Julius Mtatiro kushitakiwa kwa uchochezi

Julius Mtatiro kushitakiwa kwa uchochezi

Vyanzo vyangu ndani ya jeshi la Polisi vinaninong'oneza kuwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa TAHLISO Bw. Julius Mtatiro anashikiliwa na Polisi kwa madai ya kuhusika na mgomo wa wanafunzi wa elimu ya juu. Bw. Mtatiro (kwa mujibu wa vyanzo hivyo) amekuwa akihojiwa bila ya kuruhusiwa mwanasheria wake kuwepo na kwa muda wa zaidi ya masaa 24. Tangu jana ambako ka nzi kamekuwa kakifuatilia Bw. Mtatiro amekuwa akihamishwa kutoka kituo kimoja cha POlisi na hatimaye kurundikwa pale Msimbazi ambako Polisi wamekataa mtu yeyote kumuona..

Licha ya kumhoji inadaiwa mbinu za "kulazimisha" zimekuwa zikitumika dhidi yake..

Kama kuna Mwanasheria yeyote natoa wito ajaribu kufika Mzimbazi ili kumwakilisha kwani inaonekana kwa mara nyingine tena kijana huyo anajikuta yuko matatani hasa baada ya serikali pia kumnyima nafasi ya kuwa Mwalimu baada ya kukataa kumpatia kazi licha ya qualifications zote alizonazo na baada ya kuambiwa kuwa hatopatiwa kazi mahali popote Tanzania...

Free Julius Mtatiro NOW!! and Stop the Harrassment!

Nijuavyo mimi, mgomo ni haki ya kikatiba - right of assembly and expression of opinions - na njia ya mwisho (last resort) kwa upande wa wanafunzi wa chuo kikuu kuwasilisha ujumbe wao, ambao mara nyingi hausikilizwi, kwa serikali.

Huyo kiongozi wa wanafunzi kukamatwa kwa uchochezi ni mbinu tu zinazotumiwa na serikali kutafuta mchawi na siyo suluhisho la migomo chuo kikuu. Suluhisho sahihi ni serikali kukaa chini na wanachuo na kupitia malalamiko yao (dialogue). Wanachokidai wanafunzi serikali bado haijui ni kitu gani na haitajua kama haisikilizi na kuelewa.

Hata katika maeneo mengine lazima kuwe na 'dialogue' kwani migomo itaendelea kuwapo tu mpaka hapo serikali itakapojifunza kusikiliza matatizo ya wananchi wake na kutenda kwa maneno na matendo.

Pia kuna wengine wanapotosha kuwa migomo inachochewa na chama fulani cha upinzani. Hii ni namna tu ya kukwepa uwajibikaji kwa upande wa serikali.
 
Mara baada ya kupata dhamana katika kesi yake ya uchochezi iliyofunguliwa mjini Dar, Bw. Julius Mtatiro alipata nafasi ya kuzungumza nasi kupitia KLHN kwa kirefu kuhusu sakata zima la kukamatwa kwake na madai mbalimbali yaliyozunguka tukio la kukamatwa na muda aliokuwa mikononi mwa Polisi. Je ni kweli aliteswa, Je alikataliwa mwanasheria, na je anahusika vipi na migomo inayoendelea kiasi cha kufunguliwa mashtaka mazito kama haya?

Sikiliza majibu kupitia MWANAKIJIJI.COM au KLHN (site zote mbili zinafanya kazi) na unaweza kusikiliza mahojiano hayo kuanzia dakika kumi na tano zijazo (tukiwa "live") na kutwa nzima ya leo.

MoDs naomba ikiexpire muinganisha na ile nyingine au vyovyote mtakavyoona inafaa.
 
Waziri Mkuu Mstaafu Chuo Kikuu Dar kortini kwa mgomo
Na James Magai na Pauline Richard

KATIBU Mkuu wa Muungano wa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu nchini (Tahliso) na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi (Daruso), Julius Itatiro amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shitaka la kusababisha vurugu katika chuo hicho.

