Just in: UDSM wafukuzwa

Just in: UDSM wafukuzwa

Kulikoni, njia pekee ya serikali kuweza kukusanya hizo asilimia 40 ni wao kuonesha kuwa kila mzazi wa mwanafunzi ana uwezo huo. Serikali iseme imetumia kigezo gani kuamua asilimia 40 ichangiwe na wanafunzi, na wakiwaelewesha jinsi wazazi wao watakapotoa hizo asilimia 40 bila ya shaka wazazi na wanafunzi watachangia kwa furaha. The burden of proof is on the government to show that the families of the students can cough up that 40%!
 
Well said mwanasiasa! Wananchi wanawatuhumu wanafunzi kwamba ni wabinafsi...wanaandamana ikiwa ni maslahi yao tuu!!! Hawajawahi kuandamana kuhusu issue nyingine yoyote ya kitaifa...wanaonekana mitaani wakiwa wanataka watatuliwe matatizo yao (tangu enzi zetu)!! Kazi kweli kweli! Tuandike, tulaumu, tufanye nini, we need to think beyond the box! Wanafunzi wetu wa elimu ya juu, bado, bado sana!!!! Uelewa wao ni mdogo sana!

Mnyika...kwa nini usiwashauri vijana ( I DONT DOUBT YOUR CAPABILITY, TULISHAWAHI KUSOTA WOTE PALE MLIMANI)....... wafanye lobbying na wabunge..sheria iibadilishwe wawe na gurantee ya kupewa hiyo mikopo! Maana jiulize hawa wadogo zetu wanao pata elimu ya bure primary...watakuwa wapi in ten years? Tuache jazba za kisiasa hapa...lets adress the root course ambayo ni sheria mbovu...kuandamana hata kama wangepewa hizo pesa leo...after two years..inflation na mengineyo yatawarudisha kwenye mgomo tena! Kila lakheri!
 
Tatizo linaloisumbua Tanzania linatokana na serikali kuchukua sera za soko huria kwa pupa bila kuweka malengo thabiti ya kitaifa. Ingawa sera hizo kwa kwaida zikitekelezwa vizuri zina faida sana kwa maendeleo ya Taifa, serikali yetu haikutekeleza sera hizo sawasawa, na hii ni kuanzia tangu enzi za Mkapa wakati akiuza mashirika ya umma hovyo hovyo kama vile yalikuwa yamepatikana bure.

Sasa leo hii utasikia serikali inasema kuwa inataka kujenga chuo kikuu kikikubwa kuliko vyote afrika mashariki na ya kati wakati ikijua kabisa kuwa kwa vile pato la mwanachi wa kawaida ni chini ya dola 600 kwa mwaka, watoto wa wananchi hao wa kawaida, amabo ni karibu asilimia 80 ya taifa lote, hawawezi kumudu kulipia gharama za masomo hayo kwa viwango vya sasa. Hii yote inaonyesha kabisa kuwa serikali inazungumza mambo bila kuyafanyia utafiti wowote. Ni lazima kabisa serikali itambue kuwa utatuzi wa matatizo ya nchi yetu unatokana na kuwa na umma ulioelevuka, siyo kuita wageni kutuendesha nchi yetu wakati raia wetu ni mbumbumbu. Hofu inayotokana na kuwa kuwa na umma mkubwa uliogubikwa na umaskini uliokubuhu na ujinga wa kutokujua dunia inakwendaje ndiyo inayosababisha watu wengi tupinge kujiunga na Jumuia ya Afrika mashariki. Kujenga umma ulioelevuka ni lazima serikali iwekeze sana kwa elimu.

Itake isitake, Tanzania inatakiwe iendelee kutoa elimu ya bure kwa raia wake wote bila masharti yoyote. Kama ni lazima wachangie basi mchango huo usizidi asilimia 33 ya pato la mwananchi wa kawaida la mwaka, ambapo kila mwanafunzi atatakiwa alipie siyo zaidi ya laki mbili kwa mwaka. Kujifanya kuwa tuna economic base ya nguvu kama mataifa mengine kiasi kuwa mwanafunzi anaweza kuuza chips pale McDonald na kupata hela ya kununua gari na kulipia gharama zote za elimu na gharama nyingine za maisha ni kujidanganya kabisa. Wanaodai kuwa wanafunzi wale wawe pia wanafanya kazi za mitaani kuweza kujilipia kama ilivyo Marekani na nchi nyingine kweli hamuwatakii mema kabisa; hakuna kazi ya mitaani hapo Dar ambayo mwanafunzi anaweza kuifanya na kuweza kulipia gharama za masomo ya chuo kikuu.

