Juhudi za Rais Samia zimesaidia kukuza mchango wa sekta ya madini kwenye pato la taifa

kalacha mateo

Senior Member
Sep 27, 2021
118
237
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliitaka wizara ya madini kuhakikisha wanafanya kazi kubwa kuongeza mchango wa sekta hiyo kwenye pato la Taifa kutoka kutoka 6.7% mwaka 2020 hadi kufikia 10% mwaka 2025.

Hadi sasa sekta hiyo inachyangia 9.7 ya pato la taifa, matokeo haya mazuri yameonekana mapema kutokana na kazi iliyofanywa ya kuboresha sera za uwekezaji kwenye sekta ya madini zilizochochea kuongezeka kwa uwekezaji kwenye sekta hiyo na uuzaji wa madini nje ya nchi.

Aidha, serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu ilifanya uwezeshaji kwa wachimbaji wadogo nchini ikiwemo ugawaji wa leseni na vitalu, mikopo, elimu ya uchimbaji pamoja na kusaini mikata ya nishati ianyolenga kupeleka umeme kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo.

Juhudi hizo zimesaidia kuongeza mchango wa wachimbaji wadogo kwenye pato la taifa kutoka 20% hadi 40%. Seriakli ianendelea kuboresha sekta mbalimbali nchini ili kukuza pato la taifa na kuhakikisha watanzania wanapata maendeleo.
1255.jpg
 
Back
Top Bottom