Wakili wa Serikali, Stanlaus Boniface aliieleza mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Victoria Nongwa kwamba, kati ya Oktoba 13 na Novemba 15, mwaka huu katika eneo la Chuo Kikuu Dar esa laam, mshitakiwa alisababisha mgomo wanafunzi wa chuo hicho.

Ilidaiwa Mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo baada ya kuwashinikiza wenzake kugoma na kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani chuoni hapo, kitendo ambacho ni kosa na kinyume cha sheria.

Mshitakiwa baada ya kusomewa shitaka, alikana kuhusika na tuhuma hiyo na mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Desemba 2, mwaka huu itakapotajwa tena na mshitakiwa ameachiwa baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamnini wa kuaminika na yeye ametakiwa kusaini dhamana ya Sh100,000 .

Hata hivyo habari zilizopatikana kutoka kwa ndugu wa karibu wa mshitakiwa, zinasema kuwa alimaliza elimu yake ya chuo kati ya Mei na Juni, mwaka huu na kwamba vurugu hizo zilitokea wakati yeye akiwa ameshaondoka chuoni hapo.

Mwananchi Read News
 
Vyanzo vyangu ndani ya jeshi la Polisi vinaninong'oneza kuwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa TAHLISO Bw. Julius Mtatiro anashikiliwa na Polisi kwa madai ya kuhusika na mgomo wa wanafunzi wa elimu ya juu. Bw. Mtatiro (kwa mujibu wa vyanzo hivyo) amekuwa akihojiwa bila ya kuruhusiwa mwanasheria wake kuwepo na kwa muda wa zaidi ya masaa 24. Tangu jana ambako ka nzi kamekuwa kakifuatilia Bw. Mtatiro amekuwa akihamishwa kutoka kituo kimoja cha POlisi na hatimaye kurundikwa pale Msimbazi ambako Polisi wamekataa mtu yeyote kumuona..

Licha ya kumhoji inadaiwa mbinu za "kulazimisha" zimekuwa zikitumika dhidi yake..

Kama kuna Mwanasheria yeyote natoa wito ajaribu kufika Mzimbazi ili kumwakilisha kwani inaonekana kwa mara nyingine tena kijana huyo anajikuta yuko matatani hasa baada ya serikali pia kumnyima nafasi ya kuwa Mwalimu baada ya kukataa kumpatia kazi licha ya qualifications zote alizonazo na baada ya kuambiwa kuwa hatopatiwa kazi mahali popote Tanzania...

Free Julius Mtatiro NOW!! and Stop the Harrassment!

So,he didn't ask for a lawyer.
Wasn't mistreated...well,except for the ''kipanda uso thing''.
What now?Change of stories?
 
that is common for tanzania, watambana huko selo na kumlazimisha abadili msimamo kwa nguvu. wakishindwa wataanza kumuahidi mambo mazuri kemkem ili asiendeleze msimamo, wakishindwa na hapo', basi tutaambiwa tu ameumwa ghafla, amepelekwa kutibiwa nje then amefariki then atazikwa huko huko, just like Balali. may God protect him and let the wishes of higher learning students prevail.
 
Zito, Slaa, Tundu Lissu tumieni nafasi hii adimu ya vuguvugu kupanga na kucheza karata zenu mtuondolee hiki chama kikongwe kilichofilisika sera na hakina jipya lolote na sasa kinaendeleza maguvu ya dola tunayoitunza kwa kodi zetu. Watanzania tupo tayari kwa mabadiliko tunamtaka Musa tu atakayetuongoza kutoka Misri utumwani

Tumieni akili sasa za usomi wenu kustrategize na kupata momentum 2010 sio mbali, tupo pamoja kuona tunaleta mabadiliko kabla Zimbabwe nyingine haijaibuka kwetu. Muungwana anakunywa juice na Gadaffi tu hajui anavyokula vimeumbwa kwa watu kuumia.

