na ccm kutaka maelezo its seems MUKANDARA haya masharti alipewa na CCM ayatoe ,ili baadaye CCM waje waagize yalegezwe mwisho wa mchezo wao ndio watatoka MRITHI[yaani wanafunzi na wananchi wataona ccm ndio imefanikisha masharti kulegezwa..siasa bwana..si mnajua mkandara ni mmoja wa wapanga mikakati wa MUUNGWANA.
 
Nimeogoa Siasa za Tanzania kwa kweli kama ni hivi basi tuna kazi mbeleni
 
Wale wanafunzi wa chuo kikuu ni watoto sana kweli kwa kutumiwa na wanasiasa kujipatia point chache za kisiasa, na hasa katika mazingiara magumu ya namna ile. Najaribu kufikiria kuwa kiongozi wa serikali akifukuzwa huwa anapewa notici ya siku thelathini hivi, inakuwaje wao wafukuzwa kwa notisi ya saa mbili tu, halafu CCM inakuja kujiingiza hapa kujifanya mkombozi huku tukijua kuwa wote waliotoa uamuzi wa kuwafukuza watoto wale kinyama vile ni viongozi hao hao wa CCM. Kwanza CCM ina nafasi gani katika maswala ya elimu ya vyuo vikuu hapa nchini? Huu siyo wakati wa chama kushika hatamu.
 
Wale wanafunzi wa chuo kikuu ni watoto sana kweli kwa kutumiwa na wanasiasa kujipatia point chache za kisiasa, na hasa katika mazingiara magumu ya namna ile. Najaribu kufikiria kuwa kiongozi wa serikali akifukuzwa huwa anapewa notici ya siku thelathini hivi, inakuwaje wao wafukuzwa kwa notisi ya saa mbili tu, halafu CCM inakuja kujiingiza hapa kujifanya mkombozi huku tukijua kuwa wote waliotoa uamuzi wa kuwafukuza watoto wale kinyama vile ni viongozi hao hao wa CCM. Kwanza CCM ina nafasi gani katika maswala ya elimu ya vyuo vikuu hapa nchini? Huu siyo wakati wa chama kushika hatamu.
Bado kinashika ndani ya jinamizi la vyama vingi!
 
Nimekutana na hili shauri nikachoka kabisa, hata sijui nani kalitunga!

NI RAHISI KUNYAMAZA, MKUBWA AKIKOSEA,
KWANI UKIMCHUKIZA, AWEZA KUKUONEA,
NI RAHISI KUNYAMAZA, WENGINE WAKIUMIA,
HAO WAJIGALAGAZA, NA KELELE ZA KULIA,
HAIKUHUSU WA WAZA, WANANGU WAMETULIA,

BUTHELEZI NA MANDELA, MWENYE BUSARA NI YUPI?
MMOJA KAENDA JELA, MWINGINE KALISHWA PIPI,
HIZO PIPI ZA MADHILA, ZITAKUFIKISHA WAPI?
KIMYA NACHO KINA HILA, USHUJAA UKO WAPI?
ISINGEKUWA MANDELA, LEO WANGEKUWA WAPI?

MFALME "KAVAA" UCHI, UKISEMA WALAUMU?,
CHAKULA HIKI KIBICHI, KULALAMIKA HARAMU?,
KUMBE SISI WANANCHI,TWASITAHILI HUKUMU...,
TULIPOITAKA NCHI, TUJISHIKIE HATAMU?,

KUSEMA KIHEREHERE, KUNYAMAZA NI BUSARA?,
NA KAMA SIO NYERERE, KUIPIGANIA BARA,
TUNGALIBAKI MILELE, WATWANA WA MALIKIA,
KUMBE KUPIGA KELELE, KWAWEZA KUSAIDIA,
 
Wazee mbona tunachanganya mambo? Mwalimu alifuata ngazi za kisheria katika kutuletea uhuru, ndio maana alienda mpaka kuzungumza UNO, akiwa na makaputula yake ndio mzee Bomani akampa suti yake,

sasa eti mnataka kulinganisha kuleta uhuru kwa Mwalimu, na hawa wahuni wa Mlimani? Guys can we for once again get serious na ishu hapa forum?
 
