Just in: UDSM wafukuzwa

Sasa mimi nitasema nini ? Maana tulisikia maneno meengi hapa mara Muungwana anatisha nk ndiyo maana walivaa magwanda ya hamas na Hezbollah , mara CCM ina chapa kazi , Mara kitengo cha CCM kimefunguliwa na CCM kusemwa kuwa ndiyo jibu pekee .Leo nitasema nini ? Poleni sana watoto wa wadanganyika .

Yaani Tanzania kila kitu cha maendeleo lazima kuna maamuzi ya ki CCM .Nasema Serikali inaweza kulipa 100% na kwa kuwa ni mkopo ni sawa mbona Malima katumia 100m mwenyewe ? Mbona ikulu imetumia kibao kwa kuzunguka kwa jina la kujitambulisha na kuomba omba ?
 
Huoni ajabu VC na wakubwa wa UD wana MAVX ya Millions wakati wanafunzi wanaowafundisha hawana vitabu? Nenda Library uone! So hilo liache.. Mgomo hauwezi kuleta suluhu!! Niligoma nikaona!!

By the way legally, mkopo si haki!! Its a privelege, not a right! (kwa TZ atleast). HAKUNA SHERIA TZ INAYOSEMA KWAMBA KILA MWANAFUNZI WA JUU APEWE MKOPO WA 100%!! Kama ingekuwepo Iam sure vijana wangeenda kudai chao mahakamani! waende wakadeal na Bodi ya Mikopo katika vyombo vya mahakama. Iam sure wangetokea vijana couregious wakaeenda Mahakamani kuomba constitutional interpretation ya hii haki ya kupata elimu, Iam sure wangekuwa na basis na wangeaatract support ya walio wengi. Ofcourse katiba imequalify hii haki ya elimu, kwamba haiko enforceable mahakamani (under directive principles of state policy, Chapter II)..Ila kama kweli tunataka kusolve hili tatizo for once and for all..vijana watafute opinion ya kisheria!!!! Iam sure there good lawyers wa Legal Aid who can take up the case! Mtikila sio mjinga..he has succeeded and failed where our elites cant dare! Hebu jaribu kumuuliza mwanafunzi wa mlimani..kwa nini anagoma? atakwambia anataka mkopo wa 100% kwa sababu ni haki yake kama mtanzania! Ukimuuliza hiyo haki iko wapi...the best atakwambia ni kwamba hata JK na mawaziri walisoma bure! Period!

Kwenda mahakamani seems an idea in air kwa walio wengi, lakini I can assure you, kama wasomi lazima tujifunze vipi haki inapatikana. sio kuandamana tuu barabarani! .... Lakini kwa sasa hivi, knowing our media frenzy..these students are considered villains wanaotaka kujinufaisha wakati wananchi hata elimu ya msingi wala aspirin hawana! Iam sure tukijenga culture ya kusolve matatizo kwa kufuata procedures..TUTACHELEWA, ILA TUTAFIKA! what the govt is doing is being smarter than students...maana wanajua they are just lumpens making noise..have no legal basis!!

Mtikila has shown us the way and Iam sure its high time wasomi wetu wafuate nyayo.... Na tukumbuke UD siku hizi sio "favourite son" tena kuna vyuo kibao vinavyoomba hiyo pesa..zamani ulikuwa ukisema UD, kila mtu anashtuka...eee bwana rules of the game have changed! Wanafunzi wanalijua hilo? Sijui!
 
Wanabodi Tunawaonea Saana Huruma Vijana Wetu ,lakini Kama Mnakumbuka Mwezi Wa Pili Mwaka Huu Hapa Ubaoni Tumeandika Sana Usiku Na Mchana Kwenye Ile Mada" Wanafunzi Ud Waoga?" Wengi Humu Waliwatetea Sana Tu ,lakini Kilichotokea Mnamo Asubuhi Tar 5/2 Nilipata Taarifa Na Nikaipost Humu Ya Ccm Kupeleka Mabasi Ya Scandinavian Kuwachukua Vijana Wakasheherekee Na Muungwana Sherehe Za Miaka 30 Ya Ccm Pale Diamond Hii Iliambatana Na Kuwagawia Fulana Na Kofia Na Wako Pia Walioambulia Vijinauli[tano Tano]....hadi Hapo Tutawasamehe Vijana Maana Labda Nao Walitaka Kumfanyia Usanii Jk [usanii Katika Jumba La Sanaa??