Wameanza na Mtatiro, itakuja Mukoba na wengine watakaofuata, mgomo wa waalimu umetuonyesha kwamba hakuna haki inayotolewa na CCM bila kuidai kwa nguvu na kuacha mazoea ya kulia chini ya miti

CCM walitoa tamko lao viongozi wa waalimu wakamatwe, tumesubiri matamko ya vyama pinzani mbona hatuoni jamani??? Semeni tuwajue mmesimamai kwa waalimu au serikali yenu haina pesa?? Na hizi zilizotumwa juzi sijui wametoa wapi?? Anazosafiria muungwana sijui wapi zatoka etc leo Libya, kesho Morogoro halafu atakatisha aende Ulaya then atarudi aendelee ili mradi Rais yuop Luhanjo anamfanyia kazi zake
 
Nijuavyo mimi, mgomo ni haki ya kikatiba - right of assembly and expression of opinions - na njia ya mwisho (last resort) kwa upande wa wanafunzi wa chuo kikuu kuwasilisha ujumbe wao, ambao mara nyingi hausikilizwi, kwa serikali.

Huyo kiongozi wa wanafunzi kukamatwa kwa uchochezi ni mbinu tu zinazotumiwa na serikali kutafuta mchawi na siyo suluhisho la migomo chuo kikuu. Suluhisho sahihi ni serikali kukaa chini na wanachuo na kupitia malalamiko yao (dialogue). Wanachokidai wanafunzi serikali bado haijui ni kitu gani na haitajua kama haisikilizi na kuelewa.

Hata katika maeneo mengine lazima kuwe na 'dialogue' kwani migomo itaendelea kuwapo tu mpaka hapo serikali itakapojifunza kusikiliza matatizo ya wananchi wake na kutenda kwa maneno na matendo.

Pia kuna wengine wanapotosha kuwa migomo inachochewa na chama fulani cha upinzani. Hii ni namna tu ya kukwepa uwajibikaji kwa upande wa serikali.

na bila kujua kuwa kwa kumshtaki huyo kijana ni kuamsha hasira za watabnzania wote ambao siku zote ananugulia na kulalamikia matatizo yao ndani ndani maana wanajua hakuna atakae wasikiliza
 
Gamba la Nyoka link ya hapa hii:

[media]http://www.klhnews.com/images/podcasts/mtatiro.MP3[/media]
 
Sijawahi kusikiliza radio yako, hivi ndio mara ya kwanza nimesikiliza haya mahojiano kwenye hiyo link.

Kwanza kelele nyingi sana mwanzo kabisa kwenye utambulisho wa kipindi (sijui unakiitaje). Kuna maneno hayasikiki kabisa yamemezwa na sijui ndio mwaiita sound track au background.

Halafu introduction ya mahojiano imekuwa ndefu sana, halafu unaongea kwa kujitafuna tafuta sana, aaah nyingi, mt'taa nyingi, na kurudia maneno kama vile hayasomwi bali yanatoka kichwani kwa mtu kama mimi ambaye sijawahi kutangaza sehemu yeyote hata siku moja (hata kwenye birthday ya mwanangu sijaweza kuwa mc).

Improvement needed, congrats though.
 
mtatilo.jpg

University of Dar es salaam student Julius Mtatiro awaits his
arraignment on incitement charges at Kisutu Resident
Magistrate's Court in dar es Salaam yesterday
 
Naona Mtatiro fasta fasta, upekuzi na mashtaka kuandaliwa chap chap. Chenge, Mramba wao kimyaaa, mafile bado yanapekuliwa.
 
okay, okay, okay...jikoni kunasubiri msosi usichelewe.
 
..then 2010 sitashangaa majority ya UD student watavote CCM kama kawaida yao,maana hata diwani sehemu yao ni wa CCM,wanaume wa shoka wako tarime na ndio wana deserve support yetu sio hawa matapeli wanaobeba gari la kikwete na makamba huku wakicheza mdundiko then wakinyimwa pesa wana act kama watoto kwa kuvunja viti na milango,hata kuendesha migomo hawajui sijui ni wasomi gani hawa? ndio maana tunaishia kuwa na mikataba ya Richmond na EPA kwa wasomi wa namna hii....akili zao ni sawa na CCM!
 
Back
Top Bottom