Augustine Moshi
JF-Expert Member
- Apr 22, 2006
- 2,556
- 1,393
Mzee ES anasema wanafunzi kwenye vyuo vya serikali hawaruhusiwi kugoma. Hakuna kitu kama kuruhusiwa kugoma. By definition, kugoma ni kitu kinafanywa bila ruhusa. Kikipata tu ruhusa kinaacha kuwa mgomo.
Kugoma, kufanya vurugu, au kususia masomo, ni njia ya kawaida ya wanafunzi dunia nzima, ya kutaka haki itendeke. Binafsi, nilikuwa kwenye mgomo nikiwa mwaka wa pili UDSM, na nikawa kwenye makundi ya wanafunzi yaliyofanya vurugu kubwa kwenye vyuo vikuu Canada kudai disinvestment from the then Apertheid Regime in SA.
Waalimu wa vyuo vikuu Kenya waligoma siku za karibuni, na hata waalimu wa UDSM wangegoma kama serikali haingeboresha mishahara yao.
Wanafunzi wa UDSM walikuwa na haki ya kugoma kudai serikali iwape support 100% Wengi wao wanatoka kwenye familia masikini ambazo haziwezi kulipa malaki ambayo JK anataka walipe. Ni sawa wanavyogoma wote. Huyo anayesema ilibidi wale wasio na uwezo tu ndio wagome hajui asemalo. Nguvu ya mgomo inatokana na umoja.
Tatizo sio kukosekana fedha, ni fedha kutumika vibaya. Hatutaki elimu a vyuo vikuu iwe ni kwa ajili ya watoto wa matajiri tu.
Watu walioko kwenye disciplined forces peke yao ndio hawana haki kugoma. Wengine wote tuna hiyo haki. Mara nyingi, ndiyo namna pekee ya kuwashinikiza wakubwa.