Kuna watu wanaosema kuwa tabia ya wanafunzi kugoma ni ya kizamani. Wanaodai hivyo kweli hawafanyii mema vijana hawa walifukuzwa shule. Ni kama mimi nilipokuwa mdogo ambapo wanafunzi wa chuo walifukuzwa sikumbuki kwa kosa gani. Wakati ule shule zote za msingi pale Tabora tukaandamana eti kumpongeza Rais kwa kufunga chuo kile; nadhani wakati huo Kikwete alikuwa bado ansoma pale. Hatukua tunajua lolote wakati huo. Baadaye miaka ya themanini wakati nikiwa nasoma pale pale Mlimani nikajikuta mimi mwenyewe ni mmoja wa waendesha “kunji” lile. Bahati nzuri sisi tulisikilizwa na wala hakuna aliyefukuzwa shule wakati ule, ila miaka kama minne baadaye nikiwa nafundisha pale nikaona chuo kinafungwa mwaka mzima wakati wafanyakazi wote ikiwa ni pamoja na wapishi tuliendelea na kazi kama kawaida na kupata mishahara yetu. Nikitafakari yote yaliyotokea wakati ule nikajua kabisa kuwa huo ulikuwa ni upumbavu sana kwa upande wa serikali.

Kwa jumla tabia ya serikali kutumia mtindo wa kufukuza na wanogoma ni ya kizamani sana iliyopitwa na wakati. Migomo na maandamo ni njia za kidemokrasi kabisa zinazoweza kutumiwa na walalamikaji ili serikali au waajili wao waweze kusikiliza kilio chao ili mradi yote ifanyike kwa msingi wa sheria. Migomo inafanyika sana nchi za magharibi ambako wana soko huria tunalojifunza kutekeleza. Utakuta kuna migomo ya mapailoti, migomo ya wandesha mabasi na kadhalika ana huwa wanafikia miafaka na wanaogomewa. Inakuwaje serikali haina muda wa kufanya hivyo? Walianza na madakitari pale Muhimbili, leo hii ni kwa wanafunzi wa chuo kikuu, je baadye mwisho wake itakuwa ni nini?
 
sasa hawa wanafunzi wameambiwa mambo yao yanashughulikiwa, tena ni maombi wamepeleka na muda wa kupokea hizo pesa bado, baada ya kufatilia pole pole bila ya ghamiza kama wafanyavyo,

hivi kweli kwa mtaji huu wa kulazimisha na kupeleka masindikizo ndio isaidie nini?

mie nnaona sisi wanafunzi wa siku hizi tunashindwa kufata nyakati.

mie kuhusu kuchangia 40% nnaamini kwa raia wa kawaida wa tanzania hazimudu, na hilo walishalisema na ndio linalofanyiwa kazi sasa hiki kiherehere cha nini?

halafu na hawa wanasiasa wabongo bab kubwa yaani ndio tiketi ya kutokea waa waaa bwana mrema sema usikike. pamoja na wenzio.

ila nnaunga mkono serikali kutoendeshwa kwa masindikizo, ifate utaratibu unaoeleweka ukisema elimu muhimu kwa hiyo pesa zote tupeleke kwenye elimu, hapa hapajaangaliwa

wako wataokuja kusema afya muhimu pesa zote zipelekwe mahospitalini .

wengine watakuja kusema ulinzi muhimu majambawazi wamekuwa wengi, pesa zote zipelekwe jeshini na polisini.

itakuwa kazi maana kila moja kina umuhimu wake na kote humo wanahitaji pesa hizo hizo.

wajameni tuangalie kwa macho mawili hili suala, na tujitahidini kutafakari na kuisaidia serikali kufikia maamuzi ambayo yatawasaidia wanetu waweze kupata elimu bora.

maana hii elimu pekee ina ngazi nyingi toka msingi hadi chuoni na kote kunahitaji pesa.

nnaitakia serikali kila la heri katika kutafuta ufumbuzi wa suala hili, pia nnawataka wanafunzi wajirudi warejee chuoni kupiga kitabu kisha kufatilia kiustaarabu tena kwa hoja maombi(sio maamuru) yao kwa serikali, kwani wenye kustahiki hizo pesa sio peke yao
 
Kichuguu

Nakubaliana na wewe, serikali iiogope migomo, kwani kwa style hii, iko mingi inakuja, mfano karaa ya usafiri wa daladala wadanganyika wamechoka, kusubiri mabasi yaendayo kasi mpaka 2009, siku ya siku akitokea mtu kama mtikala akaongoza maandamano patakuwa hapatoshi, kwani wanafunzi wanalia, wafanyakazi ndio usiseme,walemavu na wagonjwa wanalia pia.
 