Tukirudi Kwenye Huu Mgomo Wanafunzi Wana Haki Maana Walipokutana Na Jk Na Kumuimbia Ule Wimbo Maarufu "kama Sioo Juhudi Zako Nyerere ...na Kikwete Angesoma Wapi!!!!!!!!!!!! Mkumbuke Palepale Jk Aliunda Task Force Ya Kutatua Matatizo Ya Vijana Na Waliondoka Na Matumaini Makubwa...

Pia Tufahamu Kuwa Hakuna Mtoto Asiyejua Uwezo Wa Baba Yake ....mara Nyingi Mtoto Hata Mdogo Hulilia Kitu Ambacho Anajua Baba Yake Anamudu..mtoto Wa Uswahilini Tunakoishi Asubuhi Atalilia Kitumbua ....hawezi Kudai Cornlex Au Lasagne...tofauti Na Wa Oybay Ambaye Anaweza Kulilia Computer Game Ya Dola 1000 Na Akapata ...sasa Vijana Ndio Wanajua Taifa Letu Masikini Hatahivyo Macho Wanayo Pale Serikali Inaposema Haina Fedha Wanaona Makusanyo Ya Kodi Yakifikia Bilioni 250 Kwa Mwezi,wanaona Mauzo Ya Dhahabu Yakipanda,wanaona Jinsi Gesi Ya Songo Inavyookoa Hadi Dola Milioni 500 Ambazo Zingeagiza Mafuta Ya Kutumika Viwandani[dar Tayari Viwanda Vikubwa Vinatumia Hii Gesi],wanaona Namna Serikali Ilivyotumia Trillion 1.2 Mwaka Huu Nje Ya Bajeti,wanaona Jinsi Rais Anavyoweza Kutumia Dola 500,000 Kutumbua Kwenye Hoteli Kubwa Katika Mapumziko Mafupi Ambayo Nyerere Angeyatumia Kulima Butiama....wanaona Hawa Vijana ,wameona Mchanganuo Wa Kuileta Real Madrid Ukifikia Billioni 7.....wameona Vikao Vya Waziri Mkuu Vya Dharura Vikitumia 160 Millioni Posho Tu...wameona Juzi Tena Kikao Cha Rais Kujadili Nakisi Kikitumia Mamilioni Kama Hayo.....ndio Maana Wameomba Waongezewe Shilingi 2,400 Ili Ziwe 6,000 Kwa Siku Wakiamini Kwa Uwezo Wa Baba Yao Na Umasikini Wake Ataweza Kuwapa...je Mnaziona Nyigi????
 
Hili jambo hakika you have to be a bit sceptic kuangalia namna ya kuchangia humu.

WANAFUNZI:

Ni kweli beyond doubt kwamba 3500 kwa tanzania haitoshelezi mahitaji ya mwanafunzi lakini how do you go about claiming the money?

Walimuomba rais 'kichama' akaahidi kufuatilia, hatukisikia chochote in between [labda kilikuwepo lakini mimi sikusikia] ghafla vroom wanafunzi haooo wanatangaza mgomo!

1.Katika hali ya kawaida mkuu wa nchi akiwaahidi kuufatilia,basi inabidi kuwe na ufuatiliaji fulani kwa waahidiwa, kuandika barua,kwenda kuonana na wasaidizi wa rais 'fizikali' nk

2. Ikishindikana vijana wetu wangeweza kuandika barua ya wazi kumkumbusha rais hadharani kuwa ile ahadi vipi,hii ingeamsha kama sio kuzindua ahadi ambayo pengine imesahaulika.

3.Mkishindwa hivyo ndio kuresort katika mgomo,katika nchi zilizostaarabika mnaambiwa siku fulani tutagoma hivyo inakuwa Serikali inakwenda spidi kufikia compromise ilikuserve face...wasomi wetu wamekwenda na kutaka majibu kwa mtindo wa papo hapo!


SERIKALI

Serikali yetu imeshaonesha mara kadhaa kutopendezewa na njia ya mgomo kama mojawapo ya shinikizo ifanye jambo fulani. Rais hakuahidi kuongeza hizi hela [kama wengine humu wanavyodai] bali aliahidi kufuatilia.

Hii inakuja wakati serikali ikijiandaa kwa bajeti mwezi julai,hivi hawa jamaa walitegemea wajibiwe nini kwa mgomo? Katika kipindi hiki cha mwaka?

