Mnyika: Mambo mawili ya msingi kwa maoni yangu. Mosi, Mimi naamini mgomo ni hatua ya mwisho katika kudai haki ikimaanisha kuwa hatua za kawaida za majadiliano zimeshindikana. Unapofanya mgomo unakuwa umesha-exhaust silaha zingine zote na umebaki nayo hiyo tu ya mgomo. Sina uhakika kama vijana wetu walisha-exhaust njia zote za majadiliano. Zaidi ya yote sina uhakika kama hata uwezo wa kujadiliana wanao! Ndio maana nikatoa mfano wa Diamond Jubilee. Ni wazi vijana walipoteza nafasi muhimu walipokutana na rRais Kikwete. Badala ya kuimba ngonjera za kumsifia Kikwete na CCM yake, walipaswa kumwambia ukweli kuwa sera ya CCM ya elimu ya juu ni mbovu na wangempa alternatives. In short, we expected them to address broaders issues about our higher education policy than the mere mkopo.
Pili, naamini kuwa lengo la mgomo kwa hali ya wanafunzi ni kutafuta huruma ya wananchi. Hakuna maana kama mtagoma au kuandama mkaishia kuzomewa na wananchi. Sasa, ili upate huruma ya wananchi katika mazingira ya Tanzania ambayo wananchi wengi wamelishwa limbwata la CCM na Kikwete, lazima kujipanga vizuri. Kwa maoni yangu kwa mgomo huu serikali itashinda na wanafunzi wataishia kuzomewa. Sio kwamba madai yao hayana msingi, yana msingi sana. Mimi nikisoma pale mlimani niliamini na ninaendelea kuamini hata sasa kuwa ili madai yenu yapate nguvu, lazima myape sura ya kiwananchi. Yaani muoneshe kwamba mnaandamana kwa kuguswa na jambo fulani la kijamii. Kwa mfano, mgomo kama huu unaoendelea pale mlimani ungekuwa wa maana zaidi kama wanafunzi wangekuwa wanapinga sera ya kuchangia gharama za elimu ya juu au kutaka serikali iongeze bajeti ya elimu. Lakini ilivyo leo kwa macho ya wananchi wengi ni kuwa haya madai yao yataonekena ya kibinafsi zaidi. Mnyika naomba uniambiwa, kwa njaa ya pesa iliyopo Tanzania leo hii ukimwambia mwananchi wa Kiteto, Gumanga, Kibondo, Chalinze, Keko Magurumbasi, Manzese kwa mfuga mbwa, etc, kwamba wanafunzi wanasema eti 3,600 kwa siku haitoshi, unafikiri watakusikiliza wewe au serikali? Tena RTD wataitungia mazungumzo baada ya habari utaona jinsi vijana watakavyosutwa! Huoni kwamba inabidi wanafunzi wabadili strategy za kudai mikopo yao, vinginevyo wataendelea kuonekana ni wabinafsi na serikali itaibuka mshindi tu?
That said, serikali yetu haina sera thabiti na muda mrefu ya elimu ya juu. Serikali ya CCM huwa haina uwezo wa kufikri zaidi ya kushinda uchaguzo ujao. Ili upate sera endelevu ya elimu ya juu lazima ufikirie beyond the next 5, 10,15 years. Ukweli unaouma pia ni kwamba hata sisi wapinzani hatuna sera inayoshikika kuhusu elimu ya juu. Pengine ndio maana kina mwanakijiji wana wasiwasi kama tungefanya tofauti kama tungepewa serikali kesho. Lazima sasa migomo hii ya wanafunzi itupe fursa ya kuchanganya bongo ili tuibuke na sera mbadala ya elimu ya juu. Ni vizuri sana kuwahurumia wanafunzi, lakini tukumbuke huruma pekee haisaidii sana maana haitatui tatizo.