Wazee mbona tunachanganya mambo? Mwalimu alifuata ngazi za kisheria katika kutuletea uhuru, ndio maana alienda mpaka kuzungumza UNO, akiwa na makaputula yake ndio mzee Bomani akampa suti yake,

sasa eti mnataka kulinganisha kuleta uhuru kwa Mwalimu, na hawa wahuni wa Mlimani? Guys can we for once again get serious na ishu hapa forum?

Mzee ES,

Najua heshima yako iko pale pale, ila I believe you can express yourself in a better language than this.
 
Mzee Kichuguuu,

Heshima mbele mkuu, kuigomea serikali ni kuvunja sheria ya nchi, ndio maana Mwalimu alikuwa akiwachapa viboko yeye mwenyewe, kina Mwabulambo,

Tutawaitaje hao vijana, maana ni matusi makubwa kuwalinganisha na mbio za Mwalimu kutafuta uhuru? Halafu naomba unifahamishe walichofanikiwa kubadilisha na huu mgomo kama sio kuwaletea wanafunzi wote na wasiohusika maisha magumu hapo chuoni?

Mzee wangu ninajua kuwa you know better, kuwa migomo kwa nchi kama yetu ni kuwapatia ushujaa wa bure viongozi wetu, ndio maana waliohusika na huu mgomo lazima waelewe kuwa kuna wananchi ambao hatukufurahishwa, maana leo kuna njia nyingi za kuweza kuibana serikali kutatua matatizo yao, badala ya mgomo, sitaki kuamini kuwa ulihusika na kuwashawishi mzee!

Halafu usisahau kuwa hawa Mlimani walikuwa mstari wa mbele kum-support Muuungwana kwenye urais! au umesahau zile "POLLS"! ndio maana ninasema sisi wabongo sometimes tunahitaji kuchomekwa waya za umeme vichwani ili vichwa viamke, and I mean it! Hivi sisi wabongo ni watu wa aina gani?

Mzee Kichuguuu, lazima ukubali kuwa hatuna mfano dunia nzima! I mean mwaka jana hawa walikuwa wanamshangilia rais ambaye leo tena wanamgomea, hivi kweli inaingia akilini mwako! Chuo gani kikuuu duniani ulikisikia duniani kinashangilia mgombea urais kama sio Cuba na Venezuela?

Inafika mahali wananchi tunachoka, maana hawa si ndio wasomi tunaowategemea?
 
Ni rahisi kumwita MWIZI mtu aliyeiba kuku kutokana na njaa yake lakini yule anayesababisha maelfu ya watanzania wakose huduma kama barabara,maji,umeme,afya,etc kwa KUIBA mabilioni kwa tamaa zake za kuifurahisha nyumba ndogo yake anaishia kuitwa MBADHIRIFU.Talk of class:mlalahoi akiiba anaitwa mwizi,kigogo akiiba anitwa mbadhirifu.
Vivyohivyo,ni rahisi kuwaita wasomi wetu WAHUNI kwa kuogmea suala lenye mantiki lakini kutowapa jina lolote waliotoa tenda kwa Richmond ilhali mabilioni mengine yanapotea kila mwezi kwa IPTL kwa uzembe wa makusudi wa watu flani.
Hivi mhuni ni nani,wanafunzi wa Mlimani waliopewa ahadi hewa ya kutatuliwa matatizo yao na JK au huyo JK aliyeahidi kutatua matatizo ya wanafunzi in the first place.
Bila kujali mtu amepitia Mlimani au la (JK alipitia hapo na kupata digrii yake pasipo kuchangia senti tano),wadogo zetu hapo Mlimani walikuwa na hoja ya msingi hasa tukizingatia uwezo halisi wa wazazi wetu katika kuchangia hizo asilimia 40 za gharama za masomo.Ni rahisi kwa watwala wetu kutoa maamuzi kama hayo kwa vile watoto wao wanasomeshwa vyuo vya gharama kubwa nje ya nchi kwa fedha za haohao walipa kodi makabwela wanaotakiwa kuchangia asilimia 40.
Mbona hatuwaiti wabunge WAHUNI kwa "kugoma" kujadili hoja ya Richmond?Au Spika MHUNI kwa kushindwa (au kugoma?) kuweka hadharani ripoti ya saga la Mengi-Malima lililokula mamilioni ya fedha za makabwela?Au Lowassa sio MHUNI kwa jitihada zake za kuua mjadala wa Richmond kila bunge linapokutana?