What to DO:

1Viongozi wa wanafunzi 'waungame' na kuomba wenzao warudishwe shuleni.

2. wafanye jitihada za kunegotiate compromise settlement na serikali. Wawe tayari hata kupokea deferred offer au a bit extra in anticipation for more....
 
Unaushangaza sana Umma

Yaani zipatikane pesa za kisiasa za kuwapa watu kila mkoa 1bn za kusomesha wanafunzi na tena wengi ni watoto wa walala hoi hazipatikani hadi bajeti ipite ? JK hakusema ataongeza ila kufuatilia Chama kina pesa ? Walifanay mistake kuweka issue ile kwenye Chama na kuvaa majoho yale .
 
Anyway huu ni upuuzi na ubinafsi wa mijitu iliyoko madarakani ikishirikiana na makafiri WB na IMF

someni maelezo ya Mzee Kyoma ktk mada ya "tunamkumbuka Sokoine" halafu utaelewa nini Serikali yetu inatufanyia. Prof Mukandara kaamua kujidhihirisha kuwa ni agent mzuri wa kutimiza malengo ya walafi/wala rushwa wanaoshirikiana na WB + IMF

Katika Elimu ndiko Serikali yetu inatakiwa iweke mkazo mkubwa na isi-entertain mambo ya kipuuzi kama haya kutokea, kwa walio soma bongo nakumbuka sana ni jinsi gani hii migomo ilivyoathiri watu na bajeti zisizo na mpango.

Halafu huyu Prof Mukandara ni mpuuzi sana tu, leo unakuja eti na watu walipe TShs 100,000.00 iliurudi darasani hivi anafikiri kwa walalahoi hiyo pesa itatika wapi. WHY kumuadhibu Baba na Mama yangu Mkulima kule kijijini anayekopwa mazao yao kila kukicha kwa ajili ya kuwatetea Walafi/Wabinafsi/Wala Rushwa ya wanaotuingiza mikataba ya hovyo hovyo wakishirikiana na WB + IMF?? WHY??
 
Nimepitia takwimu za wanafunzi wa mwaka wa Vyuo vyote vikuu vya umma (public universities) kwa mwaka 04/05 (ndio takwimu nilizoanzia nazo). Mhula huo kulikuwa na jumla ya wanafunzi wapatao 10718. Tukifikiria kuwa kuna ongezeko la kati ya asilimi 3 na 5 kwa miaka miwili inayofuata basi idadi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza haizidi 12,000. Hata tukijaribu ongezeko la asilimia 10 bado wanafunzi wa mwaka wa kwanza hawazidi 15,000.


Je inawezekana kutengeneza bajeti inayoweza kuwahudumia wanafunzi hawa kwa mwaka mzima na kuwaacha wasome badala ya kuwa na wasiwasi wa kulala na kula wapi?
 
nilijawa simanzi sana jana kwenye taarifa ya habari kumwona prof Rwekaza Mkandara akiongea kwa jazba kuwa sasa itamlazimu yule atayetaka arudi chuoni aje na 40% cash au aonyeshe risiti kuwa ameshalifa la sivyo hatapokelewa. Du amesound kama mwanajeshi vile???amedhihirishia umma jinsi anavyojitenga wa wazawa, ni kama vile hakuzaliwa TZ au hana ndugu au watoto wanaohotaji elimu. To me amesound kama Mramba alivyolazimisha ndege ya raisi inunuliwe kwa kusema "watanzania watakula hata nyasi ili mradi ndege ya raisi inunuliwe"
poor students hawakujua kuwa serikali yao ya CCM walioivalia jezi ingewageuka kiasi hicho???

pili Mkandara akadai kuwa chuo kinaendeshwa kwa milion 100 kila siku kulipa wafanyakazi, kuendesha mitambo n.k sasa hawa wanafunzi watakitia gharama chuo maana lazima tuendelee kutumia hizi mil.100 kulipa wafanyakazi,umeme n.k. Kwa kweli sikuona Logic ya kufunga chuo kama gharama bado zitaendelea kulipwa na wanafunzi hamna???

serikali hapa ina mtihani mgumu tena sana na kwa mtindo huu hatujengi wasomi na hatuwezi kucompete hata east africa.

