Mwendapole Old
JF-Expert Member
- Dec 4, 2006
- 249
- 53
Hebu tuliangalie hili kwa pande zote.
1. Hawa wanafunzi wanahitaji elimu ; wanahitaji msaada wa serikali ya CCM ili waweze kupata hiyo elimu.
2.Katika suala la migomo, kati ya serikali na DARUSO, DARUSO ndio wako katika hasara (at a disadvantaged position). Serikali imashika mpini, wao wameshika Magali, wakivuta wao ndo wanaumia wakati serikali inapela.
3. Wakati wanagoma, hakuna aliyesimama kuwatetea. Wananchi, kuanzia hapa kwenye JF kuna waliowakandia, tukadidiriki thata kusema kuwa wanafunzi wenyewe wanaishia kwenye mabaa na madisko. Huko mitaani ndo kabisa hawakueleweka.
Ni baada ya wao kutimuliwa na dada zetu kuwa matatani ndo vyama vya upinzani wamesikika, na juzi tu ndo Dons wa Versity nao wakajitia kuwasupport. Hawa Dons ndo waliokuwaga wa kwanza kutoa tamko mara wanafunzi wanpaofukuzwa, leo wamesubiri kimbunga kimepita na vyama vya upinzani wameanza kujikusanya, ndo na wao tunawasikia.
4. Hawa wanafunzi, tupende tusiopende, ni mtaji kwa vyama vya siasa, be it CCM au wapinzani. Kila upande unawatumia kwa manufaa yao. Kumbuka ni majuzi tu CCM iliweka mkakati wa kufungua matawi katika vyuo vikuu. Wapinzani wakalivalia njuga, lakini nao katika hili nao wanaonekana kulifuatilia kwa namna Ambato itawasaidia wao, sio wanafunzi. Ikiwa walikuwa na nia ya kuwasaidia kikwelikweli walipaswa kujua kuwa hao wanafunzi walikuwa wanatakiwa kufanya mitihani mapema mwezi huu, na kwamba kufukuzwa kwao ni hasar asio tu kwao wao wanafunzi bali kwa Taifa mabalo linaishia kupata graduates fake, maana ili wasifeli watafanya biashara na mitihani hiyo ili tu wa-graduate. Wapinzani walijua sheria z anchi, wana wanasheria, walikuwa na uwezo wa kufungua kesi mahakamani mapema yalipotokea ili itolewe amri ya kuwarejesha wanafunzi madarasani. Lakini cha kushangaza waliendelea na vikao vyao ambavyo iliripotiwa kuwa vingime vilikuwa vikifanyika kwenye mabaa n ama-Don wa vyuo, sio viongozi wa DARUSO.
CCM nao hali wakijua kuwa sasa hili suala la wanfunzi limekuwa barata, wakaamua kuwazidi kete wapinzani kwa kutumia mbinu zao za medani, wakawaingia viongozi wa DARUSO kuwa hapa lazima muandike barua kuomba radhi, na sisi tutafanya yaliyobaki.
Sasa kwa barua hii wanafunzi wametumika kuwafunga wapinzani mdomo.
CCM ambao walikuwa mstari wa mbele kuwalaumu wapinzani kwa kutumia huo mgomo kama suala la kampeni wao ndo wameutumia kisawasawa. Nani anaumia?
5. Nini nafasi ya wazazi/wananchi katika hili.
Wale wanafunzi ni watoto/ndugu/rafiki zetu; wametoka katika jamii yetu; leo kwao kesho kwa wengine, ambao nao ni watoto/ndugu zetu. Hawa sio wakenye wala waganda, ni Watanzania wenzetu; uko wapi mshikamano wa wananchi katika hili. Imeonekana kama hawa wanafunzi ni wasaliti wakati wanatetea haki zao na kujaribu kuwapunguzia mzigo wazazi wetu.
Tumesoma mapato yaliyokusanywa na TRA, ni kodi zetu; yet inapokuja suala la kuzirudisha kwa jamii kama huduma muhimu serikali inajifanya hiyo ni favour. Bila aibu CCM na seriali yake inachota fedha hizo kama ruzuku;; ikifika wakati wa kampeni za uchaguzi wanachota kutoka kila idara, taasisi na ofisi ya umma; hiyo sio siri, ni situ kilo wazi; fedha halali za matumizi ya umma zinachotwa kwa ajili ya kampeni za CCM. Leo imekuwa vigumu kuzichota kuwapatia wanetu elimu amabayo hata sio kwa manufaa yao binafsi, bali ya Taifa.
6. Historia ya migomo vyuo vikuu inaonyesha wanaoumia ni viongozi wa DARUSO au wa migomo as the case may be. Hakuna mmoja wao ambaye hakuona joto ya jiwe haswa ile mogomo imara. Mbatia, Kaishozi na wenzao watakumbuka vizuri. Wakati wanafunzi wengine wanaruhusiwa kuendelea kusoma wao walifungiwa kusoma chuo chochote for some years, mpaka Mbatia akaamua kuingia zake upinzani jumala wakati Kaishozi alikuja rudia chuo na watoto wa nyuma yake sana baada ya kifungo chake baridi kuisha.
Ikifikia hapo linakuwa suala la everybody for himself and God for us all
Sitawalaumu uongozi wa DARUSO kwa kuomba radhi bila kufikiria yote haya , na hasa kujiuliza ni nini kiliendelea behind the scenes ambacho kimepelekea wao kuandika barua katika wakati ambao wapinzani na uongozi wa waalimu umeanza kuwasupport.