sasa hawa wanafunzi wameambiwa mambo yao yanashughulikiwa, tena ni maombi wamepeleka na muda wa kupokea hizo pesa bado, baada ya kufatilia pole pole bila ya ghamiza kama wafanyavyo,

hivi kweli kwa mtaji huu wa kulazimisha na kupeleka masindikizo ndio isaidie nini?

mie nnaona sisi wanafunzi wa siku hizi tunashindwa kufata nyakati.

mie kuhusu kuchangia 40% nnaamini kwa raia wa kawaida wa tanzania hazimudu, na hilo walishalisema na ndio linalofanyiwa kazi sasa hiki kiherehere cha nini?
Unajua mnapowalaumu hawa wanafunzi hamuwatendi haki labda kwa kutoelewa mazingira ya Tanzania au kutoelewa viongozi wa serikali yetu wanafanyaje kazi.Katika kipindi cha mwaka mmoja unamzungusha mwanafunzi ktk swala la mikopo wakati wanaanza chuo waliambiwa watakopeshwa 100%,wamefikia katikati unawaambia mtachangia 40%,Bila hata kuwashirikisha hivi hii 40% kwenye gharama ya millioni tano ni milioni mbili inahitajika hivi kwa mzazi wa kawaida atapata wapi hizo millioni ili mwanae ambaye amemsomesha ktk mazingira duni na kufika hapo alipofikia ahakikishe anaendelea na masomo.Wakati hawakuliafiki hili unawaita diamond Jubilee na kuwaeleza nitalishughulikia swala lenu na katika kipindi cha miezi mitatu nitakuwa nimekwisha lishughulikia miezi mitatu imepita umefika wakati wa kufanya mitihani na kwenda field unawaambia itabidi wajilipie 40% ktk posho ya kila siku ya kumuwezesha kuwa field sasa hapa umetimiza ahadi yako ya miezi mitatu kulimaliza tatizo au umeongeza tatizo kwani kwa kanuni za chuo kama hukuenda field na kumaliza kwa ufanisi hutahitimu,Sasa ni nani wa kulaumiwa viongozi wetu wanaotoa ahadi za matumaini wakati hawatekelezi au wanafunzi ambao wamesubiri hadi muda ukapita walioahidiwa na kuletewa kasheshe jingine?Serikali inabidi ibadilike sio kutafuta mchawi na inabidi itekeleze majukumu yake na hili la kusomesha wananchi wake ni moja wapo, hasa kwa wale ambao hawana uwezo ambao ndiyo wengi.
 
hawa wanafunzi kudai wakopeshwe 100% hatulilalamikii, maana ni haki yao kudai na kulalama, na nnaomba wapewe. ila huu usulubu mie ndio nnaopingana nao.

sisi watu wazima tumeambiwa hata 40% pacenti hatupewi, kwani sisi si watanzania? jee hatulalamiki? tunalalamika.

mkuu wa chuo aliwaambia warejee madarasani na kunasihiwa kuwa mambo yao yanashughulikiwa, ikiwa mkuu wa chuo anasema hivyo una wasi wasi wa nini kuhusu field? si yakiwa hayajawa mnarudi kwake na kumwambia tumefata nasaha zako mlezi wetu na ndio mambo hayajawa, na wazee wetu hawana uwezo halafu tuangalie nini kitatokea kwa nini tuharakishe mambo?

halafu baya zaidi kuzarau kauli za walimu wao, za serikali na kujitia undava pahala pasipostahiki.

wangesubiri, mie hata ule mkutano pia walifanya vizuri just kupressurelize lkn kuzidi ule mstari hawa watoto hawajipendi.

ushauri wanafunzi wakuwe na mazingira, hawa ndio viongozi wa kesho, na hawa viongozi waliokuwepo leo walikuwa wanafunzi wa jana na wengine walishagoma kama wao na wanajua machungu yake.

nnashauri wanafunzi waombe kurejea chuoni na kutubu kwa utovu wa nidhamu, pia serikali iliangalie hili suala kwa umakini.

serikali kabla ya kuandaa sera au kukopia huko kwa wenzetu tuangalie na mazingira yetu.