mkjj
wanafunzi waliopo kwenye vyuo vya umma ni wachache sana serikali bado haijashindwa kuwapa mkopo ( leave alone kuwalipia) 100% kama kuna mipango bora na vipaumbele. ndio maana kuna thread huko nyuma mwana bodi anataka ajue malengo/dira ya taifa ni nini.
Hivi bila elimu bora walau degree tutapata hao watangfeneza mikataba au tutaomba norway kila leo???
kwa mtindo huu serikali inatoa mianya kwa elimu feki watu wajitafutie degree feki ( kama kina fulani huko bungeni ) basi life goes on.
Nionavyo mimi Tanzania baada ya miaka 20 ( kama staili za uongozi, mipango na indeshaji ni huu huu ) itakuwa nyuma kabla hata ya wakolini kuja hatutakuwa na chochote kilicho chetu kuanzia wasomi, rasilimali, waendesha mashirika/makampuni na zutabaka historia ( if at all anyone will bother to write ) kuwa hapo zamani enzi za nyerere kulikuwa na Tanzania watu walienda shule, viongozi waliwajibika, n.k, n.k
lah I feel bad to keep writing wacha nikome hapa.
 
Hivi kwanini hii migomo inajirudia rudia. Aidha kuna uongozi mbovu kwenye wizara husika, au tumeshindwa kuwashawishi wanafunzi kuwa suluhisho la kudumula matatizo yao linaweza kupatikana. Vinginevyo, basi Watanzania ni watu wa ajabu sana kiasi cha kushindwa kushughulikia suala la elimu ya juu. Vyovyote vile, Prof. Peter Msolla anaendelea kuthibitisha kauli yangu ya huko nyuma kuwa kaishindwa wizara na anawatia aibu wasomi wenzake! Kwanini asing'atuke? I've got an interesting proposal to end this cycle of demonstrations and student ejections!

http://mwanakijiji.podomatic.com
 
Kufungwa kwa chuo kikuu, ni ishara nyingine inayotuonyesha ni jinsi gani serikali yetu ilivyodhaifu, kwa kutumia nguvu nyingi kwa wanyonge na kuwakumbatia wenye mali.

Mahojiano ya Prof Mkandara, wakati akiongea na waandishi wa habari inadhiirisha yao.

-Prof Mkandara alikiri kuwa kuondesha chuo kwa siku inagharimu kiasi cha Tzs 100 million.

-Amezungumzia pia misaada inayotolewa na wafadhili wa nje kuendesha chuo inatokana na stability ya chuo, kama chuo kitafungwa kila mara kuna hatari ya kuwapoteza hawa fadhili.

-Elimu ni biashara, amekiri pia kuna hatari ya kuwapoteza wanafunzi wanaotoka nchi za nje ambao wao huchangia kwa kiasi kikubwa, kwani wanalipa kwa fedha za kigeni.

Kwa kukubaliana na serikali kufunga chuo, prof mkandara ameonyesha udhaifu mkubwa, huyu si yule mkandara wa miaka ya 1998 nilipokuwa UD.

Prof mkandara, anatamka mbele ya waandishi wa habari, kuwa hakuna mwananfunzi atakayeruhusiwa kurejea chuo, ila kwa kuja na cash au bank deposit slip ya 40%, hii ni dhihaka ya mwaka.

Kwanini wauza madawa ya kulevya, walarushwa, na wakwepa kodi anakumbatiwa ili hali nguvu nyingi inatumika kuwakandamiza wanyonge wasio na sauti.

heshima itakuja pale damu itakapo mwagika.
 
Nimefuatilia kwa makini hili sakata nikisubiri mtu mmoja mwenye akili huko serikalini atoe tamko lenye hekima hasa wakati huu wanaposhinikiza kuingia katika shirikisho la Afrika Mashariki, nikidhani wataona umuhimu wa elimu kwa kizazi hiki kinacholazimika kuingia kwenye ushindani na soko la ajira; nikitegemea Jeikei atakumbuka kauli yake kuwa 'hatuna wataalam' hivyo ajenge mazingira ya kupata hao 'wataalam'....Ninachoshuhudia kinanifanya niamini kuwa serikali ya Jeikei ni ya wasanii watupu, sifa yao nyingine ni ujangili usio na huruma..watu waliotumia milioni 100 kwenye kesi ya Mengi vs Malima, watu wanaotumia fedha za wazazi wetu kule kijijini kujadili ujinga bungeni na wengi wao kuuchapa usingizi bila haya leo wanawarudisha wanetu vijijini wakalete asilimia 40%; itatoka wapi? Hivi Mfanya kazi wa serikali anayelipwa shs 96,000 kwa mwezi , ambaye mwanae kabahatika kwenda chuo kikuuu na bado anao watoto wengine, analipa pango la nyumba, analipa umeme huu ambao bei yake haishikiki, analipa maji, analipa daladala asubuhi na jioni..laki moja ni mchezo? Ndio maana huko nyuma tuliwahi kusema kuwa kwa mazingira yaliyopo kila atakaepata uongozi ataiba tu, na hawa wanafunzi tunaowaharass hivi kesho wakipata cheo wataiba tu kulipiza kisasi.

