Jukwaa linahusu Kenya lakini waanzisha thread karibia wote ni wa TZ

Wachache sababu wakenya na waganda wako nyuma Sana kutumia mitandao ya kijamii kuliko wa Tanzania
Are you serious? Tukiacha ushabiki, Kenya inashika nafasi ya 3 Afrika (nyuma ya Misri yenye watumiaji milioni 49.23 na Nigeria inayoongoza ikiwa na watumiaji milioni 126.078) kwa kuwa watumiaji wengi wa intaneti, ina watu milioni 46.87 wanaotumia intaneti sawa na 87.2% ya population; Uganda (milioni 18.50) sawa na 40.4% ya population na Tanzania (milioni 23.14) sawa na 38.7% ya population, hii ni kwa mujibu wa internet world statistic ya March, 2020...
 
Wakenya wengi Ni Twitter, YouTube na Facebook ingawa kunazo forums Kama Kenyanlist na Kenya talk( hili jina like censored humu i.e JamiiForums.com) jukwaa walilokimbilia Watanzania wakati JF ilifungwa.
 
Wakenya wengi Ni Twitter, YouTube na Facebook ingawa kunazo forums Kama Kenyanlist na Kenya talk( hili jina like censored humu i.e *********) jukwaa walilokimbilia Watanzania wakati JF ilifungwa.
Hata ukienda huko Twitter FB na YouTube bado utaona hivyo kwenye mada comments za Watanzania zinakua bado nyingi tena afadhar kenya kuliko hao Uganda ndio hawapo kabisaa mi nadhani tatizo lugha maana asilimia kubwa Uganda ukimpeleka kwenye Kingereza unamuona kwenye Kiswahili ndio kabisa
 
Are you serious? Tukiacha ushabiki, Kenya inashika nafasi ya 3 Afrika (nyuma ya Misri yenye watumiaji milioni 49.23 na Nigeria inayoongoza ikiwa na watumiaji milioni 126.078) kwa kuwa watumiaji wengi wa intaneti, ina watu milioni 46.87 wanaotumia intaneti sawa na 87.2% ya population; Uganda (milioni 18.50) sawa na 40.4% ya population na Tanzania (milioni 23.14) sawa na 38.7% ya population, hii ni kwa mujibu wa internet world statistic ya March, 2020...
Sasa kama hawa waganda mtandao gani walipokua wengi kuliko Tz hivi unajua wasanii sasa TZ soko lao kuu YouTube? Na imefiki Tz kama kuna skendo mtandaoni inavuma na kipindi hicho msanii alipanga achie wimbo anaghairi ili upepo utulie ndio anaitoa sasa utasemaje TZ wapo wachache mtandaoni kuliko Uganda ? Hizi takwimu labda za upande mmoja
 
Wakuu, nimetafakari sana baada ya kupitia threads za kwenye jukwaa hili. Utakuta waanzilishi wa threads zilizo nyingi ni wa TZ badala ya wakenya. Hii imekaaje? Tujadiliane.
Kwakuwa msingi wa JF ni Tanzania

Jr
 
tumia kichwa kufikiri,unajua kenya ina watu wangapi???
watu milioni 49,ni sawa na kusema hamna watoto kenya,wazee,wala watu wasio na kipato cha chini.

mna mahaba na takwimu hata mkidanganywa hamna habari.
 
Sasa kama hawa waganda mtandao gani walipokua wengi kuliko Tz hivi unajua wasanii sasa TZ soko lao kuu YouTube? Na imefiki Tz kama kuna skendo mtandaoni inavuma na kipindi hicho msanii alipanga achie wimbo anaghairi ili upepo utulie ndio anaitoa sasa utasemaje TZ wapo wachache mtandaoni kuliko Uganda ? Hizi takwimu labda za upande mmoja
Sijasema kuwa Waganda ni wengi kuliko Watanzania, soma tena posti yangu. Lakini kitu cha pili ni kwamba wingi pekee bado hausaidii bali pia ni jinsi gani watu wanachangamkia posti zinazohusu mambo ya nchi yao (uzalendo), na pia kuna suala la ubaguzi. Waganda wana tabia ya ubaguzi, wanabaguana, hasa kama mtu anatumia lugha isiyokuwa ya Kiingereza au Kiganda. Kwa mfano Jose Chameleon alikuwa anabagulia sana nchini Uganda kwa kuwa anaimba kwa Kiswahili...
 
Are you serious? Tukiacha ushabiki, Kenya inashika nafasi ya 3 Afrika (nyuma ya Misri yenye watumiaji milioni 49.23 na Nigeria inayoongoza ikiwa na watumiaji milioni 126.078) kwa kuwa watumiaji wengi wa intaneti, ina watu milioni 46.87 wanaotumia intaneti sawa na 87.2% ya population; Uganda (milioni 18.50) sawa na 40.4% ya population na Tanzania (milioni 23.14) sawa na 38.7% ya population, hii ni kwa mujibu wa internet world statistic ya March, 2020...
Wengi wa watanzania wenzako ni mihemko tu hawana data yoyote kuunga mkono hoja zao ila wabishi kweli....tushawazoea tu
 
tumia kichwa kufikiri,unajua kenya ina watu wangapi???
watu milioni 49,ni sawa na kusema hamna watoto kenya,wazee,wala watu wasio na kipato cha chini.

mna mahaba na takwimu hata mkidanganywa hamna habari.
Wewe ndiyo utumie akili na usitumie kichwa kufugia nywele tu. Hizi siyo takwimu zangu ni za mamlaka ya mawasiliano duniani. Soma hapa Africa Internet Users, 2020 Population and Facebook Statistics labda utatoa tongotongo na uache ushabiki maandazi...
 
Wakuu, nimetafakari sana baada ya kupitia threads za kwenye jukwaa hili. Utakuta waanzilishi wa threads zilizo nyingi ni wa TZ badala ya wakenya. Hii imekaaje? Tujadiliane.
Na wewe ni Mtanzania au Mkenya?
 
Wewe ndiyo utumie akili na usitumie kichwa kufugia nywele tu. Hizi siyo takwimu zangu ni za mamlaka ya maswaliano duniani. Soma hapa Africa Internet Users, 2020 Population and Facebook Statistics labda utatoa tongotongo na uache ushabiki maandazi...
mamlaka ni nini wewe!!!!umefungwa na uwezo wa wazungu kufikiri kwa niaba yako,kwani leo ukiabiwa watz milioni 58 kati ya 60 wanatumia mitandao utakubali tu,sababu ni takwimu za mamlaka ya mtandao duniani!!!!???

au ndio nyinyi mliokuwa mkiamini wodi zimejaa wagonjwa wa corona,mpaka manesi na madaktari wanakimbia wagonjwa???
 
mamlaka ni nini wewe!!!!umefungwa na uwezo wa wazungu kufikiri,kwani leo ukiabiwa watz milioni 58 kati ya 60 wanatumia mitandao utakubali tu,sababu ni takwimu za mamlaka ya mtandao duniani!!!!???

au ndio nyinyi mliokuwa mkiamini wodi zimejaa wagonjwa wa corona,mpaka manesi na madaktari wanakimbia wagonjwa???
Povu lote kwa kuwa tu tafiti zimewabeba Wakenya, ila zingetu-favour Watanzania usingepiga kelele! Kaazi kwelikweli...
 
povu liko wapi!!!!kwani sisi namba tulizopewa wewe unakubaliana nazo au sababu kenya iko mbele basi mengine hayana maana???
 
Back
Top Bottom