Mhuni mwingine ni Profesa Mkandara,ambaye kimsingi ni REDET yake iliyokuwa ikiendesha POLLS za kuonyesha Muungwana anakubalika miongoni mwa watanzania.Well,kishalipwa fadhila zake na Muungwana na sasa anapeta.KUGOMA NI KUVUNJA SHERIA ZA NCHI,LAKINI JE PALE HAKI ZINAPOCHEZEWA TUNAPASWA KUFANYA NINI?Twende mbele zaidi ya hapo.Hivi kama vijana hao wanatambua bayana kuwa wazazi wetu hawana uwezo wa kuwalipia hiyo asilima 40 (wangekuwa na uwezo wasingekuwa hapo Mlimani in the first place) walipaswa wafanyeje?Pengine ni kweli kuwa serikali haina uwezo wa kuwagharamia wanafunzi hao kwa asilimia 100 (I doubt it kutokana na ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali,ukichanganya na kauli ya Chenge kuwa serikali itaendelea kununua mashangingi...) lakini kilichopaswa kufanyika ni kuandaa mazingira mazuri,prefarrably kabla wanafunzi hawajajiunga na chuo,kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anayetia mguu hapo Mlimani anafahamu mzigo anaopaswa kuubeba.Kwa namna hiyo,wale wasio na uwezo wangeweza ku-opt kutojiunga kabisa na chuo huko wale wanaojimudu kidogo wangekwenda hivyohivyo.

Tusiwasahau makabwela wenzetu....
 
Mzee wangu tunafikia mahali wote wananchi na viongozi tunakuwa wababaishaji, Tanzania, kiongozi yoyote anayekuja kutoa ahadi za kushughulikia ili wanafunzi wasilipe hela za shule ni muongo, kama sio muhuni, sasa sielewi mimi ninaye msikiliza hizi ahadi na kuamini, nita-fit wapi kwenye dunia ya leo?

Elimu lazima ilipiwe, na haiwezi kuwa chini ya 40%, sasa hiyo itakuwa ni kusoma bure kwa standards za dunia, serikali haina hela za kuendesha shule bure kama zamani, if anything serikali yetu inapaswa kuanzisha tabia kama za huko majuu za wanafunzi kusoma na kufanya kazi, na sidhani kama hilo linahitaji serikali kuingilia kati, maana ninawajua wanafunzi kibao tena toka nje ya nchi yetu, ambao wako bongo wakisoma na kufanya kazi, kwa maana nyingine wakijisomesha wenyewe, kwa nini sisis wabonbgo hatuwezi, lakini tukienda nje tunaweza?

Elimu ya bure haipo tena ndugu zangu, ili serikali ifidie hizo hela zinazolalamikiwa, somebody has to pay for, sasa nani atakayelipia? Mzee Mlalahoi, unazo points za kutosha kuwaita viongozi wetu wahuni, ila only kama kuna ushahidi na huo usanii wote uliousema maana so far hakuna mwenye ukweli zaidi ya blah! blah!

Ninaukumbuka kwa macho yangu mkutano wa Muungwana na wanafunzi wa vyuo vya juu pale IFM, kabla hata hajatangaza kugombea urasi, jinsi walivyokuwa wakimshangilia mpaka kujaribu kumbeba juu wakati akitoka ukumbini, sasa imekuwaje tena? Yaani zile polls alikuwa akizitoa Mkandara peke yake?

Tutaendelea siku zote kuwalilia makabwela, lakini sio hawa wa Mlimani, kweli mwanafunzi wa University chuo kikuuu, kiongozi anawezaje kuja kukupa ahadi za kijuu juu tu ukakubali? Si palitakiwa kuwe na kamati ya kuchaguliwa pale pale, itakayo co-ordinate na rais katika kufuatilia hizo ahadi au?
 
Mzee wangu tunafikia mahali wote wananchi na viongozi tunakuwa wababaishaji, Tanzania, kiongozi yoyote anayekuja kutoa ahadi za kushughulikia ili wanafunzi wasilipe hela za shule ni muongo, kama sio muhuni, sasa sielewi mimi ninaye msikiliza hizi ahadi na kuamini, nita-fit wapi kwenye dunia ya leo?

Elimu lazima ilipiwe, na haiwezi kuwa chini ya 40%, sasa hiyo itakuwa ni kusoma bure kwa standards za dunia, serikali haina hela za kuendesha shule bure kama zamani, if anything serikali yetu inapaswa kuanzisha tabia kama za huko majuu za wanafunzi kusoma na kufanya kazi, na sidhani kama hilo linahitaji serikali kuingilia kati, maana ninawajua wanafunzi kibao tena toka nje ya nchi yetu, ambao wako bongo wakisoma na kufanya kazi, kwa maana nyingine wakijisomesha wenyewe, kwa nini sisis wabonbgo hatuwezi, lakini tukienda nje tunaweza?

Elimu ya bure haipo tenba ndugu zangu, ili serikali ifidie hizo hela zinazolalamikiwa, somebody has to pay for, sasa nani atakayelipia? Mzee Mlalahoi, unazo points za kutosha kuwaita viongozi wetu wahuni, ila only kama kuna ushahidi na huo usanii wote uliousema maana so far hakuna mwenye ukweli zaidi ya blah! blah!

Mzee ES,ushahidi wa uhuni wa viongozi wetu zaidi ya ule uliopo kwenye ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali ni upi tena?Hivi kweli Mzee ni blah blah kwa Bunge kutumia mamilioni kamjadili Mengi na Malima then ishu inamalizwa kwa "kuomba wahusika wapatane" ilhali ripoti inaishia kupata vumbi kwenye makabrasha?Hivi kauli ya Chenge kuwa serikali itaendelea kununua mashangingi "kwa vile haijathibitika kuwa kutoyanunua hakutaleta maendeleo ya nchi" sio uhuni huo?Na je no balh blah unaposikia Lowassa,WAZIRI MKUU,akidai kuwa alimwonya junior wake Msabaha kuhusu suala la Richmond,then "aliyotabiri yakatokea" na Lowassa huyohuyo anaendela kuhakikisha kuwa suala la Richmond halizijadiliwi bungeni.Na unapomsikia Lowassa akidai kuwa hakuna haja ya mjadala kuhusu Richmond na Dowans kwa vile mabwawa yameshajaa na umeme unapatikana,unapata picha gani kama sio uhuni wa viongozi wetu?

Nakubaliana nawe kuwa ni vigumu kwa serikali kuchangia asilimia 40 au kutoa elimu ya bure (japo fedha inayotumika kuwapatia watoto wa wateule wachache huku ughaibuni ni zaidi ya asilimia 100 japo wengine wamekuja kusoma diploma za hotel management ambazo zinapatikana kwa gharama nafuu huko nyumbani).Lakini hivi kweli hilo linashindikana kwa serikali inayoweza kulipa mabilioni kwa IPTL au Dowans huku ikiwa na baraza kubwa kabisa la mawaziri duniani ambalo kila baada ya miezi mitatu linahitaji semina zinazogharimu mamilioni kwa ajili ya kukubushana majukumu?
 
Back
Top Bottom