Nasubiri na hao wa Sokoine waliogoma nao wafukuzwe (au nao tayari nini?)
Kweli hapa ni everybody for himself and God for us all!
 
Mkandara alipata U Vice baada ya kuwa mshikaji wa JK kwa siku nyingi na kudhihirisha kwamba yeye ni CCM wa damu kwa kupitia ile Redet. Niliyasema haya mwanzoni watu mkasema Lunyungu unaona mabaya tu kila mara lakini haya ndiyo nilikuwa naashiria . Kazi bado sana huko tuendako na wasomi ni kama Mkandara .
 
Ni jambo la kusikitisha kuona serikali inafunga chuo kikuu kutokana na mgomo. Mimi nafikiri serikali yetu haipo serious kwa sababu muda sio mrefu sana uliopita serikali ilifanya research kuhusu kwa nini wanafunzi wa vyuo wanagoma na solution nini. Je matokeo ya hiyo reseach yaligundua chanzo cha migomo nini? na solution yake nini? je ni sababu zilizoifanya serikali yetu tukufu isichapishe hayo matokeo hadharani ili kila mwananchi mzalendo wa nchi aijadili?. Naamini haya yakitimizwa suala la migomo vyuoni itakuwa historia isiyoweza kujirudia.

Kwa upande mwingine nafikiri madai ya wanafunzi ya kupewa mkopo asilimia 100% ni ya msingi kabisa. Kwa wanafunzi walio wengi wanatoka familia maskini sana na ukifuatilia sana utakuta hata "A" level wamemaliza kwa mbinde japo ada ni tshs 70,000.00 kwa mwaka. Wapo wengine hata nauli ya kuja Dar toka kijijini kujiunga na UD wazazi wameuza mashamba au wanakijiji wamemchangia nauli. Naamini serikali ingekuwa makini kwenye mikataba kama ya madini, iptl, richmond, n.k. ingeweza kabisa kuwapa wanafunzi wote mikopo bila kikwazo.

Ushauri wangu wa bure kwa serikali naiomba iitanue bodi ya mikopo iwe na ofisi kila wilaya (najua hili linawezekana). Ofisi hizo za wilaya ziwe na jukumu la kukusanya taarifa muhimu (uwezo wa wazazi, shule anayosoma, ada anayolipa kwa mwaka, mdhamini wake nani n.k) za kila mwanafunzi wilayani kisha zitumwe makao makuu. Hii ikifanyika baada ya mwaka mmoja itajulikana nani anastahili kukopeshwa na kwa kiasi gani na nani hastahili kukopeshwa.
 
Tatizo kubwa hapa ni kwamba serikali yetu haina sera iliyosimama kuhusu mikopo. Tangu Kikwete aingie madarakani wameshabadilisha taratibu za mikopo zaidi ya mara tatu. Kwanza, walianza wakasema kila mwanafunzi atapatiwa mkopo na serikali. Pili, wakasema wanafunzi waliopo vyuo binafsi hawatapewa mkopo. Tatu, Walipozomewa na kwa kupenda sifa, wakabadilisha tena ghafla kuwa serikali sasa itawapatia wanafunzi wote wa vyuo vya serikali na binafsi. Nne, wakaibuka na utaratibu mpya kuwa serikali itawapa mikopo wale tu waliopata division 1 (mme) na division II (ke). Tano, sasa limekuja na hili la wazazi kuchangia 40%.