mshahara anaolipwa mtanzania kwa sasa jee unaweza kuchangia 40%, jee mtu akiwa na watoto watatu fanya mmoja yuko chuoni na wengine wako sekondari na chukulia ni mtu wa kipato cha laki tatu(ambacho hadi sasa ni watanzania wachache wanamiliki) vipi ataweza kuwasomesha watoto hao na kuweza kulipia 40% na kulipia gharama nyengine ambazo nazo zinapanda kama umeme, maji na mengineyo, nimesikia tungule moja (wenzetu mnaita nyanya) ni sh 100. hapa waandaa sera jitahidini kuja na mchanganuo ambao utawasaidia watanzania na kuweza kufanikisha suala hjili la elimu.
]
imani yangu kuu serikali itatumia busara zake kuhakikisha inalinda eshima ya taifa letu na wananchi wake.

pia kwa vile tunajiandaa na ushindani wa soko huria tunahitaji kuandaa mazingira mazuri ya kielimu, nnakiri kuubeba mzigo huu wote serikali ni kazi ila ijaribu kuandaa mazingira na ufafanuzi ambao utawakinaisha watanzania wengi.

nnaomba kuwasilisha
 
Mtumwitu,
Naomba unielimishe kidogo juu ya vile tunavyojiandaa na ushindani wa soko huria. Tumefanya matayarisho gani?
 
Nakumbuka wakati wanatetea faida za Mlimani City Project tuliambiwa kuwa mradi huo utaajiri pia wanafunzi wa UDSM kama part-timers...sijui kama hilo limeanza kufanyika.
 
Kinachoendelea Chuo Kikuu ni kushindwa kwa viongozi wa Wizara kubuni na kutekeleza mikakati ya uhakika ambayo inaweza kuondoa tatizo hilo mara moja. Kuendelea kuongoza kwa vikao na kamati hatutafika. Waziri awaambie wananchi kuwa walipoamua wanafunzi wachangie asilimia 40 walijua wazazi na wananchi wana uwezo huo. Watuambie walijuaje na kwa kutumia vigezo gani? Wale ambao tunanunua vitu mitumbani tunajua jinsi bei ya vitu inavyobadilika kwa kadiri "mtu anavyoonekana" mwenye uwezo. Shati moja mtu mmoja anaweza kuanza kuuziwa kwa shilingi 5000 wakati akija mtu mwingine shati hilo hilo laweza kuuzwa shilingi 3000. Yule mwenye uwezo wa shilingi 5000 anaweza hata asilalamike, atalipa na kuishia zake. Yule mwenye uwezo wa shilingi 3000 atalalama kwanza hadi muuza mtumba atashusha bedi hadi 2700!!

Sasa, wanafunzi wa vyuo vyote vitano ambao wamerudishwa nyumbani familia zao zina uwezo wa kulipia asilimia 40? Serikali iseme wanao!!
 
Viongozi wenyewe ndo hao kina waziri wa Ulinzi walosema ati wanafunzi walogoma hawakwenda jeshi la kujenga taifa, as if that explains everything!
 
Mimi bado nasisitiza serikali ianzishe database itakayoiwezesha kujua uwezo wa kila mwanafunzi wa nchi hii aliyepo shule ya msingi na sekondari. Na hii itawezekana kwa kufungua ofisi kila wilaya itakayoshughulika na kukusanya taarifa muhimu za kumhusu kila mwanafunzi na kuzipeleka kwenye bodi ya mikopo. Kwa hiyo inapofika wakati mwanafunzi anachaguliwa kujiunga na chuo chochote na anahitaji mkopo itakuwa rahisi kujua anahitajika akopeshwe kiasi gani kwani taarifa zote zitakuwa zipo tayari bodi ya mikopo badala ya kuweka asilimia 40% bila kujua uwezo wa kila mwanafunzi.
 
The buck stops with JK. Kwa nini imekuwa tabu kuongeza kodi kwa makampuni yote ya madini kwa asilimia 2 across the board ili itumike kuwasomesha WTZ hasa kwenye vyuo vyetu vikuu. Ni maendeleo gani na maisha bora ambayo wanayapigia kelele wakati wanashindwa kufanya uamuzi mdogo kama huu. JK wakati unasoma hukulipa hata senti moja - Kulikoni leo umesahau?

Inatia aibu kuona serikali iliyochaguliwa na wananchi ina suasua kwa suala muhimi kama hili. Je kama tunashindwa kuwahudumia wanafunzi hivi sasa ni lini tutakuwa na uwezo huo. Serikali inabidi ifanye uamuzi tena haraka sana kufuta malipo au karo kwa vyuo vyetu vikuu na kugharimia kwa kuongeza kodi, kama hamuwezi kuwakaba hawa wawekezaji basi iongezwe kwenye kodi ya kila mlipaji kodi ili vijana waende shule ambao tunawategemea kuikwamua TZ kwenye ulofa na umasikini.
 
joo wane.. wakianzisha ofisi ya namna hiyo nafikiri utakuwa mwanzo wa Taifa la Kidikteta!!
 
Hapa bongo ni vurugu mechi tu,serikali na wananchi tumeshachanganyikiwa hakuna wa kumshika mkono mwenzake kila mtu anaangalia ugali wake.maisha yametuchapa kiasi kwamba unapozungumzia maswala ya kijamii inakuwa kama mchezo wa kuigiza.
Tunaitaji mabadiliko ya makubwa ktk sekta zote ili kurudisha heshima ya mtanzania.
tufanyenini ili tuweze kufikia malengo ?kwa sasa hatuna wabunge wa kutuwakilisha zaidi ya matumbo yao.
 
; hakuna kazi ya mitaani hapo Dar ambayo mwanafunzi anaweza kuifanya na kuweza kulipia gharama za masomo ya chuo kikuu.

Are you sure??

Inawezekana mimi sina data kamaili; hebu Mzee Mikuki tupe data kuhusu gharama za masomo ya chuo kikuu na ujira wa kawaida wa part time mtaani hasa ukizingatia kuwa vijana hawa ndio wametokea form 6 hawana experience ya kazi yoyote.

Baada ya hapo, wanafunzi wakishaanza kufanya part time kulipia masomo yao, itabidi chuo pia kifanye mabadiliko makubwa katika mitaala yake na kuondoa kile kitu kinachoitwa "DISCO." Kwa vyuo vingi vya Marekani hakuna kabisa kitu hicho na mtu anaweza kuendelea kuwapo shuleni kwa muda mrefu sana.
 
Hapa bongo ni vurugu mechi tu,serikali na wananchi tumeshachanganyikiwa hakuna wa kumshika mkono mwenzake kila mtu anaangalia ugali wake.maisha yametuchapa kiasi kwamba unapozungumzia maswala ya kijamii inakuwa kama mchezo wa kuigiza.
Tunaitaji mabadiliko ya makubwa ktk sekta zote ili kurudisha heshima ya mtanzania.
tufanyenini ili tuweze kufikia malengo ?kwa sasa hatuna wabunge wa kutuwakilisha zaidi ya matumbo yao.

Maneo yako yanatia uchungu sana; majibu yapo mengi tu.

- Tunahitaji elimu zaidi kwa raia wetu.
- Tujenge utamaduni wa kupiga vita vitendo vya unyanyasji kwa raia kutoka kwa viongozi.
- Vile vile tuwajenge raia wetu kutambua kuwa viongozi wapo pale kuwatumikia raia na hivyo kuwapa nguvu ya kuwahoji viongozi bila kuwaogopa.

- Turudishe miiko ya uongozi ilyotajwa katika Azimio la Arusha

- Tuandike KATIBA MPYA inayopunguza madaraka ya viongozi kwani madaraka hayo ndiyo yanayowafanya wajione miungu watu.
 
The buck stops with JK. Kwa nini imekuwa tabu kuongeza kodi kwa makampuni yote ya madini kwa asilimia 2 across the board ili itumike kuwasomesha WTZ hasa kwenye vyuo vyetu vikuu. Ni maendeleo gani na maisha bora ambayo wanayapigia kelele wakati wanashindwa kufanya uamuzi mdogo kama huu. JK wakati unasoma hukulipa hata senti moja - Kulikoni leo umesahau?

Inatia aibu kuona serikali iliyochaguliwa na wananchi ina suasua kwa suala muhimi kama hili. Je kama tunashindwa kuwahudumia wanafunzi hivi sasa ni lini tutakuwa na uwezo huo. Serikali inabidi ifanye uamuzi tena haraka sana kufuta malipo au karo kwa vyuo vyetu vikuu na kugharimia kwa kuongeza kodi, kama hamuwezi kuwakaba hawa wawekezaji basi iongezwe kwenye kodi ya kila mlipaji kodi ili vijana waende shule ambao tunawategemea kuikwamua TZ kwenye ulofa na umasikini.


Wewe umesema:

Tulileta wawekezaji na wengine tukawapa makampuni yetu "bure" kusudi watusaidie kujenga uchumi wetu kwa kutoa ajira kwa watu wetu na kuongeza pato la serikali kwa kulipa kodi. Mojawapo ya matumizi ya kodi hiyo ni kwenye swala nyeti kama hili la elimu.

Tuone aibu ya kuomba wataalam kutoka Norway kwa kuwekeza kwenye watu wetu. Miaka 46 ya uhuru bado tunashindwa kusomesha watu wetu?
 
Back
Top Bottom