Sasa kila siku nikisema tunaongozwa na serikali ambao ingekuwa ni dereva hajui tunakwenda wapi. Dereva kujua kuendesha gari tu haitoshi, inabidi ujue unapoenda na ujue njia pia. Serikali yetu inaongozwa na viongozi ambao shida yao ni kesho wawe kwenye kurasa za mbele za magazeti. Hawatabiriki. Sasa tujiulize hata kama ni wewe, wewe unajua utalipwa sh.6,000 kwa siku kwa ajili ya fieldwork, ghafla unaambiwa sasa utalipwa sh.3,500. Zingine na wewe uchangie! Ghafla bin vuu! Jamani!
 
Salaaaallleee

Jamani kuishi nyumbani wakati mwingine ni kama uko vitani wakati wote..!!!

Kuna watu huku tuliko wana nia ya kwenda ya kwenda kufundisha kwenye vyuo vyetu huko nyumbani lakini lakini mambo kama haya wala hayasaidii kuongeza confidence yao.

Mimi mwenzenu huwa naupenda sana ule msemo wa "KUSOMA na KUELIMIKA ni VITU 2 TOFAUTI" hao viongozi wetu wanaongoza sera za elimu tena wote ni Ma-Prof Msola na Mukandara wamesoma; lakini kuelimika baaadooooo sana.

Mungu awalinde vijana wasikate tamaa na kuamua kuwa majambazi.
 
Kufungwa kwa chuo kikuu, ni ishara nyingine inayotuonyesha ni jinsi gani serikali yetu ilivyodhaifu, kwa kutumia nguvu nyingi kwa wanyonge na kuwakumbatia wenye mali.

Mahojiano ya Prof Mkandara, wakati akiongea na waandishi wa habari inadhiirisha yao.

-Prof Mkandara alikiri kuwa kuondesha chuo kwa siku inagharimu kiasi cha Tzs 100 million.

-Amezungumzia pia misaada inayotolewa na wafadhili wa nje kuendesha chuo inatokana na stability ya chuo, kama chuo kitafungwa kila mara kuna hatari ya kuwapoteza hawa fadhili.

-Elimu ni biashara, amekiri pia kuna hatari ya kuwapoteza wanafunzi wanaotoka nchi za nje ambao wao huchangia kwa kiasi kikubwa, kwani wanalipa kwa fedha za kigeni.

Kwa kukubaliana na serikali kufunga chuo, prof mkandara ameonyesha udhaifu mkubwa, huyu si yule mkandara wa miaka ya 1998 nilipokuwa UD.

Prof mkandara, anatamka mbele ya waandishi wa habari, kuwa hakuna mwananfunzi atakayeruhusiwa kurejea chuo, ila kwa kuja na cash au bank deposit slip ya 40%, hii ni dhihaka ya mwaka.

Kwanini wauza madawa ya kulevya, walarushwa, na wakwepa kodi anakumbatiwa ili hali nguvu nyingi inatumika kuwakandamiza wanyonge wasio na sauti.

heshima itakuja pale damu itakapo mwagika.


Inauma jamani...hivi tumemkosea nini Mungu sisi mpaka anatupa viongozi wa namna hii...??
 
You are all wrong
Shida hapa kwa mawazo yangu mimi nadhani ni siasa kuwa mbele na Chama na kuacha maslahi ya watanzania , Tanzania na Taifa kwa ujumla. Maisha ya mwana siasa yana thamani zaidi kuliko maisha ya mtanzania leo hii . Ni hatari kubwa kuingiza Siasa kila mahala .
 
Kwa wanaojua mahesabu; ni ipi rahisi: vyuo kupata hasara kwa wanafunzi kufukuzwa, au serikali kupata hasara kwa wanafunzi kuchelewa kulipa 40% au kutolipa kabisa. Wakati tunafanya hayo mahesabu tujiulize, hizo hela za wafadhili alizozungumzia Pro-comfuser Mkandara, ni msaada, au mkopo? na kama ni mkopo, tunalipia riba wakati chuo hakina wanafunzi? na kama ni msaada, ni wa masharti gani..kiasi kwamba unakuwa si wa kuwasaidia wanafunzi kusoma bali kulipia mambo mengine...maana kama ni mishahara serikali ina uwezo wa kulipa; basi na huo 'msaada' usimamishwe maana chuo hakifanyi kazi ambayo kinatakiwa kuifanya(kufundisha wanachuo).
Hao wafanyakazi wanaendelea kufanya kazi na kulipwa for whose benefit while in the real sense chuo hakifanyi kazi? Kweli sasa naanza kuamini maneno ya Jeikei to the extent that hasara nyingine tunazipata kwa "kutokuwa na wataalam"
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom